Trump - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Sun, 19 Jul 2026 11:32:22 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=7.0.4 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg Trump - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 Trump naye amlaumu Tuchel https://www.greensports.co.tz/2026/07/19/trump-naye-amlaumu-tuchel/ https://www.greensports.co.tz/2026/07/19/trump-naye-amlaumu-tuchel/#respond Sun, 19 Jul 2026 11:32:21 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=14805 New York, MarekaniRais wa Marekani, Donald Trump naye ameibuka na kumlaumu kocha wa England, Thomas Tuchel kwa mbinu alizotumia katika mechi ya nusu fainali ya Kombe la Dunia dhidi ya Argentina.Katika hoja yake hiyo, Trump kwa kiasi kikubwa amehoji majukumu ya ulinzi ambayo Thuchel alimpa mshambuliaji wa timu hiyo, Harry Kane hasa katika kipindi cha […]

The post Trump naye amlaumu Tuchel first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

New York, Marekani
Rais wa Marekani, Donald Trump naye ameibuka na kumlaumu kocha wa England, Thomas Tuchel kwa mbinu alizotumia katika mechi ya nusu fainali ya Kombe la Dunia dhidi ya Argentina.
Katika hoja yake hiyo, Trump kwa kiasi kikubwa amehoji majukumu ya ulinzi ambayo Thuchel alimpa mshambuliaji wa timu hiyo, Harry Kane hasa katika kipindi cha pili.
Tuchel ameshutumiwa baada ya England kufungwa mabao 2-1 na Argentina na kutolewa katika hatua ya nusu ya fainali ingawa bado anaungwa mkono na mabosi wa Chama cha Soka England na inaaminika ndiye atakayeiongoza timu hiyo kwenye fainali za Kombe la Ulaya 2028 au Euro 2028.
England walikuwa wa kwanza kupata bao lililofungwa na Anthony Gordon dakika ya 55 na baada ya hapo Tuchel alijaza mabeki sita nyuma lakini Argentina walimzidi ujanja na kufunga mabao mawili dakika za 85 na 92 (90+2).
Akitoa hoja yake dhidi ya mbinu za Tuchel, Trump awali alianza kwa kumsifia Kane na kukumbushia walivyowahi kucheza naye golfu kwenye ufukwe wa West Palm takriban miezi 18 iliyopita.

“England mna mchezaji mzuri, mchezaji ambaye niliwahi kucheza naye golfu, mnamjua huyo? ni Harry ambaye amekuwa mchezaji mahiri, nafikiri walikosea kumfanya awe mchezaji wa ulinzi,” alisema Trump.

Trump alifafanua akisema kilichotokea ni kwamba England walipata bao la kuongoza na baada ya hapo walichofanya ni kumchukua mchezaji wao bora na kumuweka katika eneo la ulinzi.

The post Trump naye amlaumu Tuchel first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2026/07/19/trump-naye-amlaumu-tuchel/feed/ 0
Trump amtia matatani Rais wa Fifa https://www.greensports.co.tz/2025/12/10/trump-amtia-matatani-rais-wa-fifa/ https://www.greensports.co.tz/2025/12/10/trump-amtia-matatani-rais-wa-fifa/#respond Wed, 10 Dec 2025 19:04:44 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=14168 Washington, MarekaniKamati ya Maadili ya Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa), imetakiwa kumchunguza rais wa shirikisho hilo, Gianni Infantino akituhumiwa kuvunja kanuni ya kutojihusisha na siasa kutokana na uhusiano wake na Rais wa Marekani, Donald Trump.Wiki iliyopita, Infantino alimpa Trump, 79, tuzo ya Fifa ya amani wakati wa hafla ya droo ya fainali za Kombe […]

The post Trump amtia matatani Rais wa Fifa first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Washington, Marekani
Kamati ya Maadili ya Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa), imetakiwa kumchunguza rais wa shirikisho hilo, Gianni Infantino akituhumiwa kuvunja kanuni ya kutojihusisha na siasa kutokana na uhusiano wake na Rais wa Marekani, Donald Trump.
Wiki iliyopita, Infantino alimpa Trump, 79, tuzo ya Fifa ya amani wakati wa hafla ya droo ya fainali za Kombe la Dunia 2026 na hapo hapo ameonesha kumuunga mkono kiongozi huyo wa Marekani katika mahojiano aliyofanya kwenye mitandao ya kijamii.
Taasisi inayojihusisha na utetezi wa haki za binadamu ya FairSquare imeandika barua ya malalamiko ikidai kuwa Infantino amevunja kanuni nne za Fifa kuhusu kutojihusisha na upande wowote katika siasa.
Infantino alikuwa sambamba na Trump kwenye ukumbi wa Kennedy katika hafla ya droo hiyo kwa ajili ya fainali za Kombe la Dunia 2026 ambazo zitafayika Marekani, Canada na Mexico kuanzia Juni 11 hadi Julai 19 mwakani.

“Tuzo ya aina ile kwa kiongozi wa kisiasa aliye madarakani yenyewe tu ni uvunjaji wa wazi wa kanuni za Fifa kuhusu kutojihusisha na upande wowote,” ilieleza sehemu ya barua ya FairSquare.


Kwa mujibu wa FairSquare, rais wa Fifa hana mamlaka ya kuamua yeye mwenyewe kuhusu dira, muelekeo, sera na taratibu za Fifa.
Sambamba na tuzo hiyo ya dhahabu, Infantino pia alimzawadia Trump medali na cheti na katika hotuba yake bosi huyo wa Fifa akasema hicho ndicho wanachokitaka kwa kiongozi na kumuhakikishia Trump kwamba atamuunga mkono.
Oktoba mwaka jana Infantino, 55, alinukuliwa akisema kwamba Trump anahaki ya kupewa tuzo ya nobeli jambo ambalo liliibua mjadala na kuongeza kuwa Trump anatakiwa kuungwa mkono na wote.
“Wote tunatakiwa kuunga mkono anachofanya Trump, ni kwa sababu nadhani ni jambo linaloonekana kuwa zuri,” alisema Infantino.

The post Trump amtia matatani Rais wa Fifa first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2025/12/10/trump-amtia-matatani-rais-wa-fifa/feed/ 0
Trump ahoji nafasi ya Marekani kubeba Kombe la Dunia https://www.greensports.co.tz/2025/03/09/trump-ahoji-nafasi-ya-marekani-kubeba-kombe-la-dunia/ https://www.greensports.co.tz/2025/03/09/trump-ahoji-nafasi-ya-marekani-kubeba-kombe-la-dunia/#respond Sun, 09 Mar 2025 10:59:55 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=13116 New York, MarekaniRais wa Fifa, Gianni Infantino amekutana na Rais wa Marekani, Donald Trump katika Ikulu ya Marekani na kuzungumzia mipango ya fainali za Kombe la Dunia 2026 huku Trump akihoji kama Marekani itabeba taji la michuano hiyo.Katika mazungumzo hayo yaliyofanyika Ijumaa hii kwenye Ikulu ya White House, Trump inadaiwa alimuuliza Infantino kama Marekani itaweza […]

The post Trump ahoji nafasi ya Marekani kubeba Kombe la Dunia first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

New York, Marekani
Rais wa Fifa, Gianni Infantino amekutana na Rais wa Marekani, Donald Trump katika Ikulu ya Marekani na kuzungumzia mipango ya fainali za Kombe la Dunia 2026 huku Trump akihoji kama Marekani itabeba taji la michuano hiyo.
Katika mazungumzo hayo yaliyofanyika Ijumaa hii kwenye Ikulu ya White House, Trump inadaiwa alimuuliza Infantino kama Marekani itaweza kushinda Kombe la Dunia na Infantino akaonesha kuwa jambo hilo linawezekana.
Sambamba na fainali za Kombe la Dunia 2026, Marekani itakuwa mwenyeji wa fainali za Kombe la Dunia kwa Klabu ambazo zitafanyika baadaye mwaka huu.
Awali baada ya Trump kumuuliza Infantino nchi ambazo zinaweza kushinda Kombe la Dunia, Infantino akazitaJa na ndipo Trump alipomuuliza kuhusu Marekani ambayo haikuwa kwenye orodha ya awali ya Infantino.
“Brazil, Argentina, England, Hispania, Ujerumani,” alizitaja Infantino na ndipo Trump alipohoji iwapo Marekani inaweza kuishangaza dunia na kubeba taji hilo.
Katika ufafanuzi wa hoja hiyo, Infantino alimwambia rais huyo wa 47 wa Marekani kwamba nchi yake inaweza kubeba taji hilo kwa msaada wa mashabiki na hata timu yao ni moja ya timu bora duniani.
“Kwa hiyo uwezekano upo?” Alihoji zaidi Trump na Infantino akamjibu hapo hapo, “Hakika nafasi hiyo ipo.”
Trump pia alimuahidi Infantino kwamba ataunda kikosi kazi kwa ajili ya fainali za Kombe la Dunia 2026 ambazo safari hii zinafanyika Marekani ya Kusini kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1994.
Marekani itakuwa mwenyeji wa fainali hizo ikishirikiana na nchi za Canada na Mexico ingawa nchi hizo kwa sasa zipo katika mzozo unaohusisha mambo ya kodi baada ya Trump kutaka bidhaa za nchi hizo majirani zake zitozwe kodi.
Trump hata hivyo anaamini mzozo wa mataifa hayo kuhusu masuala ya kodi utazifanya fainali hizo ziwe na hamasa zaidi.
Katika historia ya fainali za Kombe la Dunia, Marekani ina rekodi ya kufikia hatua ya nusu fainali mwaka 1930 katika fainali za kwanza katika historia ya michuano hiyo na baada ya hapo Marekani pia ilifikia hatua ya robo fainali mwaka 2002.

The post Trump ahoji nafasi ya Marekani kubeba Kombe la Dunia first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2025/03/09/trump-ahoji-nafasi-ya-marekani-kubeba-kombe-la-dunia/feed/ 0