Uchaguzi - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Wed, 01 Feb 2023 07:14:55 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=7.0.2 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg Uchaguzi - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 Kaluwa: Nataka kuweka mambo sawa Simba https://www.greensports.co.tz/2023/02/01/kaluwa-nataka-kuweka-mambo-sawa-simba/ https://www.greensports.co.tz/2023/02/01/kaluwa-nataka-kuweka-mambo-sawa-simba/#respond Wed, 01 Feb 2023 07:10:01 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=4936 Na mwandishi wetuAliyekuwa mgombea wa nafasi ya Mwenyekiti wa Klabu ya Simba, Moses Kaluwa amefunguka kuwa hana mpango wa kuivuruga Simba kwa sababu ya kutoshinda kwenye uchaguzi.Badala yake Kaluwa amesema kwamba anachotaka ni kuweka sawa baadhi ya vitu kwa faida ya klabu hiyo kongwe Tanzania na hata Afrika.Kaluwa alishindwa na Murtaza Mangungu anayeendelea kuwa mwenyekiti […]

The post Kaluwa: Nataka kuweka mambo sawa Simba first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Aliyekuwa mgombea wa nafasi ya Mwenyekiti wa Klabu ya Simba, Moses Kaluwa amefunguka kuwa hana mpango wa kuivuruga Simba kwa sababu ya kutoshinda kwenye uchaguzi.
Badala yake Kaluwa amesema kwamba anachotaka ni kuweka sawa baadhi ya vitu kwa faida ya klabu hiyo kongwe Tanzania na hata Afrika.
Kaluwa alishindwa na Murtaza Mangungu anayeendelea kuwa mwenyekiti katika uchaguzi uliofanyika Jumapili iliyopita jijini Dar es Salaam ambapo Mangungu alipata kura 1,311 dhidi ya 1,045 za Kaluwa.
Kaluwa ambaye hakusaini karatasi za matokeo ya uchaguzi huo alisema hakufanya hivyo si kwamba anataka kuleta migongano ndani ya Simba bali angependa kuona baadhi ya mambo yananyooka kwenye chaguzi zijazo za klabu hiyo.
“Siwezi kusema sijakubaliana na matokeo maana itakuwa ni suala la ugomvi na utengamano, ninachoamini ni kwenye Simba imara, hiyo ndiyo kitu namba moja kwamba inapaswa kuwa na Simba imara kuliko haya tunayosema.

“Haya yanarekebishika sababu niliyofanyiwa mimi sikuyapenda, yasijirudie na kwa kuwa sikuyapenda siyo lazima sasa niseme sikuyapenda lakini mwisho wa siku kutopenda kwangu sitaki kuwe na athari ya kudumu,” alisema Kaluwa.


Pia aliongeza kwamba alijaribu kuwashauri kamati ya uchaguzi kuhusu kutumia wino kwa wapiga kura ili kulinda haki za wapiga na wapigiwaji kura lakini ukatumika utaratibu wa kufunga karatasi mikononi ambao anadai haukufanya kazi zaidi ya kuvuruga uchaguzi huo kwa wengine kurudia kupiga kura.
Kaluwa pia alisema anaamini idadi iliyotangazwa kwa wapiga kura ilikuwa kubwa kuliko uhalisia wenyewe ingawa aliwapongeza Wanasimba kwa mwamko waliokuwa nao kujitokeza kutimiza haki yao ya msingi siku hiyo kwa kuwa wao ndiyo wenye maamuzi.
“Kulikuwa na mapungufu mengi, inabidi hii itushtue kwamba tunapokwenda tufanye maboresho. Sikusaini kuonesha sikuridhishwa na zile hatua na sitaki kuwa sehemu ya vurugu, nazungumza tu ukweli ili tujirekebishe kuwe na uchaguzi wa kweli kwa wapiga kura,” alisema Kaluwa.
Katika uchaguzi huo, Mangungu alishinda nafasi hiyo pamoja na wajumbe watano wa Bodi ya Wakurugenzi ambao ni Seif Muba, Asha Baraka, Issa Iddi, Rodney Chiduo na Seleman Harubu.

The post Kaluwa: Nataka kuweka mambo sawa Simba first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/02/01/kaluwa-nataka-kuweka-mambo-sawa-simba/feed/ 0
Mangungu ashinda uenyekiti Simba https://www.greensports.co.tz/2023/01/30/mangungu-ashinda-uenyekiti-simba/ https://www.greensports.co.tz/2023/01/30/mangungu-ashinda-uenyekiti-simba/#respond Mon, 30 Jan 2023 09:55:47 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=4913 Na mwandishi wetuMurtaza Mangungu ameitetea nafasi ya uenyekiti wa klabu ya Simba baada ya kupata kura 1,311 katika uchaguzi uliofanyika Jumapili hii usiku akimbwaga wakili Moses Kaluwa aliyepata kura 1,045.Mbali na Mangungu, katika nafasi ya wajumbe washindi na idadi ya kura walizopata zikiwa kwenye mabano ni Dr Seif Muba (1,636), Asha Baraka (1,564), Issa Masoud […]

The post Mangungu ashinda uenyekiti Simba first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Murtaza Mangungu ameitetea nafasi ya uenyekiti wa klabu ya Simba baada ya kupata kura 1,311 katika uchaguzi uliofanyika Jumapili hii usiku akimbwaga wakili Moses Kaluwa aliyepata kura 1,045.
Mbali na Mangungu, katika nafasi ya wajumbe washindi na idadi ya kura walizopata zikiwa kwenye mabano ni Dr Seif Muba (1,636), Asha Baraka (1,564), Issa Masoud Idd (1,285), Rodney Chiduo (1,267) na Seleman Harubu (1,250).
Wakati akijinadi katika kampeni zake, Mangungu pamoja na mambo mengine aliahidi kufuta uteja kwa mahasimu wao Yanga na kuhakikisha Simba inafanya vizuri katika mashindano mbalimbali.
Uchaguzi huo uliofanyika jijini Dar es Salaam, ulitanguliwa na mkutano mkuu ambapo watendaji wa klabu hiyo walipata fursa ya kuanika mipango na mikakati ya timu ya Simba.
Katika mkutano huo, wanachama walielezwa kuwa bajeti ya klabu hiyo kwa mwaka 2021-22 ilikuwa ni Sh 11.94 bilioni wakati makusanyo kwa kipindi hicho hicho yalikuwa ni Sh 12.73 bilioni.
Katika matumizi, wanachama walielezwa kuwa yalihusisha malipo ya mishahara ya wachezaji na benchi la ufundi (Sh 4.3 bilioni) kambi ndani na nje ya nchi (Sh 2.2 bilioni) kambi timu ya wanawake (Sh 100 milioni) usajili (Sh 1.2 bilioni) katika fedha hizo Mohammed Dewji au Mo aliongeza Sh 2 bilioni pamoja na malipo mengineyo ikiwamo mishahara ya watendaji.


Mkutano huo pia ulipambwa na washiriki kutoka nje ya nchi akiwamo kocha wa Al Hilal ya Sudan, Florent Ibenge ambaye aliwapongeza wanachama na viongozi wa Simba akidai amefurahishwa na mualiko huo.
Mgeni mwingine kutoka nje aliyehudhuria mkutano huo ni mchezaji wa zamani wa Vipers ya Uganda ambaye pia alikuwa akicheza soka la kulipwa nchini China, Cesar Manzoki ambaye aliwafurahisha wanachama wa Simba kwa kudai kwamba hawezi kuichezea timu yenye rangi ya nyoka.
Kauli hiyo ilitafsiriwa na wanachama wengi katika mkutano huo kuwa mchezaji huyo alikuwa akiwananga mahasimu wa Simba, Yanga ambao wanatumia jezi za kijani na njano.
Mchezaji huyo amekuwa akihusishwa na mipango ya kujiunga na Simba na hapana shaka kwa kitendo chake cha kushiriki mkutano huo, haitoshangaza akivaa jezi nyekundu na nyeupe wakati wowote kuanzia sasa.
Mangungu aliingia madarakani Febuari 7, 2021 katika uchaguzi mdogo uliofanyika kuziba nafasi ya mwenyekiti iliyoachwa wazi na Swedi Nkwabi aliyejiuzulu miezi 10 baada ya kuchaguliwa katika nafasi hiyo kwenye uchaguzi uliofanyika Novemba 5, 2018.

The post Mangungu ashinda uenyekiti Simba first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/01/30/mangungu-ashinda-uenyekiti-simba/feed/ 0
Wagombea Simba kujulikana Jmosi https://www.greensports.co.tz/2022/12/23/wagombea-simba-kujulikana-jmosi/ https://www.greensports.co.tz/2022/12/23/wagombea-simba-kujulikana-jmosi/#respond Fri, 23 Dec 2022 20:57:32 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=4462 Na mwandishi wetuKamati ya Uchaguzi ya Klabu ya Simba imeeleza kuwa kesho Jumamosi itaweka wazi majina ya wagombea waliopita kwenye usaili wa uchaguzi wa viongozi wapya wa klabu hiyo unaotarajiwa kufanyika Januari, mwakani.Hayo ni matokeo ya wagombea takriban 23 ambao wamekuwa wakiitwa kwa awamu tangu juzi na kamati hiyo huku baadhi ambao hawakuitwa wameelezwa pia […]

The post Wagombea Simba kujulikana Jmosi first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Kamati ya Uchaguzi ya Klabu ya Simba imeeleza kuwa kesho Jumamosi itaweka wazi majina ya wagombea waliopita kwenye usaili wa uchaguzi wa viongozi wapya wa klabu hiyo unaotarajiwa kufanyika Januari, mwakani.
Hayo ni matokeo ya wagombea takriban 23 ambao wamekuwa wakiitwa kwa awamu tangu juzi na kamati hiyo huku baadhi ambao hawakuitwa wameelezwa pia kufahamu hatma yao na sababu zilizopelekea kutofanyiwa usaili huo.
Akizungumza leo Ijumaa jijini Dar es Salaam, mwenyekiti wa kamati hiyo, Boniface Lihamwike alisema wanafahamu kumekuwa na maswali na sintofahamu kutoka kwa baadhi ya wagombea wa nyadhifa mbalimbali lakini majibu yote yatayawekwa wazi kesho Jumamosi baada ya kumalizika kwa kikao cha kamati.

“Tutakachofanya kwa kuwa leo ndiyo tunamaliza usaili, tukishamaliza hilo Jumamosi (kesho) tutatoa majina yote ya ambao wamepita kwenye usaili na pia tutawajulisha watu wote ambao walikuwa hawajapita, tutajua ni njia gani ya kuwajulisha na tutawapa sababu.


“Kusiwe na wasiwasi kwani tukimaliza zoezi hili tutatoa taarifa kwa nini wameitwa na kwa nini wameachwa na walioingia kwenye usaili haimaanishi kwamba wote wanaweza kupita, lakini yote tutayaweka hadharani, wapo ambao hawakuvuka hatua na huo ni utaratibu wa kawaida,” alisema Lihamwike.
Kwa mujibu wa kamati hiyo, baada ya kuweka majina ya waliopita katika usaili, zoezi litakalofuata ni kupokea na kusikiliza mapingamizi waliyowekewa wagombea, kabla ya kutangaza tena waliopita kwenye awamu hiyo na kisha kuanza rasmi kampeni kuelekea Januari 29, siku ya uchaguzi wenyewe.

The post Wagombea Simba kujulikana Jmosi first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2022/12/23/wagombea-simba-kujulikana-jmosi/feed/ 0