Vital’O - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Sat, 24 Aug 2024 21:21:00 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=6.8 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg Vital’O - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 Yanga yaipiga Vital’O 6-0, Azam hoi https://www.greensports.co.tz/2024/08/25/yanga-yaipiga-vitalo-6-0-azam-hoi/ https://www.greensports.co.tz/2024/08/25/yanga-yaipiga-vitalo-6-0-azam-hoi/#respond Sat, 24 Aug 2024 21:20:59 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=11811 Na mwandishi wetuYanga leo Jumamosi imeilaza Vital’O ya Burundi mabao 6-0 na kusonga mbele katika Ligi ya Mabingwa Afrika wakati Azam FC ikitupwa nje ya michuano hiyo kwa kipigo cha mabao 2-0 mbele ya APR ya Rwanda.Ushindi wa Yanga iliyokuwa kwenye Uwanja wa Azam Complex unaifanya timu hiyo kusonga mbele kwa ushindi wa jumla wa […]

The post Yanga yaipiga Vital’O 6-0, Azam hoi first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Yanga leo Jumamosi imeilaza Vital’O ya Burundi mabao 6-0 na kusonga mbele katika Ligi ya Mabingwa Afrika wakati Azam FC ikitupwa nje ya michuano hiyo kwa kipigo cha mabao 2-0 mbele ya APR ya Rwanda.
Ushindi wa Yanga iliyokuwa kwenye Uwanja wa Azam Complex unaifanya timu hiyo kusonga mbele kwa ushindi wa jumla wa mabao 10-0 baada ya ushindi wa mechi ya kwanza wa mabao 4-0.
Yanga sasa inasubiri kuumana na Commercial Bank of Ethiopia (CBE) ambayo imesonga mbele baada ya kuitoa Sports Club Villa ya Uganda kwa jumla ya mabao 3-2.
Ukurasa wa mabao ya Yanga ulifunguliwa dakika ya 13 kwa bao la mkwaju wa penalti uliojazwa wavuni kiufundi na Pacome Zouzoua.
Penalti hiyo ilitotolewa baada ya mchezaji wa APR, Amedee Ndavyutse kutumia mkono kuokoa shuti la Pacome lililokuwa likielekea langoni mwa APR na kabla ya kutoa penalti hiyo mwamuzi alimpa Amedee kadi nyekundu.
APR wakiwa pungufu uwanjani walipambana na kufanikiwa kumaliza nusu ya kwanza ya mchezo wakiwa nyuma kwa bao hilo pekee kabla balaa halijaanza kuwaangukia kipindi cha pili.
Dakika tatu baada ya kuanza kipindi hicho, Yanga waliandika bao la pili lililofungwa na Clement Mzize wakati bao la tatu lilifungwa na Clatous Chama katika dakika ya 50.
Prince Dube aliandika bao la nne dakika ya 72 kabla Stephane Aziz Ki na Mudathir Yahya hawajakamilisha karamu ya mabao ya Yanga kwa kutupia nyavuni katika dakika za 79 na 86.
Yanga leo ilizidi kuwa moto kipindi cha pili wakati Vital’O ikipata pigo baada ya mchezaji wake mwingine kupewa kadi nyekundu na hivyo kubaki na wachezaji tisa uwanjani.
Vital’O ilijikuta ikiwa na kazi ngumu ya kuokoa, lango lao lilishambuliwa mara kwa mara huku kipa wa Yanga, Djigui Diarra kwa kipindi kirefu akiwa kama hayupo uwanjani kwa namna alivyokosa misukosuko ya mara kwa mara.
Kocha wa Yanga, Miguel Gamondi alifanya mabadiliko kadhaa yaliyozidi kuipa uhai Yanga katika kipindi cha pili akimtoa Aziz Andambwile na kumuingiza Aziz Ki.
Wachezaji wengine ambao Gamondi aliwatoa ni Clement Mzize, Kennedy Musonda, Pacome na Duke Abuya na nafasi zao kuingia Prince Dube, Mudathir Yahya, Salum Aboubakar na Maxi Nzengeli.
Baada ya kuwatoa Vital’O Yanga pia wana kila sababu ya kufurahia zawadi ya Sh milioni tano kwa kila bao walilofunga maarufu ‘Zawadi ya Mama’ ambayo imetolewa na Rais Samia Suluhu Hassan kwa timu zinazoshiriki michuano ya klabu Afrika.
Kwa upande mwingine mambo si mazuri kwa Azam ambao katika hali isiyotarajia walishindwa kuulinda ushindi wao wa bao 1-0 walioupata dhidi ya APR katika mechi yao ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
Azam wamechapwa mabao 2-0 na APR wakiwa ugenini Rwanda na sasa watarudi nyumbani wakiwa wametolewa kwa jumla ya mabao 2-1.

The post Yanga yaipiga Vital’O 6-0, Azam hoi first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/08/25/yanga-yaipiga-vitalo-6-0-azam-hoi/feed/ 0
Yanga yaibugiza Vital’O 4-0 https://www.greensports.co.tz/2024/08/17/yanga-yaibugiza-vitalo-4-0/ https://www.greensports.co.tz/2024/08/17/yanga-yaibugiza-vitalo-4-0/#respond Sat, 17 Aug 2024 16:58:46 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=11789 Na mwandishi wetuYanga imezianza fainali za Ligi ya Mabingwa Afrika kwa kishindo baada ya kuibugiza Vital’O ya Burundi mabao 4-0, mechi iliyopigwa leo Jumamosi kwenye dimba la Azam Complex, Dar es Salaam.Prince Dube ndiye aliyekuwa wa kwanza kuwainua vitini mashabiki wa Yanga alipoandika bao la kwanza dakika ya tano tu ya mchezo akiyatumia makosa ya […]

The post Yanga yaibugiza Vital’O 4-0 first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Yanga imezianza fainali za Ligi ya Mabingwa Afrika kwa kishindo baada ya kuibugiza Vital’O ya Burundi mabao 4-0, mechi iliyopigwa leo Jumamosi kwenye dimba la Azam Complex, Dar es Salaam.
Prince Dube ndiye aliyekuwa wa kwanza kuwainua vitini mashabiki wa Yanga alipoandika bao la kwanza dakika ya tano tu ya mchezo akiyatumia makosa ya beki wa Vital’O aliyejichanganya wakati akiokoa mpira.
Vital’O licha ya kuonekana kuwa timu dhaifu mbele ya Yanga lakini kuingia kwa bao hilo bado haikuwa tatizo kwao, waliendelea kucheza soka la kutulia wakijihami na kusogelea langoni mwa Yanga mara chache.
Hali hiyo iliwaweka Yanga pagumu na haikushangaza hadi kipindi cha kwanza kinamalizika Yanga walikuwa mbele kwa bao hilo pekee la Dube.
Kipindi cha pili hata hivyo mambo yalikuwa magumu kwa Vital’O ambao katika dakika ya 70 walipachikwa bao la pili mfungaji akiwa Clatous Chota Chama.
Dakika mbili tu baada ya kuingia bao hilo, Clement Mzize aliwainua tena vitini mashabiki wa timu hiyo alipopachika bao la tatu kabla ya Stephane Aziz Ki hajakamilisha karamu ya mabao dakika ya 89 kwa kuandika bao la nne.
Aziz Ki alifunga bao hilo kwa mkwaju wa penalti ambayo ilitolewa baada ya mchezaji huyo kufanyiwa madhambi wakati akielekea kuonana na kipa wa Vital’O, Hussein Ndiyeshimana.
Matokeo hayo yameiweka Yanga katika nafasi nzuri ya kusonga mbele na sasa inachohitaji ni sare au ushindi wa aina yoyote katika mechi ya marudiano ambayo pia itapigwa jijini Dar es Salaam hapo Agosti 24.
Ikimalizana na Vital’O Yanga itakuwa na kibarua cha pili katika michuano hiyo kwa msimu huu wa 2024-25 kwa kuumana na mshindi wa mechi kati ya SC Villa ya Uganda na Commercial Bank ya Ethiopia ambazo pia zinaumana hii leo jijini Kampala, Uganda.

The post Yanga yaibugiza Vital’O 4-0 first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/08/17/yanga-yaibugiza-vitalo-4-0/feed/ 0