TotalEnergies - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Wed, 29 Jan 2025 19:14:16 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=7.0.2 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg TotalEnergies - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 CAF, TotalEnergies wasaini mkataba https://www.greensports.co.tz/2025/01/29/caf-totalenergies-wasaini-mkataba/ https://www.greensports.co.tz/2025/01/29/caf-totalenergies-wasaini-mkataba/#respond Wed, 29 Jan 2025 19:14:15 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=12951 Na mwandishi wetuShirikisho la Soka Afrika (CAF) na Kampuni ya TotalEnergies wameendeleza ushirikiano wao kwa kusaini mkataba wa udhamini wa miaka minne ambao utafikia ukomo mwaka 2028.Rais wa CAF, Patrice Motsepe amesaini mkataba huo na mwenyekiti na mtendaji mkuu wa TotalEnergues, Patrick Pouyane katika hafla fupi iliyofanyika jijini Dar es Salaam, Tanzania Jumanne ya Januari […]

The post CAF, TotalEnergies wasaini mkataba first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Shirikisho la Soka Afrika (CAF) na Kampuni ya TotalEnergies wameendeleza ushirikiano wao kwa kusaini mkataba wa udhamini wa miaka minne ambao utafikia ukomo mwaka 2028.
Rais wa CAF, Patrice Motsepe amesaini mkataba huo na mwenyekiti na mtendaji mkuu wa TotalEnergues, Patrick Pouyane katika hafla fupi iliyofanyika jijini Dar es Salaam, Tanzania Jumanne ya Januari 28, 2025.
Udhamini huo wa TotalEnergies kwa CAF utahusisha mashindano makubwa yanayosimamiwa na shirikisho hilo yakiwamo mashindano mawili ya soka ya Afrika ya Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon) kwa wanaume na Afcon kwa wanawake pamoja na Ligi ya Mabingwa Afrika.
Thamani ya mkataba huo hata hivyo haikuwekwa wazi ingawa Motsepe katika taarifa yake alisema udhamini huo unachangia ushindani na maendeleo ya soka katika nchi 54 za Afrika ambazo ni wanachama wa CAF.
Katika miaka ya karibuni CAF imekuwa mstari wa mbele kuanzisha mashindano yakiwamo ya vijana na yale ya mashule ambapo vijana wa kiume na wale wa kike kwa wingi wamekuwa wakishiriki katika soka.
Mashindano hayo pamoja na mengine yamekuwa yakiendeshwa kwa udhamini wa TotalEnergies ambao kwa muda mrefu wamekuwa wadau wakubwa wa maendeleo ya soka la Afrika kwa kushirikiana na CAF.
Motsepe alisema kwamba kampuni kadhaa ziliwafuata kwa ahadi kubwa zaidi ya fedha lakini wamethamini uhusiano wao na TotalEnergies na kwa heshima kubwa wanaendelea kufanya nao kazi.
Naye Pouyane alisema Total Energies inajivunia kutoa mchango wao katika kukua kwa mchezo maarufu wa soka kutokana na hadhi na namna unavyochangia umoja katika bara la Afrika ambapo kampuni yao ina historia ya kipekee.

The post CAF, TotalEnergies wasaini mkataba first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2025/01/29/caf-totalenergies-wasaini-mkataba/feed/ 0