Sir Jim Ratcliffe - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Wed, 22 Oct 2025 19:39:26 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=7.0 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg Sir Jim Ratcliffe - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 Bilionea Man Utd amtetea kocha https://www.greensports.co.tz/2025/10/09/bilionea-man-utd-amtetea-kocha/ https://www.greensports.co.tz/2025/10/09/bilionea-man-utd-amtetea-kocha/#respond Thu, 09 Oct 2025 08:36:25 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=14006 Manchester, EnglandBilionea na mmiliki mwenza wa klabu ya Manchester United, Sir Jim Ratcliffe amesema kocha wa timu hiyo, Ruben Amorim anahitaji miaka mitatu kuthibisha kwamba yeye ni kocha bora.Kauli ya tajiri huyo imekuwa wakati huu ambapo mwezi ujao, Amorim atatimiza mwaka mmoja tangu akabidhiwe jukumu la kuinoa Man United akitokea Sporting ya Ureno lakini timu […]

The post Bilionea Man Utd amtetea kocha first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Manchester, England
Bilionea na mmiliki mwenza wa klabu ya Manchester United, Sir Jim Ratcliffe amesema kocha wa timu hiyo, Ruben Amorim anahitaji miaka mitatu kuthibisha kwamba yeye ni kocha bora.
Kauli ya tajiri huyo imekuwa wakati huu ambapo mwezi ujao, Amorim atatimiza mwaka mmoja tangu akabidhiwe jukumu la kuinoa Man United akitokea Sporting ya Ureno lakini timu imekuwa na matokeo yasiyovutia kiasi cha kuibua uvumi wa kufutwa kazi kwa kocha huyo.
Msimu uliopita Man United ilimaliza Ligi Kuu England (EPL) ikiwa nafasi ya 15, nafasi ambayo ni ya chini mno katika historia ya timu hiyo ikiwakumbusha hali iliyowakuta msimu wa 1973-74, timu hiyo ilipojikuta ikishuka daraja.
Hali imeendelea kuwa mbaya licha ya Pauni milioni 200 kutumika katika usajili na tayari wameshapoteza mechi tatu za EPL msimu huu lakini pia timu hiyo imetolewa kwenye michuano ya Kombe la EFL na timu ya Ligi Two ya Grimsby.
Kabla ya mechi ya wikiendi iliyopita dhidi ya Sunderland, mechi ambayo Man United ilishinda kwa mabao 2-0, habari kubwa ilikuwa ni kuhusu siku za kocha huyo kuhesabika na kwamba angetimuliwa wakati wowote.
Habari hizo zilikolezwa na Amorim mwenyewe ambaye alisema kibarua chake kipo hatarini kutokana na matokeo mabaya akisisitiza kuwa hawezi kamwe kuvumiliwa kama hatokuwa na matokeo mazuri.
Katika mahojiano ya hivi karibuni, Ratcliffe amekuja tofauti na mtazamo wa kumfuta kazi kocha huyo badala yake amesema suala la Amorim haliwasumbui na kufafanua kwamba kocha huyo anahitaji muda zaidi kudhihirisha ubora wake.

“Hana msimu mzuri, Ruben anahitaji kuthibitisha kuwa yeye ni kocha bora kwa kipindi cha miaka mitatu, hivyo ndivyo itakavyokuwa,” alisema Ratcliffe.


Amorim amekuwa akilaumiwa na wachambuzi mbalimbali kwa mfumo anaoutumia wa 4-3-2-1 kwa madai kwamba hauwezi kuipa ushindi timu hiyo lakini mwenyewe ameshikilia msimamo wake akikataa kubadili mfumo.
Kuhusu hoja hiyo, Ratcliffe alisema mazungumzo hayo hayamsumbui lolote akidai kwamba yanatokana na ujinga na zaidi ya hilo kuna wakati havielewi vyombo vya habari.
“Kuna wakati sivielewi vyombo vya habari, wanataka mafanikio ya ghafla, wanadhani ni kama kuwasha taa, wanajua ni kama kubonyeza swichi ya taa na kesho mambo yanakuwa mazuri, huwezi kuendesha klabu kama ya Manchester United kwa kauli za waandishi,” alisema Ratcliffe.

The post Bilionea Man Utd amtetea kocha first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2025/10/09/bilionea-man-utd-amtetea-kocha/feed/ 0
Fernandes ampasha bilionea Man United https://www.greensports.co.tz/2025/03/15/fernandes-ampasha-bilionea-man-united/ https://www.greensports.co.tz/2025/03/15/fernandes-ampasha-bilionea-man-united/#respond Sat, 15 Mar 2025 18:52:58 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=13140 Manchester, EnglandNahodha wa Man United, Bruno Fernandes amemjibu bilionea na mmiliki mwenza wa klabu hiyo, Sir Jim Ratcliffe katika madai yake kuhusu baadhi ya wachezaji aliodai wanalipwa fedha nyingi.Bilionea huyo pia aliwataja wachezaji wengine akidai si wazuri kiasi cha kutosha ingawa wanalipwa fedha nyingi ambapo Fernandes alimjibu kwamba ni klabu ndiyo inayokubali kusaini mikataba na […]

The post Fernandes ampasha bilionea Man United first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
Manchester, England
Nahodha wa Man United, Bruno Fernandes amemjibu bilionea na mmiliki mwenza wa klabu hiyo, Sir Jim Ratcliffe katika madai yake kuhusu baadhi ya wachezaji aliodai wanalipwa fedha nyingi.
Bilionea huyo pia aliwataja wachezaji wengine akidai si wazuri kiasi cha kutosha ingawa wanalipwa fedha nyingi ambapo Fernandes alimjibu kwamba ni klabu ndiyo inayokubali kusaini mikataba na wachezaji hao.
Fernandes ametoa kauli hiyo huku kukiwa na kumbukumbu ya kiungo huyo kupongezwa na bilionea huyo katika mahojiano akimtaja kuwa ni mchezaji mahiri wa soka.
Akifafanua Fernandes ambaye Alhamisi iliyopita alifunga mabao matatu (hat trick) na kuiwezesha Man United kupata ushindi wa jumla wa mabao 5-2 dhidi ya Real Sociedad katika Europa Ligi, pia aliwatetea wachezaji wenzake.

“Ukweli ni kwamba si vizuri kusikia baadhi ya mambo, sidhani kama kuna mchezaji ambaye anapenda kusikia shutuma au mambo yanayozungumzwa kumhusu, eti hauko vizuri kiasi cha kutosha na unalipwa fedha nyingi au mambo mengine kama hayo,” alisema Fernandes.
Fernandes alisema kila mchezaji ana mkataba wake na klabu imekubali kusaini mikataba wakati mchezaji anapokuja au anaposaini mkataba mpya na kwamba hayo ni mambo binafsi yanayomhusu mchezaji mmoja mmoja ambaye anatakiwa kuonesha ubora wake.
Wakati Ractliffe akimsifia Fernandes, nahodha wa zamani wa Man United, Roy Keane amemponda kiungo huyo kutoka Ureno akisema si mpambanaji na hata kipaji alichonacho bado hakitoshi.
Akizungumzia hoja ya Roy Keane, Fernandes alisema kila mtu ana mawazo yake na yeye hawezi kubadili hilo badala yake anachotakiwa kufanya ni kwenda uwanjani na kujaribu kufanya kilicho bora kadri awezavyo kwa ajili ya klabu.

The post Fernandes ampasha bilionea Man United first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2025/03/15/fernandes-ampasha-bilionea-man-united/feed/ 0
Bilionea Man United atishia kujitoa https://www.greensports.co.tz/2025/03/15/bilionea-man-united-atishia-kujitoa/ https://www.greensports.co.tz/2025/03/15/bilionea-man-united-atishia-kujitoa/#respond Sat, 15 Mar 2025 17:18:16 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=13134 Manchester, EnglandMmoja wa wamiliki wa klabu ya Manchester United, Sir Jim Ratcliffe amesema anaweza kuachana na klabu hiyo kama atakuwa mwenye kudhalilishwa na mashabiki kama ilivyokuwa kwa familia ya Glazer.Ratcliffe, bilionea maarufu Uingereza, mwaka jana alitoa Pauni 1.3 bilioni na kununua asilimia 28.93 ya hisa za klabu hiyo na kumfanya awe na jukumu la kusimamia […]

The post Bilionea Man United atishia kujitoa first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
Manchester, England
Mmoja wa wamiliki wa klabu ya Manchester United, Sir Jim Ratcliffe amesema anaweza kuachana na klabu hiyo kama atakuwa mwenye kudhalilishwa na mashabiki kama ilivyokuwa kwa familia ya Glazer.
Ratcliffe, bilionea maarufu Uingereza, mwaka jana alitoa Pauni 1.3 bilioni na kununua asilimia 28.93 ya hisa za klabu hiyo na kumfanya awe na jukumu la kusimamia mambo ya soka.
Katika mazugumzo yake hivi karibuni, Ratcliffe, bilionea ambaye kwa sasa ana umri wa miaka 72 alinukuliwa akisema kwamba hatojali hata kama hatokuwa na umaarufu.
Mapema mwezi uliopita kulikuwa na taarifa kwamba klabu hiyo ina mpango wa kupunguza gharama ambapo wafanyakazi takriban 200 wataachishwa kazi, hiyo ni mbali na wengine 250 walioachishwa kazi mwaka jana.
Sambamba na hilo pia kumekuwa na ongezeko la bei ya tiketi katikati ya msimu, jambo ambalo linawaathiri watoto wa umri chini ya miaka 16 pamoja na wazee wastaafu.
Jumatatu iliyopita, Ratcliffe alinukuliwa akisema kwamba kuna wachezaji wa klabu hiyo ambao si wazuri na wanalipwa fedha nyingi na kwamba klabu ipo katika muelekeo mbaya.
Siku moja baadaye, Ratcliffe alitangaza mpango wa klabu hiyo kujenga uwanja mpya ambao utachukua watu 100,000 ambapo Pauni 2 bilioni zinatarajiwa kutumika katika mpango huo.
“Namaanisha naweza kuachana na haya mambo, sijali kutokuwa maarufu kwa sababu hakuna anayependa kuiona Manchester United inakuwa chini ilipo na hakuna anayependa maamuzi tunayoyachukua kwa sasa,” alisema Ratcliffe.
Bilionea huyo alisema anaweza kuchoshwa kwa sababu na yeye hana tofauti yoyote na mtu wa kawaida kwa kuwa kinachoendelea si kizuri hasa kwa marafiki na familia.

“Kwa hiyo kama itafikia kiwango ambacho familia ya Glazer ilikutana nacho katika kudhalilishwa nitalazimika kusema jamani imetosha, ngoja mwingine aje,” alisema Ratcliffe.


Mara baada ya Ratcliffe kununua hisa Man United, mashabiki wengi walimpokea kwa furaha bilionea huyo ambaye ni shabiki wa klabu hiyo tangu utotoni wakimkaribisha kwa imani kwamba atasaidia kuweka mambo sawa.

The post Bilionea Man United atishia kujitoa first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2025/03/15/bilionea-man-united-atishia-kujitoa/feed/ 0
Bilionea Man United amkataa Mbappe https://www.greensports.co.tz/2024/06/21/bilionea-man-united-amkataa-mbappe-2/ https://www.greensports.co.tz/2024/06/21/bilionea-man-united-amkataa-mbappe-2/#respond Fri, 21 Jun 2024 08:26:49 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=11387 Manchester, EnglandBilionea na mmiliki mwenza wa klabu ya Manchester United, Sir Jim Ratcliffe (pichani) amesema hadhani suluhisho la klabu hiyo linaweza kupatikana kwa kumsajili Kylian Mbappe badala yake ni kuhakikisha wanakuwa na kikosi kilichokamilika kila idara.Mapema mwezi huu, Real Madrid ilitangaza matarajio yake ya kumsajili Mbappe akiwa mchezaji huru baada ya kumuwinda kwa muda mrefu […]

The post Bilionea Man United amkataa Mbappe first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Manchester, England
Bilionea na mmiliki mwenza wa klabu ya Manchester United, Sir Jim Ratcliffe (pichani) amesema hadhani suluhisho la klabu hiyo linaweza kupatikana kwa kumsajili Kylian Mbappe badala yake ni kuhakikisha wanakuwa na kikosi kilichokamilika kila idara.
Mapema mwezi huu, Real Madrid ilitangaza matarajio yake ya kumsajili Mbappe akiwa mchezaji huru baada ya kumuwinda kwa muda mrefu na zipo habari za ndani kwamba tayari mshambuliaji huyo ameshasaini mkataba na timu hiyo.
Wakati vuguvugu la usajili wa Mbappe likipamba moto baada ya mshambuliaji huyo kutangaza kuwa angeachana na klabu ya PSG baada ya msimu wa 2023-24, Man United nayo iliwahi kutajwa kati ya klabu zilizohitaji huduma yake.
Ratcliffe hata hivyo alisema kwamba hadhani kama suluhisho ni kumnunua Mbappe akisisitiza kwamba mchezaji mmoja kamwe hawezi kumaliza tatizo la Manchester United.

“Jambo la kwanza tunalotakiwa kulifanya ni kutengeneza kikosi kilichokamili, na baada ya hapo labda kuongeza zaidi wachezaji wawili wa hadhi ya Mbappe, itachukua misimu miwili au mitatu kujiweka sehemu nzuri,” alisema Ratcliffe.


Akiizungumzia Real Madrid na mafanikio yake, Ratcliffe aliwataja wachezaji sita wa timu hiyo ambao thamani yake inaweza walau kufikia Dola 100 milioni ambao ni Jude Bellingham, Eduardo Camavinga, Vinícius Júnior, Federico Valverde, Rodrygo na Aurélien Tchouaméni.
“Kama utaangalia vikosi vya Man United na Real Madrid utaona Real Madrid wana wachezaji sita ambao thamani yao ni zaidi ya Dola milioni 100, Man United haina wachezaji ambao thamani yao ni zaidi ya Dola 70 milioni,” alisema Ratcliffe.

The post Bilionea Man United amkataa Mbappe first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/06/21/bilionea-man-united-amkataa-mbappe-2/feed/ 0
Ten Hag ampa tahadhari bilionea Ratcliffe https://www.greensports.co.tz/2024/04/04/ten-hag-ampa-tahadhari-bilionea-ratcliffe/ https://www.greensports.co.tz/2024/04/04/ten-hag-ampa-tahadhari-bilionea-ratcliffe/#respond Thu, 04 Apr 2024 19:49:39 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=10506 Manchester, EnglandKocha wa Man United, Erik ten Hag amesema kwamba mmiliki mwenza wa klabu hiyo, bilionea Sir Jim Ratcliffe anatakiwa kuwa makini ili asivuruge maendeleo yaliyofanywa na klabu hiyo katika kipinid cha kocha huyo.Ratcliffe na kamapuni yake ya INEOS, ameanza kufanya mabadiliko kadhaa ikiwamo kumuajiri Omar Berrarda katika nafasi ya Ofisa Mtendaji Mkuu (CEO) na […]

The post Ten Hag ampa tahadhari bilionea Ratcliffe first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Manchester, England
Kocha wa Man United, Erik ten Hag amesema kwamba mmiliki mwenza wa klabu hiyo, bilionea Sir Jim Ratcliffe anatakiwa kuwa makini ili asivuruge maendeleo yaliyofanywa na klabu hiyo katika kipinid cha kocha huyo.
Ratcliffe na kamapuni yake ya INEOS, ameanza kufanya mabadiliko kadhaa ikiwamo kumuajiri Omar Berrarda katika nafasi ya Ofisa Mtendaji Mkuu (CEO) na wanadaiwa kuwa mbioni kuwaajiri, Jason Wilcox na Dan Ashworth katika majukumu ya msingi ya ukuzaji wa vipaji.
Ten Hag, 54, kocha kutoka Uholanzi ametoa kauli hiyo wakati huu kukiwa na uvumi kwamba menendo usiovutia wa timu hiyo unaweza kuwa sababu ya kocha huyo kutimuliwa mara baada ya msimu huu.
Pamoja na uvumi huo, Ten Hag ambaye ana mkataba hadi mwaka 2025 ameonesha dalili zote za utayari wa kutaka kuendelea kuwa na timu hiyo hadi msimu ujao.

“Nafikiri unahitaji kufuata mfumo, tuna wachezaji wazuri vijana walioingia, wapo katika mfumo na wanaendelea vizuri, tuko vizuri, katika mwelekeo mzuri na tunahitaji kwenda hatua inayofuata, usivuruge huu mfumo,” alisema Ten Hag.


Man United Alamisi hii itakuwa uwanjani kukabiliana na Chelsea katika mechi ya Ligi Kuu England (EPL) ikijaribu kufuta makosa baada ya sare ya bao 1-1 dhidi ya Brentford katika mechi ya Jumamosi iliyopita.

The post Ten Hag ampa tahadhari bilionea Ratcliffe first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/04/04/ten-hag-ampa-tahadhari-bilionea-ratcliffe/feed/ 0
Bilionea Man United amkataa Mbappe https://www.greensports.co.tz/2024/03/21/bilionea-man-united-amkataa-mbappe/ https://www.greensports.co.tz/2024/03/21/bilionea-man-united-amkataa-mbappe/#respond Thu, 21 Mar 2024 08:21:53 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=10284 Manchester, EnglandBilionea na mmiliki mwenza wa Manchester United, Sir Jim Ratcliffe amefuta hesabu zozote za kumsajili mshambuliaji wa PSG, Kylian Mbappe badala yake anataka klabu hiyo imsajili ‘Mbappe ajaye’.Ratcliffe na jopo lake wakiongozwa na Sir Dave Brailsford wanajiandaa kufanya usajili wa nguvu katika majira ya kiangazi ambao utakuwa ni usajili wa kwanza kwa bilionea huyo […]

The post Bilionea Man United amkataa Mbappe first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Manchester, England
Bilionea na mmiliki mwenza wa Manchester United, Sir Jim Ratcliffe amefuta hesabu zozote za kumsajili mshambuliaji wa PSG, Kylian Mbappe badala yake anataka klabu hiyo imsajili ‘Mbappe ajaye’.
Ratcliffe na jopo lake wakiongozwa na Sir Dave Brailsford wanajiandaa kufanya usajili wa nguvu katika majira ya kiangazi ambao utakuwa ni usajili wa kwanza kwa bilionea huyo tangu anunue hisa asilimia 27.7 katika klabu hiyo.
Mbappe katika kipindi cha majira ya kiangazi msimu huu atakuwa huru baada ya kumaliza mkataba wake na PSG na tayari ametangaza kuihama timu hiyo huku akihusishwa zaidi na mpango wa kujiunga na Real Madrid.
Ukiacha Real Madrid, Mbappe pia amewahi kuhusishwa na klabu za Liverpool, Arsenal na sasa Man United lakini Ratcliffe amefuta rasmi mpango huo akisema kwamba anadhani watakachoangalia ni kusajili vipaji vinavyoibukia badala ya mastaa ambao tayari wana majina.
“Nafikiri katika hilo jambo ambalo naona ni bora kulifanya ni kujaribu kumsajili Mbappe ajaye badala ya kutumia rasilimali kununua mafanikio,” alisema Ratcliffe.

“Si jambo la busara kumnunua Mbappe, kila mmoja anaweza kulifanyia tafakuri jambo hilo, changamoto kubwa zaidi ni kumtafuta Mbappe ajaye au Jude Bellingham au Roy Keane,” alisema Ratcliffe.


Bilionea huyo alifafanua kuwa suluhisho si kutumia fedha nyingi kwa kununua wachezaji wakubwa kwani jambo hilo limeshafanyika ukiangalia kipindi cha miaka 10 iliyopita namna fedha zilivyotumika kusajili wachezaji wakubwa.

“Jambo la kwanza unalotakiwa kufanya ni kuwa na watu sahi katika eneo sahihi la kuongoza klabu na kuhakikisha kuna utaratibu sahihi wa kukuza vipaji, hilo ni eneo muhimu katika klabu ya soka, kukuzavipaji kwa namna sahihi,” alisema Ratcliffe.
Ratcliffe (pichani) tayari ameanza kufanya mabadiliko kadhaa katika klabu hiyo, amemuajiri Omar Berrada kuwa Ofisa Mtendaji Mkuu (CEO) mpya akitokea Man City pamoja na Dan Ashworth kutoka Newcastle United ambaye anakuwa mkurugenzi mpya wa michezo.
Swali lililobaki ni kuhusu nafasi ya kocha Erik ten Hag kama ataendelea naye au atamuacha ingawa bilionea huyo anatajwa kuvutiwa na utendaji wa Jurgen Klopp wa Liverpool ambaye ameshatangaza kuachana na timu hiyo baada ya msimu huu.

The post Bilionea Man United amkataa Mbappe first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/03/21/bilionea-man-united-amkataa-mbappe/feed/ 0
Bilionea Man United amtaka Southgate https://www.greensports.co.tz/2024/03/20/bilionea-man-united-amtaka-southgate/ https://www.greensports.co.tz/2024/03/20/bilionea-man-united-amtaka-southgate/#respond Wed, 20 Mar 2024 06:16:44 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=10260 Manchester, EnglandBilionea na mmiliki mwenza wa klabu ya Man United, Sir Jim Ratcliffe inadaiwa amemtaja kocha wa England, Gareth Southgate kuwa chaguo la kwanza kuchukua nafasi ya Erik ten Hag katika timu hiyo.Mpango wa kumchukua Southgate unatajwa kuwa ni mojawapo ya mikakati ya bilionea huyo yenye lengo la kuibadili timu hiyo jambo ambalo aliahidi kulifanya […]

The post Bilionea Man United amtaka Southgate first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Manchester, England
Bilionea na mmiliki mwenza wa klabu ya Man United, Sir Jim Ratcliffe inadaiwa amemtaja kocha wa England, Gareth Southgate kuwa chaguo la kwanza kuchukua nafasi ya Erik ten Hag katika timu hiyo.
Mpango wa kumchukua Southgate unatajwa kuwa ni mojawapo ya mikakati ya bilionea huyo yenye lengo la kuibadili timu hiyo jambo ambalo aliahidi kulifanya tangu anunue hisa.
Mambo mengine ambayo bilionea huyo ana mpango wa kuyafanya ni pamoja na kuboresha uwanja unaomilikiwa na klabu hiyo wa Old Trafford licha ya upinzani uliojitokeza.
Wiki kadhaa zilizopita mpango wa bilionea huyo kumtaka Southgate uliibuka na kupata nguvu kutokana na matokeo mabaya ya Man United na sasa umeibuka kwa mara nyingine licha ya timu hiyo kuanza kupata mafanikio katika mechi za hivi karibuni.
Bilionea huyo hata hivyo inadaiwa ameshikilia mpango wa kumtaka kocha huyo mwenye umri wa miaka 53 ili ajiunge na timu hiyo wakati wa majira ya kiangazi na anataka uamuzi wa jambo hilo ufikiwe haraka.
Swali linabaki kwa Southgate, je atakuwa tayari kuachana na timu ya England ili apate nafasi ya kuinoa Man United licha ya ukweli kwamba England imeonekana kuwa bora chini yake na bado anahitajika.

The post Bilionea Man United amtaka Southgate first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/03/20/bilionea-man-united-amtaka-southgate/feed/ 0
EPL wampitisha Bilionea Ratcliffe Man Utd https://www.greensports.co.tz/2024/02/15/epl-wampitisha-bilionea-ratcliffe-man-utd/ https://www.greensports.co.tz/2024/02/15/epl-wampitisha-bilionea-ratcliffe-man-utd/#respond Thu, 15 Feb 2024 05:25:47 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=9733 London, EnglandMpango wa bilionea wa Uingereza, Sir Jim Ratcliffe kununua asilimia 25 ya hisa za klabu za Manchester United umepitishwa rasmi na mamlaka ya Ligi Kuu England (EPL).Bilionea huyo amenunua hisa hizo kwa thamani ya Dola 1.3 bilioni na kwa sasa kinachosubiriwa ni baraka za Chama cha Soka England au FA ili aanze rasmi kuwajibika […]

The post EPL wampitisha Bilionea Ratcliffe Man Utd first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

London, England
Mpango wa bilionea wa Uingereza, Sir Jim Ratcliffe kununua asilimia 25 ya hisa za klabu za Manchester United umepitishwa rasmi na mamlaka ya Ligi Kuu England (EPL).
Bilionea huyo amenunua hisa hizo kwa thamani ya Dola 1.3 bilioni na kwa sasa kinachosubiriwa ni baraka za Chama cha Soka England au FA ili aanze rasmi kuwajibika katika klabu hiyo.
Wamiliki kutoka Familia ya Glazer wataendelea kubaki na asilimia kubwa katika klabu hiyo ingawa Ratcliffe kupitia kampuni yake ya Ineos Group watakuwa na nguvu ya usimamizi na uendeshaji soka.
“Kwa sasa Ligi Kuu tunasubiri uthibitisho wa kukamilika kwa muamala,” ilieleza taarifa ya mamlaka ya Ligi Kuu ikithibitisha kwamba, Ractliffe mwenye umri wa miaka 71 amesaini na nyaraka nyingine husika.
Mpango wa Ratcliffe kununua hisa Man United ulikubaliwa mwaka jana mwishoni wakati wa Sikukuu ya Krismasi na miongoni mwa uwekezaji unaotarajiwa kufanya na bilionea huyo ni uboreshaji wa Uwanja wa Old Trafford.
Katika usimamizi wa mambo ya soka, Ineos sasa watakuwa na majukumu kwenye timu ya soka ya wanaume na ile ya wanawake pamoja na akademi zinazomilikiwa na klabu hiyo.
Sambamba na hilo pia Ineos watakuwa na nafasi mbili za ushiriki kwenye vikao vya bodi ya klabu ya Manchester United.
Bilionea Ratcliffe tayari ameshafanya ziara kwenye Uwanja wa Old Trafford pamoja na kufanya vikao na maofisa kadhaa wa Man United akiwamo kocha wa timu hiyo, Erik ten Hag.

The post EPL wampitisha Bilionea Ratcliffe Man Utd first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/02/15/epl-wampitisha-bilionea-ratcliffe-man-utd/feed/ 0
Ten Hag, bilionea mpya wateta https://www.greensports.co.tz/2024/01/05/ten-hag-bilionea-mpya-wateta/ https://www.greensports.co.tz/2024/01/05/ten-hag-bilionea-mpya-wateta/#respond Fri, 05 Jan 2024 18:36:35 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=9181 Manchester, EnglandKocha wa Man United, Erik ten Hag amesema kwamba amefanya mazungumzo yenye mwelekeo mzuri katika kikao chake na wawekezaji wapya wa klabu hiyo, kampuni ya Ineos inayomilikiwa na bilionea wa Uingereza, Sir Jim Ratcliffe.Ten Hag alikutana na Ratcliffe Jumanne iliyopita kwenye uwanja wa mazoezi wa timu hiyo ikiwa ni mara yake ya kwanza tangu […]

The post Ten Hag, bilionea mpya wateta first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Manchester, England
Kocha wa Man United, Erik ten Hag amesema kwamba amefanya mazungumzo yenye mwelekeo mzuri katika kikao chake na wawekezaji wapya wa klabu hiyo, kampuni ya Ineos inayomilikiwa na bilionea wa Uingereza, Sir Jim Ratcliffe.
Ten Hag alikutana na Ratcliffe Jumanne iliyopita kwenye uwanja wa mazoezi wa timu hiyo ikiwa ni mara yake ya kwanza tangu bilionea huyo anunue asilimia 25 ya hisa za klabu hiyo wakati wa Krismasi.
Akizungumzia kikao hicho, Ten Hag alisema alitumua muda mwingi na Ratcliffe pamoja na Sir Dave Brailsford na John-Claude Blanc ambao pia ni wawakilishi wa kampuni ya Ineos.
“Yalikuwa mazungumzo yenye mwelekeo mzuri, kilikuwa kikao kirefu kilichotumia saa kadha, tulikaa pamoja na kujadili ishu mbalimbali na tulikuwa katika mtazamo sahihi, kilikuwa ni kikao cha kujenga na tunaangalia namna ya kufanya kazi pamoja,” alisema Ten Hag.
Mabosi wa Ineos wanatarajia kufanya mabadiliko makubwa katika mfumo wa klabu hiyo ingawa kuna kanuni za soko la hisa zinazowakataza kufanya jambo hilo kwa wakati huu.
Ten Hag hata hivyo alisema bado ni mapema mno kufanya mambo makubwa hasa kwa kuwa Ratcliffe na washirika wake ndio kwanza wamewasili Jumanne na kutumia muda wao mwingi katika klabu hiyo.
Alisema kwamba bilionea huyo na washirika wake walifika katika klabu hiyo pamoja na mambo mengine kwa ajili ya kuwajua maofisa wa klabu na kujua taratibu za uendeshaji wa klabu zilivyo.

The post Ten Hag, bilionea mpya wateta first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/01/05/ten-hag-bilionea-mpya-wateta/feed/ 0
Bilionea Man United ataka apewe muda https://www.greensports.co.tz/2023/12/28/bilionea-man-united-ataka-apewe-muda/ https://www.greensports.co.tz/2023/12/28/bilionea-man-united-ataka-apewe-muda/#respond Wed, 27 Dec 2023 21:20:51 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=9032 Manchester, EnglandBilionea mpya aliyewekeza katika klabu ya Manchester United, Sir Jim Ratcliffe amesema inahitaji muda na subira kuirudisha klabu hiyo katika mafanikio yake ya zamani.Ratcliffe ambaye ni bilionea wa nchini Uingereza na mzaliwa wa jiji la Manchester, alikubali kununua hisa asilimia 25 katika klabu hiyo kwa thamani ya Pauni 1.03 bilioni kupitia kampuni yake ya […]

The post Bilionea Man United ataka apewe muda first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Manchester, England
Bilionea mpya aliyewekeza katika klabu ya Manchester United, Sir Jim Ratcliffe amesema inahitaji muda na subira kuirudisha klabu hiyo katika mafanikio yake ya zamani.
Ratcliffe ambaye ni bilionea wa nchini Uingereza na mzaliwa wa jiji la Manchester, alikubali kununua hisa asilimia 25 katika klabu hiyo kwa thamani ya Pauni 1.03 bilioni kupitia kampuni yake ya Ineos.
Kampuni ya Ineos ambayo itasimamia uendeshaji na usimamizi wa soka pia itawekeza Pauni 236 milioni kwa ajili ya maendeleo ya uwanja wa klabu hiyo wa Old Trafford.
Katika taarifa yake Ratcliffe aliwaambia mashabiki wa klabu hiyo kwamba wao Ineos wanajua wajibu wao kwa kuwa walezi wa klabu hiyo kwa niaba ya mashabiki.
“Naamini tunaweza kuleta maendeleo kwenye michezo ili kuendana na mafanikio ya kibiashara ambayo hakuna shaka kuwa klabu imekuwa ikiyafurahia,” alisema Ratcliffe na kuongeza, “Yote hayo yatahitaji muda, subira pamoja na usimamizi mzuri wa kitaalamu.”

“Mna shauku kubwa na Manchester United, na sisi hivyo hivyo, hakuna uhakika wa moja kwa moja katika michezo na mabadiliko yanahitaji muda, nasi tuko hapa kwa ajili ya hilo, pamoja tunataka kusaidia kuirudisha Manchester United mahali pake, katika kilele cha soka la England, Ulaya na dunia,” alisema Ratcliffe.


The post Bilionea Man United ataka apewe muda first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/12/28/bilionea-man-united-ataka-apewe-muda/feed/ 0