Van Dijk - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Wed, 05 Nov 2025 08:18:22 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=7.0 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg Van Dijk - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 Van Dijk amjibu Rooney https://www.greensports.co.tz/2025/11/04/van-dijk-amjibu-rooney/ https://www.greensports.co.tz/2025/11/04/van-dijk-amjibu-rooney/#respond Tue, 04 Nov 2025 15:23:21 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=14061 Liverpool, EnglandNahodha wa Liverpool, Virgil van Dijk amesema shutuma zilizotolewa na mshambuliaji wa zamani wa England, Wayne Rooney akilaumu kukosekana uongozi katika Liverpool, ni shutuma zenye ugoigoi.Rooney ambaye pia alikuwa mshambuliaji wa Man United kabla ya kugeukia kazi ya ukocha na sasa uchambuzi wa soka, katika hoja yake alihusisha tatizo la kiuongozi katika Liverpool na […]

The post Van Dijk amjibu Rooney first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Liverpool, England
Nahodha wa Liverpool, Virgil van Dijk amesema shutuma zilizotolewa na mshambuliaji wa zamani wa England, Wayne Rooney akilaumu kukosekana uongozi katika Liverpool, ni shutuma zenye ugoigoi.
Rooney ambaye pia alikuwa mshambuliaji wa Man United kabla ya kugeukia kazi ya ukocha na sasa uchambuzi wa soka, katika hoja yake alihusisha tatizo la kiuongozi katika Liverpool na kiwango kibovu cha timu uwanjani.
Liverpool ambao msimu uliopita walibeba taji la Ligi Kuu England (EPL) wakati kocha wao Arne Slot akiwa katika msimu wake wa kwanza, mambo yamekuwa mabaya kwao msimu huu kwa kutopata matokeo mazuri.
Mwenendo huo wa Liverpool ndio uliomuibua Rooney ambaye pia amewalaumu wachezaji Van Dijk na Mohamed Salah akidai kwamba hawajaiongoza vyema timu hiyo katika msimu huu ingawa mambo ya timu hiyo yalianza kunyooka Jumamosi iliyopita.
Akimjibu Rooney, Van Dijk alisema kwamba hakumsikia Rooney kusema lolote msimu uliopita ambao walibeba taji na hata anachokisema mshambuliaji huyo wa zamani hakimuumizi chochote.

“Hainuimizi mimi, ni kauli ya mchezaji mkongwe, mkubwa na aliyewavutia wengi, ninachoweza kusema ni mambo mazuri kumhusu yeye (Rooney) lakini alichokisema naweza kusema ni shutuma zenye ugoigoi,” alisema Van Dijk.


Kwa upande wake Rooney alisema anashikilia msimamo wa maoni yake kuhusu Liverpool ingawa alimsifu Van Dijk akisema kwamba amekuwa mmoja wa mabeki bora duniani kwa miaka mitano iliyopita.
“Namheshimu, Virgil, nafikiri ni mchezaji mzuri, ila kwa sasa kazi yangu nikiwa mchambuzi wa soka ni kutoa maoni yangu kwa kile ninachokiona,” alisema.
Rooney pia alisema ana uhakika kama ataulizwa mchezaji huyo au kocha Arne Slot atakiri kwamba hajawa mzuri kama alivyokuwa miaka michache iliyopita na kwa maana hiyo ndio maana yeye (Rooney) anasimamia maoni aliyoyatoa.

The post Van Dijk amjibu Rooney first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2025/11/04/van-dijk-amjibu-rooney/feed/ 0
Van Dijk awaombea mashabiki waliojeruhiwa https://www.greensports.co.tz/2025/05/27/van-dijk-awaombea-mashabiki-waliojeruhiwa/ https://www.greensports.co.tz/2025/05/27/van-dijk-awaombea-mashabiki-waliojeruhiwa/#respond Tue, 27 May 2025 18:40:56 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=13514 Liverpool, EnglandNahodha wa timu ya Liverpool, Virgil van Dijk (pichani) anawaombea mashabiki wa Liverpool wapone haraka baada ya kugongwa na gari wakati wa maandamano ya kushangilia taji la Ligi Kuu England (EPL).Watu wapatao 50 wamejeruhiwa wakiwamo watoto wanne baada ya gari moja kuvamia kundi la mashabiki hao waliokuwa wakisherehekea taji hilo katikati ya jiji la […]

The post Van Dijk awaombea mashabiki waliojeruhiwa first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
Liverpool, England
Nahodha wa timu ya Liverpool, Virgil van Dijk (pichani) anawaombea mashabiki wa Liverpool wapone haraka baada ya kugongwa na gari wakati wa maandamano ya kushangilia taji la Ligi Kuu England (EPL).
Watu wapatao 50 wamejeruhiwa wakiwamo watoto wanne baada ya gari moja kuvamia kundi la mashabiki hao waliokuwa wakisherehekea taji hilo katikati ya jiji la Livepool jana Jumatatu.
Mtu mmoja ambaye umri wake unatajwa kufikia miaka 53 amekamatwa akihusishwa na tukio hilo ambalo limeendelea kuwa mjadala.
Habari zaidi zinadai kwamba miongoni mwa watu waliojeruhiwa katika tukio hilo, wanne kati yao hali zao ni mbaya.

“Fikra zangu na maombi yangu yapo kwa kila mmoja aliyeumizwa, nawaombea wapone haraka wote waliopata ajali, tuko pamoja nanyi,” alisema Van Dijk.


Naye kocha wa zamani wa Liverpool, Jurgen Klopp pia alisema kwamba wapo pamoja na wote waliopata ajali na madhara mengine kutokana na tukio hilo.
Kwa upande wake Waziri Mkuu wa Uingereza, Sir Keir Starmer alisema katika mkutano na waandishi wa habari kwamba Liverpool ipo pamoja na waliojeruhiwa na nchi yote ipo pamoja nao.
Mashuhuda wa tukio hilo walisema kwamba maelfu ya mashabiki wa Liverpool walikuwa kwenye maandamano ya kufurahia ushindi wa taji la EPL msimu wa 2024-25 kabla ya gari moja kuvamia maandamano hayo na kuwagonga baadhi yao.
Awali polisi waliweka kizuizi katika mitaa ambayo mashabiki hao walipita lakini dereva wa gari hilo alipuuza na kutumia njia hiyo ndipo alipowagonga mashabiki hao.
Taarifa ya polisi baadaye ilieleza kuwa tukio hilo hawajalichukulia kama la kigaidi ingawa hawakuweka wazi nini hasa sababu ya mtu huyo kupuuzia katazo la polisi na hatimaye kuwagonga mashabiki.

The post Van Dijk awaombea mashabiki waliojeruhiwa first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2025/05/27/van-dijk-awaombea-mashabiki-waliojeruhiwa/feed/ 0
Van Dijk ataka Mbappe adhibitiwe https://www.greensports.co.tz/2024/06/17/van-dijk-ataka-mbappe-adhibitiwe/ https://www.greensports.co.tz/2024/06/17/van-dijk-ataka-mbappe-adhibitiwe/#respond Mon, 17 Jun 2024 16:44:13 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=11357 Munich, UjerumaniNahodha na beki wa timu ya taifa ya Uholanzi, Virgil van Dijk amesema kwamba timu yao ni lazima imzuie Kylian MbappĂ© kwa pamoja badala ya kutegemea mtu mmoja aifanye kazi hiyo.Ufaransa na Uholanzi zinakutana Juni 21 katika mechi ya Kundi D kwenye fainali za soka za Euro 2024 zinazoendelea nchini Ujerumani mechi zote zikiwa […]

The post Van Dijk ataka Mbappe adhibitiwe first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Munich, Ujerumani
Nahodha na beki wa timu ya taifa ya Uholanzi, Virgil van Dijk amesema kwamba timu yao ni lazima imzuie Kylian Mbappé kwa pamoja badala ya kutegemea mtu mmoja aifanye kazi hiyo.
Ufaransa na Uholanzi zinakutana Juni 21 katika mechi ya Kundi D kwenye fainali za soka za Euro 2024 zinazoendelea nchini Ujerumani mechi zote zikiwa katika hatua ya makundi.
Uholanzi tayari imeshaandika ushindi wake wa kwanza katika fainali hizo baada ya kuinyuka Poland mabao 2-1 na sasa itahitaji kushinda mechi ya pili dhidi ya Ufaransa ili kujiweka mguu sawa kwa ajili ya kucheza hatua ya mtoano.
Namna mojawapo ya vijana hao wanaonolewa na Ronaldo Koeman kushinda mechi na Ufaransa kwa mujibu wa Van Dijk ni kuhakikisha wanamdhibiti Mbappe, nyota wa PSG ambaye inadaiwa amekamilisha mipango ya kujiunga na Real Madrid.

“Angalia, kila mmoja anajua ubora wake, lazima tuwe katika ubora wetu kama timu ili kumzuia (Mbappe) asifunge lakini vyovyote ilivyo yeye ni mchezaji wa hadhi ya juu duniani, katika sekunde chache tu anaweza kubadili mambo” alisema Van Dijk.


Van Dijk ambaye pia ni beki wa Liverpool anasema ni lazima wawe tayari kama timu kwa mtihani wa aina hiyo na anadhani tayari Uholanzi wameonesha wanachokiweza katika mechi kadhaa zilizopita.
“Tuna safu ya ulinzi iliyo tayari kwa ajili ya majaribu hayo hapo Ijumaa, hiyo kwa sasa ni mechi kubwa, tuliwapa tabu kidogo katika mechi chache zilizopita dhidi yao, lakini kwa sasa najiandaa kwa mechi hiyo, ni suala la kuwa tayari kwa mtihani mkubwa wa aina hiyo,” alisema Van Dijk.

The post Van Dijk ataka Mbappe adhibitiwe first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/06/17/van-dijk-ataka-mbappe-adhibitiwe/feed/ 0
Van Dijk ampinga Roy Keane https://www.greensports.co.tz/2023/12/19/van-dijk-ampinga-roy-keane/ https://www.greensports.co.tz/2023/12/19/van-dijk-ampinga-roy-keane/#respond Tue, 19 Dec 2023 09:06:49 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=8935 Liverpool, EnglandNahodha wa Liverpool, Virgil van Dijk ameikana hoja ya Roy Keane kwamba kauli yake kuhusu mechi yao na Man United mwishoni mwa wiki inaonesha jinsi mchezaji huyo alivyo na kiburi.Akiizungumzia mechi hiyo, Van Dijk alisema kwamba kulikuwa na timu moja tu iliyocheza ikitafuta ushindi, kauli ambayo Keane hakuifurahia na kuitafsiri kuwa ni ya mtu […]

The post Van Dijk ampinga Roy Keane first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Liverpool, England
Nahodha wa Liverpool, Virgil van Dijk ameikana hoja ya Roy Keane kwamba kauli yake kuhusu mechi yao na Man United mwishoni mwa wiki inaonesha jinsi mchezaji huyo alivyo na kiburi.
Akiizungumzia mechi hiyo, Van Dijk alisema kwamba kulikuwa na timu moja tu iliyocheza ikitafuta ushindi, kauli ambayo Keane hakuifurahia na kuitafsiri kuwa ni ya mtu mwenye kiburi.
Keane, nahodha wa zamani wa Man United ambaye kwa sasa ni mchambuzi wa soka wa kituo cha televisheni cha Sky alisema kuna kauli ya kiburi iliyotoka kwa mchezaji huyo kwa kuipuuza United kwa kiasi kile.

“Nampenda Roy Keane na kama alisema hivyo ni sawa, amekuwa mtu wa Manchester United kwa wakati wote na naelewa angejibu mapigo kwa namna ile lakini nilijua nilichokisema na hakika sioni kiburi cha aina yoyote,” alisema Van Dijk.


“Kila mtu aliyeangalia ile mechi huenda aliiona hali ile, tulikuwa tukienda mbele, tulipata nafasi na hatukufunga na hilo ni jambo linalokera,” alisema Van Dijk.
Liverpool ilitawala mchezo kwa asilimi 69 na kushambulia mara 34 lakini haikuweza kupata goli dhidi ya Man United ambayo katika mechi hiyo ilitumia zaidi mfumo wa kujihami.
Mechi hiyo iliyopigwa Jumapili ni ya kwanza ya nyumbani kwa Liverpool msimu huu kutoka bila ushindi na matokeo hayo yanaifanya ibaki nafasi ya pili katika msimamo wa Ligi Kuu England nyuma ya vinara Arsenal.

The post Van Dijk ampinga Roy Keane first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/12/19/van-dijk-ampinga-roy-keane/feed/ 0