Skudu - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Wed, 05 Jun 2024 17:59:53 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=7.0.4 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg Skudu - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 Skudu aelekea APR ya Rwanda https://www.greensports.co.tz/2024/06/05/skudu-aelekea-apr-ya-rwanda/ https://www.greensports.co.tz/2024/06/05/skudu-aelekea-apr-ya-rwanda/#respond Wed, 05 Jun 2024 17:59:52 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=11237 Na mwandishi wetuImeelezwa kuwa Klabu ya APR ya Rwanda iko kwenye hatua nzuri za kuinasa saini ya nyota wa Yanga SC, Mahaltse Makudubela ‘Skudu’ raia wa Afrika kusini kuelekea msimu ujao.APR ambao watashiriki michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kuwa mabingwa wa Rwanda, wameonesha kuvutiwa na huduma ya Skudu aliyetua Yanga msimu wa […]

The post Skudu aelekea APR ya Rwanda first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Imeelezwa kuwa Klabu ya APR ya Rwanda iko kwenye hatua nzuri za kuinasa saini ya nyota wa Yanga SC, Mahaltse Makudubela ‘Skudu’ raia wa Afrika kusini kuelekea msimu ujao.
APR ambao watashiriki michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kuwa mabingwa wa Rwanda, wameonesha kuvutiwa na huduma ya Skudu aliyetua Yanga msimu wa 2023-24 wakiamini atakua sehemu ya msaada kwenye michuano hiyo.
Licha ya mitandao mbalimbali nchini Rwanda kufafanua kuhusu dili hilo lakini pia klabu iliyopanda daraja Afrika Kusini, Magesi FC inatajwa kumhitaji Skudu ambaye mkataba wake na Yanga unafikia ukingoni mwisho wa msimu huu.
Duru mbalimbali zinaeleza kuwa maisha ya Skudu Yanga yamefika mwisho na yumo kwenye orodha ya watakaoachwa katika kikosi hicho kwani amekuwa hapati nafasi ya mara kwa mara chini ya kocha Muargentina, Miguel Gamondi.
Skudu aliyewahi kukipiga Orlando Pirates, Chippa United, Platinum Stars, alisajiliwa Yanga akitokea Marumo Gallants ya Afrika Kusini na kukabidhiwa urithi wa jezi namba sita iliyokuwa ikivaliwa na Feisal Salum ‘Fei Toto’ aliyetimkia Azam FC.

The post Skudu aelekea APR ya Rwanda first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/06/05/skudu-aelekea-apr-ya-rwanda/feed/ 0
Skudu akiri ligi ngumu https://www.greensports.co.tz/2023/12/19/skudu-akiri-ligi-ngumu/ https://www.greensports.co.tz/2023/12/19/skudu-akiri-ligi-ngumu/#respond Mon, 18 Dec 2023 21:03:07 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=8931 Na mwandishi wetuLicha ya winga wa Yanga, Skudu Makudubela (pichani) kukiri kuwa Ligi ya Tanzania ni ngumu lakini ameahidi kuendeleza moto wa kufunga mabao msimu huu.Skudu amezungumza hayo baada ya juzi kufanikiwa kuifungia Yanga bao la kwanza tangu atue Jangwani mwanzoni mwa msimu huu, walipoumana na Mtibwa Sugar kwenye Uwanja wa Azam Complex, Dar es […]

The post Skudu akiri ligi ngumu first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Licha ya winga wa Yanga, Skudu Makudubela (pichani) kukiri kuwa Ligi ya Tanzania ni ngumu lakini ameahidi kuendeleza moto wa kufunga mabao msimu huu.
Skudu amezungumza hayo baada ya juzi kufanikiwa kuifungia Yanga bao la kwanza tangu atue Jangwani mwanzoni mwa msimu huu, walipoumana na Mtibwa Sugar kwenye Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam na kuibuka na ushindi wa mabao 4-1.
“Ligi ya Tanzania ni nzuri na ina ushindani mkubwa sana, nafikiri kila timu inayocheza na Yanga inapambana kwa kadri iwezavyo kuonesha kuwa mshindani hivyo kila.mechi kwetu tunahitaji kucheza kwa bora wa hali ya juu.

“Nashukuru Mungu kufunga bao la kwanza, haikuwa kitu rahisi kwa kweli maana pia ilikuwa mechi yangu ya kwanza nacheza kwa dakika 90 lakini nimefurahi kufunga na natazamia kufunga zaidi katika siku za usoni msimu huu,” alisema Skudu.


Winga huyo raia wa Afrika Kusini aliyewahi kuzitumikia Orlando Pirates, Mamelodi Sundowns, Chippa United na nyinginezo, ametua Yanga akitokea Marumo Gallants.
Skudu bado anapambana kutafuta namba ya kudumu kwenye kikosi cha kwanza cha Yanga kutokana na ushindani uliopo kwenye kikosi hicho licha ya ufundi alionao.

The post Skudu akiri ligi ngumu first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/12/19/skudu-akiri-ligi-ngumu/feed/ 0
Morrison shabiki namba moja wa Skudu https://www.greensports.co.tz/2023/07/22/morrison-shabiki-namba-moja-wa-skudu/ https://www.greensports.co.tz/2023/07/22/morrison-shabiki-namba-moja-wa-skudu/#respond Sat, 22 Jul 2023 09:44:01 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=7069 Na mwandishi wetuAliyekuwa winga wa Yanga, Bernard Morrison amesema yeye ni shabiki namba moja wa winga mpya wa Yanga, Mahlatse Makudubela ‘Skudu’ na anasubiri kwa hamu kuona Skudu atakavyowaonesha Watanzania vitu vya mpira ambavyo hata yeye alifundishwa na winga huyo.Skudu aliyesajiliwa na Yanga kutoka Marumo Gallants ya Afrika Kusini amewahi kucheza na Morrison wakiwa Orlando […]

The post Morrison shabiki namba moja wa Skudu first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Aliyekuwa winga wa Yanga, Bernard Morrison amesema yeye ni shabiki namba moja wa winga mpya wa Yanga, Mahlatse Makudubela ‘Skudu’ na anasubiri kwa hamu kuona Skudu atakavyowaonesha Watanzania vitu vya mpira ambavyo hata yeye alifundishwa na winga huyo.
Skudu aliyesajiliwa na Yanga kutoka Marumo Gallants ya Afrika Kusini amewahi kucheza na Morrison wakiwa Orlando Pirates, lakini pia wakishabihiana aina ya uchezaji, wote wakitumika kama washambuliaji wa pembeni wakiwa na chenga za maudhi na mbwembwe nyingi.
Morrison ameeleza kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii kwamba anajivunia kuhusika kumleta Skudu katika timu hiyo bila kufafanua namna alivyohusika.
“Namna furaha inavyoonekana, sihitaji kuzunguma sana kwa sasa. Nitazungumza baadaye jinsi gani ninajivunia kukuleta hapa, nenda kaioneshe Tanzania vyote uliyowahi kunifundisha. Mimi shabiki yako namba moja, nakupenda kijana wangu,” aliandika Morrison.
Morrison kuonesha kuwa amevutiwa mno na Skudu kutua Yanga, aliibuka kwenye mazoezi ya kwanza ya mchezaji huyo na Yanga akiwa amevalia jezi namba sita yenye jina Skudu akimkumbatia na kufurahi kwa kumuona.
Yanga iliachana na Morrison baada ya kumalizika kwa msimu wa 2022-23 na sasa duru mbalimbali za michezo zinafafanua kuwa raia huyo wa Ghana anatarajia kutambulishwa na Singida Fountain Gate hivi karibuni.

The post Morrison shabiki namba moja wa Skudu first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/07/22/morrison-shabiki-namba-moja-wa-skudu/feed/ 0
Uzoefu wa Skudu kuibeba Yanga https://www.greensports.co.tz/2023/07/19/uzoefu-wa-skudu-kuibeba-yanga/ https://www.greensports.co.tz/2023/07/19/uzoefu-wa-skudu-kuibeba-yanga/#respond Wed, 19 Jul 2023 12:43:20 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=7022 Na mwandishi wetuYanga jana imemtambulisha winga wa kushoto wa Marumo Gallants ya Afrika Kusini, Mahlatse Makudubela ‘Skudu’ (pichani) huku baadhi ya wadau wakiamini uzoefu wa mchezaji huyo unaweza kuisaidia timu hiyo kimataifa.Wakizungumza na GreenSports kwa nyakati tofauti baadhi ya makocha wazawa; Kenny Mwaisabula, Juma Mwambusi, Charles Mkwasa wamezungumzia usajili huo uliokuwa ukisubiriwa kwa hamu hasa […]

The post Uzoefu wa Skudu kuibeba Yanga first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Yanga jana imemtambulisha winga wa kushoto wa Marumo Gallants ya Afrika Kusini, Mahlatse Makudubela ‘Skudu’ (pichani) huku baadhi ya wadau wakiamini uzoefu wa mchezaji huyo unaweza kuisaidia timu hiyo kimataifa.
Wakizungumza na GreenSports kwa nyakati tofauti baadhi ya makocha wazawa; Kenny Mwaisabula, Juma Mwambusi, Charles Mkwasa wamezungumzia usajili huo uliokuwa ukisubiriwa kwa hamu hasa baada ya kuelezwa ndiye aliyerithi namba ya kiungo Feisal Salum ‘Fei Toto’ aliyetimkia Azam.
Mwaisabula alisema anaamini Yanga imemchagua mchezaji huyo ambaye ni mtu mzima kwa umri, (miaka 33) kutokana na uzoefu kwani anaweza kuwasaidia hasa katika mechi za kimataifa.
Alikwenda mbali akijaribu kumfananisha kwa ubora na mchezaji wa zamani wa Majimaji, Pamba na Yanga aliyefahamika kama Celestine Mbunga ‘Sikinde’ akisema huenda anaweza kuwa kama huyo.
“Kwa namna nilivyomuona akiwa na Marumo Gallants ni kama Celestine Sikinde, alikuwa winga hatari hivyo, kama atafanya kama nilivyomuona atawasaidia mno,”alisema.


Kwa upande wake, kocha wa zamani wa Mbeya City, Yanga na Azam, Juma Mwambusi alisema huenda Yanga kuna kitu walikiona kwa mchezaji huyo kinachoweza kuwasaidia katika michuano watakayoshiriki msimu ujao.
“Hatuwezi kubeza kwa sababu ni lazima tumuone, naamini wamesajili kulingana na taarifa za benchi la ufundi lililopita, na kama kuna kitu walikiona kwake atawasaidia kuziba mapungufu wanayoyaona,” alisema.
Kocha wa zamani wa Taifa Stars, Charles Boniface Mkwasa alisema mchezaji huyo kwanza anatoka katika ligi yenye ushindani nchini Afrika Kusini, hivyo kwa maana nyingine huenda akaleta kitu tofauti katika soka nchini.
Ingawa alieleza wasiwasi wake kuwa licha ya uzuri wa mchezaji huyo lakini umri alionao huenda hatokuwa na muda mrefu katika soka, hivyo akatumika kidogo na Wanajangwani hao.
Naye mchambuzi wa soka nchini, Dominic Salamba alisema Yanga ilikuwa na udhaifu wa kupata mabao ya pembeni hivyo usajili wa winga huyo huenda utasaidia kuongeza kasi na ufungaji wa mabao mengi yanayotoka pembeni.

“Yanga ilikuwa inapata shida kufunga mabao ya pembeni ndio maana hata magoli yao yalikuwa machache na mpira wa kisasa unahitaji magoli mengi yanayotoka pembeni, kwa hiyo ujio wa Skudu pengine ataongeza ubunifu, na pia ana mbinu ambazo wachezaji wengi wa Tanzania hawana,” alisema Salamba..


Skudu amewahi kucheza klabu mbalimbali zikiwemo United FC, Platnum Stars, Golden Arrows, Chippa United, Orlando Pirates, Highland Parks na University of Pretoria.
Huo ni usajili mpya wa tano kwa Yanga baada ya Nickson Kibabage kutoka Singida Fountain Gate, Max Nzengeli kutoka AS Maniema ya DR Congo, Yao Attohoula (Asec Mimosas), Jonas Mkude (Simba) na Gift Fred aliyekuwa SC Villa ya Uganda.

The post Uzoefu wa Skudu kuibeba Yanga first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/07/19/uzoefu-wa-skudu-kuibeba-yanga/feed/ 0