Ange Postecoglou - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Mon, 06 Jul 2026 19:15:26 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=7.0.5 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg Ange Postecoglou - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 Postecoglou kocha mpya Al-Nassr https://www.greensports.co.tz/2026/07/05/postecoglou-kocha-mpya-al-nassr/ https://www.greensports.co.tz/2026/07/05/postecoglou-kocha-mpya-al-nassr/#respond Sun, 05 Jul 2026 15:39:50 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=14757 Riyadh, Saudi ArabiaKocha wa zamani wa timu ya Tottenham Hotspur ya England, Ange Postecoglou ameteuliwa kuwa kocha mkuu wa timu ya Al-Nassr ya Saudi Arabia.Al-Nassr, timu ambayo pia anaichezea mwanasoka wa zamani wa timu za Real Madrid na Man United, Cristiano Ronaldo, kwa mara ya kwanza Mei mwaka huu ilifanikiwa kutwaa taji la Ligi Kuu […]

The post Postecoglou kocha mpya Al-Nassr first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Riyadh, Saudi Arabia
Kocha wa zamani wa timu ya Tottenham Hotspur ya England, Ange Postecoglou ameteuliwa kuwa kocha mkuu wa timu ya Al-Nassr ya Saudi Arabia.
Al-Nassr, timu ambayo pia anaichezea mwanasoka wa zamani wa timu za Real Madrid na Man United, Cristiano Ronaldo, kwa mara ya kwanza Mei mwaka huu ilifanikiwa kutwaa taji la Ligi Kuu Saudi Arabia maarufu Saudi Pro League.
Kabla ya kumteua Ange, Al-Nassr ilikuwa ikinolewa na kocha kutoka Ureno, Jorge Jesus lakini kocha huyo mwenye umri wa miaka 71, aliachana na klabu hiyo baada ya kumalizika kwa msimu uliopita.
Kwa kipindi kirefu Postecoglou amekuwa bila ya kazi yangu atimuliwe katika klabu ya Nottingham Forest Oktoba mwaka jana, timu ambayo aliinoa kwa siku zisizozidi 40.
Postecoglou, kocha mwenye umri wa miaka 60, raia wa Australia na mzaliwa wa Ugiriki, amesaini mkataba wa miaka miwili na Al-Nassr.
Moja ya mafanikio ya kukumbukwa na Postecoglou ni wakati akiwa na Spurs ambayo mwaka 2025 aliiwezesha kubeba taji la Europa Ligi lakini kabla ya hapo alikuwa Celtic ya Uskochi, timu ambayo aliiwezesha kutwaa taji ya ligi kuu nchini humo mara mbili.
Kwa siku za karibuni, Postecoglou amekuwa akifanya kazi ya uchambuzi wa mechi za soka kwenye fainali za Kombe la Dunia 2026 zinazoendelea katika nchi za Marekani, Canada na Mexico.

The post Postecoglou kocha mpya Al-Nassr first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2026/07/05/postecoglou-kocha-mpya-al-nassr/feed/ 0
Postecoglou kocha mpya Spurs https://www.greensports.co.tz/2023/06/06/postecoglou-kocha-mpya-spurs/ https://www.greensports.co.tz/2023/06/06/postecoglou-kocha-mpya-spurs/#respond Tue, 06 Jun 2023 20:33:29 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=6490 London, EnglandTottenham Hotspur imethibitisha kuwa Ange Postecoglou ndiye kocha mpya wa timu hiyo baada ya kusaini mkataba wa miaka minne na hivyo kuwa kocha wa kwanza kutoka Australia kuinoa timu ya Ligi Kuu England (EPL).Postecoglou (pichani) mwenye umri wa miaka 57 ambaye hapo kabla alikuwa akiinoa Celtic ya Scotland, ataanza rasmi kazi katika klabu hiyo […]

The post Postecoglou kocha mpya Spurs first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

London, England
Tottenham Hotspur imethibitisha kuwa Ange Postecoglou ndiye kocha mpya wa timu hiyo baada ya kusaini mkataba wa miaka minne na hivyo kuwa kocha wa kwanza kutoka Australia kuinoa timu ya Ligi Kuu England (EPL).
Postecoglou (pichani) mwenye umri wa miaka 57 ambaye hapo kabla alikuwa akiinoa Celtic ya Scotland, ataanza rasmi kazi katika klabu hiyo Julai Mosi huku mwenyekiti wa Spurs, Daniel Levy akiamini kocha huyo atafanya kazi yake vizuri.
“Ange atabadili mtazamo na kwa haraka atakuwa na timu yenye mfumo wa kushambulia, ana rekodi nzuri ya kuwaendeleza wachezaji na mwenye uelewa kuhusu umuhimu wa muunganiko wa kuanzia kwenye akademi,” alisema Levy katika taarifa yake.

“Kila kitu ni muhimu kwa klabu yetu, tumefurahishwa kwa Ange kuungana nasi wakati huu tukijiandaa kwa ajili ya msimu ulio mbele yetu,” aliongeza Levy.


Habari za Alhamisi iliyopita zilidai kwamba Spurs iliwasiliana na mabosi wa Celtic kuhusu kumtaka kocha huyo na mazungumzo yakaenda vizuri jana Jumatatu na kwa haraka baada ya Postecoglou mwenyewe kuonesha shauku ya kutaka kuinoa timu ya EPL.
Postecoglou ambaye ameiwezesha Celtic kubeba mataji matatu ya ndani msimu huu, anarithi mikoba ya kocha Mtaliano Antonio Conte ambaye mambo yalimshinda katika klabu hiyo na kuamua kuondoka.

The post Postecoglou kocha mpya Spurs first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/06/06/postecoglou-kocha-mpya-spurs/feed/ 0