Spurs - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Sat, 02 Dec 2023 15:49:35 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=6.8 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg Spurs - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 Kocha Spurs ajiandaa kusajili Januari https://www.greensports.co.tz/2023/12/02/kocha-spurs-ajiandaa-kusajili-januari/ https://www.greensports.co.tz/2023/12/02/kocha-spurs-ajiandaa-kusajili-januari/#respond Sat, 02 Dec 2023 15:49:34 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=8709 London, EnglandTottenham Hotspurs inajiandaa kujiimarisha kwa usajili wakati wa dirisha dogo la Januari lengo likiwa ni kuimarisha safu ya kiungo ya timu hiyo ambayo inaonekana kuanza kupoteza makali.Kocha wa Spurs, Ange Postecoglou (pichani) amesema timu yake kwa sasa inaandamwa na wachezaji majeruhi akiwamo Rodrigo Bentancur ambaye hivi karibuni aliongeza idadi ya majeruhi katika timu hiyo.Januari […]

The post Kocha Spurs ajiandaa kusajili Januari first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

London, England
Tottenham Hotspurs inajiandaa kujiimarisha kwa usajili wakati wa dirisha dogo la Januari lengo likiwa ni kuimarisha safu ya kiungo ya timu hiyo ambayo inaonekana kuanza kupoteza makali.
Kocha wa Spurs, Ange Postecoglou (pichani) amesema timu yake kwa sasa inaandamwa na wachezaji majeruhi akiwamo Rodrigo Bentancur ambaye hivi karibuni aliongeza idadi ya majeruhi katika timu hiyo.
Januari mwakani timu hiyo inaweza kujikuta pabaya zaidi kwa kuwakosa nyota wake ambao watakuwa wakiziwakilisha timu zao za taifa kwenye fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika nchini Ivory Coast.
Spurs iliuanza msimu huu vizuri na kuanza kutajwa kutoa upinzani katika mbio za kulibeba taji la Ligi Kuu England (EPL) baada ya kushika usukani kabla ya kuanza kupotea njia kutokana na vipigo katika mechi za hivi karibuni.
Timu hiyo ilijikuta pagumu baada ya kukubali kichapo cha mabao 4-1 mbele ya Chelsea lakini pia ikalala kwa mabao 2-1 mbele ya Wolverhampton Wanderers kabla ya Aston Villa nao kuwachapa 2-1.
Matokeo hayo yameibua hofu na sasa kocha Postecoglou anaamini upo umuhimu wa kukiimarisha kikosi chake kabla mambo hayajaendelea kuwa mabaya.
Kwa sasa Spurs inashika nafasi ya tano ikiwa na pointi 26 baada ya kucheza mechi 13 na Jumapili kesho itakuwa na kibarua kigumu kwenye dimba la Etihad dhidi ya Man City, mabingwa watetezi EPL.

The post Kocha Spurs ajiandaa kusajili Januari first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/12/02/kocha-spurs-ajiandaa-kusajili-januari/feed/ 0
Kocha Spurs abeba tuzo ya mwezi https://www.greensports.co.tz/2023/10/14/kocha-spurs-abeba-tuzo-ya-mwezi/ https://www.greensports.co.tz/2023/10/14/kocha-spurs-abeba-tuzo-ya-mwezi/#respond Sat, 14 Oct 2023 20:57:55 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=8109 London, EnglandKocha wa Tottenham Hotspur, Ange Postecoglou (pichani) ameweka historia kwa kutwaa kwa mara ya pili tuzo ya kocha bora wa mwezi na kuwa kocha wa kwanza katika Ligi Kuu England kubeba tuzo hiyo katika miezi yake miwili ya kwanza.Postecoglou, 58, kocha kutoka Australia ameiongoza vyema Spurs na kuipaisha juu katika msimamo wa EPL akiwa […]

The post Kocha Spurs abeba tuzo ya mwezi first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

London, England
Kocha wa Tottenham Hotspur, Ange Postecoglou (pichani) ameweka historia kwa kutwaa kwa mara ya pili tuzo ya kocha bora wa mwezi na kuwa kocha wa kwanza katika Ligi Kuu England kubeba tuzo hiyo katika miezi yake miwili ya kwanza.
Postecoglou, 58, kocha kutoka Australia ameiongoza vyema Spurs na kuipaisha juu katika msimamo wa EPL akiwa na rekodi ya kutopoteza hata mechi moja kati ya nane, akishinda sita na kutoka sare mara mbili.
Kocha wa mwisho kubeba tuzo hiyo mara mbili mfululizo ni Jurgen Klopp wa Liverpool ambaye alifanya hivyo msimu wa 2019-20, msimu ambao Livepool pia ilibeba taji la EPL.
Huu ni msimu wa kwanza kwa Postecoglou na Spurs ambapo alikabidhiwa jukumu hilo kutoka kwa kocha Mtaliano, Antonio Conte ambaye aliingia katika mzozo na wamiliki wa klabu hiyo kabla ya kujikuta akilazimika kuachia ngazi.
Mambo hata yanaonekana kuwa mazuri kwa Spurs msimu huu kwani mbali na Postecoglou, nahodha wa timu hiyo, Son Heung-min alitwaa tuzo ya mchezaji bora wa mwezi Septemba.

The post Kocha Spurs abeba tuzo ya mwezi first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/10/14/kocha-spurs-abeba-tuzo-ya-mwezi/feed/ 0
Kocha Spurs haipendi VAR https://www.greensports.co.tz/2023/10/02/kocha-spurs-haipendi-var/ https://www.greensports.co.tz/2023/10/02/kocha-spurs-haipendi-var/#respond Mon, 02 Oct 2023 07:13:50 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=7918 London, EnglandKocha wa Tottenham Hotspur, Ange Postecoglou (pichani) amesema hapendi matumizi ya VAR kwa kuwa yanasababisha utata licha ya timu yake kunufaika na makosa ya mfumo huo katika mechi yao na Liverpool Jumamosi.Jopo la waamuzi walikiri kwamba yalifanyika makosa kukataa bao la Liverpool lililofungwa na winga, Luis Díaz kipindi cha kwanza na mwishowe ni Spurs […]

The post Kocha Spurs haipendi VAR first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

London, England
Kocha wa Tottenham Hotspur, Ange Postecoglou (pichani) amesema hapendi matumizi ya VAR kwa kuwa yanasababisha utata licha ya timu yake kunufaika na makosa ya mfumo huo katika mechi yao na Liverpool Jumamosi.
Jopo la waamuzi walikiri kwamba yalifanyika makosa kukataa bao la Liverpool lililofungwa na winga, Luis Díaz kipindi cha kwanza na mwishowe ni Spurs iliyokuwa nyumbani ambayo ilitoka na ushindi wa mabao 2-1.
“Nafikiri nipo kwenye rekodi kwa kauli yangu ya kwamba sikuwahi kuwa shabiki wa VAR tangu kuanza kwake kutumika,” alisema Postecoglou, kocha wa zamani wa Celtic.
“Si kwa sababu nyingine yoyote zaidi ya fikra kwamba inasababisha utata katika baadhi ya maeneo ya mchezo ambayo nilidhani yalikuwa wazi siku za nyuma lakini naweza kuona kwamba ni teknolojia ambayo ingekuja tu, ni lazima tukabiliane nayo,” alisema Postecoglou mbele ya waandishi wa habari.
“Mchezo wa soka una historia ya kugubikwa na maamuzi ya waamuzi ambayo hayawi sahihi lakini sote tuliyakubali kama sehemu ya mchezo kwa sababu tunafanya kazi na binadamu,” alisema Postecoglou.

“Nafikiri watu walikuwa na fikra zisizo sahihi kwamba VAR haitokuwa na makosa, sidhani kama kuna teknolojia ya hivyo kwa sababu mambo mengi katika mchezo wetu hayako sahihi, ni suala la tafsiri na yote yanafanywa kwa uwezo wa binadamu,” alisema Postecoglou.


Katika mechi hiyo Joel Matip wa Liverpool alijifunga katika dakika za lala salama wakati timu yake ikiwa na wachezaji tisa uwanjani baada ya kutolewa kwa kiungo Curtis Jones na winga Diogo Jota.
Akizungumzia matokeo hayo, kocha wa Liverpool, Jurgen Klopp alisema kwamba uamuzi wa VAR kuwanyima bao ulibadili kwa kiasi kikubwa mwelekeo na kasi ya mchezo.

The post Kocha Spurs haipendi VAR first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/10/02/kocha-spurs-haipendi-var/feed/ 0
Kane kurudishwa Spurs? https://www.greensports.co.tz/2023/09/20/kane-kurudishwa-spurs/ https://www.greensports.co.tz/2023/09/20/kane-kurudishwa-spurs/#respond Wed, 20 Sep 2023 12:54:40 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=7809 London, EnglandMwenyekiti wa klabu ya Tottenham Hotspur, Daniel Levy amesema katika mkataba wa mshambuliaji wa Bayern Munich, Harry Kane kuna kipengele kinachowapa nafasi wao kumsajili kwa mara nyingine.Kwa mujibu wa chanzo kimoja cha habari, Levy ametoa kauli hiyo ambayo haikufahamika kwa wengi hapo kabla ingawa hakusema moja kwa moja kama wana nia ya kukitumia kifungu […]

The post Kane kurudishwa Spurs? first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

London, England
Mwenyekiti wa klabu ya Tottenham Hotspur, Daniel Levy amesema katika mkataba wa mshambuliaji wa Bayern Munich, Harry Kane kuna kipengele kinachowapa nafasi wao kumsajili kwa mara nyingine.
Kwa mujibu wa chanzo kimoja cha habari, Levy ametoa kauli hiyo ambayo haikufahamika kwa wengi hapo kabla ingawa hakusema moja kwa moja kama wana nia ya kukitumia kifungu hicho kumrudisha katika klabu hiyo mshambuliaji huyo ambaye pia ni nahodha wa timu ya England.
Kane, 30, aliihama Tottenham mwanzoni mwa msimu huu akiacha rekodi ya kuwa mfungaji bora wa wakati wote katika historia ya timu hiyo na kujiunga Bayern Munich ambapo pia ameanza kutema cheche kwa kupachika mabao.
Uhamisho wa mchezaji huyo kwenda Bayern ulikutana na vikwazo vya hapa na pale, sababu kubwa ikiwa ni Spurs kusita kumuachia mshambuliaji huyo ambaye pia alikuwa akiwindwa na klabu za Man United na Real Madrid.
Real Madrid ilishatangaza dau la Pauni 60 milioni lakini Kane ambaye pia alikuwa akiwindwa na PSG tangu awali alisema kwamba angependa zaidi kujiunga na Bayern.
Kwa upande wa Man United ilikuwa ikivizia kumsajili mshambuliaji huyo mara baada ya kumaliza mkataba wake na Tottenham na hivyo kumpata akiwa mchezaji huru.

The post Kane kurudishwa Spurs? first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/09/20/kane-kurudishwa-spurs/feed/ 0
Kane apania kwenda Bayern https://www.greensports.co.tz/2023/07/12/kane-apania-kwenda-bayern/ https://www.greensports.co.tz/2023/07/12/kane-apania-kwenda-bayern/#respond Wed, 12 Jul 2023 05:54:55 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=6910 Munich, UjerumaniMshambuliaji wa Tottenham Hotspur, Harry Kane amepania kujiunga na klabu ya Bayern Munich ya Ujerumani ambayo inadaiwa kujipanga kuwasilisha ofa ya mchezaji huyo kwa mara ya tatu.Tayari Bayern imeshawasilisha ofa mbili za kumtaka nahodha huyo wa Engand huku ofa ya pili ikidaiwa kufikia Dola 103 milioni na sasa huenda ofa ya tatu ikaboreshwa zaidi.Kane […]

The post Kane apania kwenda Bayern first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Munich, Ujerumani
Mshambuliaji wa Tottenham Hotspur, Harry Kane amepania kujiunga na klabu ya Bayern Munich ya Ujerumani ambayo inadaiwa kujipanga kuwasilisha ofa ya mchezaji huyo kwa mara ya tatu.
Tayari Bayern imeshawasilisha ofa mbili za kumtaka nahodha huyo wa Engand huku ofa ya pili ikidaiwa kufikia Dola 103 milioni na sasa huenda ofa ya tatu ikaboreshwa zaidi.
Kane ambaye pia anadaiwa kuwindwa na PSG na Real Madrid, atakuwa mchezaji huru mwishoni mwa msimu ujao wa 2023-24, inadaiwa pia amepania kuhakikisha anajiunga na wababe hao wa Ujerumani.
Habari za ndani zinadai kwamba kocha wa Bayern, Thomas Tuchel alikutana na mchezaji huyo jijini London wiki chache zilizopita na Kane mwenyewe alivutiwa na mpango huo akiamini ataenda kubeba mataji na timu hiyo.
Inadaiwa kwamba kaka wa mchezaji huyo ambaye pia ndiye wakala wake, katika siku za karibuni amekuwa na mazungumzo na mabosi wa Bayern yaliyojadili uhamisho wa mchezaji huyo.
Wakati Bayern ikiendelea na harakati hizo, kocha mpya wa Spurs, Ange Postecoglou alisema kwamba hawezi kuwa na uhakika wa kuwa na mchezaji huyo ingawa angependa kufanya naye mazungumzo mara baada ya mchezaji huyo kumaliza mapumziko na angependa abaki katika timu hiyo.
Habari nyingine zinadai kwamba pamoja na Bayern kumtaka Kane lakini klabu hiyo iko makini katika ofa itakayotolewa huku mabosi Spurs wakipania kuvuna pesa ndefu kupitia mshambuliaji huyo mwenye rekodi za kuvutia za mabao.

The post Kane apania kwenda Bayern first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/07/12/kane-apania-kwenda-bayern/feed/ 0
Kocha Spurs amtaka Kane https://www.greensports.co.tz/2023/07/11/kocha-spurs-amtaka-kane/ https://www.greensports.co.tz/2023/07/11/kocha-spurs-amtaka-kane/#respond Tue, 11 Jul 2023 05:35:09 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=6895 London, EnglandKocha mpya wa Tottenham Hotspur, Ange Postecoglou amesema anataka mshambuliaji, Harry Kane anayewindwa na Bayern Munich abaki katika timu hiyo ingawa bado hajapewa uhakika wa jambo hilo.Habari za ndani zinadai kwamba Kane ambaye mkataba wake na Spurs unafikia ukomo mwakani ameshaarifiwa kwamba hauzwi lakini mwenyewe anadaiwa kutaka kusaka changamoto mpya nje ya timu hiyo.Awali […]

The post Kocha Spurs amtaka Kane first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

London, England
Kocha mpya wa Tottenham Hotspur, Ange Postecoglou amesema anataka mshambuliaji, Harry Kane anayewindwa na Bayern Munich abaki katika timu hiyo ingawa bado hajapewa uhakika wa jambo hilo.
Habari za ndani zinadai kwamba Kane ambaye mkataba wake na Spurs unafikia ukomo mwakani ameshaarifiwa kwamba hauzwi lakini mwenyewe anadaiwa kutaka kusaka changamoto mpya nje ya timu hiyo.
Awali Kane alikuwa akiwindwa na klabu za PSG, Real Madrid, Man United ambayo baadaye ilijitoa pamoja na Bayern Munich ambayo tayari imetangaza kuwa tayari kutoa Pauni 70 milioni.
Akizungumza katika mkutano wa kwanza na waaandishi wa habari tangu ajiunge na Spurs, Postecoglou, alisema Kane ni mchezaji muhimu na angependa awe naye katika safari ya mafanikio ya Spurs.
“Harry tayari ni mtu muhimu katika historia ya klabu hii, ni mmoja wa wachezaji bora duniani, nataka aendelee kuwa hapa na nataka kuipa mafanikio klabu hii, naamini na yeye anataka hivyo hivyo,” alisema kocha huyo.
Jumatano hii Kane anatarajia kuanza mazoezi na kikosi cha Spurs kujiandaa na msimu mpya wa 2023-24 na Postecoglou alisema kwamba angependa kuzungumza na mshambuliaji huyo.

“Ninachotaka ni kujitambulisha na nataka afahamu ninachohitaji kifanyike ili kuifanya hii klabu ya soka iwe na mafanikio na baada ya hapo tutaenda mazoezini,” alisema Postecoglou.


Postecoglou alipewa majukumu ya kuinoa Spurs Juni mwaka huu baada ya Antonio Conte kutimuliwa, awali alikuwa akiinoa Celtic ya Scotland ambayo katika msimu wa 2022-23 aliiwezesha kutwaa mataji ya ligi kuu, taji la ligi na taji la Scotland.

The post Kocha Spurs amtaka Kane first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/07/11/kocha-spurs-amtaka-kane/feed/ 0
Postecoglou kocha mpya Spurs https://www.greensports.co.tz/2023/06/06/postecoglou-kocha-mpya-spurs/ https://www.greensports.co.tz/2023/06/06/postecoglou-kocha-mpya-spurs/#respond Tue, 06 Jun 2023 20:33:29 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=6490 London, EnglandTottenham Hotspur imethibitisha kuwa Ange Postecoglou ndiye kocha mpya wa timu hiyo baada ya kusaini mkataba wa miaka minne na hivyo kuwa kocha wa kwanza kutoka Australia kuinoa timu ya Ligi Kuu England (EPL).Postecoglou (pichani) mwenye umri wa miaka 57 ambaye hapo kabla alikuwa akiinoa Celtic ya Scotland, ataanza rasmi kazi katika klabu hiyo […]

The post Postecoglou kocha mpya Spurs first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

London, England
Tottenham Hotspur imethibitisha kuwa Ange Postecoglou ndiye kocha mpya wa timu hiyo baada ya kusaini mkataba wa miaka minne na hivyo kuwa kocha wa kwanza kutoka Australia kuinoa timu ya Ligi Kuu England (EPL).
Postecoglou (pichani) mwenye umri wa miaka 57 ambaye hapo kabla alikuwa akiinoa Celtic ya Scotland, ataanza rasmi kazi katika klabu hiyo Julai Mosi huku mwenyekiti wa Spurs, Daniel Levy akiamini kocha huyo atafanya kazi yake vizuri.
“Ange atabadili mtazamo na kwa haraka atakuwa na timu yenye mfumo wa kushambulia, ana rekodi nzuri ya kuwaendeleza wachezaji na mwenye uelewa kuhusu umuhimu wa muunganiko wa kuanzia kwenye akademi,” alisema Levy katika taarifa yake.

“Kila kitu ni muhimu kwa klabu yetu, tumefurahishwa kwa Ange kuungana nasi wakati huu tukijiandaa kwa ajili ya msimu ulio mbele yetu,” aliongeza Levy.


Habari za Alhamisi iliyopita zilidai kwamba Spurs iliwasiliana na mabosi wa Celtic kuhusu kumtaka kocha huyo na mazungumzo yakaenda vizuri jana Jumatatu na kwa haraka baada ya Postecoglou mwenyewe kuonesha shauku ya kutaka kuinoa timu ya EPL.
Postecoglou ambaye ameiwezesha Celtic kubeba mataji matatu ya ndani msimu huu, anarithi mikoba ya kocha Mtaliano Antonio Conte ambaye mambo yalimshinda katika klabu hiyo na kuamua kuondoka.

The post Postecoglou kocha mpya Spurs first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/06/06/postecoglou-kocha-mpya-spurs/feed/ 0
Mourinho na Spurs mbali mbali https://www.greensports.co.tz/2023/05/26/mourinho-na-spurs-mbali-mbali/ https://www.greensports.co.tz/2023/05/26/mourinho-na-spurs-mbali-mbali/#respond Fri, 26 May 2023 19:30:09 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=6302 Roma, ItaliaKocha wa AS Roma ya Italia, Jose Mourinho amesema kwamba Tottenham Hotspur ni klabu pekee ambayo amewahi kuwa kocha wake lakini hana mawasiliano nayo baada ya kuondoka kwake.Mourinho ambaye pia amewahi kuzinoa klabu za Chelsea, Inter Milan, Real Madrid, Man United na FC Porto, alitimuliwa Spurs Aprili 2021 ikiwa ni miezi 17 baada ya […]

The post Mourinho na Spurs mbali mbali first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Roma, Italia
Kocha wa AS Roma ya Italia, Jose Mourinho amesema kwamba Tottenham Hotspur ni klabu pekee ambayo amewahi kuwa kocha wake lakini hana mawasiliano nayo baada ya kuondoka kwake.
Mourinho ambaye pia amewahi kuzinoa klabu za Chelsea, Inter Milan, Real Madrid, Man United na FC Porto, alitimuliwa Spurs Aprili 2021 ikiwa ni miezi 17 baada ya kupewa kibarua cha kuinoa timu hiyo.
“Ni matumaini yangu kwamba mashabiki wa Tottenham hawatanichukulia vibaya lakini klabu pekee katika maisha yangu ya kuwa kocha ambayo nimeendelea kutovutiwa nayo ni Tottenham,” alisema Mourinho.
“Labda kwa sababu uwanja ulikuwa hauna mashabiki kipindi cha korona, labda kwa sababu Bwana Levy (mwenyekiti wa Tottenham Daniel Levy) hakunipa nafasi ya mwisho ya kushinda kombe.”
Kauli za Mourinho zimekuja siku chache baada ya jana Alhamisi, kocha wa Feyenoord ya Uholanzi, Arne Slot kukataa kibarua cha kuinoa Spurs.
Mourinho aliulizwa kuhusu mambo yake ya baadaye na Roma ambapo alisema ataendelea kuwa na uhusiano wa moja kwa moja na klabu hiyo kama ilivyo kwa klabu nyingine alizowahi kuzifundisha.
“Tutaendelea kuwa na mawasiliano kwa wakati wote, ni kama ilivyo kwa klabu zangu nyingine za hapo kabla, ukiacha klabu ya Bwana Levy,” alisema Mourinho.

“Hiyo ndiyo klabu pekee, ukiacha hiyo (Spurs) nyingine za FC Porto, Chelsea, Inter Milan, Manchester United, Real Madrid, klabu zote hizo najiona niko pamoja nazo, watu wanaweza kusema huwezi kupenda klabu zote, ndio mimi nazipenda klabu zote hizo,” aliongeza Mourinho.


Mourinho alitimuliwa Spurs wiki moja kabla ya timu hiyo kucheza mechi ya fainali ya Kombe la Ligi dhidi ya Man United, mechi ambayo Spurs ililala kwa bao 1-0 wakati huo ikinolewa na kocha wa muda, Ryan Mason.
Baada ya kutimuliwa Spurs, Mourinho aliibukia AS Roma ambayo msimu uliopita aliiwezesha kubeba taji la michuano mipya ya klabu barani Ulaya ya Europa Conference Ligi na kwa sasa Roma inasubiri kuumana na Sevilla katika mechi ya fainali ya Europa Ligi itakayopigwa Mei 31.
Mambo yakienda vizuri, Mourinho anaweza kutangaza taji lake la pili la Ulaya na klabu hiyo. Hadi sasa ana rekodi ya mataji matano Ulaya, mawili ya Ligi ya Mabingwa, mawili ya Europa Ligi na moja la Europa Conference Ligi.

The post Mourinho na Spurs mbali mbali first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/05/26/mourinho-na-spurs-mbali-mbali/feed/ 0
Slot akataa kumrithi Conte Spurs https://www.greensports.co.tz/2023/05/25/slot-akataa-kumrithi-conte-spurs/ https://www.greensports.co.tz/2023/05/25/slot-akataa-kumrithi-conte-spurs/#respond Thu, 25 May 2023 09:13:56 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=6279 London, EnglandKocha Arne Slot (pichani) amekataa kumrithi Antonio Conte katika klabu ya Tottenhham Hostspur akisema kwamba anataka kubaki katika klabu yake ya sasa ya Feyenoord ya Uholanzi.Slot aliyejiunga na Feyenoord Desemba 2020 akitokea, AZ Alkmaar, katika siku za karibuni amekuwa akihusishwa na mipango ya kuhamia Spurs baada ya klabu hiyo kuachana na Conte, Machi mwaka […]

The post Slot akataa kumrithi Conte Spurs first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

London, England
Kocha Arne Slot (pichani) amekataa kumrithi Antonio Conte katika klabu ya Tottenhham Hostspur akisema kwamba anataka kubaki katika klabu yake ya sasa ya Feyenoord ya Uholanzi.
Slot aliyejiunga na Feyenoord Desemba 2020 akitokea, AZ Alkmaar, katika siku za karibuni amekuwa akihusishwa na mipango ya kuhamia Spurs baada ya klabu hiyo kuachana na Conte, Machi mwaka huu.
Kocha huyo ambaye ameiwezesha Feyenoord kubeba taji la Ligi Kuu Uholanzi maarufu Eredivisie, jana Jumatano alifanya mazungumzo na mabosi wake, mazungumzo yaliyolenga kumuongezea mkataba.
“Nimekuwa nikisikia uvumi kuhusu upande mwingine kunihitaji, kwanza nashukuru kwa hilo lakini ninachotaka kwa sasa ni kubaki Feyenoord na kuendelea na kazi tuliyoianza mwaka jana,” alisema.

“Sijawahi na hakujawahi kuwa na mazungumzo ya kuhama na kikao cha jana (Jumatano) kilikuwa maalum kwa ajili ya kuongeza mkataba, mazungumzo yote na klabu wakati wote yamehusu jambo hilo, napiga hesabu za msimu ujao na Feyenoord,” alisema Slot.


Mara baada ya Spurs kuachana na Conte, Cristian Stellini alipewa jukumu la kuinoa timu hiyo akiwa kocha wa muda lakini alitimuliwa baada ya mechi nne na nafasi yake kukabidhiwa, Ryan Mason huku uvumi wa kocha ajae ukiendelea na jina la Slot likitajwa mara kwa mara.
Spurs imekuwa na mwenendo mbaya kwenye Ligi Kuu England (EPL) hasa katika mechi za mwisho ikishindwa kupambana katika ‘top four’, kwa sasa inashika nafasi ya nane na Jumapili itacheza mechi yake ya mwisho ya EPL dhidi ya Leeds United.
Makocha wengine ambao wamekuwa wakihusishwa na Spurs ni kocha wa zamani wa Bayern Munich, Julian Nagelsmann, Roberto de Zerbi wa Brighton na Vincent Kompany wa Burnley.
Slot mwenye umri wa miaka 44, Spurs inakuwa klabu ya pili ya EPL kuikataa, awali alihusishwa na mipango ya kuinoa Leeds baada ya kutimuliwa kwa Jesse Marsch lakini aliikataa timu hiyo.

The post Slot akataa kumrithi Conte Spurs first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/05/25/slot-akataa-kumrithi-conte-spurs/feed/ 0
Spurs yamrudia Nagelsmann https://www.greensports.co.tz/2023/05/21/spurs-yamrudia-nagelsmann/ https://www.greensports.co.tz/2023/05/21/spurs-yamrudia-nagelsmann/#respond Sun, 21 May 2023 17:51:10 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=6247 London, EnglandKlabu ya Tottenhham Hotspur imeanza mazungumzo kwa mara nyingine na kocha wa zamani wa Bayern Munich, Julian Nagelsmann ili ainoe timu hiyo ambayo hivi karibuni iliachana na Antonio Conte.Nagelsmann (pichani) hata hivyo ametaka kabla ya kukubali kibarua hicho ajue nani atakuwa mkurugenzi wa michezo wa klabu hiyo ambayo kwa sasa mambo yake si mazuri […]

The post Spurs yamrudia Nagelsmann first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

London, England
Klabu ya Tottenhham Hotspur imeanza mazungumzo kwa mara nyingine na kocha wa zamani wa Bayern Munich, Julian Nagelsmann ili ainoe timu hiyo ambayo hivi karibuni iliachana na Antonio Conte.
Nagelsmann (pichani) hata hivyo ametaka kabla ya kukubali kibarua hicho ajue nani atakuwa mkurugenzi wa michezo wa klabu hiyo ambayo kwa sasa mambo yake si mazuri kwenye Ligi Kuu England (EPL).
Hii si mara ya kwanza kwa Spurs kuhusishwa na kocha huyo ingawa kinachoonekana sasa ni kwamba klabu hiyo imeongeza nguvu katika mpango huo na matumaini ya kumpata kocha huyo ni makubwa.
Mambo si mazuri kwa Spurs kwani imetoka katika mbio za kuwania nafasi ya kushiriki Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao ikiiacha vita hiyo kwa klabu za Man United, Newcastle na Liverpool.
Timu hiyo pia huenda ikakimbiwa na mshambuliaji wake mahiri, Harry Kane ambaye amekuwa akihusishwa na mipango ya kujiunga na klabu kadhaa ikiwamo Man United na PSG ya Ufaransa.
Na ingawa Kane hajaamua atakapoelekea kitendo cha Spurs kutoshiriki Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao ni sababu tosha kwa mshambuliaji huyo ambaye pia ni nahodha wa timu ya England aondoke.

The post Spurs yamrudia Nagelsmann first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/05/21/spurs-yamrudia-nagelsmann/feed/ 0