Singida BS - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Sun, 25 Jan 2026 11:06:35 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=6.9.1 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg Singida BS - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 Yanga yaibwaga Singida BS https://www.greensports.co.tz/2026/01/10/yanga-yaibwaga-singida-bs/ https://www.greensports.co.tz/2026/01/10/yanga-yaibwaga-singida-bs/#respond Sat, 10 Jan 2026 18:08:13 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=14265 Na mwandishi wetuTimu ya Yanga imefuzu hatua ya fainali ya Kombe la Mapinduzi kwa kuichapa Singida Black Stars bao 1-0 katika mechi iliyochezwa Ijumaa Januari 9, 2026 kwenye dimba la New Amaan Complex, Zanzibar.Bao hilo pekee lililoipa Yanga ushindi lilifungwa na Maxi Nzengeli katika dakika ya 54 baada ya kuinasa pasi ndefu ya Pacome Zouzoua […]

The post Yanga yaibwaga Singida BS first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Timu ya Yanga imefuzu hatua ya fainali ya Kombe la Mapinduzi kwa kuichapa Singida Black Stars bao 1-0 katika mechi iliyochezwa Ijumaa Januari 9, 2026 kwenye dimba la New Amaan Complex, Zanzibar.
Bao hilo pekee lililoipa Yanga ushindi lilifungwa na Maxi Nzengeli katika dakika ya 54 baada ya kuinasa pasi ndefu ya Pacome Zouzoua na kuujaza mpira wavuni.
Singida BS baada ya kufungwa bao hilo waliendelea kuonesha umahiri wao wakisaka bao lakini juhudi zao zilishindwa kupenya mbele ya safu ya ulinzi ya Yanga.
Mechi hiyo ilikuwa ya vuta nikuvute kwa timu zote kiasi cha kusababisha kila timu ipoteze mchezaji mmoja uwanjani kwa kupewa kadi nyekundu kutokana na kucheza rafu.
Hali hiyo iliifanya kila timu ibaki na wachezaji 10 uwanjani, kwa Yanga alitolewa Mohamed Damaro na kwa upande wa Singida BS janga hilo lilimkuta, Morice Chukwu.
Kwa ushindi huo Yanga itaumana na Azam FC katika mechi ya fainali ambayo imepangwa kuchezWa Januari 13 kwenye Uwanja wa Gombani, Pemba.

The post Yanga yaibwaga Singida BS first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2026/01/10/yanga-yaibwaga-singida-bs/feed/ 0
Singida Black yabeba taji Cecafa https://www.greensports.co.tz/2025/09/16/singida-black-yabeba-taji-cecafa/ https://www.greensports.co.tz/2025/09/16/singida-black-yabeba-taji-cecafa/#respond Tue, 16 Sep 2025 09:48:09 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=13910 Na mwandishi wetuSingida Black Stars ya Tanzania imeuanza kwa kishindo msimu wa 2025-26 kwa kubeba taji la michuano ya klabu Afrika Mashariki na Kati (Cecafa) maarufu Kombe la Kagame kwa kuinyuka Al Hilal ya Sudan mabao 2-1.Shujaa wa Singida BS katika mechi hiyo ya fainali iliyipigwa Jumatatu hii Septemba 15, 2025 kwenye Uwanja wa KMC, […]

The post Singida Black yabeba taji Cecafa first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Singida Black Stars ya Tanzania imeuanza kwa kishindo msimu wa 2025-26 kwa kubeba taji la michuano ya klabu Afrika Mashariki na Kati (Cecafa) maarufu Kombe la Kagame kwa kuinyuka Al Hilal ya Sudan mabao 2-1.
Shujaa wa Singida BS katika mechi hiyo ya fainali iliyipigwa Jumatatu hii Septemba 15, 2025 kwenye Uwanja wa KMC, Dar es Salaam alikuwa ni kiungo mpya wa timu hiyo, Clatous Chama aliyefunga mabao yote mawili.
Chama aliyejiunga na Singida msimu huu akitokea Yanga, alifunga mabao hayo kipindi cha kwanza na cha pili, alianza kuandika bao la kwanza dakika ya 21 lakini Al Hilal walipambana na kusawazisha bao hilo dakika ya 31 kupitia kwa Abdelrazaq Taha.
Kipindi cha pili timu zote zilikianza kwa kasi zikisaka bao la ushindi lakini alikuwa ni Chama aliyewainua vitini mashabiki wa Singida alipoandika bao la pili na la ushindi kwa shuti lililomshinda kipa Soufiane Farid wa Al Hilal.
Ushindi wa Singida unakuwa mwanzo mzuri kwa Chama na nyota mwenzake waliyekuwa naye kutokea Yanga, Khalid Aucho ambao wameungana kwa mara nyingine na kocha wao wa zamani wa Yanga, Miguel Gamondi ambaye kwa sasa anainoa timu hiyo.
Akizungumzia ushindi huo, Gamondi alisema kwamba timu yake ilicheza kwa nidhamu na ana furaha kwa kuibuka washindi akiwa na timu hiyo mpya ambayo ndiyo mara ya kwanza inabeba taji lenye hadhi ya kimataifa.
Kwa ushindi huo, Singida BS wameondoka na kitita cha Dola 30,000 pamoja na medali ya dhahabu wakati Al Hilal walioshika nafasi ya pili wamepata Dola 20,000 na medali ya fedha.
APR ya Rwanda imeshika nafasi ya tatu baada ya kuinyuka KMC ya Kinondoni, Dar es Salaam bao 1-0 na kukabidhiwa medali ya shaba pamoja na Dola 10,000.
Kwa upande mwingine nyota wa APR, Raouf Dao Memel ametangazwa kuwa mchezaji bora wa michuano hiyo wakati tuzo ya mfundaji bora ikienda kwa Chama wa Singida na kipa bora ni Metacha Mnata wa Singida huku Al Hilal wakibeba tuzo ya Fair Play.
Michuano hiyo ilishirikisha timu kutoka Tanzania Bara, Kenya, Somalia, Zanzibar, Djibouti, Brurundi, Ethiopia, Rwanda, Sudan Kusini na Sudan.

The post Singida Black yabeba taji Cecafa first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2025/09/16/singida-black-yabeba-taji-cecafa/feed/ 0
Singida BS yaitoa Simba Shirikisho CRDB https://www.greensports.co.tz/2025/06/02/singida-bs-yaitoa-simba-shirikisho-crdb/ https://www.greensports.co.tz/2025/06/02/singida-bs-yaitoa-simba-shirikisho-crdb/#respond Mon, 02 Jun 2025 18:37:30 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=13537 na mwandishiSimba imetolewa katika Kombe la Shirikisho CRDB baada ya kulala kwa mabao 2-1 mbele ya Singida Black Stars katika mechi ya nusu fainali iliyopigwa Jumamosi hii Mei 31, 2025 kwenye Uwanja wa Tanzanite Kwaraa mjini Manyara.Kipigo hicho kinaifanya Simba kutolewa katika mbio za kulisaka taji hilo na sasa imebakiwa na taji moja tu la […]

The post Singida BS yaitoa Simba Shirikisho CRDB first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
na mwandishi
Simba imetolewa katika Kombe la Shirikisho CRDB baada ya kulala kwa mabao 2-1 mbele ya Singida Black Stars katika mechi ya nusu fainali iliyopigwa Jumamosi hii Mei 31, 2025 kwenye Uwanja wa Tanzanite Kwaraa mjini Manyara.
Kipigo hicho kinaifanya Simba kutolewa katika mbio za kulisaka taji hilo na sasa imebakiwa na taji moja tu la Ligi Kuu NBC baada ya kushindwa kutamba mbele ya RS Berkane kwenye Kombe la Shirikisho Afrika.
Singida BS walianza mapema kulichachafya lango la Simba na kuandika bao la kwanza katika dakika ya 17 mfungaji akiwa Jonathan Sowah ambaye alifunga bao hilo kupitia pasi ya Arthur Bada.
Dakika 10 baada ya bao hilo, Simba walipata pigo kwa kipa wao namba moja, Musa Camara kuumia alipogongana na Sowah na hivyo kutolewa nje na nafasi yake kuingia Ally Salim.
Mambo yalizidi kuwa mabaya kwa Simba kwani dakika saba baada ya kuingia kwa kipa huyo, Singida waliandika bao la pili lililofungwa na Emmanuel Keyekeh.
Keyekeh alifunga bao hilo akiyatumia makosa ya kipa Salim ambaye alirudisha mpira vibaya na kumkuta mfungaji ambaye hakufanya ajizi kufumua shuti lililojaa wavuni.
Keyekeh alikamilisha karamu ya mabao ya Singida dakika ya tatu baada ya kuanza kipindi cha pili kwa kufunga bao lililotokana na mpira wa adhabu.
Adhabu hiyo ilitolewa na mwamuzi Ahmed Arajiga baada ya Edmund John kuchezewa rafu akiwa nje kidogo ya eneo la 18 na ndipo Keyekeh alipopiga mpira uliokwenda moja kwa moja hadi wavuni
Baada ya mabao hayo, Singida waliimarisha ulinzi lakini Simba walipambana na kupata bao pekee la kufutia machozi dakika ya 68 lililofungwa na Jean Ahoua kwa mpira wa adhabu uliotokana na rafu aliyochezewa Elly Mpanzu.
Mechi ya fainali ya michuano hiyo kati ya Singida na Yanga inatarajiwa kupigwa kati ya Juni 26 na 28 mwaka huu.

The post Singida BS yaitoa Simba Shirikisho CRDB first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2025/06/02/singida-bs-yaitoa-simba-shirikisho-crdb/feed/ 0
Mukwala aitungua Singida BS https://www.greensports.co.tz/2025/05/28/mukwala-aitungua-singida-bs/ https://www.greensports.co.tz/2025/05/28/mukwala-aitungua-singida-bs/#respond Wed, 28 May 2025 19:06:55 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=13517 Na mwandishi wetuBao pekee la Steven Mukwala limeiwezesha Simba kutoka na pointi tatu katika mechi ya Ligi Kuu NBC dhidi ya Singida BS iliyopigwa leo Jumatano, Mei 28, 2025 kwenye Uwanja wa KMC, Dar es Salaam.Mukwala alifunga bao hilo dakika ya 42 akiitumia pasi ya Jean Ahoua kabla ya kufumua shuti kali baada ya kuwapangua […]

The post Mukwala aitungua Singida BS first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
Na mwandishi wetu
Bao pekee la Steven Mukwala limeiwezesha Simba kutoka na pointi tatu katika mechi ya Ligi Kuu NBC dhidi ya Singida BS iliyopigwa leo Jumatano, Mei 28, 2025 kwenye Uwanja wa KMC, Dar es Salaam.
Mukwala alifunga bao hilo dakika ya 42 akiitumia pasi ya Jean Ahoua kabla ya kufumua shuti kali baada ya kuwapangua mabeki wa Singida na kipa Amos Obasogi ambaye alitoka golini.
Simba walianza kulisakama lango la Singida mapema dakika ya 24 lakini Joshua Mutale alishindwa kuitumia vizuri krosi ya Shomari Kapombe kuipa Simba bao la kuongoza.
Singida walijibu mapigo dakika 10 baadaye kwa Vicoria Adebayor aliyeufumania mpira akiwa nje kidogo ya eneo la penalti lakini shuti alilopiga lilitoka nje.
Dakika ya 59, Singida walifanya shambulizi jingine baada ya Jonathan Sowah kuyatumia makosa ya Joshua Mutale aliyepoteza pasi ya Ahoua.
Sowah baada ya kuinasa pasi hiyo aliukokota mpira na kufumua shuti ambalo hata hivyo kipa wa Simba, Musa Camara alilidaka.
Simba nao walifanya shambulizi kali dakika ya 65 baada ya Mutale na Mukwala kugongeana wakiwa eneo la Singida na Mutale kufumua shuti ambalo kipa Obasogi aliokoa na mpira kumkuta Shomari Kapombe ambaye alifumua shuti kali lililopaa.
Timu zote zilifanya mabadiliko kadhaa ambayo hata hivyo hayakuweza kubadili matokeo ya mechi hiyo iliyokuwa na rabsha za hapa na pale zilizomlazimu mwamuzi kutoa kadi za njano.
Camara alipewa kadi ya njano kwa kile kilichoonekana kuwa ni kuchelewesha muda baada ya kuanguka chini na kutibiwa kwa muda mrefu wakati Sowah wa Singida alipewa kadi ya njano kwa kumchezea rafu Camara.
Kwa ushindi huo Simba sasa inakuwa imefikisha pointi 72 katika mechi 27 ikiwa imezidiwa na vinara wa ligi hiyo ambao pia ni mahasimu wao Yanga, kwa tofauti ya pointi moja.
Kwa msimamo ulivyo mechi ya Simba na Yanga iliyopangwa kupigwa Juni 15 ndiyo iliyobeba hatma ya ubingwa wa ligi hiyo msimu huu wa 2024-25.

The post Mukwala aitungua Singida BS first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2025/05/28/mukwala-aitungua-singida-bs/feed/ 0
Yanga yajiimarisha kileleni https://www.greensports.co.tz/2025/02/17/yanga-yajiimarisha-kileleni-3/ https://www.greensports.co.tz/2025/02/17/yanga-yajiimarisha-kileleni-3/#respond Mon, 17 Feb 2025 18:48:37 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=13021 Na mwandishi wetuMabao ya Clement Mzize na Prince Dube yameiwezesha Yanga kutoka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Singida Black Stars na kujiimarisha kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu NBC.Katika mechi hiyo iliyopigwa leo Jumatatu, Februari 17, 2025 kwenye Uwanja wa KMC, Dar es Salaam, wenyeji Yanga waliandika bao lao la kwanza dakika ya […]

The post Yanga yajiimarisha kileleni first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Mabao ya Clement Mzize na Prince Dube yameiwezesha Yanga kutoka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Singida Black Stars na kujiimarisha kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu NBC.
Katika mechi hiyo iliyopigwa leo Jumatatu, Februari 17, 2025 kwenye Uwanja wa KMC, Dar es Salaam, wenyeji Yanga waliandika bao lao la kwanza dakika ya 14 kupitia kwa Mzize.
Dakika mbili kabla ya timu kwenda mapumziko, Dube aliipatia Yanga bao la pili na kuzifanya timu hizo ziende mapumziko Yanga wakiwa mbele kwa mabao 2-0.
Juhudi za Singida BS kusaka bao zilizaa matunda katika dakika ya pili ya nyongeza baada ya dakika 90 kukamilika mfungaji akiwa nyota wa timu hiyo kutoka Ghana, Jonathan Sowah.
Kwa ushindi huo Yanga sasa imefikisha pointi 52 katika michezo 20 wakati mahasimu wao Simba wanashika nafasi ya pili wakiwa na pointi 47 ingawa Yanga wamecheza mechi 20 wakati Simba wamecheza 18.
Katika mechi nyingine ya ligi hiyo iliyochezwa leo kwenye Uwanja wa Tanzanite, Kwaraa mjini Manyara, wenyeji Fountain Gate walitoka sare ya 0-0 na Tabora United.

The post Yanga yajiimarisha kileleni first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2025/02/17/yanga-yajiimarisha-kileleni-3/feed/ 0
Yanga yashika usukani ligi kuu https://www.greensports.co.tz/2024/10/30/yanga-yashika-usukani-ligi-kuu/ https://www.greensports.co.tz/2024/10/30/yanga-yashika-usukani-ligi-kuu/#respond Wed, 30 Oct 2024 20:34:13 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=12167 Na mwandishi wetuYanga imefanikiwa kuushika usukani wa Ligi Kuu NBC msimu huu kwa mara ya kwanza baada ya kuichapa Singida BS bao 1-0 katika mechi iliyochezwa leo Jumatano kwenye Uwanja wa New Amaan, Zanzibar.Kwa ushindi huo Yanga ambao ni mabingwa watetezi wa ligi hiyo wamefikisha pointi 24 na kuwazidi Singida BS kwa pointi mbili ingawa […]

The post Yanga yashika usukani ligi kuu first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
Na mwandishi wetu
Yanga imefanikiwa kuushika usukani wa Ligi Kuu NBC msimu huu kwa mara ya kwanza baada ya kuichapa Singida BS bao 1-0 katika mechi iliyochezwa leo Jumatano kwenye Uwanja wa New Amaan, Zanzibar.
Kwa ushindi huo Yanga ambao ni mabingwa watetezi wa ligi hiyo wamefikisha pointi 24 na kuwazidi Singida BS kwa pointi mbili ingawa Singida imecheza mechi tisa wakati Yanga hadi sasa imecheza mechi nane.
Bao hilo pekee la Pacome lilipatikana katika dakika ya 67 baada ya mchezaji huyo kufumua shuti kali la mguu wa kushoto lililompita kipa wa Singida BS, Metacha Mnata.
Metacha ambaye aliwahi kuichezea Yanga, licha ya kufungwa bao hilo lakini mara kadhaa alikuwa mwiba kwa safu ya ushambulizi ya Yanga na haikushangaza Yanga kupata bao hilo pekee licha ya mashambulizi kadhaa waliyoyafanya.
Yanga ilipata pigo la mapema baada ya beki wake wa kushoto mwenye uwezo mkubwa wa kupanda kupeleka mashambulizi, Shedrack Boka kuumia dakika ya saba na baadaye kutolewa dakika ya 17 na nafasi yake kuingia Nickson Kibabage.
Kibabage hakuwangusha Yanga, dakika ya 31, aliambaa vyema na mpira akitokea upande wa kushoto wa timu yake na kumpa pasi ya chinichini Aziz Ki ambaye shuti lake liligonga mwamba kabla ya kuokolewa na Metacha.
Singida BS walijibu shambulizi hilo dakika 10 baadaye kwa kufanya shambulizi lililotokana na mpira wa kurushwa ambao D Camara aliuunganisha kwa kichwa na Elvis Rupia naye akapiga tena kwa kichwa na mpira kutoka sentimita chache juu ya lango la Yanga.
Yanga walifanya shambulizi tena dakika ya 61, Clatous Chama alimpasia mpira Aziz Ki ambaye alipiga shuti la juu na Metacha kuonesha umahiri wake kwa kuufuata mpira huo juu na kuutoa kona ambayo haikuzaa matunda.
Mambo yaliendelea kuwaharibikia Yanga ambao walilazimika kumtoa Kibabage na nafasi yake kuingia Ibrahim Bacca baada ya Kibabage kuumia.

The post Yanga yashika usukani ligi kuu first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/10/30/yanga-yashika-usukani-ligi-kuu/feed/ 0