Varane - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Wed, 25 Sep 2024 09:42:39 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=6.8 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg Varane - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 Varane astaafu soka https://www.greensports.co.tz/2024/09/25/varane-astaafu-soka/ https://www.greensports.co.tz/2024/09/25/varane-astaafu-soka/#respond Wed, 25 Sep 2024 09:42:37 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=11939 Milan, ItaliaBeki wa zamani wa Man United, Real Madrid na timu ya taifa ya Ufaransa, Raphael Varane ambaye Julai mwaka huu alijiunga na klabu ya Como ya Italia, ametangaza kustaafu soka.Varane alijiunga na Como, akiwa mchezaji huru aljikuta katika wakati mgumu baada ya kupata maumivu ya goti katika mechi yake ya kwanza na timu yake […]

The post Varane astaafu soka first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Milan, Italia
Beki wa zamani wa Man United, Real Madrid na timu ya taifa ya Ufaransa, Raphael Varane ambaye Julai mwaka huu alijiunga na klabu ya Como ya Italia, ametangaza kustaafu soka.
Varane alijiunga na Como, akiwa mchezaji huru aljikuta katika wakati mgumu baada ya kupata maumivu ya goti katika mechi yake ya kwanza na timu yake hiyo mpya dhidi ya Sampdoria.
Beki huyo wa kati alisema kwamba pamoja na uamuzi huo lakini ataendelea kuwa katika klabu hiyo lakini akiwa si mwenye kulipwa chochote hadi hapo atakapofikia uamuzi mwingine.
Akifafanua zaidi kuhusu uamuzi wake wa kustaafu soka wakati huu akiwa na miaka 31, Varane alisema kwamba inahitaji ujasiri mkubwa kuusikiliza moyo pamoja na shauku zako.
Jina la Varane lilianza kupata umaarufu kwenye soka nchini Ufaransa na Ulaya akiwa na klabu ya Lens ambapo alidumu msimu mmoja tu katika kikosi cha kwanza kabla ya kuhamia Real Madrid mwaka 2011.
Alicheza kwa mafanikio Real Madrid kwa miaka 10 akishinda mataji zaidi ya 10 yakiwamo ya La Liga pamoja na mataji manne ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kabla ya kutua Man United mwaka 2021.
Akiwa Man United aliichezea timu hiyo jumla ya mechi 95 za mashindano yote kabla ya kuanza kuandamwa na majeraha na baadaye kutimkia Como na hatimaye amestaafia katika timu hiyo.
Varane pia ametamba na timu ya taifa ya Ufaransa ambayo alianza kuichezea mwaka 2013 na hadi sasa ameichezea mara 93 na alikuwamo katika kikosi cha timu hiyo kilichobeba Kombe la Dunia mwaka 2018.

The post Varane astaafu soka first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/09/25/varane-astaafu-soka/feed/ 0