Zizou - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Sat, 20 Apr 2024 12:41:14 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=6.8.1 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg Zizou - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 Zizou aipigia hesabu Man United https://www.greensports.co.tz/2024/04/20/zizou-aipigia-hesabu-man-united/ https://www.greensports.co.tz/2024/04/20/zizou-aipigia-hesabu-man-united/#respond Sat, 20 Apr 2024 12:41:13 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=10691 Paris, UfaransaKocha wa zamani wa Real Madrid, Zinedine Zidane au Zizou inadaiwa anafuatilia kwa karibu kinachoendelea kwa kocha wa Man United, Erik ten Hag na angependa kuinoa timu hiyo kuliko Bayern Munich.Zizou ambaye pia ni mchezaji wa zamani wa Real Madrid na timu ya taifa ya Ufaransa, amekuwa hana kazi kwa kipindi kirefu tangu kufeli […]

The post Zizou aipigia hesabu Man United first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Paris, Ufaransa
Kocha wa zamani wa Real Madrid, Zinedine Zidane au Zizou inadaiwa anafuatilia kwa karibu kinachoendelea kwa kocha wa Man United, Erik ten Hag na angependa kuinoa timu hiyo kuliko Bayern Munich.
Zizou ambaye pia ni mchezaji wa zamani wa Real Madrid na timu ya taifa ya Ufaransa, amekuwa hana kazi kwa kipindi kirefu tangu kufeli kwa mpango uliodaiwa wa yeye kuinoa timu ya taifa ya Ufaransa.
Chanzo kimoja cha habari nchini Ufaransa kimeeleza kuwa Zizou ambaye amewahi pia kuhusishwa na mpango wa kuinoa Bayern Munich na ingawa klabu hiyo haijawasiliana naye rasmi lakini mwenyewe inadaiwa angependa zaidi kuinoa Man United.
Zizou amejipatia mafanikio makubwa akiwa mchezaji wa Real Madrid kwa kubeba mataji kadhaa likiwamo la Ligi ya Mabingwa Ulaya kabla ya kugeukia ukocha na kujipatia heshima nyingine kwa kubeba taji hilo hilo hilo na Real Madrid.
Kocha huyo hata hivyo baada ya hapo amekuwa hana kazi licha ya kuhusishwa na klabu kadhaa ikiwamo PSG pamoja na timu ya taifa ya Ufaransa, mipango ambayo yote ilifeli lakini kwa sasa ameanza kuhusishwa na klabu za Bayern Munich na Man United.
Bayern inasaka kocha wa kumrithi Thomas Tuchel ambaye mkataba wake umesitishwa na huu ni msimu wake wa mwisho na timu hiyo wakati Man United inadaiwa kuwa mbioni kufanya mabadiliko makubwa.
Mabadiliko hayo yanayosimamiwa na mmiliki mwenza mpya wa klabu hiyo bilionea, Sir Jim Ratcliffe yameshaanza kufanywa na huenda yakamkuta Ten Hag hasa kwa kuwa mwenendo wa timu hiyo si mzuri kwa sasa.

The post Zizou aipigia hesabu Man United first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/04/20/zizou-aipigia-hesabu-man-united/feed/ 0
Ancelotti awachambua Bellingham, Zizou https://www.greensports.co.tz/2023/11/30/ancelotti-awachambua-bellingham-zizou/ https://www.greensports.co.tz/2023/11/30/ancelotti-awachambua-bellingham-zizou/#respond Thu, 30 Nov 2023 12:44:07 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=8691 Madrid, HispaniaKiwango cha soka la kiungo wa Real Madrid, Jude Bellingham kimeendelea kumfurahisha kocha wake, Carlo Ancelotti ambaye amechambua sifa za mchezaji huyo na nyota wa zamani wa timu hiyo, Zinedine Zidane au Zizou.Ancelotti alitoa uchambuzi huo jana Jumatano mara baada ya mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Napoli, mechi ambayo Real Madrid […]

The post Ancelotti awachambua Bellingham, Zizou first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Madrid, Hispania
Kiwango cha soka la kiungo wa Real Madrid, Jude Bellingham kimeendelea kumfurahisha kocha wake, Carlo Ancelotti ambaye amechambua sifa za mchezaji huyo na nyota wa zamani wa timu hiyo, Zinedine Zidane au Zizou.
Ancelotti alitoa uchambuzi huo jana Jumatano mara baada ya mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Napoli, mechi ambayo Real Madrid ilitoka na ushindi wa mabao 4-2 huku Bellingham akicheza soka la kuvutia.
Katika mechi hiyo iliyopigwa katika dimba la Santiago Bernabeu, Bellingham ndiye aliyefunga kwa kichwa bao la pili la Real Madrid baada ya Napoli kupata bao la kwanza kupitia Giovanni Simeone na Rodrygo kusawazisha.
Napoli walisawazisha kupitia Frank Zambo na kufanya matokeo kuwa 2-2 lakini Madrid waliongeza bao la tatu lililofungwa na Nico Paz na Bellingham kutoa pasi iliyozaa bao la nne mfungaji akiwa Joselu.
“Ni vigumu kulinganisha vizazi viwili tofauti, ninachokiona ni uwezo wa Bellingham kuingia kwenye boksi, Zidane hakuwa na hilo lakini kuna sifa na hadhi ya kipekee ambayo Zidane alikuwa nayo na Bellingham hana,” alisema Ancelotti alipotakiwa na waandishi kutoa tathmini yake kuhusu Bellingham na Zidane ambaye alikuwa jukwaani akiangalia mechi hiyo.

Ancelotti hata hivyo alisema kwamba kinachotokea sasa ni soka la zama hizi ambalo linahitaji mchezaji mwenye nguvu zinazohitajika kama ilivyo kwa Bellingham, ambaye kwa haraka unaweza kumuona katika sehemu kubwa ya uwanja.

“Anatushangaza kila siku na katika kila mechi, si kwamba anatushangaza sisi tu bali anamshangaza kila mtu, Bellingham ni zawadi ya soka, kocha wake na wachezaji wenzake wanafurahia kuwa naye na mashabiki pia wanafurahia lakini kila mmoja anafurahia kuona mchezaji mwenye sifa zake na mwenye mtazamo chanya,” alisema Ancelotti.


Bellingham hadi sasa amefunga jumla ya mabao 15 katika mechi 16 za Real Madrid, na zaidi ya hilo ana rekodi ya kufunga goli katika kila mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya aliyocheza hadi sasa.

The post Ancelotti awachambua Bellingham, Zizou first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/11/30/ancelotti-awachambua-bellingham-zizou/feed/ 0