Xavi - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Sat, 26 Oct 2024 10:45:44 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=7.0.4 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg Xavi - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 Xavi, Amorim watajwa Man United https://www.greensports.co.tz/2024/10/26/xavi-amorim-watajwa-man-united/ https://www.greensports.co.tz/2024/10/26/xavi-amorim-watajwa-man-united/#respond Sat, 26 Oct 2024 10:45:43 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=12080 Manchester, EnglandNafasi ya kocha Erik ten Hag katika kikosi cha Man United imeendelea kujadiliwa huku makocha Xavi Hernandez na Ruben Amorim (pichani chini) wa Sporting Lisbon wakianza kutajwa.Hii si mara ya kwanza kwa Xavi aliyeachana na Barcelona msimu uliopita kutajwa akihusishwa na nafasi hiyo lakini kwa Amorin hii ni mara yake ya kwanza kuingizwa katika […]

The post Xavi, Amorim watajwa Man United first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Manchester, England
Nafasi ya kocha Erik ten Hag katika kikosi cha Man United imeendelea kujadiliwa huku makocha Xavi Hernandez na Ruben Amorim (pichani chini) wa Sporting Lisbon wakianza kutajwa.
Hii si mara ya kwanza kwa Xavi aliyeachana na Barcelona msimu uliopita kutajwa akihusishwa na nafasi hiyo lakini kwa Amorin hii ni mara yake ya kwanza kuingizwa katika mbio hizo.
Habari za ndani zilizopatikana kwenye vyanzo mbalimbali vya habari hii leo Jumamosi vimeeleza kuwapo kwa mpango huo ingawa makocha hao hawajasema lolote kuhusu kuhusishwa kwao.
Kilichopo wazi kwa Ten Hag ni kwamba mwenendo wa Man United si wa kuvutia katika Ligi Kuu England (EPL) hivyo mjadala kuhusu hatma ya kocha huyo ni jambo linalotarajiwa.


Mara baada ya msimu uliopita wa 2023-24 kumalizika ilitarajiwa ingekuwa mwisho wa Ten Hag kuinoa Man United lakini ubingwa wa Kombe la FA inasemekana ulimbeba na kuwafanya vigogo wa timu hiyo kumuongezea mkataba wa mwaka mmoja.
Katika EPL hadi sasa Man United inashika nafasi ya 12 ikiwa imecheza mechi nane, imepoteza tatu na kushinda mitatu na kutoka sare mara mbili.
Na ingawa kocha huyo amekuwa akijifariji mara kwa mara kutokana na janga la wachezaji majeruhi kwenye kikosi chake lakini kiujumla hali halisi hairidhishi na haishangazi kuona nafasi yake ikizidi kugeuzwa mjadala.

The post Xavi, Amorim watajwa Man United first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/10/26/xavi-amorim-watajwa-man-united/feed/ 0
Xavi: Kocha mpya Barca atapata tabu https://www.greensports.co.tz/2024/05/27/xavi-kocha-mpya-barca-atapata-tabu/ https://www.greensports.co.tz/2024/05/27/xavi-kocha-mpya-barca-atapata-tabu/#respond Mon, 27 May 2024 18:38:55 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=11133 Barcelona, HispaniaKocha aliyetimuliwa Barcelona, Xavi Hernandez amesema kwamba kocha mpya atakayebeba majukumu yake katika timu hiyo atapata tabu.Xavi, 44, alitangazwa kutimuliwa rasmi na timu hiyo kabla ya kuiongoza katika mechi ya mwisho ya kumaliza msimu dhidi ya Sevilla juzi Jumamosi, mechi ambayo Barca ilipata ushindi wa mabao 2-1.Mara baada ya Xavi kutimuliwa habari zilizopo ni […]

The post Xavi: Kocha mpya Barca atapata tabu first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
Kocha wa Barcelona

Barcelona, Hispania
Kocha aliyetimuliwa Barcelona, Xavi Hernandez amesema kwamba kocha mpya atakayebeba majukumu yake katika timu hiyo atapata tabu.
Xavi, 44, alitangazwa kutimuliwa rasmi na timu hiyo kabla ya kuiongoza katika mechi ya mwisho ya kumaliza msimu dhidi ya Sevilla juzi Jumamosi, mechi ambayo Barca ilipata ushindi wa mabao 2-1.
Mara baada ya Xavi kutimuliwa habari zilizopo ni kwamba kocha wa zamani wa timu ya taifa ya Ujerumani na klabu ya Bayern Munich, Hansi Flick anatazamiwa kubeba majukumu yake.
Xavi, ambaye alikuwa na mkataba Barca unaofikia ukomo mwaka 2025, Januari mwaka huu alitangaza angeondoka mara baada ya msimu huu lakini alibadili msimamo mwezi uliopita akidai kwamba anatarajia kuendelea na mkataba wake.
Akimzungumzia kocha mpya wa Barca, Xavi alisema kwamba atapata tabu kwa sababu klabu hiyo ni sehemu iliyojaa utata na ni kazi ngumu.

“Nakwambia ‘utapata tabu’, hii ni sehemu yenye utata na ni kazi ngumu na unalazimika kuwa mtulivu,” alisema Xavi.


Xavi aliyekabidhiwa jukumu la ukocha Barca, Novemba 2021, katika msimu wake wa kwanza kamili alibeba taji la La Liga na Spanish Super lakini msimu huu mambo hayajawa mazuri, timu hiyo imemaliza ligi nafasi ya pili nyuma ya mahasimu wao Real Madrid kwa tofauti ya pointi 10.
“Ninachokiona ni kwamba kila nilichokifanya kwa miaka miwili na nusu kimezua mabalaa, nimekuwa nikiwindwa mara nyingi na katika mazingita mengi,” alisema Xavi.

The post Xavi: Kocha mpya Barca atapata tabu first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/05/27/xavi-kocha-mpya-barca-atapata-tabu/feed/ 0
Xavi atimuliwa rasmi Barca https://www.greensports.co.tz/2024/05/24/xavi-atimuliwa-rasmi-barca/ https://www.greensports.co.tz/2024/05/24/xavi-atimuliwa-rasmi-barca/#respond Fri, 24 May 2024 18:59:04 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=11108 Barcelona, HispaniaHatimaye klabu ya Barcelona imetangaza rasmi kumfuta kazi kocha Xavi huku kocha wa zamani wa Bayern Munich, Hansi Flick akitarajiwa kuchukua nafasi yake.Hatua ya kumtimua Xavi imekuja baada ya hivi karibuni kuibuka mjadala juu ya hatma yake hasa baada ya kuwapo madai kwamba klabu hiyo ilipanga kumbakisha licha ya kocha huyo kutangaza Januari mwaka […]

The post Xavi atimuliwa rasmi Barca first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Barcelona, Hispania
Hatimaye klabu ya Barcelona imetangaza rasmi kumfuta kazi kocha Xavi huku kocha wa zamani wa Bayern Munich, Hansi Flick akitarajiwa kuchukua nafasi yake.
Hatua ya kumtimua Xavi imekuja baada ya hivi karibuni kuibuka mjadala juu ya hatma yake hasa baada ya kuwapo madai kwamba klabu hiyo ilipanga kumbakisha licha ya kocha huyo kutangaza Januari mwaka huu kwamba ataondoka baada ya msimu huu.
Xavi, 44, hata hivyo keshokutwa Jumapili atakuwa uwanjani katika mechi ya mwisho ya msimu wa 2023-24 wa La Liga ambapo Barca itakuwa nyumbani ikiumana na Sevilla.
Mkataba wa Xavi na Barca unafikia ukomo mwaka 2025 lakini uamuzi wa kuachana naye umekuja baada ya kikao kati ya rais wa klabu hiyo, Joan Laporta na mkurugenzi wa michezo, Deco ambacho kilifanyika leo Ijumaa.
Habari za Xavi kuendelea kuinoa Barca zilipata nguvu mwezi uliopita lakini inadaiwa aliponzwa na kauli yake alipozungumzia matatizo ya kiuchumi ya Barca akidai itakuwa vigumu kwa timu hiyo kushindana na Real Madrid na klabu nyingine kubwa za Ulaya.
Taarifa ya Barca ilimshukuru Xavi kwa kazi aliyoifanya tangu akabidhiwe majukumu ya kuinoa timu hiyo mwaka 2021 na msimu uliopita wa 2022-23 aliiwezesha kutwaa taji la La Liga.

“Haijawahi kuwa rahisi kuiacha klabu ya maisha yako lakini najivunia miaka miwili na nusu kuwa kiongozi kwenye vyumba vya kubadilishia nguo, hii imekuwa kama familia yangu ya pili,” alisema Xavi.


Xavi alisema baada ya Jumapili atabaki kuwa shabiki wa Barca jukwaani, na hilo halimpi shida kwa sababu kabla ya kuwa mchezaji au kocha yeye ni shabiki wa Barca na amekuwa katika maisha yake yote akiitakia mema klabu hiyo.
Baada ya kutangaza kuachana na Xavi, Barca ilidai kwamba mfumo mpya wa uendeshaji imu hiyo na benchi la ufundi vitawekwa wazi katika siku chache zijazo baada ya Flick kuanza kazi.
Flick, 59 amekuwa bila kazi tangu Septemba 2023 alipotimuliwa Bayern, timu ambayo anajivunia rekodi yake ya mwaka 2020 alipoiwezesha kubeba mataji matatu ya Ligi Kuu Ujerumani au Bundesliga, DFB-Pokal na Ligi ya Mabingwa Ulaya.

The post Xavi atimuliwa rasmi Barca first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/05/24/xavi-atimuliwa-rasmi-barca/feed/ 0
Xavi, Rais Barca kufanya kikao https://www.greensports.co.tz/2024/05/23/xavi-rais-barca-kufanya-kikao/ https://www.greensports.co.tz/2024/05/23/xavi-rais-barca-kufanya-kikao/#respond Thu, 23 May 2024 09:32:42 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=11092 Barcelona, HispaniaRais wa Barcelona, Joan Laporta anatarajia kukutana na kocha wa klabu hiyo, Xavi Hernandez mapema wiki ijayo huku kukiwa na habari kwamba klabu hiyo inatafakari juu ya uamuzi wa kumuacha au kuendelea na kocha huyo.Habari za ndani zinadai kwamba licha ya Xavi kutangaza mapema kwamba ataachana na timu hiyo baada ya msimu huu, uamuzi […]

The post Xavi, Rais Barca kufanya kikao first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Barcelona, Hispania
Rais wa Barcelona, Joan Laporta anatarajia kukutana na kocha wa klabu hiyo, Xavi Hernandez mapema wiki ijayo huku kukiwa na habari kwamba klabu hiyo inatafakari juu ya uamuzi wa kumuacha au kuendelea na kocha huyo.
Habari za ndani zinadai kwamba licha ya Xavi kutangaza mapema kwamba ataachana na timu hiyo baada ya msimu huu, uamuzi wa mwisho hadi sasa haujafikiwa na kumekuwa na sintofahamu kama aabaki au ataondoka.
Mkurugenzi wa michezo wa klabu hiyo, Deco na jopo la wasaidizi wake nao inatarajia watashiriki katika mkutano wa Xavi na Laporta ambao utafanyika baada ya mechi za mwisho za La Liga ambazo zitapigwa Jumapili ijayo.
Moja ya mambo ambayo imeelezwa kuwa yanatarajiwa kujadiliwa katika kikao hicho ni pamoja na timu kumaliza msimu bila taji lakini pia mustakabali wa Xavi katika timu kama ataendelea kuwapo au wataachana naye.
Kwa kipindi kirefu zimekuwapo habari kwamba Laporta anamkubali Xavi na angependa aendelee kuinoa timu hiyo lakini baadhi ya wajumbe wa bodi wanaamini mabadiliko yanahitajika kwenye timu hiyo hasa baada ya kumaliza msimu bila taji.
Ikitokea Xavi akatimuliwa baadhi ya makocha wanaotajwa kuchukua nafasi yake ni Rafa Marquez wa timu ndogo ya Barca, Hans Flick, Thomas Tuchel, Thiago Motta na kocha wa zamani wa Brighton, Roberto De Zerbi.
Mapema mwezi uliopita zilikuwapo habari kwamba Xavi amebadili uamuzi wa kuachana na Barca na kwamba angeutumikia mkataba wake wa sasa hadi mwakani utakapofikia mwisho lakini kauli ya hivi karibuni ya kocha huyo kuhusu hali ngumu ya uchumi wa klabu hiyo huenda ikamponza.

The post Xavi, Rais Barca kufanya kikao first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/05/23/xavi-rais-barca-kufanya-kikao/feed/ 0
Xavi hatihati kubaki Barca https://www.greensports.co.tz/2024/05/18/xavi-hatihati-kubaki-barca/ https://www.greensports.co.tz/2024/05/18/xavi-hatihati-kubaki-barca/#respond Sat, 18 May 2024 10:47:18 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=11005 Barcelona, HispaniaMpango wa Barcelona ‘Barca’ kumbakisha kocha Xavi baada ya msimu huu unaonekana kugonga mwamba kutokana na kauli ya kocha huyo aliyoitoa kabla ya mechi dhidi ya Almeria kuwachukiza vigogo wa klabu hiyo.Januari mwaka huu Xavi, 44 alitangaza ataachana na Barca baada ya msimu huu lakini baadaye rais wa klabu hiyo, Joan Laporta alimshawishi aendelee […]

The post Xavi hatihati kubaki Barca first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Barcelona, Hispania
Mpango wa Barcelona ‘Barca’ kumbakisha kocha Xavi baada ya msimu huu unaonekana kugonga mwamba kutokana na kauli ya kocha huyo aliyoitoa kabla ya mechi dhidi ya Almeria kuwachukiza vigogo wa klabu hiyo.
Januari mwaka huu Xavi, 44 alitangaza ataachana na Barca baada ya msimu huu lakini baadaye rais wa klabu hiyo, Joan Laporta alimshawishi aendelee na kibarua hicho na kukawa na kila dalili hizo lakini kauli yake huenda ikaufuta mpango huo.
Akiwa kwenye mkutano na waandishi wa habari, Xavi alizungumzia ugumu wa Barca kupambana kwenye soka la hadhi ya juu akihusisha jambo hilo na masuala ya fedha na sasa Rafael Marquez, kocha wa timu B anatajwa kuchukua nafasi yake.
Xavi ambaye alianza kuinoa Barca Novemba 2021 na kufanikiwa kuipa taji la La Liga msimu wa 2022-23, alisema itakuwa vigumu kwao kupambana kwenye nguvu ya kifedha na mahasimu wao Real Madrid pamoja na timu nyingine kubwa za Ulaya.

“Nafikiri mashabiki wa Barca wanahitaji kuelewa kwamba mazingira ni magumu kweli hasa katika masuala ya kiuchumi ili kuwa na uwezo wa kushindana na Real Madrid nchini Hispania pamoja na timu nyingine za Ulaya,” alisema Xavi.


Xavi hata hivyo alisema kwamba kauli yake hiyo haimaanishi kwamba wataacha kupambana na kupigania mataji bali watajitahidi kuendana na hali hiyo hivyo hivyo lakini hiyo ndiyo hali halisi ya klabu na kwa sasa wanahitaji kuwa imara na kupata muda.


Mahasimu wa Barca, Real Madrid kwa sasa wameshabeba taji la La Liga msimu huu na wapo hatua ya fainali Ligi ya Mabingwa Ulaya wakisubiri kuumana na Borussia Dortmund hapo Juni Mosi kwenye dimba la Wembley.
Real Madrid pia inadaiwa kuwa katika hatua za mwisho kumsajili mshambuliaji Kylian Mbappe kutoka PSG na wameiacha Barca nyuma kwa tofauti ya pointi 14 kwenye La Liga zikiwa zimesalia mechi mbili kabla ya msimu wa ligi hiyo kufikia tamati.

The post Xavi hatihati kubaki Barca first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/05/18/xavi-hatihati-kubaki-barca/feed/ 0
Xavi kushawishiwa asiondoke Barca https://www.greensports.co.tz/2024/04/23/xavi-kushawishiwa-asiondoke-barca/ https://www.greensports.co.tz/2024/04/23/xavi-kushawishiwa-asiondoke-barca/#respond Tue, 23 Apr 2024 07:22:13 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=10710 Barcelona, HispaniaKocha wa Barca, Xavi Hernández ambaye tayari ametangaza nia yake ya kuachana na timu hiyo baada ya msimu huu inadaiwa atakutana na mabosi wake katika kikao chenye lengo la kumshawishi abadili uamuzi huo.Januari mwaka huu, Xavi alitangaza mpango wake wa kuachana na timu hiyo lakini katika siku za karibuni kumekuwa na habari za ndani […]

The post Xavi kushawishiwa asiondoke Barca first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
Kocha wa Barcelona

Barcelona, Hispania
Kocha wa Barca, Xavi Hernández ambaye tayari ametangaza nia yake ya kuachana na timu hiyo baada ya msimu huu inadaiwa atakutana na mabosi wake katika kikao chenye lengo la kumshawishi abadili uamuzi huo.
Januari mwaka huu, Xavi alitangaza mpango wake wa kuachana na timu hiyo lakini katika siku za karibuni kumekuwa na habari za ndani zinazodai kwamba kocha huyo anashawishiwa ili afute mpango huo.
Rais wa klabu hiyo, Joan Laporta na wasaidizi wake wa karibu, Rafa Yuste ambaye ni makamu rais na mkurugenzi wa michezo, Deco wote wamewahi kuzungumzia nia yao ya kumtaka Xavi aendelee kuinoa Barca.
Xavi pamoja na kutakiwa abaki katika timu hiyo, mambo yake kimsingi si mazuri kwani Barca huenda ikamaliza msimu bila taji, tayari imetolewa na PSG kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Katika Ligi Kuu Hispania au La Liga, zikiwa zimebaki mechi sita kabla ya ligi hiyo kufikia tamati, Barca imeachwa na vinara Real Madrid kwa tofuati ya pointi 11.


Habari za ndani zinadai kwamba kikao na kocha huyo kinatarajia kufanyika wiki hii au wiki ijayo huku ikieleweka kwamba mabosi wanataka kuanza maandalizi ya msimu ujao huku wakitaka kujua kama shauku yao ya kutaka kuendelea na kocha huyo itafanikiwa.
Pamoja na ukweli kwamba huu si msimu mzuri kwa klabu hiyo, bado vigogo wanathamini kazi iliyofanywa na Xavi tangu akabidhiwe majukumu mwaka 2021.
Zaidi ya hilo klabu hiyo isingependa kujiingiza katika gharama za kuajiri kocha mwingine kutokana na mazingira magumu ya kifedha yaliyowazunguka kwa mujibu wa kanuni za La Liga.

The post Xavi kushawishiwa asiondoke Barca first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/04/23/xavi-kushawishiwa-asiondoke-barca/feed/ 0
Kocha, kipa Barca walalama https://www.greensports.co.tz/2024/04/22/kocha-kipa-barca-walalama/ https://www.greensports.co.tz/2024/04/22/kocha-kipa-barca-walalama/#respond Mon, 22 Apr 2024 07:42:53 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=10700 Madrid, HispaniaKocha wa Barca, Xavi Hernandez na kipa wake Marc-Andre ter Stegen wamelalamikia kukosekana teknolojia ya ‘goal line’ baada ya timu yao kulala kwa mabao 3-2 mbele ya mahasimu wao, Real Madrid jana Jumapili.Real Madrid walipata ushindi huo kwa bao la dakika za lala salama lililofungwa na Jude Bellingham na kuifanya timu hiyo kuendelea kushika […]

The post Kocha, kipa Barca walalama first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Madrid, Hispania
Kocha wa Barca, Xavi Hernandez na kipa wake Marc-Andre ter Stegen wamelalamikia kukosekana teknolojia ya ‘goal line’ baada ya timu yao kulala kwa mabao 3-2 mbele ya mahasimu wao, Real Madrid jana Jumapili.
Real Madrid walipata ushindi huo kwa bao la dakika za lala salama lililofungwa na Jude Bellingham na kuifanya timu hiyo kuendelea kushika usukani katika La Liga kwa tofauti ya pointi 11 zikiwa zimebaki mechi sita kabla ya kumalizika kwa ligi hiyo.
La Liga ni kati ya ligi ambazo hazijaanza kuitumia teknolojia hiyo jambo ambalo limewakera Barca kutokana na tukio la mpira uliopigwa na Lamine Yamal na kuokolewa na Andriy Lunin wakati huo matokeo yakiwa sare ya 1-1 wakiamini mpira huo ulishavuka mstari.
“Nakosa neno la kuelezea kuhusu kilichotokea kwenye mstari wa goli, inakera sana kwenye soka, pesa zipo nyingi mno kwenye soka lakini hazitumiki kwa mambo muhimu,” alisema Ter Stegen.
Kipa huyo aliongeza kwa kusema kwamba anashindwa kuelewa ni kwa nini haziwezi kuwepo pesa za kuifanyia kazi teknolojia hii ambayo ipo kwenye ligi nyingine.
Kwa upande wake Xavi (pchani juu) aliponda kukosekana kwa teknolojia ya ‘goal line’ nchini Hispania baada ya timu yake kupoteza mechi hiyo maarufu El Classico iliyopigwa kwenye dimba la Santiago Bernabeu.

“Nakubaliana kabisa na Ter Stegen, inakera mno kwa kukosa teknolojia ya ‘goal line’, kama tunataka kusema kuwa hii ni ligi bora duniani, tunahitaji teknolojia hii, kila kitu kilionekana, picha zipo, mtazamo wetu leo ni wa kukosekana haki,” alisema Xavi.


Rais wa La Liga, Javier Tebas aliwahi kujibu madai ya kutokuwapo kwa teknolojia hiyo kwenye ligi hiyo kwa kutolea mifano kwenye nchi ambazo teknolojia hiyo imekuwa na makosa.
Barca waliianza mechi vizuri kwa kupata bao la kwanza mapema dakika ya sita lililofungwa na Andreas Christensen kabla ya Vinicius kusawazisha kwa mkwaju wa penalti.
Barca walifanikiwa kuongeza bao la pili lililofungwa na Fermin Lopez lakini Real Madrid wakajajibu mapigo kwa kusawazisha safari hii kupitia Vazquez na hatimaye Bellingham kukamilisha bao la tatu.

The post Kocha, kipa Barca walalama first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/04/22/kocha-kipa-barca-walalama/feed/ 0
Xavi adai mwamuzi kaiua Barca https://www.greensports.co.tz/2024/04/17/xavi-adai-mwamuzi-kaiua-barca/ https://www.greensports.co.tz/2024/04/17/xavi-adai-mwamuzi-kaiua-barca/#respond Wed, 17 Apr 2024 06:41:34 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=10627 Barcelona, HispaniaKocha wa Barca, Xavi Hernández amemlalamikia mwamuzi kwa kumpa kadi nyekundu mchezaji wake, Ronald Araújo kuwa ndiyo sababu iliyochangia timu yake kufungwa mabao 4-1 na PSG na kutolewa kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya.Ushindi wa PSG umekuja saa takriban 24 baada ya kocha wa timu hiyo, Luis Enrique kusema kwamba ana matumaini ya timu yake […]

The post Xavi adai mwamuzi kaiua Barca first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Barcelona, Hispania
Kocha wa Barca, Xavi Hernández amemlalamikia mwamuzi kwa kumpa kadi nyekundu mchezaji wake, Ronald Araújo kuwa ndiyo sababu iliyochangia timu yake kufungwa mabao 4-1 na PSG na kutolewa kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Ushindi wa PSG umekuja saa takriban 24 baada ya kocha wa timu hiyo, Luis Enrique kusema kwamba ana matumaini ya timu yake kuishinda Barca na kufuzu hatua ya nusu fainali ya ligi hiyo.
Xavi ambaye timu yake ilikuwa nyumbani alikiita majanga kitendo cha mwamuzi Istvan Kovacs kumpa kadi Araujo dakika ya 29 kwa kumchezea rafu, Bradley Barcola wakati Barca ikiwa mbele kwa bao 1-0.
Kwa matokeo hayo, Barca inakuwa imetolewa katika ligi hiyo kwa jumla ya mabao 6-4 licha ya kupata ushindi wa mabao 3-2 katika mechi ya kwanza iliyopigwa mjini Paris na sasa PSG inasubiri kuumana na Borussia Dortmund katika nusu fainali.
Mabao ya ushindi ya PSG yalifungwa na Kylian Mbappe aliyefunga mawili pamoja na Ousmanne Dembele na Vitinha wakati bao pekee la Barca lilifungwa na Raphinha mapema dakika ya 10.
“Tumekerwa, kadi nyekundu ndiyo iliyoamua mchezo, tulikuwa tumejipanga vizuri, ilikuwa ni 11 kwa 11, kadi ilibadili kila kitu, kwangu mimi mwamuzi alikwenda mbali kwa kumpa kadi Araujo,” alisema Xavi.
“Kwa hakika mwamuzi alikuwa mbaya, nilimwambia, alikuwa janga, aliua mchezo, huwa sipendi kuzungumza kuhusu waamuzi lakini ilikuwa lazima kusema, sikuelewa,” alisema Xavi.
Xavi aliongeza kuwa halikuwa jambo zuri kubaki na wachezaji 10 kwa kuwa kuanzia hapo mchezo ukaanza kuwa tofauti na kwa vyovyote wanavyoweza kuuzungumzia mchezo huo, kadi nyekundu ndio kila kitu.

“Ni aibu, kazi ngumu iliyofanywa kwa msimu mzima inamalizika kwa sababu ya maamuzi ya mwamuzi mmoja, nilipenda mechi iwe ya wachezaji 11 kwa 11 mwanzo hadi mwisho, lakini imetolewa kadi nyekundu ambayo haikuwa na ulazima,” alisema Xavi.


Xavi naye baadaye kipindi cha pili alipewa kadi nyekundu wakati akipinga maamuzi ya kuinyima Barca penalti baada ya Marquinhos kumchezea rafu Ilkay Gundogan ingawa alikubali kujibebesha lawama kwa kadi hiyo akidai lilikuwa kosa lake.
Mechi za nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya zitapigwa kati ya Aprili 30 na Mei Mosi na marudiano itakuwa ni Mei 7 na 8 ambapo PSG itaumana na Borussia Dortmund wakati mshindi kati ya Man City na Real Madrid ataumana na mshindi wa mechi ya Arsenal na Bayern Munich.
Matokeo mechi za Ligi ya Mabingwa Ulaya
Barcelona 1-4 PSG
B Dortmund 4-2 Atl Madrid
Mechi za Ligi ya Mabingwa Ulaya leo Jumatano
Bayern Munich v Arsenal
Man City v Real Madrid

The post Xavi adai mwamuzi kaiua Barca first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/04/17/xavi-adai-mwamuzi-kaiua-barca/feed/ 0
Guti: Xavi hakujiandaa kuinoa Barca https://www.greensports.co.tz/2024/02/08/guti-xavi-hakujiandaa-kuinoa-barca/ https://www.greensports.co.tz/2024/02/08/guti-xavi-hakujiandaa-kuinoa-barca/#respond Thu, 08 Feb 2024 06:48:53 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=9623 Barcelona, HispaniaKiungo wa zamani wa Real Madrid, Guti (pichani) anaamini Xavi hakuwa amejiandaa kuinoa Barcelona na amepewa timu hiyo katika wakati ambao si sahihi.Xavi, kiungo wa zamani wa Barca, hivi karibuni ametangaza kwamba atang’atuka kuinoa timu hiyo baada ya msimu huu kwa kinachoaminika kuwa hafurahishwi na mambo yanavyokwenda na amewahi kusema kwamba hathaminiwi.Kocha huyo alianza […]

The post Guti: Xavi hakujiandaa kuinoa Barca first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Barcelona, Hispania
Kiungo wa zamani wa Real Madrid, Guti (pichani) anaamini Xavi hakuwa amejiandaa kuinoa Barcelona na amepewa timu hiyo katika wakati ambao si sahihi.
Xavi, kiungo wa zamani wa Barca, hivi karibuni ametangaza kwamba atang’atuka kuinoa timu hiyo baada ya msimu huu kwa kinachoaminika kuwa hafurahishwi na mambo yanavyokwenda na amewahi kusema kwamba hathaminiwi.
Kocha huyo alianza kuinoa Barca mwaka 2021 akitokea klabu ya Al-Sadd ya Qatar na mwaka 2023 aliiwezesha kubeba taji la La Liga pamoja na lile la Spanish Super Cup.
Kwa sasa Barca inashika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa La Liga ikiwa na pointi 50, tofauti ya pointi nane dhidi ya vinara wa ligi hiyo Real Madrid na sita dhidi ya Gerona inayoshika nafasi ya pili.
“Xavi Hernandez hakujiandaa kuja kuinoa Barcelona, alidhani kwamba kila kitu kingekuwa rahisi lakini hapana, unapokuwa Qatar na kuiandaa timu mbele kukiwa na mashabiki 300, hiyo si sawa na kuwa kwenye benchi la Barcelona, huo ndio ukweli,” alisema Guti ambaye amewahi kunukuliwa akidai kwamba ana ndoto ya kuinoa Real Madrid miaka ijayo.
Xavi ameichezea Barca kwa miaka 17 na kucheza jumla ya mechi 767 na kushinda mataji 25, hata hivyo amesema kwamba hafuti moja kwa moja uwezekano wa yeye kurudi kwa mara nyingine kuinoa Barca hapo baadaye.

The post Guti: Xavi hakujiandaa kuinoa Barca first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/02/08/guti-xavi-hakujiandaa-kuinoa-barca/feed/ 0
Xavi adai hathaminiwi Barca https://www.greensports.co.tz/2024/01/31/xavi-adai-hathaminiwi-barca/ https://www.greensports.co.tz/2024/01/31/xavi-adai-hathaminiwi-barca/#respond Wed, 31 Jan 2024 17:57:53 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=9532 Barcelona, HispaniaKocha anayejiandaa kuachana na klabu ya Barcelona, Xavi Hernández amesema kazi yake katika klabu hiyo ilikuwa haithaminiwi na kutahadharisha kuwa itakuwa vigumu kwa kocha ajaye kuifurahia kazi hiyo.Jumamosi iliyopita, Xavi ambaye ana mkataba na Barca hadi mwaka 2025, alitangaza kuachana na timu hiyo mwishoni mwa msimu huu, kauli iliyokuja baada ya kupokea kichapo cha […]

The post Xavi adai hathaminiwi Barca first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
Kocha wa Barcelona, Xavi.

Barcelona, Hispania
Kocha anayejiandaa kuachana na klabu ya Barcelona, Xavi Hernández amesema kazi yake katika klabu hiyo ilikuwa haithaminiwi na kutahadharisha kuwa itakuwa vigumu kwa kocha ajaye kuifurahia kazi hiyo.
Jumamosi iliyopita, Xavi ambaye ana mkataba na Barca hadi mwaka 2025, alitangaza kuachana na timu hiyo mwishoni mwa msimu huu, kauli iliyokuja baada ya kupokea kichapo cha mabao 5-3 mbele ya Villarreal.
Msimu uliopita, Xavi aliiwezesha Barca kubeba taji la Ligi Kuu Hispania au La Liga ikimaliza kinara kwa pointi 10 zaidi ingawa msimu huu mambo yanaonekana kuwa magumu, tayari timu hiyo imetolewa kwenye Cope De Rey, Super Copa na kwenye La Liga mambo si mazuri.
“Ni kazi ya kikatili na isiyo na uungwana, inakufanya ujione huna thamani kila siku, Pep (Guardiola) aliwahi kuniambia, niliona pia jinsi Luis Enrique alivyopata shida,” alisema Xavi.
“Tuna tatizo katika yale tunayoyataka, hufurahii, unacheza wakati wote kwa ajili ya maisha yako, ni ukatili, kazi tuliyoifanya haithamiwi kwa kiasi kinachotakiwa, tulikuja hapa mwaka 2021 klabu ikiwa katika moja ya vipindi vigumu zaidi,” alisema Xavi.
Alipoulizwa ni nani hasa ambaye haithamini kazi aliyoifanya, Xavi alijibu kwamba hathaminiwi kwa ujumla.
“Nimekuwa na mtazamo kwamba kila ninachokifanya, sithaminiwi, si suala la kujikuta katika presha, tumetoka katika kipindi kigumu na sidhani kama kazi yetu itatokea ikathaminiwa,” alisema Xavi.

“Wakati wote nimekuwa nikisema kile ninachofikiri, kama nikisema tuna timu ambayo tunaijenga unanishambulia, kama nikisema kwamba hatujawa na Barca ya 2010 pia kunakuwa na shutuma,” alisema Xavi.


Xavi hata hivyo alisema kwamba kwa upande mwingine amejiona ni mtu mwenye kuthaminiwa na rais wa klabu hiyo, Joan Laporta na anamshukuru kwa fursa na imani aliyokuwa akimuonesha.
Akizungumzia mambo ya baadaye ya Barca, Xavi alisema anaamini hata kocha ajaye badala yake katika timu hiyo naye atajikuta akiwa tatizo.
“Ndoto yangu ilikuwa kuwa kocha wa Barca, timu iwe inashinda na kucheza soka zuri, ninajivunia kwa kile nilichoweza kukifanya, ushauri wangu kwa anayekuja badala yangu ni kuhakikisha anafurahia kazi yake lakini hilo haliwezekani,” alisema Xavi.
Pamoja na yote hayo, Xavi ambaye amekuwa na timu ya Barca kwa miaka 17 katika kikosi cha kwanza kabla ya kutimkia Qatar mwaka 2015, amesema hajafunga mlango kuhusu uwezekano wa yeye kurudi Barca kwa mara nyingine.
“Sifuti kabisa uwezekano wa kurudi siku moja, mimi ni mtu wa klabu hii na nipo kwa ajili ya klabu hii pale watakaponihitaji,” alisema Xavi.

The post Xavi adai hathaminiwi Barca first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/01/31/xavi-adai-hathaminiwi-barca/feed/ 0