Steve B - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Thu, 19 Mar 2026 13:01:19 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=7.0.2 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg Steve B - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 Kocha Simba atwaa tuzo Februari https://www.greensports.co.tz/2026/03/17/kocha-simba-atwaa-tuzo-februari/ https://www.greensports.co.tz/2026/03/17/kocha-simba-atwaa-tuzo-februari/#respond Tue, 17 Mar 2026 14:33:02 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=14453 Na mwandishi wetuKocha wa timu ya Simba, Steve Barker au Steve B ametwaa tuzo ya kocha bora wa mwezi Februari wakati mshambuliaji wa Yanga, Laurindo Dilson ‘Depu’ ametwaa tuzo hiyo kwa upande wa mchezaji bora..Kwa mujibu wa taarifa ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) iliyopatikana Jumatatu Machi 16, 2026, Depu ametwaa tuzo hiyo baada […]

The post Kocha Simba atwaa tuzo Februari first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Kocha wa timu ya Simba, Steve Barker au Steve B ametwaa tuzo ya kocha bora wa mwezi Februari wakati mshambuliaji wa Yanga, Laurindo Dilson ‘Depu’ ametwaa tuzo hiyo kwa upande wa mchezaji bora..
Kwa mujibu wa taarifa ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) iliyopatikana Jumatatu Machi 16, 2026, Depu ametwaa tuzo hiyo baada ya kufunga mabao mawili katika mechi mbili na kuiwezesha Yanga kujiimarisha kileleni mwa msimamo wa ligi hiyo.
Katika tuzo hiyo, Depu alikuwa akishindana na Idd Suleiman ‘Nado’ wa Azam FC na Rushine de Reuck wa Simba lakini kamati ya tuzo ikamtangaza Depu kuwa ndiye mshindi.
Kwa upande wa Steve alikuwa akiwania tuzo hiyo na Pedro Concalves wa Yanga na Florent Ibenge wa Azam lakini ushindi wa mechi mbili na sare moja vilitosha kuishawishi kamati kumpa ushindi Steve.
Naye Said Mpuche ambaye ni meneja wa Uwanja wa Isamuhyo amechaguliwa kuwa meneja bora wa uwanja kwa mwezi Februari kwa kufanya vizuri katika miundombinu ya uwanja na katika menejimenti ya matukio uwanjani.
Katika Ligi ya NBC Championship, Ramadhan Karanje wa B19 amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa mwezi Februari wa ligi hiyo baada ya kufunga mabao manne katika mechi tano na kuwashinda Obrey Chirwa wa Kagera Sugar na Tariq Seif wa Polisi Tanzania.
Kwa upande wa makocha kwenye ligi hiyo hiyo, Mbwana Makata wa Polisi Tanzania ametwaa tuzo hiyo baada ya kuiwezesha timu yake kushinda mechi nne na kutoa sare moja akiwashinda Juma Kaseja wa Kagera Sugar na Zubeir Katwila wa Geita Gold.
Mabao bora katika kipindi cha mwezi Februari kwa mujibu wa kamati ya tuzo yamefungwa na Mathew Tegisi (dk ya 89) katika mechi kati ya Pamba na Coatal Union, Shekhan Ibrahim (DK 89) mechi kati ya Yanga na JKT Tanzania na Ismail Mhesa (dk 86) mechi kati ya Mtibwa na Prisons.

The post Kocha Simba atwaa tuzo Februari first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2026/03/17/kocha-simba-atwaa-tuzo-februari/feed/ 0
Steve B kocha mkuu mpya Simba https://www.greensports.co.tz/2025/12/19/steve-b-kocha-mkuu-mpya-simba/ https://www.greensports.co.tz/2025/12/19/steve-b-kocha-mkuu-mpya-simba/#respond Fri, 19 Dec 2025 18:37:10 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=14211 Na mwandishi wetuHatimaye klabu ya soka ya Simba imemtangza rasmi Steve Barker au Steve B (pichani) kuwa kocha mkuu wa timu hiyo ikiwa ni wiki kadhaa zimepita baada ya kutimuliwa kwa Dimitar Pantev.Steve B ambaye kabla ya kutua Simba alikuwa akiinoa timu ya Stellenbosch inayoshiriki Ligi Kuu Afrika Kusini anakabidhiwa jukumu la kuinoa Simba baada […]

The post Steve B kocha mkuu mpya Simba first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Hatimaye klabu ya soka ya Simba imemtangza rasmi Steve Barker au Steve B (pichani) kuwa kocha mkuu wa timu hiyo ikiwa ni wiki kadhaa zimepita baada ya kutimuliwa kwa Dimitar Pantev.
Steve B ambaye kabla ya kutua Simba alikuwa akiinoa timu ya Stellenbosch inayoshiriki Ligi Kuu Afrika Kusini anakabidhiwa jukumu la kuinoa Simba baada ya mambo kwenda kombo chini ya Pantev.
Pantev alitimuliwa Desemba 2 mwaka huu ikiwa ni takriban miezi miwili imepita tangu apewe jukumu hilo na ingawa Simba walimtangaza kama meneja wa timu lakini inadaiwa alikuwa akifanya kazi ya kocha mkuu akisaidiwa na Seleman Matola.
Ujio wa Steve B unakuwa umezima minong’ono iliyotawala katika siku za karibuni kuhusu nani hasa angebeba jukumu hilo tangu kutimuliwa kwa Pantev ambaye alishindwa kufikia matumaini ya mashabiki wa timu hiyo.
Pantev alikabidhiwa jukumu hilo kutoka kwa Fadlu Davids lakini mwenendo wa Simba kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya makundi umekuwa si wa kuridhisha baada ya timu kupoteza mechi mbili za hatua ya makundi.
Steve B ni kocha mwenye heshima Afrika Kusini kutokana na mafanikio aliyojipatia akiwa na Stellenbosch, timu iliyoanzishwa mwaka 2016 na ni yeye aliyeipandisha ligi kuu nchini humo mwaka 2019.
Mwaka jana Steve B aliifikisha timu hiyo nusu fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika na sasa amekabidhia jukumu la kuifundidha Simba bila shaka akibeba matumaini ya kuendelea alipoishia Fadlu Davids.

The post Steve B kocha mkuu mpya Simba first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2025/12/19/steve-b-kocha-mkuu-mpya-simba/feed/ 0