TPBRC - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Fri, 10 May 2024 22:22:10 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=7.0.4 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg TPBRC - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 Palasa ajivunia uongozi wake TPBRC https://www.greensports.co.tz/2024/05/11/palasa-ajivunia-uongozi-wake-tpbrc/ https://www.greensports.co.tz/2024/05/11/palasa-ajivunia-uongozi-wake-tpbrc/#respond Fri, 10 May 2024 22:22:09 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=10924 Na mwandishi wetuRais wa Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa Tanzania (TPBRC), Chaurembo Palasa ambaye siku tatu zilizopita alisimamishwa kupisha uchunguzi dhidi ya uongozi wake amesema pamoja na yote lakini anajivunia kuona ngumi sasa zinapigwa kote nchini bila ya malalamiko.Palasa na viongozi wenzake wa TPBRC walisimamishwa na serikali kupitia Wizara ya Utamaduni Sanaa na Michezo ingawa […]

The post Palasa ajivunia uongozi wake TPBRC first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Rais wa Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa Tanzania (TPBRC), Chaurembo Palasa ambaye siku tatu zilizopita alisimamishwa kupisha uchunguzi dhidi ya uongozi wake amesema pamoja na yote lakini anajivunia kuona ngumi sasa zinapigwa kote nchini bila ya malalamiko.
Palasa na viongozi wenzake wa TPBRC walisimamishwa na serikali kupitia Wizara ya Utamaduni Sanaa na Michezo ingawa kiongozi huyo anaendelea anajivunia mafanikio na kupungua malalamiko tofauti na ilivyokuwa miaka ya nyuma.
Palasa amezungumza hayo leo Ijumaa alipokuwa akihojiwa na Green Sports juu ya tuhuma zinazomkabili ambapo alisema kwa sasa hana lolote la kuzungumza.
Badala yake alisema kwamba anasubiri kujibu hoja zinazomkabili mbele ya tume ya uchunguzi iliyoteuliwa juzi na Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Damas Ndumbaro.
“Bado sijahojiwa na kamati kwa hiyo siwezi kusema lolote, sababu hata nikisema sasa itakuwa haisaidii, nasubiri kwanza waniite nizungumze nao kisha nitakuwa na lolote la kusema kuhusiana na hilo,” alisema Palasa.
Palasa ambaye ni bondia wa zamani alisisitiza kuwa anafurahi kuona ngumi zinapigwa sehemu nyingi Tanzania bila malalamiko kama ilivyokuwa miaka ya nyuma.

“Huko awali kulikuwa na shida ya malipo lakini sasa watu wanapewa malipo yao, wanapata stahiki zao ndiyo maana hizo kelele hazipo, kilichobaki sasa ni mtu kulalamika inapotokea ameguswa kwenye masuala mengine binafsi lakini nafurahi kuona ngumi kama ngumi zinakwenda vizuri na hakuna malalamiko,” alisema Palasa.


Juzi Waziri Ndumbaro aliusimamisha uongozi TPBRC kupisha uchunguzi dhidi yao juu ya tuhuma zinazowakabili ikiwemo matumizi mabaya ya madaraka, ukiukaji wa katiba ya kamisheni na mgongano wa maslahi.

The post Palasa ajivunia uongozi wake TPBRC first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/05/11/palasa-ajivunia-uongozi-wake-tpbrc/feed/ 0
Serikali yausimamisha uongozi TPBRC https://www.greensports.co.tz/2024/05/10/serikali-yausimamisha-uongozi-tpbrc/ https://www.greensports.co.tz/2024/05/10/serikali-yausimamisha-uongozi-tpbrc/#respond Fri, 10 May 2024 07:29:02 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=10899 Na mwandishi wetuUongozi wa Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa Tanzania (TPBRC) umesimamishwa ili kupisha uchunguzi wa tuhuma zinazowakabili ikiwemo ya matumizi mabaya ya madaraka, ukiukaji wa Katiba ya Kamisheni hiyo na mgongano wa maslahi.Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Gerson Msigwa (pichani), hatua hiyo imechukuliwa na […]

The post Serikali yausimamisha uongozi TPBRC first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Uongozi wa Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa Tanzania (TPBRC) umesimamishwa ili kupisha uchunguzi wa tuhuma zinazowakabili ikiwemo ya matumizi mabaya ya madaraka, ukiukaji wa Katiba ya Kamisheni hiyo na mgongano wa maslahi.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Gerson Msigwa (pichani), hatua hiyo imechukuliwa na Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt Damas Ndumbaro baada ya kikao cha jana Jumatano kilichofanyika jijini Dodoma.
Imeelezwa zaidi kuwa kufuatia uamuzi huo, Waziri Ndumbaro ameunda kamati ya mpito ya kuongoza kamisheni hiyo ambayo itaongozwa na Mwenyekiti Emmanuel Salehe na viongozi wengine wakiwa ni Alex Galinoma (Makamu Mwenyekiti), Joseph Mpuya (Katibu Mkuu) na wajumbe ni Patrick Nyembela, Shaffi Dauda na Irene Mwasanga.
Ndumbaro pia ameunda kamati ya kufanya uchunguzi kwa kamisheni iliyosimamishwa kuhusu tuhuma hizo mbalimbali zilizoibuliwa na wanachama wao.
Kamati hiyo itafanya kazi kwa muda wa mwezi mmoja kuanzia Mei 8 mwaka huu ikiongozwa na mwenyekiti Christopher Kamugisha akiwa na katibu Ingridy Kimario, wajumbe ni Mariam Aziz Faki na Sophia Alponary.
Ndumbaro pia amewataka wadau wa michezo kote nchini kufuata sheria, kanuni na miongozo iliyopo kwenye vyama na mashirikisho ya michezo ili azma ya serikali ya kukuza na kuendeleza

michezo nchini itimie.

The post Serikali yausimamisha uongozi TPBRC first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/05/10/serikali-yausimamisha-uongozi-tpbrc/feed/ 0