usyk - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Fri, 29 Sep 2023 20:17:48 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=6.9.1 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg usyk - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 Tyson Fury kuzichapa na Usyk Saudi Arabia https://www.greensports.co.tz/2023/09/29/tyson-fury-kuzichapa-na-usyk-saudi-arabia/ https://www.greensports.co.tz/2023/09/29/tyson-fury-kuzichapa-na-usyk-saudi-arabia/#respond Fri, 29 Sep 2023 20:17:48 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=7895 London, UingerezaPambano la ngumi za uzito wa juu linalotajwa kuwa la kihistoria kati ya Tyson Fury na Oleksandr Usyk limesainiwa na sasa mabondia hao wataoneshana umwamba mjini Riyadh, Saudi Arabia.Fury, (pichani juu) bondia wa Uingereza mwenye umri wa miaka 35, ni bingwa wa mkanda wa WBC wakati Usky, bondia wa Ukraine mwenye miaka 36, ni […]

The post Tyson Fury kuzichapa na Usyk Saudi Arabia first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

London, Uingereza
Pambano la ngumi za uzito wa juu linalotajwa kuwa la kihistoria kati ya Tyson Fury na Oleksandr Usyk limesainiwa na sasa mabondia hao wataoneshana umwamba mjini Riyadh, Saudi Arabia.
Fury, (pichani juu) bondia wa Uingereza mwenye umri wa miaka 35, ni bingwa wa mkanda wa WBC wakati Usky, bondia wa Ukraine mwenye miaka 36, ni bingwa anayeshikilia mikanda ya WBA, WBO na IBF.
“Nimefurahi baada ya pambano hili kusainiwa, hili linaweza kuwa pambano kubwa katika mchezo wetu huu,” alisema Frank Warren promota wa pambano hilo ambalo bingwa wake atatajwa kuwa bingwa asiye na mpinzani wa ngumi za uzito wa juu.
Na ingawa tarehe rasmi ya pambano hilo haijawekwa wazi lakini habari zisio rasmi zinadai kuwa huenda mabondia hao wakapambana kati ya Desemba 23 au mapema Januari mwakani.
Fury ana rekodi ya kushinda mapambano 33 tangu aingie kwenye ngumi za kulipwa mwaka 2008 wakati Usyk (pichani chini) ana rekodi ya kushinda mapambano yote 21 ya ngumi za kulipwa na Agosti mwaka huu aliutetea mkanda wake dhidi ya Daniel Dubois.


“Ngumi za mabondia wa uzito wa juu wakati wote huteka hisia za mashabiki wa ngumi na sina shaka kwamba hili litakuwa pambano kubwa la ngumi, ni tukio la karne,” alisema Warren.
Kwa kipindi kirefu mabondia hao wamekuwa wakihusishwa na pambano hilo lakini mipango imekuwa ikikwama na Aprili mwaka huu, Fury alijikuta akilaumiwa kwa kushindwa kufikia makubaliano ya kupambana na Usyk, pambano ambalo lilitarajia kufanyika London kwenye dimba la Wembley.

“Tyson Fury na Oleksandr Usyk ni mabondia wawili bora wa uzito wa juu kwa kizazi chao, na nina hamu ya kuwaona wakipanda ulingoni mjini Riyadh,” alisema Promota wa Fury, Bob Arum.


Mara ya mwisho pambano la ubingwa wa uzito wa juu lenye hadhi kama hii lilifanyika mwaka 1999 wakati bondia Lennox Lewis alipomtwanfa Evander Holyfield na kuitetea mikanda ya IBF, WBC na wba.

The post Tyson Fury kuzichapa na Usyk Saudi Arabia first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/09/29/tyson-fury-kuzichapa-na-usyk-saudi-arabia/feed/ 0