Uganda Cranes - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Sat, 27 Dec 2025 20:50:08 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=7.0.4 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg Uganda Cranes - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 Stars, Cranes zatoka sare ya 1-1 https://www.greensports.co.tz/2025/12/27/stars-cranes-zatoka-sare-ya-1-1/ https://www.greensports.co.tz/2025/12/27/stars-cranes-zatoka-sare-ya-1-1/#respond Sat, 27 Dec 2025 20:50:06 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=14226 Rabat, MoroccoTimu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars imetoka sare ya bao 1-1 na Uganda Cranes katika mechi ya Kundi C ya fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon 2025) iliyochezwa leo Jumamosi, Desemba 27, 2025.Stars ndio waliokuwa wa kwanza kupata bao dakika ya 59 kwa mkwaju wa penalti uliopigwa na Simon Msuva na […]

The post Stars, Cranes zatoka sare ya 1-1 first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Rabat, Morocco
Timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars imetoka sare ya bao 1-1 na Uganda Cranes katika mechi ya Kundi C ya fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon 2025) iliyochezwa leo Jumamosi, Desemba 27, 2025.
Stars ndio waliokuwa wa kwanza kupata bao dakika ya 59 kwa mkwaju wa penalti uliopigwa na Simon Msuva na kumshinda kipa mkongwe wa Cranes, Dennis Onyango.
Penalti hiyo ilitolewa na mwamuzi baada ya Baba Alhassan wa Cranes, kuunawa mpira uliopigwa na Alphonce Mabula na Alhassan kujichanganya katika harakati za kuokoa na kujikuta akiuzuia mpira huo kwa mkono ingawa kipa wake aliokoa.
Cranes baada ya kufungwa bao hilo walianza kulisakama lango la Stars mara kwa mara huku Stars wakiwa na kazi ya kuzuia kabla ya mambo kuharibika dakika ya 69 baada ya Cranes kupata bao la kusawazisha.
Bao hilo lilitokana na mpira ulioanzia kwa kipa Onyango aliyetoa pasi ndefu kabla ya kupigwa krosi ambayo ilipigwa na Denis Omedi na Uche Ikpeazu akaujaza mpira wavuni kwa kichwa.
Kuingia kwa bao hilo ni kama vile kuliwaamsha Cranes ambao dakika chache baadaye nusura waandike bao la pili baada ya kupata penalti iliyotokana na makosa ya Haji Mnoga aliyemshika mchezaji mmoja wa Cranes lakini mpigaji wa penalti, Allan Okelo akaupaisha mpira.
Cranes ndio waliouanza mpira kwa kasi kwa kupeleka mashambulizi ya mapema yaliyoanzia kwa beki wa kushoto Abdul Aziz Kayondo ambaye alikuwa akipanda na kupiga krosi chonganishi ambazo hata hivyo ziliokolewa na kipa Zubeir Foba.
Stars nao walijibu mapigo na kutengeneza nafasi kadhaa ikiwamo dakika ya 41 baada ya Kelvin John akiwa katika nafasi nzuri lakini mpira alioupiga ulipaa juu ya lango la Cranes.


Katika mechi ya leo, kocha wa Stars Miguel Gamondi alianza kwa kumuweka benchi nahodha Mbwana Samatta kabla ya kumuingiza dakika ya 63 akichukua nafasi ya Kelvin John.
Mechi ya leo ilikuwa na neema mara mbili kwa Msuva kwani licha ya kufunga bao lililoibeba Stars pia ndiye aliyetajwa kuwa mchezaji bora wa mechi hiyo.
Kwa matokeo hayo, Stars na Cranes ambazo zimepangwa kundi moja na timu za Nigeria na Tunisia, sasa zitakuwa na kazi ya kuhakikisha zinashinda mechi zao za mwisho zilizobaki ili kufufua matumaini ya kusonga mbele hatua ya mtoano (16 bora).
Timu hizo zimepoteza mechi zao za kwanza, Stars ikilala kwa Nigeria na Cranes mbele ya Tunisia na katika mechi zao za mwisho hatua ya makundi zitakazochezwa Jumanne Desemba 30, 2025, Stars itaivaa Tunisia na Cranes itaumana na Nigeria.

The post Stars, Cranes zatoka sare ya 1-1 first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2025/12/27/stars-cranes-zatoka-sare-ya-1-1/feed/ 0
Amrouche aanza vizuri Stars https://www.greensports.co.tz/2023/03/24/amrouche-aanza-vizuri-stars/ https://www.greensports.co.tz/2023/03/24/amrouche-aanza-vizuri-stars/#respond Fri, 24 Mar 2023 19:29:24 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=5590 Na mwandishi wetuKocha mpya wa timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’, Adel Amrouche leo Ijumaa ameanza na mguu mzuri mechi yake ya kwanza na timu hiyo baada ya kuichapa Uganda Cranes bao 1-0.Katika mechi hiyo ya kuwania kufuzu fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon 2023) iliyopigwa nchini Misri, Stars ilinufaika na bao […]

The post Amrouche aanza vizuri Stars first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Kocha mpya wa timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’, Adel Amrouche leo Ijumaa ameanza na mguu mzuri mechi yake ya kwanza na timu hiyo baada ya kuichapa Uganda Cranes bao 1-0.
Katika mechi hiyo ya kuwania kufuzu fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon 2023) iliyopigwa nchini Misri, Stars ilinufaika na bao hilo pekee lililofungwa na Simon Msuva katika dakika ya 68.
Msuva nyota wa zamani wa Yanga ambaye kwa sasa anacheza soka nchini Saudi Arabia katika klabu ya Al-Qadsiah, alifunga bao hilo baada ya kuitumia vizuri pasi ya beki wa kulia wa Stars, Dickson Job.
Dakika tatu baada ya kuingia bao hilo, Cranes waliokuwa wenyeji wa mchezo huo walimtoa nahodha wao, Emmanuel Okwi ambaye pia amewahi kuzichezea timu za Yanga na Simba za Tanzania na kumuingiza Mato Kassim.
Stars nayo ilifanya mabadiliko ya mapema dakika ya 57 kwa kumtoa mshambuliaji Hamis Said Jr na nafasi yake kuchukuliwa na Abdul Seleman ‘Sopu’ mabadiliko ambayo yaliipatia Stars bao hilo pekee.
Mabadiliko mengine yaliyofanywa na Amrouche ni katika dakika ya 79 alipowatoa Mudathir Yahya na nafasi yake kuingia Feisal Salum au Fei Toto na zikiwa zimebaki dakika tano mpira kumalizika Msuva ambaye aliumia alitoka na nafasi yake kuingia Kelvin John.
Kwa ushindi huo Stars sasa inashika nafasi ya pili katika kundi lake ikiwa na pointi nne wakati Algeria ikiwa kinara wa kundi hilo Niger ni ya tatu na Uganda ambayo itarudiana na Stars Jumanne ijayo
jijini Dar es Salaam inaburuza mkia.

The post Amrouche aanza vizuri Stars first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/03/24/amrouche-aanza-vizuri-stars/feed/ 0
Stars yajiweka pagumu CHAN https://www.greensports.co.tz/2022/08/29/stars-yajiweka-pagumu-chan/ https://www.greensports.co.tz/2022/08/29/stars-yajiweka-pagumu-chan/#respond Mon, 29 Aug 2022 08:16:12 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=2604 Na mwandishi wetuJumapili haikuwa nzuri kwa Taifa Stars baada ya kushindwa kuutumia vyema uwanja wa nyumbani wa Benjamin Mkapa kwa kufungwa bao 1-0 na Uganda Cranes katika mechi ya kuwania kufuzu fainali za Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ndani (CHAN).Stars ililala kwa bao la dakika ya 87 lililofungwa na Travis Muytaba na hivyo kuiweka […]

The post Stars yajiweka pagumu CHAN first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Jumapili haikuwa nzuri kwa Taifa Stars baada ya kushindwa kuutumia vyema uwanja wa nyumbani wa Benjamin Mkapa kwa kufungwa bao 1-0 na Uganda Cranes katika mechi ya kuwania kufuzu fainali za Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ndani (CHAN).
Stars ililala kwa bao la dakika ya 87 lililofungwa na Travis Muytaba na hivyo kuiweka katika wakati mgumu timu hiyo kwani sasa itakuwa na kazi ya kuhakikisha inapata ushindi wa ugenini katika mechi ya marudiano wikiendi ijayo ni jambo gumu lakini dakika 90 zinaweza kuja na matokeo yanayoweza kuwafurahisha Watanzania, tusubiri.
Stars ilianza kwa kuitoa Somalia kwa jumla ya mabao 3-1, ilianza kwa ushindi wa bao 1-0 na kufuatiwa na ushindi mwingine wa mabao 2-1 katika mechi ambazo zote zilipigwa kwenye Uwanja wa Mkapa kutokana na hofu ya usalama iliyopo nchini Somalia.
Michuano ya CHAN ilizinduliwa rasmi mwaka 2009 na kufanyika nchini Ivory Coast kwa mara ya kwanza ambako Tanzania ilifuzu lakini iliishia katika hatua za awali wakati huo ikinolewa na kocha kutoka Brazil, Marcio Maximo.

The post Stars yajiweka pagumu CHAN first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2022/08/29/stars-yajiweka-pagumu-chan/feed/ 0