SimbavsYanga - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Sat, 30 Apr 2022 07:45:08 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=7.0 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg SimbavsYanga - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 Ni Inonga au Onyango vs Mayele? https://www.greensports.co.tz/2022/04/30/mechi-ya-kibabe/ https://www.greensports.co.tz/2022/04/30/mechi-ya-kibabe/#respond Sat, 30 Apr 2022 07:33:15 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=613 Na mwandishi wetuFiston Mayele amedhihirisha ubora wake katika Ligi Kuu ya NBC akiwa na mabao 12 na hapana shaka ndiye mfungaji tegemeo wa Yanga. Yote hayo kwa leo unaweza kuyaweka kando, habari kubwa ikawa ni je Mayele ataweza kuiadhibu Simba jioni ya leo kama ambavyo amekuwa akiziadhibu timu nyingine za ligi hiyo. Amekuwa kwenye kasi […]

The post Ni Inonga au Onyango vs Mayele? first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Fiston Mayele amedhihirisha ubora wake katika Ligi Kuu ya NBC akiwa na mabao 12 na hapana shaka ndiye mfungaji tegemeo wa Yanga.

Yote hayo kwa leo unaweza kuyaweka kando, habari kubwa ikawa ni je Mayele ataweza kuiadhibu Simba jioni ya leo kama ambavyo amekuwa akiziadhibu timu nyingine za ligi hiyo.

Amekuwa kwenye kasi ya ajabu katika mechi sita zilizopita, amefunga mfululizo huku Yanga ikiendelea kujiimarisha kileleni, ameziadhibu
KMC, Geita Gold, Mtibwa Sugar, Namungo, Kagera Sugar na Azam.

Rekodi hiyo tamu leo inaweza kuwekwa kando na swali linabaki je ataiua Simba na kuendeleza rekod hiyo?

Bao alilofunga dhidi ya Azam katika mechi iliyokuwa na ushindani mkali
limeendelea kuwa gumzo, ni bao tamu ambalo mashabiki wanazi wa Yanga wanaliita bao la ‘kideo’, nalo pia kwa leo linawekwa kando na hoja ya msingi inabaki pale pale kwamba je Mayele ataweza kuiadhibu Simba?
Nje ya mjadala wa Mayele kuiadhibu Simba kuna mjadala mwingine wa nani wa kumdhibiti Mayele, hapo wanatajwa zaidi mabeki wawili wapambanaji,
Joash Onyango na Enock Inonga.

Mabeki hawa katika mechi iliyopita walikuwa kama vile wamepangiana na kupokezana majukumu ya kuhakikisha Mayele hatetemi, ukimkosa Inonga
utamkuta Onyango, ingawa ni Onyango aliyeonekana zaidi katika matukio kadhaa akimdhibiti Mayele.

Katika dakika ya 20 ya mchezo huo, Mayele alipenyezewa pasi na kushindana kwa kasi na Onyango kwa kila mmojawao kutaka kuuwahi mpira,
wakati ikiaminika hiyo ilikuwa nafasi ya Mayele kuiadhibu Simba mapema, Onyango alimzidi kwa kasi kidogo na kuondoa hatari.
Dakika nne baadaye, Mayele aliunasa mpira na kuupenyeza katikati ya miguu ya Onyango, wakati Mayele akikimbia kwa kasi kuuwahi mpira huo
ili kuiadhibu Simba, alichofanya Onyango ni kumzuia Mayele kwenye njia, tukio hilo lilimfanya Onyango apewe kadi ya njano na Yanga
kupewa mpira wa adhabu.
Mayele na Onyango walikutana katika tukio jingine katika dakika ya 33, safari hii wakishindania mpira wa juu, alichofanya Onyango ni kumpa
mwili Mayele, alitumia bega kumtoa kwenye mstari na hivyo kumfanya ashindwe kuutumia mpira huo kuifunga Simba.
Dakika mbili kabla ya mapumziko, Mayele aliunganishiwa mpira wa juu
ambao kipa wa Simba, Aishi Manula alidhamiria kuudaka lakini hesabu
zilikataa baada ya kuteleza jambo lililompa Mayele nafasi ya kuuwahi mpira huo huku Onyango akimfukuzia lakini akiwa ameudhibiti mpira
vizuri Mayele naye akataleza na kumrahisishia Onyango kazi ya kuondo hatari langoni mwake.

Ukimuweka kando Onyango, Inonga naye mara kwa mara alikuwa karibu na mchezaji huyo pale ambapo Onyango alikosekana, na hadi wakati Mayele
anatolewa katika dakika ya 83, ni Inonga aliyemsindikiza kwenda kwenye
benchi.

Inonga, beki mwingine kisiki wa Simba alikuwa akihaha kila kona kuhakikisha Simba haifungwi hapo hapo ni kama alijipa kazi nyingine ya kumdhibiti Mayele asiteteme.

Matukio yote hayo yanabaki kuwa tisa, je leo nani kati yao atakayehakikisha Mayele hafanyi yake na je Mayele ataitumia Simba kuendeleza rekodi yake ya mabao mfululizo? Yanga hadi sasa inaongoza ligi ikiwa imekusanya pointi 54 katikamichezo 20 wakati Simba ina pointi 41 ikiwa imecheza michezo 19.

The post Ni Inonga au Onyango vs Mayele? first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2022/04/30/mechi-ya-kibabe/feed/ 0
Kulikoni mashabiki Simba, Yanga kuzimia uwanjani! https://www.greensports.co.tz/2022/04/29/kulikoni-mashabiki-simba-yanga-kuzimia-uwanjani/ https://www.greensports.co.tz/2022/04/29/kulikoni-mashabiki-simba-yanga-kuzimia-uwanjani/#respond Fri, 29 Apr 2022 19:54:08 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=610 Na mwandishi wetuJumamosi hii, mahasimu wa jadi, Simba na Yaanga wanatoana jasho. Sikukadhaa kabla ya mechi hii, mashabiki hucharurana kwa majigambo naahadi mbalimbali na mwisho wa mechi wako wanaotoka vichwa chini nawengine wakiwa na furaha.Katika miaka ya karibuni mashabiki wameingia katika matukio auutamaduni mpya wa kuzimia uwanjani mara inapotokea timu yao kufungwawakati mechi ikiendelea, matukio […]

The post Kulikoni mashabiki Simba, Yanga kuzimia uwanjani! first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Jumamosi hii, mahasimu wa jadi, Simba na Yaanga wanatoana jasho. Siku
kadhaa kabla ya mechi hii, mashabiki hucharurana kwa majigambo na
ahadi mbalimbali na mwisho wa mechi wako wanaotoka vichwa chini na
wengine wakiwa na furaha.
Katika miaka ya karibuni mashabiki wameingia katika matukio au
utamaduni mpya wa kuzimia uwanjani mara inapotokea timu yao kufungwa
wakati mechi ikiendelea, matukio ambayo huko nyuma hayakuwa ya kawaida
au hayakuwahi kuripotiwa.
Mechi ya mwaka 2014 ya Nani Mtani Jembe ambayo Yanga ililala kwa mabao
2-0 wakati huo ikinolewa na Mbrazil Marcio Maximo na Simba ikinolewa
na Mzambia Patrick Phiri, inaweza kuwa mfano mzuri wa matukio ya
mashabiki wengi kuzimia.
Wakati wikiendi hii timu hizi zikiumana, si vibaya kujiuliza ni kwa
nini mashabiki kwa miaka ya karibuni wamekuwa wakianguka na kuzimia
majukwaani wakati mechi ikiendelea, na kwa nini hali hiyo haikuwapo
miaka ya nyuma au haikuwa kubwa miaka ya nyumba.
Je ni kweli kwamba mapenzi ya soka katika klabu hizi yamekuwa makubwa
sana kwa miaka ya karibuni kuliko ilivyokuwa miaka ya nyuma? Kwamba
hiyo ndiyo sababu kubwa ya mashabiki kuzimia uwanjani wakati mechi
ikiendelea?.
Je ni kweli kwamba mashabiki wa sasa hawana uvumilivu, hamasa yao iko
juu kwamba soka kwao ni burudani ya kuwapa matokeo mazuri tu na si
vinginevyo na hivyo inapotokea timu yao kushindwa huona kama
wameumizwa kiasi kikubwa na hivyo kuishiwa nguvu na hatimaye kuzimia?
Vipi kuhusu madai kwamba kizazi cha sasa si sawa na cha zamani katika
mambo ya lishe, yaani chakula kinacholiwa sasa si cha asili,
kinawasababishia madhara watu wengi wakiwamo mashabiki wa soka ambao
wakiumizwa kidogo tu moyo hushindwa kuhimili na hivyo kujikuta
wakianguka na kuzimia.
Na vipi kuhusu mfumo wa maisha kwamba maisha ya sasa ni tofauti na
yale ya zamani ya watu kufanya kazi za kuushughulisha mwili, kutembea
umbali mrefu bila usafiri hali ambayo ni tofauti na maisha ya sasa
ambayo yanadaiwa kuwafanya watu kuwa legelege, wavivu ambao hushindwa
kukabiliana na matukio ya kuumizwa moyo, misukosuko kidogo tu mtu
anajikuta akizimia.
Mtaalam wa saikolojia jijini Dar es Salaam ambaye hakutaka kutajwa
jina anasema tatizo mojawapo linaweza kuwa ni matumaini makubwa
anayokuwa nayo shabiki.
“Mtu anaingia uwanjani akiwa tayari amewatambia wenzake akiamini
anatoka na ushindi na wengine hadi kutoa ahadi za ajabu ajabu, sasa
mtu wa aina hii anaposhindwa sishangai kusikia amezimia,” anasema.
Akifafanua kuhusu ahadi anasema kuna wanaowekeana pesa tena nyingi,
sasa mtu wa aina hii anaposhindwa anakuwa katika mazingira magumu,
anaifikiria pesa yake na hasara anayoipata na hiyo inaweza kuwa sababu
mojawapo ya mtu huyo kuzimia.
Anaongeza kuwa wapo mashabiki ambao huenda uwanjani na matokeo kabla
hata mechi haijachezwa na matokeo yanapokuwa tofauti anajikuta akiwa
mnyonge na hapo ndipo nguvu zinamuishia na kujikuta akizimia au kuwa
mnyonge isivyo kawaida.
Akizungumzia suluhisho la tatizo, anasema kwamba kwanza shabiki yeyote
anatakiwa kufahamu kwamba mpira ni burudani hivyo aingie uwanjani
akiamini atashinda lakini atambue kwamba kushindwa pia kupo.
Anaongeza kuwa mashabiki waache tabia ya kujiwekea malengo makubwa
kwenye mechi kwani wao si wanaocheza, “fulani leo lazima atoke
uwanjani na bao, kauli za aina hii ni za kujiamini mno lakini kibaya
zaidi ni kwamba unajiaminisha kupitia mtu mwingine ambaye huna uhakika
kama naye ana malengo kama hayo, mwengine atasema Mayele, mwengine
atamtaja Bocco, hili si jambo zuri.
“Kweli hawa ni washambuliaji wazuri na wana uwezo mkubwa wa kufunga na
kila shabiki ana haki ya kujivunia mchezaji wake lakini pia tambua
kwamba wanakutana na mabeki wazuri wenye uwezo wa kuzuia hivyo si
sahihi kuamini kwamba ni lazima watoke uwanjani na bao,” anasema.
Anashauri mashabiki kuwa na tabia ya kujipa matumaini na si kuweka
malengo huku wakijiamini hadi kufikia hatua ya kuwekeana ahadi ya
kutoa pesa au mke au nyumba, shabiki wa aina hii anapofungwa
akifikiria ahadi aliyoitoa anaishiwa nguvu na si ajabu kuzimia.
“Ni kweli kwamba ushindi ni mtamu na kila shabiki anaiamini timu yake
itashinda, hilo si jambo baya lakini imani hiyo isipitilize, matumaini
yawe ya kawaida, malengo yawe ya kawaida, weka akiba kwamba kushindwa
pia kupo.
“Jipe imani ya ushindi kwani ushindi ni mtamu lakini pia si vibaya
kujiandaa kukabiliana na kushindwa na kuikubali hali hiyo, ukifanya
hivyo hutoumia sana unaposhindwa na kama ni kuwekeana ahadi utaweka za
kawaida tu ambazo unazimudu, hutoweka ahadi za ajabu ajabu za kumtoa
mke wako, nyumba yako au pesa nyingi,” anasema.
Maswali yanaweza kuwa mengi kuhusu huu utamaduni wa kuzimia, mwingine
anaweza kwenda mbali na kujiuliza, vipi kuhusu mabadiliko ya tabia
nchi? Kwamba siku hizi mazingira yameharibiwa kiasi kwamba hewa chafu
imekuwa ikiathiri watu, je hili nalo linaweza kuchangia mashabiki
kuzimia uwanjani wakati timu zao zikiumana baada ya kuumizwa na
matokeo mabaya?
Vipi kuhusu kucharurana na majigambo? Je nayo hayana nafasi katika
kuwakatisha tamaa mashabiki baada ya timu zao kushindwa na kuona
kwamba watakuwa na wakati mgumu mitaani na vijiweni kwamba zamani
mashabiki hawakuwa wakicharurana katika namna inayoumiza vibaya na
hivyo shabiki wa sasa anapolifikiria hilo anaumia, anakata tamaa na
kujikuta akianguka na kuzimia.
Tunaweza kuwa na hoja nyingi lakini matukio haya au utamaduni huu mpya
katika soka nchini unaacha maswali mengi kwamba kulikoni yamekuwa
yakitokea miaka ya karibuni wakati miaka ya nyuma hali haikuwa hivyo.
Vipi ongezeko la idadi ya watu nalo limechangia?

The post Kulikoni mashabiki Simba, Yanga kuzimia uwanjani! first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2022/04/29/kulikoni-mashabiki-simba-yanga-kuzimia-uwanjani/feed/ 0
Yanga kuzuia taji la tano Simba? https://www.greensports.co.tz/2021/12/10/yanga-kuzuia-taji-la-tano-simba/ https://www.greensports.co.tz/2021/12/10/yanga-kuzuia-taji-la-tano-simba/#respond Fri, 10 Dec 2021 12:22:36 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=524 Na mwandishi wetu Wakati fulani mwaka 2000, Yanga ikiwa imetoka kuchukua taji la Ligi Kuu msimu wa 1999/2000 aliyekuwa mwenyekiti wa kamati ya muda ya Yanga, Tarimba Abbas alifanya mkutano na waandishi wa habari. Baada ya kujibu maswali kadhaa, Tarimba (sasa mbunge Kinondoni) aliwachekesha waandishi alipowaambia kwamba mitaa ya Kariakoo kuna klabu moja ina miaka […]

The post Yanga kuzuia taji la tano Simba? first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
Kikosi cha Simba

Na mwandishi wetu

Wakati fulani mwaka 2000, Yanga ikiwa imetoka kuchukua taji la Ligi Kuu msimu wa 1999/2000 aliyekuwa mwenyekiti wa kamati ya muda ya Yanga, Tarimba Abbas alifanya mkutano na waandishi wa habari.

Baada ya kujibu maswali kadhaa, Tarimba (sasa mbunge Kinondoni) aliwachekesha waandishi alipowaambia kwamba mitaa ya Kariakoo kuna klabu moja ina miaka mingi haijachukua taji.

Tarimba alikuwa akiizungumzia Simba ambayo tangu ichukue taji mwaka 1995 ililisotea hadi kulibeba tena mwaka 2001.

Simba iliyochekwa mwaka 2000, leo hii inashikilia rekodi ya kulibeba taji hilo kwa miaka minne mfululizo yaani 2018, 2019, 2020 na 2021 na kama 2022 watalibeba tena itakuwa rekodi ya kipekee yaani miaka mitano mfululizo (mkono).

Na sasa ligi ikiwa inachanja mbuga swali ni je nani wa kuizuia Simba kutwaa taji la tano mfululizo? Timu zote zinaweza kufanya hivyo lakini inayotajwa zaidi ni Yanga.

Pamoja na ukweli kwamba Yanga ndiyo inayotajwa zaidi lakini inahitaji utulivu wa hali ya juu kung’amua viwango vya Simba na Yanga hasa kwa msimu huu unaoendelea.

Mchezo wa Ngao ya Jamii ndio uliotajwa zaidi kuwa mwanzo wa kuwapa Yanga jeuri na imani kwamba wana timu imara ya kuizuia Simba kutwaa taji la tano mfululizo.

Mchezo ule pamoja na ubora wa Yanga lakini ulituachia maswali fikirishi, kwamba kile kiwango cha Simba siku ile ndiyo inaelekea mwisho wa enzi za utawala au Yanga baada ya kupotea misimu minne imejitathmini upya na kuja kivingine safari hii. Si rahisi kupata jibu la haraka kwa wakati huu.

Si suala la ushindi wa Yanga dhidi ya Simba kwani takwimu zinaisaliti Simba kuwa haina maajabu sana katika mechi zake dhidi ya Yanga hata katika misimu hii yote ikikomba mataji manne mfululizo na kutamba kimataifa.

Kwenye mechi tano za mwisho walizokutana (kwa ujumla), wameshinda mechi moja tu ya Kombe la FA, sare moja (Ligi kuu raundi ya kwanza) na kuchezea kichapo mara tatu (Fainali Kombe la Mapinduzi, Ligi Kuu raundi ya pili, Ngao ya Jamii).

Kwa kuzungumzia kiwango cha kwenye mchezo wao wa Ngao ya Jamii, Simba walizidiwa kwa kila takwimu uwanjani, tofauti na mechi nyingine zote walizokutana hivi karibuni.

Katika mechi ile ya Ngao ya Jamii, Simba walimjaribu kwa mashuti matatu tu kipa Djigui Diarra lakini pia Simba hii ya kupata kona tatu tu ndani ya dakika 90, hasa wakiwa wamefungwa?

Simba tuliyoifahamu ingeipiga Yanga msako wa nyoka lakini kulikuwa na utofauti kadri muda ulivyokwenda, ndivyo Yanga ilizidi kuwabana, kiasi cha kucheza rafu nyingi (26) na kadi nyekundu juu, Thadeo Lwanga.

Simba imeyaanza maisha bila ya Luis Miquissone na Clatous Chama, watu muhimu waliotajwa kuifanya Simba ya sasa ionekane ya tofauti kwani zile ‘one-two’ za Chama pale kati hazipo tena badala yake ‘transition’ yake imekuwa ni kucheza mipira mirefu na spidi ya mawinga (ikumbuke mechi ya Mazembe).

Ingawa Sadio Kanoute na Ousmane Sakho ndio waliotajwa kuwarithi Chama na Luis, bado staili ya uchezaji au ubora wao wameonekana ni watu tofauti.

Kama utaizungumzia mechi ya Ngao ya Jamii, Yanga si tu ilishinda taji bali iliishinda Simba kwa kila kitu. Yanga ilikuwa na kiwango bora siku hiyo, kuanzia kipa hadi safu ya ushambuliaji, ilikuwa na muunganiko, mawasiliano mazuri na kwa tahadhari muda wote.

Kwa ligi ilipofikia pamoja na umuhimu wa mechi za Simba na Yanga ikiwamo ile ya Ngao ya Jamii, bado mechi hiyo haitoshi kuwa kigezo pekee cha kuamini kuwa Yanga wana ubavu wa kuzuia taji la tano kwenda Msimbazi.

Badala yake kinachoonekana sasa ni kwamba timu zote zimeonyesha uhai katika ligi zikishika nafasi mbili za juu, Yanga ikiongoza na pointi 19 ikifuatiwa na Simba yenye pointi 17, kila moja imefungwa magoli mawili, hazijapoteza mechi hata moja, kinachowatofautisha ni matokeo ya sare, Yanga ina sare moja Simba mbili. Matokeo hayo yanatoa picha ya ushindani mkali baina ya timu hizo mbili.

Zaidi ya yote Jumamosi, Desemba 11 timu hizi zitakutana katika mechi nyingine ngumu ya ligi ambayo hapana shaka matokeo yake yatakuwa ni sehemu tu ya furaha au huzuni lakini hayawezi kutoa jibu la moja kwa moja kwamba Simba itatwaa taji la tano mfululizo au Yanga itaizuia Simba kutwa taji la tano.

The post Yanga kuzuia taji la tano Simba? first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2021/12/10/yanga-kuzuia-taji-la-tano-simba/feed/ 0