Zimamoto - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Tue, 29 Apr 2025 19:51:58 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=6.8 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg Zimamoto - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 Penalti zaipeleka Yanga fainali Kombe la Muungano https://www.greensports.co.tz/2025/04/29/penalti-zaipeleka-yanga-fainali-kombe-la-muungano/ https://www.greensports.co.tz/2025/04/29/penalti-zaipeleka-yanga-fainali-kombe-la-muungano/#respond Tue, 29 Apr 2025 19:48:33 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=13343 Na mwandishi wetuYanga imefuzu hatua ya fainali Kombe la Muungano baada ya kuitoa Zimamoto kwa penalti 3-1 katika mechi ya nusu fainali iliyochezwa leo Jumanne Aprili 29, 2025 kwenye Uwanja wa Gombani, Pemba.Timu hizo zilipigiana penalti baada ya sare ya bao 1-1 katika dakika 90 za kawaida, bao la Yanga likifungwa na Maxi Nzengeli dakika […]

The post Penalti zaipeleka Yanga fainali Kombe la Muungano first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Yanga imefuzu hatua ya fainali Kombe la Muungano baada ya kuitoa Zimamoto kwa penalti 3-1 katika mechi ya nusu fainali iliyochezwa leo Jumanne Aprili 29, 2025 kwenye Uwanja wa Gombani, Pemba.
Timu hizo zilipigiana penalti baada ya sare ya bao 1-1 katika dakika 90 za kawaida, bao la Yanga likifungwa na Maxi Nzengeli dakika ya 28 na la Zimamoto lilifungwa na Said Mwinyi dakika ya 69 kwa penalti.
Katika mikwaju ya penalti, Zimamoto walikuwa wa kwanza ambapo Said Mwinyi aliyefunga penalti dakika ya 69 safari hii alishindwa kumtungua kipa Abutwalib Mshery na hivyo kuinyima bao Zimamoto.
Yanga nao walipiga penalti yao ya kwanza na Israel Mwenda akafanikiwa kuujaza mpira wavuni wakati Zimamoto wakakosa kwa mara ya pili baada ya shuti la Yusuf Idriss kugonga mwamba.
Yanga nao walikosa baada ya shuti la Nzengeli kwenda nje licha ya kufanikiwa kumpoteza kipa na Ndipo Zimamoto wakasawazisha kwa kufunga penalti kwa mara ya kwanza kwa bao lililofungwa na Abdulhamid Ramadhan.
Penalti ya tatu ya Yanga ilipigwa na Bakari Mwamnyeto ambaye alifunga lakini mambo yakawa mabaya kwa Suleiman Said wa Zimamoto ambaye penalti yake iliokolewa.
Clement Mzize alikuwa mpigaji wa penalti ya mwisho ya Yanga na mpira wake kwenda wavuni hali iliyoibua shangwe kwenye benchi la Yanga na mashabiki wao wakifurahia kufikia hatua ya fainali.
Mechi hiyo hata hivyo ilikuwa ngumu kwa Yanga kwani licha ya Zimamoto kubaki 10 uwanjani baada ya kutolewa kwa Seif Mmadi bado Yanga ilishindwa kupata bao liha ya mashambulizi ya mara kwa mara.
Mmadi alipewa kadi nyekundu na kutoka nje baada ya kumshika mabega Nzengeli ili kumzuia asilete madhara lakini Yanga hawakuweza kuitumia nafasi hiyo kupata bao la pili katika dakika 90 za kawaida.
Zimamoto ilijifariji kwa kutoa mchezaji bora wa mechi hiyo ambaye ni kiungo wao, Haruna Abdallah huku kipa wao Hassan Mwinyi naye akionesha ushujaa katika dakika 90 za kawaida.
Kipa huyo mara kadhaa aliokoa michomo ya wachezaji wa Yanga kina Stephane Aziz Ki, Mzize na Mudathir Yahya ambao walishindwa kuipatia Yanga mabao kutokana na umahiri wa kipa huyo..
Kwa ushindi huo Yanga sasa itacheza mechi ya fainali keshokutwa Alhamisi dhidi ya JKU ambayo ilitoa Azam FC kwa mabao 2-1 katika mechi nyingine ya nusu fainali iliyochezwa jana Jumatatu.

The post Penalti zaipeleka Yanga fainali Kombe la Muungano first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2025/04/29/penalti-zaipeleka-yanga-fainali-kombe-la-muungano/feed/ 0