VAR - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Sun, 02 Mar 2025 09:11:56 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=6.8 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg VAR - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 Waamuzi 20 kushiriki kozi ya VAR https://www.greensports.co.tz/2025/03/02/waamuzi-20-kushiriki-kozi-ya-var/ https://www.greensports.co.tz/2025/03/02/waamuzi-20-kushiriki-kozi-ya-var/#respond Sun, 02 Mar 2025 09:11:55 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=13074 Na mwandishi wetuWaamuzi wa soka 20 wanatarajia kushiriki kozi maalum ya teknolojia ya VAR ambayo itafanyika jijini Dar es Salaam kuanzia Machi 3 hadi 7 mwaka huu.Taarifa iliyopatikana kwenye vyanzo mbalimbali vya habari vya TFF imewataja waamuzi hao kuwa ni Ahmed Arajiga, Henry Sasii, Tatu Malogo, Nassir Siyah, Ramadhan Kayoko na Mohammed Simba.Waamuzi wengine ni […]

The post Waamuzi 20 kushiriki kozi ya VAR first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Waamuzi wa soka 20 wanatarajia kushiriki kozi maalum ya teknolojia ya VAR ambayo itafanyika jijini Dar es Salaam kuanzia Machi 3 hadi 7 mwaka huu.
Taarifa iliyopatikana kwenye vyanzo mbalimbali vya habari vya TFF imewataja waamuzi hao kuwa ni Ahmed Arajiga, Henry Sasii, Tatu Malogo, Nassir Siyah, Ramadhan Kayoko na Mohammed Simba.
Waamuzi wengine ni Hamdan Said, Ally Ramadhan, Kassin Seif, Frank Komba, Alex Pangras, Abdallah Mwinyimkuu, Ester Adabert na Amina Kyando.
Wengine waliomo kwenye orodha hiyo ni Shaaban Mussa, Janeth Balama, Mohammed Mkono, Glory Tesha, Zawadi Yusuph na Siraji Mkwaju.
Kozi hiyo huenda ikawa mwanzo wa teknolojia ya VAR kuanza kutumika katika mechi za soka nchini hasa baada ya TFF kuahidi takriban miaka miwili iliyopita kwamba ina mpango wa kuanza kuitumia teknolojia hiyo.
Hoja ya utumiaji wa VAR imewahi pia kujadiliwa kwenye Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na serikali kulazimika kutoa ufafanuzi wa lini hasa teknolojia hiyo ingeanza baada ya muda mrefu kupitia tangu ahadi hiyo itolewe.
Teknolojia ya VAR inamsaidia mwamuzi kufikia maamuzi sahihi kwa kutumia picha za video zilizorekodiwa kwa kusimamisha mchezo na kujiridhisha kupitia picha hizo baada ya kuhisi kuna utata katika baadhi ya matukio ya uwanjani.

The post Waamuzi 20 kushiriki kozi ya VAR first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2025/03/02/waamuzi-20-kushiriki-kozi-ya-var/feed/ 0
Majaliwa: Klabu zisizo na viwanja bora zitengwe https://www.greensports.co.tz/2024/07/16/majaliwa-klabu-zisizo-na-viwanja-bora-zitengwe/ https://www.greensports.co.tz/2024/07/16/majaliwa-klabu-zisizo-na-viwanja-bora-zitengwe/#respond Tue, 16 Jul 2024 07:08:48 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=11622 Na mwandishi wetuWaziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa ameagiza klabu za soka ambazo hazina viwanja vilivyo katika ubora utakaoidhinishwa na Shirikisho la Soka Tanania (TFF) ziwekwe pembeni.Kiongozi huyo wa serikali, ametoa agizo hilo Jumatatu hii wakati wa hafla ya uzinduzi wa mtambo wa Teknolojia ya VAR iliyoandaliwa na Kampuni ya Azam […]

The post Majaliwa: Klabu zisizo na viwanja bora zitengwe first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa ameagiza klabu za soka ambazo hazina viwanja vilivyo katika ubora utakaoidhinishwa na Shirikisho la Soka Tanania (TFF) ziwekwe pembeni.
Kiongozi huyo wa serikali, ametoa agizo hilo Jumatatu hii wakati wa hafla ya uzinduzi wa mtambo wa Teknolojia ya VAR iliyoandaliwa na Kampuni ya Azam Media na kufanyika katika viwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.
Akisitiza umuhimu wa viwanja bora, Waziri Mkuu aliwataka TFF kuwapa masharti wanachama wao wanaomiliki viwanja na atakayeshindwa kutimiza masharti hayo awekwe pembeni
Alisema kwamba Tanzania inahitaji kufika mbali kwenye viwango vya ubora Afrika na kutaka washindane na nchi za Misri na Morocco ambazo zimepiga hatua kubwa katika ubora barani Afrika.
Waziri Mkuu alisema serikali imeipa kipaumbele michezo na hilo linadhihirishwa na namna ambavyo Rais Samia Suluhu Hassan amekuwa akitoa mchango wake katika sekta hiyo na kuondoa ile dhana ya Tanzania kichwa cha mwendawazimu.
Akiizungumzia teknolojia ya VAR alisema kwamba itasaidia kupunguza malalamiko kwa timu pamoja na kupunguza makosa ya kibinadamu kwa waaamuzi na kuwafanya wawe makini katika kazi yao.
Teknolojia ya VAR au Video Assistance Referee hutumika kwa lengo la kumsaidia mwamuzi kujiridhisha na maamuzi hasa yale yenye utata kwa kuyarejea kupitia picha za video za mechi husika.
Teknolojia hiyo ambayo imekuwa ikitumika katika Ligi Kuu England (EPL), Kombe la Dunia 2018 na 2022 na Euro 2024 hata hivyo imekuwa ikilalamikiwa kwa kuchelewesha kutoa maamuzi na hata maamuzi yake wakati mwingine kuonekana yamejaa utata.
Ni hivi karibuni tu katika fainali za soka za Euro 2024 nchini Ujerumani, kocha wa Uholanzi, Ronald Koeman alisema kwamba VAR inaua soka.

The post Majaliwa: Klabu zisizo na viwanja bora zitengwe first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/07/16/majaliwa-klabu-zisizo-na-viwanja-bora-zitengwe/feed/ 0
Tanzania isiharakishe matumizi VAR https://www.greensports.co.tz/2024/06/14/tff-isiharakishe-matumizi-ya-var/ https://www.greensports.co.tz/2024/06/14/tff-isiharakishe-matumizi-ya-var/#respond Fri, 14 Jun 2024 08:02:01 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=11329 Na Hassan KinguMoja ya mambo ambayo Waziri wa Fedha wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk Mwigulu Nchemba aliyazungumza bungeni wakati akiwasilisha bajeti ya Serikali ni kuhusu matumizi ya VAR katika mechi za ligi kuu ya soka.VAR au Video Assistance Referee ni teknolojia ambayo imekuwa ikitumika katika mechi za soka hasa Ligi Kuu England (EPL) […]

The post Tanzania isiharakishe matumizi VAR first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na Hassan Kingu
Moja ya mambo ambayo Waziri wa Fedha wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk Mwigulu Nchemba aliyazungumza bungeni wakati akiwasilisha bajeti ya Serikali ni kuhusu matumizi ya VAR katika mechi za ligi kuu ya soka.
VAR au Video Assistance Referee ni teknolojia ambayo imekuwa ikitumika katika mechi za soka hasa Ligi Kuu England (EPL) pale panapokuwa na utata wa maamuzi ambapo mwamuzi hulazimika kujiridhisha kwa kutumia VAR.
Miongoni mwa matukio ambayo huwakanganya waamuzi na kujikuta katika wakati mgumu kufanya maamuzi ni matukio ya mchezaji kuotea, rafu, penalti, goli na mengineyo, mwamuzi anapoona hana uhakika na tukio husika hujiridhisha kwa kutumia VAR.
Kauli ya Waziri Nchemba kuhusu matumizi hayo inawezekana ikapokelewa vizuri na baadhi ya mashabiki wa soka lakini nadhani Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kwa wakati huu halina haja ya kuharakisha matumizi ya teknolojia hiyo.
Nasema hivyo kwa kuwa baadhi ya watu wenye heshima zao katika soka wanaamini teknolojia ya VAR imeshafeli na tayari kampeni za kuipiga vita zimeanza hasa England ambako hapo kabla iliaminika kuwa teknolojia hiyo ingekuwa mwarubaini wa matatizo mengi.
Kocha wa Tottenham Hotspur, Ange Postecoglou amewahi kunukuliwa akisema kwamba matumizi ya VAR yanafifisha nguvu za mamlaka ya mwamuzi katika matukio ya uwanjani na hivyo ni bora kuachana na teknolojia hiyo.
Ange alitoa kauli hiyo siku ambayo timu yake ilifungwa mabao 4-1 na Chelsea hapo hapo kukawa na matukio tisa ya kupitiwa kwenye VAR na hivyo kusababisha muda wa nyongeza kuwa mrefu baada ya dakika 90 za kawaida.
Katika mechi hiyo hiyo pia kulikuwa na matukio ya kukataliwa kwa mabao matano ambapo Ange alisema kwamba hapendi mambo ya kukaa na kusubiri muda mrefu kabla ya uamuzi sahihi kufikiwa.
Ange aliema amekuwa katika soka kwa miaka mingi na wakati wote amekuwa ni mtu wa kusubiri maamuzi yanayotolewa na mwamuzi, na katika hilo amekuwa akikutana na maamuzi ya kumuumiza na kumfurahisha.
Kocha huyo anaamini kuwa matumizi ya VAR ni ushahidi kwamba mwamuzi ameporwa mamlaka ya kuusimamia mchezo wa soka uwanjani badala yake mamlaka hayo sasa yanatoka nje.
Ange hata hivyo anakubaliana na ‘goal line technology’ kwa sababu ni jambo rahisi na lililo wazi lakini kwenye VAR kwa mapana yake ni kama vile imani kwa waamuzi haipo tena.
Mikel Arteta, kocha wa Arsenal naye amewahi kuilalamikia VAR baada ya timu yake kufungwa bao 1-0 na Newcastle katika mechi ya EPL, bao ambalo lilikubaliwa baada ya mapitio ya VAR.
Arteta alisema wazi kuwa bao hilo lilikuwa fedheha kubwa katika EPL na kujikuta akiingia matatani na mamlaka za soka England ingawa hakupewa adhabu yoyote.
Baadhi ya mashabiki Arsenal hadi sasa wanaamini matokeo ya mechi yao na Newcastle ambayo yalibebwa na matumizi ya VAR yalichangia pia kwa timu yao kulikosa taji la EPL.
Ni hivi karibuni tu klabu ya Wolverhampton Wanderers ilitangaza nia yake ya kuendesha kampeni kuzishawishi klabu za EPL kukataa matumizi ya VAR katika mechi zote za ligi msimu wa 2024-25.
Wolves, moja ya klabu ambazo zinadai kuumizwa na VAR inaamini matumizi ya teknolojia hiyo huwachanganya mashabiki na kuibua utata hasa kwa kuwa muda mrefu unatumika kuangalia VAR kabla ya kuja na majibu.
Kocha wa England, Gareth Southgate yeye alisema waziwazi kwamba hapendi matumizi ya VAR, na kuonesha jinsi alivyokerwa kuangalia mechi ya Chelsea na Spurs ambayo mashabiki mara kadhaa walitakiwa kusubiri VAR kwa ajili ya maamuzi.
Southgate alisema kwamba VAR imeharibu mechi hiyo maarufu London Derby kwa namna ambavyo mchezo umekuwa ukisimama mara kadhaa.
Kwa hiyo TFF nao wanatakiwa kuwa makini na ni vyema kujipa muda zaidi kabla ya kuamua kuhusu matumizi ya teknolojia ya VAR kwani huenda hayo ambayo tunayaona na kuyasikia EPL huku kwetu yakawa makubwa zaidi.
Kabla ya kuamua kuanza kutumia VAR, TFF ifanye tafakari isiharakishe, ijue tatizo likoje huko ilikoanza kutumiwa na kwa nini mambo yako hovyo kiasi cha kuanza kupigwa vita na watu mbalimbali wakiwamo makocha.
VAR awali ilionekana ingekuwa mwarubaini wa maamuzi tata uwanjani lakini kilichoonekana katika EPL ni kama teknolojia hiyo imeongeza utata, sasa ni muhimu kujiuliza hapa kwetu itakuwaje?

The post Tanzania isiharakishe matumizi VAR first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/06/14/tff-isiharakishe-matumizi-ya-var/feed/ 0
Kura kuikataa VAR kukwama? https://www.greensports.co.tz/2024/06/06/kura-kuikataa-var-kukwama/ https://www.greensports.co.tz/2024/06/06/kura-kuikataa-var-kukwama/#respond Thu, 06 Jun 2024 05:25:20 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=11241 London, EnglandMpango wa klabu za Ligi Kuu England (EPL) kupitia klabu ya Wolves wa kutaka matumizi ya teknolojia ya VAR yafutwe huenda ukakwama katika mkutano mkuu wa klabu za EPL Alhamisi hii.Mapema mwezi uliopita Wolves waliwasilisha azimio katika mamlaka za EPL, azimio ambalo hata hivyo inadaiwa limeshawishi kuwapo kura za kutaka kuendelea na matumizi ya […]

The post Kura kuikataa VAR kukwama? first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

London, England
Mpango wa klabu za Ligi Kuu England (EPL) kupitia klabu ya Wolves wa kutaka matumizi ya teknolojia ya VAR yafutwe huenda ukakwama katika mkutano mkuu wa klabu za EPL Alhamisi hii.
Mapema mwezi uliopita Wolves waliwasilisha azimio katika mamlaka za EPL, azimio ambalo hata hivyo inadaiwa limeshawishi kuwapo kura za kutaka kuendelea na matumizi ya VAR au la.
Wolves wameendelea kusimamia msimamo wao wa kuliwasilisha suala hilo baada ya kukutana na maamuzi mengi mabaya dhidi yao katika mechi zao za msimu huu.
Azma hiyo ya Wolves hata hivyo huenda ikakwama kwani bado hakuna uhakika kama itaweza kupata kura 14 zinazohitajika ili azimio lao likubaliwe.
Habari zinadai kwamba baadhi ya klabu zinataka matumizi ya teknolojia ya VAR yaendelee kuwapo lakini hapo hapo klabu hizo zimesisitiza kuwapo maboresho katika teknolojia hiyo.
Klabu nyingine hata hivyo zinaamini matumizi ya VAR kwa wakati huu hayana faida na kuna mambo ya kuweka sawa katika jambo hilo.
Zipo habari kwamba klabu zenye nguvu katika EPL zinaamini mfumo wa VAR na mazingira ambayo yamekuwa yakijitokeza ni mambo ambayo yanaonyesha kuna tatizo ambalo linahitaji kuangaliwa kwa mapana.
Misimamo yote hiyo inatoa kila dalili za kuwapo hoja kinzani za kufuta au kutofuta matumizi ya VAR na uamuzi wowote utakaofikiwa utakuja baada ya kuwapo mjadala.
Mwamuzi mkongwe, Howard Webb ambaye pia ni kiongozi katika bodi ya waamuzi amewahi kusema kwamba mabadiliko katika VAR ni jambo ambalo linatakiwa kuangaliwa.

The post Kura kuikataa VAR kukwama? first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/06/06/kura-kuikataa-var-kukwama/feed/ 0
VAR kupingwa kwa kura EPL https://www.greensports.co.tz/2024/05/16/var-kupingwa-kwa-kura-epl/ https://www.greensports.co.tz/2024/05/16/var-kupingwa-kwa-kura-epl/#respond Thu, 16 May 2024 05:34:55 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=10973 London, EnglandKlabu ya Wolverhampton Wanderers imeanzisha kampeni ya kuachana na matumizi ya VAR katika Ligi Kuu England (EPL) ambapo klabu 20 za ligi hiyo zitapiga kura mwezi ujao kupitisha uamuzi huo.Katika mpango huo, Wolves itahitaji kuungwa mkono na klabu nyingine 13 kwenye mkutano mkuu ambao utafanyika Juni 6 mwaka huu ambao pamoja na mambo mengine […]

The post VAR kupingwa kwa kura EPL first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

London, England
Klabu ya Wolverhampton Wanderers imeanzisha kampeni ya kuachana na matumizi ya VAR katika Ligi Kuu England (EPL) ambapo klabu 20 za ligi hiyo zitapiga kura mwezi ujao kupitisha uamuzi huo.
Katika mpango huo, Wolves itahitaji kuungwa mkono na klabu nyingine 13 kwenye mkutano mkuu ambao utafanyika Juni 6 mwaka huu ambao pamoja na mambo mengine utahusika kupitisha azimio hilo.
Uamuzi huo azma yake ni kuhakikisha matumizi ya VAR yanaachwa mara moja katika mechi zote za EPL lakini klabu pia zimepewa nafasi ya kuwasilisha hoja kinzani katika mkutano huo.
Taarifa ya Wolves iliyopatikana Jumatano ilieleza, “Hakuna suala la kulaumu, sote tunatafuta uamuzi ulio bora kwa ajili ya soka na wadau wake ambao wamefanya bidii kubwa kuanzisha teknolojia ambayo ilitakiwa iwe na mafanikio.”
“Hata hivyo baada ya misimu mitano ya VAR katika ligi kuu, tunadhani huu ni wakati wa kufanya mjadala wa kina kuhusu mustakabali wa jambo hili.

“Msimamo wetu ni kwamba madhara ambayo yanajitokeza kwa faida ndogo ya kutafuta usahihi ni makubwa na yenye sintofahamu hasa katika suala zima la kuinua ari ya soka hivyo tunataka tuondoe teknolojia hii kuanzia msimu wa 2024-25 na kuendelea,” ilieleza taarifa hiyo.


Miongoni mwa malalamiko ambayo yameainishwa na Wolves kuhusu VAR ni kuwachanganya mashabiki na kuibua utata viwanjani kutokana na muda ambao unatumika kuangalia VAR hadi kupata jibu.
Jingine ni hali ya furaha wanayokuwa nayo mashabiki baada ya kufungwa goli na hamasa inayokuwa kwenye soka vyote hivyo kuvurugwa.
Mashabiki kuzomea na kupinga matumizi ya VAR katika mechi ya ligi kuu ikiwamo kuukataa hadi wimbo wa ligi hiyo.
Wolves pia wanadai licha ya kuwapo kwa VAR lakini bado kumekuwa na makosa na kuwafanya mashabiki kutokubali makosa ya kibinadamu baada ya kuirudia mechi mara kadhaa hali ambayo pia inaathiri uwezo wa kujiamini wa waamuzi.

The post VAR kupingwa kwa kura EPL first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/05/16/var-kupingwa-kwa-kura-epl/feed/ 0
Ligi Kuu NBC kutumia VAR https://www.greensports.co.tz/2023/12/17/ligi-kuu-nbc-kutumia-var/ https://www.greensports.co.tz/2023/12/17/ligi-kuu-nbc-kutumia-var/#respond Sun, 17 Dec 2023 16:53:53 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=8903 Na mwandishi wetuImebainika kuwa muda mfupi ujao baadhi ya mechi za Ligi Kuu NBC zitaanza kuamuliwa kwa usaidiziwa teknolojia ya video ya waamuzi (VAR).Hayo yameelezwa lumamosi hii na Rais wa TFF, Wallace Karia akifafanua kuwa huo ni uamuzi waShirikisho la Soka Afrika (CAF), kuipa Tanzania vifaa vya VAR ambavyo vitafungwa katika baadhi yaviwanja.Karia akizungumza kwenye […]

The post Ligi Kuu NBC kutumia VAR first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Imebainika kuwa muda mfupi ujao baadhi ya mechi za Ligi Kuu NBC zitaanza kuamuliwa kwa usaidizi
wa teknolojia ya video ya waamuzi (VAR).
Hayo yameelezwa lumamosi hii na Rais wa TFF, Wallace Karia akifafanua kuwa huo ni uamuzi waShirikisho la Soka Afrika (CAF), kuipa Tanzania vifaa vya VAR ambavyo vitafungwa katika baadhi yaviwanja.
Karia akizungumza kwenye Mkutano Mkuu wa TFF unaofanyika Iringa, alisema: “Niwape habari njema kuwa tumepata VAR kutoka CAF na hii ni mwendelezo wa uhusiano mzuri na CAF. Wataalamu wameingia jana (juzi) kutoa mafunzo. Itafungwa katika viwanja vyenye ubora.”
Karia alisema kuwa wanaangalia pia uwezekano wa VAR kufungwa katika Uwanja wa Amaan, Zanzibar ikiwa ni katika kuhakikisha kwamba mchezo wa soka unaendelea kupata mafanikio zaidi nchini.
TFF imeanza mkutano wake huo wa mwaka baada ya kutanguliwa na kikao cha kamati ya utendaji kilichofanyika juzi katika Hotel ya Hans Poppe kunakoendelea pia mkutano huo.

The post Ligi Kuu NBC kutumia VAR first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/12/17/ligi-kuu-nbc-kutumia-var/feed/ 0
VAR yamchukiza Southgate https://www.greensports.co.tz/2023/10/06/var-yamchukiza-southgate/ https://www.greensports.co.tz/2023/10/06/var-yamchukiza-southgate/#respond Fri, 06 Oct 2023 07:50:05 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=7978 London, EnglandKocha wa timu ya taifa ya England, Gareth Southgate (pichani) amelalamikia uwapo wa mfumo wa VAR akidai kwamba umekuwa kero kwa mashabiki wanaokwenda viwanjani.Maofisa wanaosimamia mfumo wa VAR walishindwa kubadili maamuzi ya bao halali la Liverpool dhidi ya Tottenham Hotspur lililofungwa na Luis Diaz ambalo kimakosa uamuzi uliotolewa ni kwamba mshambuliaji huyo aliotea na […]

The post VAR yamchukiza Southgate first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

London, England
Kocha wa timu ya taifa ya England, Gareth Southgate (pichani) amelalamikia uwapo wa mfumo wa VAR akidai kwamba umekuwa kero kwa mashabiki wanaokwenda viwanjani.
Maofisa wanaosimamia mfumo wa VAR walishindwa kubadili maamuzi ya bao halali la Liverpool dhidi ya Tottenham Hotspur lililofungwa na Luis Diaz ambalo kimakosa uamuzi uliotolewa ni kwamba mshambuliaji huyo aliotea na mwishowe Liverpool ikalala kwa mabao 2-1.
Kocha wa Liverpool, Jurgen Klopp ametaka mechi hiyo irudiwe kutokana na makosa hayo ingawa uwezekano wa jambo hilo kukubaliwa ni mdogo mno.
“Kwa wakati wote, tangu nikiwa mtoto mdogo, nimekuwa nikifahamu kwamba uamuzi wa refa ni wa mwisho, unaweza ukubaliane naye au usikubaliane naye lakini tunatakiwa kwenda na hali hiyo,” alisema Southgate.
Southgate hata hivyo alikubaliana na hoja ya kwamba soka haitoweza kuachana na dunia ambayo teknolojia imekuwa ni sehemu ya kufanyia maamuzi.
Kocha huyo hata hivyo akifafanua zaidi kuhusu VAR alisema, “Ninachoweza kusema ni kwamba kila mtu alijikuta akienda katika klabu ya pombe na kulalamika kuhusu mwamuzi, waliendelea kwenda kwenye klabu na kulalamika. Kwa hiyo sina hakika ni kipi hasa ambacho tumekirekebisha.”

“Ninakaa uwanjani pembeni nikiwa na watu wengine, na nina bahati kwa sababu huwa napata tiketi ya bure na baadhi ya watu wanalipa fedha nyingi lakini wanashindwa kuelewa au wanampigia simu mtu aliye nyumbani na kumuuliza kinachoendelea,” alisema.


The post VAR yamchukiza Southgate first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/10/06/var-yamchukiza-southgate/feed/ 0
Makosa ya VAR yamtibua Arteta https://www.greensports.co.tz/2023/02/15/makosa-ya-var-yamtibua-arteta/ https://www.greensports.co.tz/2023/02/15/makosa-ya-var-yamtibua-arteta/#respond Wed, 15 Feb 2023 08:59:27 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=5143 London, EnglandKocha wa Arsenal, Mikel Arteta amemshutumu ofisa Lee Mason akidai hajui kazi yake katika kufuatilia picha za VAR na sasa timu yake ina kazi ya kupigania pointi mbili ilizopoteza katika mechi na Brentford.Jumamosi iliyopita, Arsenal ilitoka sare ya 1-1 na Brentford katika Ligi Kuu England (EPL), ikiumizwa na bao la dakika ya 74 lililofungwa […]

The post Makosa ya VAR yamtibua Arteta first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

London, England
Kocha wa Arsenal, Mikel Arteta amemshutumu ofisa Lee Mason akidai hajui kazi yake katika kufuatilia picha za VAR na sasa timu yake ina kazi ya kupigania pointi mbili ilizopoteza katika mechi na Brentford.
Jumamosi iliyopita, Arsenal ilitoka sare ya 1-1 na Brentford katika Ligi Kuu England (EPL), ikiumizwa na bao la dakika ya 74 lililofungwa kwa kichwa na Ivan Toney licha ya mtoaji pasi Christian Norgaard kutoa pasi hiyo akiwa eneo la kuotea.
Baada ya kubaini ofisa huyo alifanya kosa, Bodi ya Wataalam Wasimamizi wa Mechi (PGMOL) ilitoa taarifa ikidai ni kosa la kibinadamu ingawa Mason alisimamishwa kazi na Arsenal kuombwa radhi.
Arteta ambaye timu yake inashika usukani katika EPL licha ya kuombwa radhi bado alililalamikia tukio zima ambalo alidai liliwaneemesha wapinzani wao Man City ambao leo Jumatano usiku wanaumana katika mechi ya EPL inayotarajiwa kuwa ngumu.
Arsenal inaongoza ligi ikiwa na pointi 51 ikifuatiwa na Man City yenye pointi 48 na kama si tukio la mechi ya Brentford, Arteta anaamini wangeizidi Man City kwa pointi tano na si tatu za sasa ingawa Arsenal imecheza mechi 21 hadi sasa na Man City 22.
Kocha huyo alisema kwamba wamesikitishwa na tukio hilo na kusisitiza kwamba halikuwa kosa la kibinadamu badala yake ni mtu kutoijua kazi yake jambo ambalo halikubaliki hata kidogo.
“Ni tukio ambalo limeinyima Arsenal pointi mbili ambazo hatuwezi kurudishiwa, tutakwenda kuzitafuta pointi hizo kwingineko kwenye ligi,” alisema Arteta.
“Wakati huo huo tunashukuru kwa kuombwa radhi na taarifa iliyotolewa, wenzetu wengi wengine katika soka wametupa pole na kusema kwamba wasingeweza kucheza soka kwa heshima kama tulivyofanya sisi, hiyo ndiyo hali halisi ni lazima tuangalie mbele,” alisema Arteta.
“Tukio hili limewafanya wachezaji, maofisa wa timu na mashabiki kuwa imara zaidi na kuwaongezea shauku ya kukipita kipindi hiki kigumu na kutupa sisi jukumu hilo, na kwa hilo tupo tayari,” alisema.
Alipoulizwa iwapo ameridhishwa na maelezo ya PGMOL, Arteta alisema, “Nitaridhika tu kama wataturudishia pointi mbili jambo ambalo haliwezekani.”

“Nashukuru na nafikiri walikuwa waungwana, wawazi na wakweli kwa kuomba msamaha na kutoa taarifa, ni jambo zuri lakini haliondoi ukweli kwamba tuna pungufu ya pointi mbili ambazo tulitakiwa kuwa nazo kwenye msimamo wa ligi,” alisema.


Kiongozi mkuu wa PGMOL, Howard Webb ambaye ni mwamuzi wa zamani aliwasiliana na Arsenal na kuwaelezea tukio zima ikiwamo kuomba radhi kabla ya kuitisha kikao na waamuzi wa EPL jana Jumanne.
Katika kikao hicho inaaminika ilielezwa kuwa walijadiliana matumizi ya VAR baada ya kuibuka malalamiko mengi katika siku za hivi karibuni licha ya matarajio ya awali kuwa VAR ingekuwa mwarobaini wa makosa katika mechi za soka.

The post Makosa ya VAR yamtibua Arteta first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/02/15/makosa-ya-var-yamtibua-arteta/feed/ 0