Southampton - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Sat, 27 May 2023 18:58:42 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=7.0 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg Southampton - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 Novatus Dismas atakiwa Southampton https://www.greensports.co.tz/2023/05/27/novatus-atakiwa-southampton/ https://www.greensports.co.tz/2023/05/27/novatus-atakiwa-southampton/#respond Sat, 27 May 2023 18:56:44 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=6326 London, EnglandBeki wa pembeni, Mtanzania Novatus Dismas anayekipiga katika klabu ya Zulte Waregem ya Ubelgiji anawaniwa na timu za Southampton na Middlesbrough za England.Novatus (pichani juu) ametajwa kuwaniwa na timu hizo kutokana na uwezo anaoendelea kuuonesha tangu ajiunge na Zulte mwanzoni mwa msimu huu akitokea Maccabi Tel Aviv ya Israel.Kwa mujibu wa gazeti la Daily […]

The post Novatus Dismas atakiwa Southampton first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

London, England
Beki wa pembeni, Mtanzania Novatus Dismas anayekipiga katika klabu ya Zulte Waregem ya Ubelgiji anawaniwa na timu za Southampton na Middlesbrough za England.
Novatus (pichani juu) ametajwa kuwaniwa na timu hizo kutokana na uwezo anaoendelea kuuonesha tangu ajiunge na Zulte mwanzoni mwa msimu huu akitokea Maccabi Tel Aviv ya Israel.
Kwa mujibu wa gazeti la Daily Mail la Uingereza, Southampton inayoshiriki Ligi Kuu England (EPL) inamuwania mchezaji huyo ikichuana na Middlesbrough.
Middlesbrough kwa sasa inapambana katika Ligi ya Championship wakati mambo si mazuri kwa Southampton ambayo tayari imeshuka daraja na inasubiri kucheza Championship msimu ujao.
Novatus mwenye umri wa miaka 20 ambaye ni kiungo mkabaji, akicheza kwa ufasaha pia kama beki wa pembeni, beki wa kati na kiungo wa kushoto, imeelezwa kuwa uwezo wake huo pia umezivutia timu hizo.
Licha ya timu yake kushuka daraja lakini bado Dismas ameendelea kuzivutia klabu kubwa kutokana na kiwango anachokionesha hata anapokuwa kwenye majukumua ya timu ya taifa, Taifa Stars.

The post Novatus Dismas atakiwa Southampton first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/05/27/novatus-atakiwa-southampton/feed/ 0
Southampton yashuka daraja https://www.greensports.co.tz/2023/05/13/southampton-yashuka-daraja/ https://www.greensports.co.tz/2023/05/13/southampton-yashuka-daraja/#respond Sat, 13 May 2023 20:14:04 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=6148 London, EnglandKlabu ya Southampton leo Jumamosi imehitimisha miaka yake 11 kwenye Ligi Kuu England (EPL) kwa kushuka daraja baada ya kukubali kipigo cha nyumbani cha mabao 2-0 mbele ya Fulham.Fulham walipata bao lao la kwanza dakika ya 48 lililofungwa na Carlos Vinicius kabla ya Alksandar Mitrovic hajamalizia bao la pili dakika ya 72 na kuhitimisha […]

The post Southampton yashuka daraja first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

London, England
Klabu ya Southampton leo Jumamosi imehitimisha miaka yake 11 kwenye Ligi Kuu England (EPL) kwa kushuka daraja baada ya kukubali kipigo cha nyumbani cha mabao 2-0 mbele ya Fulham.
Fulham walipata bao lao la kwanza dakika ya 48 lililofungwa na Carlos Vinicius kabla ya Alksandar Mitrovic hajamalizia bao la pili dakika ya 72 na kuhitimisha safari ya Southampton katika EPL.
Kwa Mitrovic bao hilo ni la 12 msimu huu na linakuwa na maana kubwa kwani hiyo ndio mechi yake ya kwanza baada ya kufungiwa mechi nane kwa kosa la kumsukuma mwamuzi Chris Kavanagh.
Mechi hiyo ilikuwa muhimu kwa Southampton kushinda ili walau kufufua matumaini ya kuendelea kucheza EPL msimu ujao lakini kwa hali ilivyo hata wakishinda mechi mbili zilizobakia watafikisha pointi 30 ambazo haziwezi kuwasaidia wasiwe moja ya timu zinazoshuka daraja.
Kwa maana hiyo, Southampton msimu ujao wa 2023-24 itaanza rasmi kushiriki ligi ya Championship ambayo mara ya mwisho ilishiriki mwaka 2012.
Matokeo ya mechi za EPL zilizochezwa leo Jumamosi ni kama ifuatavyo…
Leeds 2-2 Newcastle
Aston Villa 2-1 Tottenham
Chelsea 2-2 Nottm Forest
Crystal Palace 2-0 Bournemouth
Man Utd 2-0 Wolves
Southampton 0-2 Fulham

The post Southampton yashuka daraja first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/05/13/southampton-yashuka-daraja/feed/ 0