TWPL - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Thu, 08 Feb 2024 06:35:14 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=7.0.4 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg TWPL - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 Simba Queens, Yanga Princess dimbani https://www.greensports.co.tz/2024/02/08/simba-queens-yanga-princess-dimbani/ https://www.greensports.co.tz/2024/02/08/simba-queens-yanga-princess-dimbani/#respond Thu, 08 Feb 2024 06:35:13 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=9616 Na mwandishi wetuSimba Queens (pichani) na Yanga Princess leo Alhamisi wanashuka dimbani kwenye viwanja tofauti kusaka pointi tatu muhimu kwenye Ligi Kuu Wanawake mzunguko wa tisa.Wekundu wa Msimbazi ambao watakuwa ugenini kwenye Uwanja wa Nyankumbu dhidi ya Geita Queens, wanashika nafasi ya pili kwa pointi 19 tofauti ya pointi mbili dhidi ya kinara JKT Queens.Simba […]

The post Simba Queens, Yanga Princess dimbani first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Simba Queens (pichani) na Yanga Princess leo Alhamisi wanashuka dimbani kwenye viwanja tofauti kusaka pointi tatu muhimu kwenye Ligi Kuu Wanawake mzunguko wa tisa.
Wekundu wa Msimbazi ambao watakuwa ugenini kwenye Uwanja wa Nyankumbu dhidi ya Geita Queens, wanashika nafasi ya pili kwa pointi 19 tofauti ya pointi mbili dhidi ya kinara JKT Queens.
Simba inashuka dimbani ikiwa imetoka kushinda mabao 4-0 dhidi ya Fountain Gate, inakutana na Geita ambayo imetoka kupoteza mabao 2-0 dhidi ya Yanga.
Geita yenyewe inaburuza mkia ikiwa na pointi moja na isipokuwa makini huenda ikachezea mvua ya mabao.
Yanga nayo iliyo nafasi ya nne kwa pointi 15, itacheza Uwanja wa Nyamagana, Mwanza dhidi ya Alliance Girls iliyo nafasi ya tisa kwa pointi sita.
Mechi nyingine zitakazochezwa leo ni vinara JKT Queens watakaorindima kwenye Uwanja wa Jenerali Isamuyo, Dar es Salaam wakiikaribisha Ceasiaa Queens.
JKT ni miongoni mwa timu mbili ambazo hazijapoteza mchezo wowote mpaka sasa ikiwa imeshinda michezo yote saba hivyo wanatazamiwa kuendeleza ubabe dhidi ya Ceasiaa.
Pia, kutakuwa na mechi ya Baobab Queens dhidi ya Amani Queens, Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma na Bunda Queens dhidi ya Fountain Gate kwenye Uwanja wa Karume, Mara.

The post Simba Queens, Yanga Princess dimbani first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/02/08/simba-queens-yanga-princess-dimbani/feed/ 0
Utata mechi ya JKT, Simba Queens https://www.greensports.co.tz/2024/01/10/utata-mechi-ya-jkt-simba-queens/ https://www.greensports.co.tz/2024/01/10/utata-mechi-ya-jkt-simba-queens/#respond Wed, 10 Jan 2024 07:39:14 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=9241 Na mwandishi wetuMechi ya Ligi Kuu ya Wanawake (TWPL) kati ya Simba Queens na JKT Queens imeshindwa kufanyika Jumanne hii baada ya kutokea utata wa viwanja kwa kila timu kwenda kwenye uwanja tofauti.Simba Queens pamoja na waamuzi na maofisa wa mechi hiyo wao walikuwa Azam Complex wakati wapinzani wao walikuwa Mbweni kwenye dimba la Jenerali […]

The post Utata mechi ya JKT, Simba Queens first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Mechi ya Ligi Kuu ya Wanawake (TWPL) kati ya Simba Queens na JKT Queens imeshindwa kufanyika Jumanne hii baada ya kutokea utata wa viwanja kwa kila timu kwenda kwenye uwanja tofauti.
Simba Queens pamoja na waamuzi na maofisa wa mechi hiyo wao walikuwa Azam Complex wakati wapinzani wao walikuwa Mbweni kwenye dimba la Jenerali Isamhuyo wakiamini mechi ingechezwa kwenye uwanja huo.
Kwenye dimba la Chamazi baada ya waamuzi kuona timu pinzani haijafika walifuata taratibu husika na kumaliza mchezo kwa maana ya kwamba JKT Queens wameshindwa kufika uwanjani.
Wachezaji wa Simba Queens waliingia uwanjani kama kawaida na kufanya mazoezi mepesi tayari kwa kuwavaan JKT Queens ambao nao walikuwa Mbweni wakiwasubiri Simba Queens.
Mkanganyiko huo hata hivyo umepokewa kwa namna tofauti na JKT Queens ambao waliamini mechi hiyo ingechezwa kwenye dimba la Ismhuyo kama alivyonukuliwa ofisa habari wa timu hiyo, Masau Bwire akifafanua jambo hilo.

Kwa mujibu wa Bwire, ratiba ya mechi hiyo iliyotolewa na TFF ilionesha kwamba mechi hiyo ilipaswa kuchezwa kwenye dimba la Isamhuyo na habari ya Chamazi wameisikia wakati wakiwa uwanjani, kwa maana nyingine jambo hilo kwao ni geni.
Hapo hapo kuna taarifa kwamba mechi baina ya timu hizo ilifutwa hali ambayo inazidisha utata wa jambo hilo.
Wadau wengi wa soka wanasubiri kwa hamu kusikia TFF itaamua nini kuhusu mkanganyiko huo ambao kimsingi ni kama vile umesababishwa na ukosefu wa taarifa sahihi na kwa wakati sahihi.

The post Utata mechi ya JKT, Simba Queens first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/01/10/utata-mechi-ya-jkt-simba-queens/feed/ 0