Simbanguvumoja - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Tue, 26 Apr 2022 07:40:12 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=7.0 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg Simbanguvumoja - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 Matumaini ya Simba yalivyotoweka Afrika Kusini https://www.greensports.co.tz/2022/04/26/matumaini-ya-simba-yalivyotoweka-afrika-kusini/ https://www.greensports.co.tz/2022/04/26/matumaini-ya-simba-yalivyotoweka-afrika-kusini/#respond Tue, 26 Apr 2022 07:39:11 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=595 Na mwandishi wetuMatumaini waliyokuwa nayo Simba ya kucheza nusu fainali ya Kombe laShirikisho Afrika yametoweka baada ya timu hiyo kutolewa na OrlandoPirates kwa mikwaju ya penalti.Hiyo ni baada ya matokeo ya jumla ya bao 1-1. Simba ilishinda bao 1-0mjini Dar es Salaam na Orlando nao kushinda bao 1-0 kwao Soweto,Afrika Kusini.Matokeo hayo yamehuzunisha wengi lakini […]

The post Matumaini ya Simba yalivyotoweka Afrika Kusini first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Matumaini waliyokuwa nayo Simba ya kucheza nusu fainali ya Kombe la
Shirikisho Afrika yametoweka baada ya timu hiyo kutolewa na Orlando
Pirates kwa mikwaju ya penalti.
Hiyo ni baada ya matokeo ya jumla ya bao 1-1. Simba ilishinda bao 1-0
mjini Dar es Salaam na Orlando nao kushinda bao 1-0 kwao Soweto,
Afrika Kusini.
Matokeo hayo yamehuzunisha wengi lakini Simba ilionesha ukomavu kwenye
michuano hiyo hasa kwa namna walivyopambana kwenye dakika 90 hizo za
mwisho za kufa au kupona.
Simba walijua fika kwamba wanacheza ugenini na timu ngumu, hivyo
walihitaji kutumia akili na mbinu za ziada ili kutafuta namna ya
kupenya nusu fainali kwa mara ya kwanza na kocha wa timu hiyo, Pablo
Franco alifanikiwa katika hilo kabla ya mambo kuanza kuharibika
baadaye.

Ukuta wa Berlin
Simba iliingia na mipango kabambe ya ulinzi madhubuti wanapokaba na
kushambulia kwa kasi kila walipopata nafasi hiyo. Simba walianza na
mabeki sita, viungo wa kati wawili, washambuliaji wawili huku
ikiwatumia mabeki wa kati watatu: Paschal Wawa, Joash Onyango na
Henock Inonga.
Mpango huo uliipa shida Orlando kupenya na kuiadhibu timu hiyo kwani
ilikaba kwa tahadhari na nidhamu na namna walivyokuwa wakigawana
kukaba kwa mawinga na katikati ya uwanja ilikuwa mtihani mkubwa kwa
Maharamia hao wa Baharini kupenya na kuleta madhara mpaka kipindi cha
kwanza kinamalizika.

Kadi ya Mugalu yatibua mambo
Uzito wa mechi uliendelea kutawala kwa Orlando licha ya kujaribu
kushambulia hapa na pale mpaka Chris Mugalu alipooneshwa kadi nyekundu
kwa kumchezea vibaya Olisa Ndah katika dakika ya 58.
Baada ya hapo, ilichukua dakika mbili kabla ya Innocent Maela kupiga
krosi iliyounganishwa kwa kichwa cha Kwame Peprah na kufanya mechi
ngumu kwa Simba ambao waliruhusu bao hilo wakiwa bado wana msongo juu
ya kadi ya Mugalu ambaye alikuwa akiwasumbua vilivyo mabeki wa
Orlando.

Sakho anyong’onyea
Pape Sakho aliyekuwa akicheza na Mugalu kwenye ushambuliaji alipunguza
makali kwa kuwa timu ilizidi kukaba na yeye akakosa msaada akiwa peke
yake mbele, safu nzima ya ulinzi ya Orlando ‘ikamuinamia’ kabla ya
baadaye kutolewa na kuingizwa Meddie Kagere.
Kwa kifupi Simba ilianza kuziba viraka wakati mechi ikiendelea na
kutoa mwanya kwa Orlando kuingiza washambuliaji wengi akiwemo
Gabadinho Mhango, mchezaji anayefahamika kwa kuwa na uwezo mkubwa.

Simba ilipambana
Pamoja na yote, Simba ilipambana kuzuia na kushambulia mara chache kwa
dakika takriban 30 zilizosalia kwa mipango ya Pablo na kufanikiwa
kutoruhusu bao jingine mpaka kipenga cha mwisho kinapulizwa na kuhamia
kwenye mikwaju ya penalti ambayo Simba hawakuwa na bahati nayo.

Ofori shujaa wa Orlando
Kipa wa Orlando, Richard Ofori alionesha ushujaa katika matuta hayo
ambapo kwanza alicheza penalti ya Jonas Mkude, penalti ya kwanza ya
Simba kabla ya baadaye kupewa penalti ya mwisho iliyokuwa ikiamua
hatma yao na kuukwamisha mpira wavuni na kuimaliza rasmi safari ya
Simba kimataifa.

Inonga ageuka gumzo
Ukiachana na matokeo hayo, ishu ya Inonga kutetemeka mwili huku
akionesha kuwa na wasiwasi mno baada ya kukosa penalti imeibua gumzo
kubwa na hali ya huzuni kwa waliokuwa wakifuatilia mchezo huo.
Inonga ambaye alionesha uimara usiotetereka kwa dakika zote 90 za
matumaini na huzuni za mechi hiyo alikosa penalti ya tatu ambayo
aliipiga kiufundi ‘akimuuza’ kipa lakini mpira ulizidi kipimo,
ukagonga mwamba wa juu na kwenda nje.
Hali hiyo ilionekana kumtesa mno Inonga kwani baadaye alioneshwa akiwa
amechuchumaa peke yake wakati penalti zikiendelea, alikuwa aking’ata
vidole, akitetemeka na kuonesha wasiwasi mkubwa mno. Baada ya hapo
wengi walimfariji na kumsikitikia kwa hali aliyokuwa akikutana nayo
kichwani mwake wakati huo.

Orlando dhidi ya Al Ahli
Orlando sasa itakutana na Al Ahli Tripoli ya Libya kwenye mchezo wa
nusu fainali. Al Ahli imetinga hatua hiyo baada ya kuichapa Al Ittihad
ya Libya pia kwa bao 1-0 kwenye ushindi wa jumla.
Nusu fainali nyingine itazikutanisha RS Berkane dhidi ya TP Mazembe
ambapo mechi za hatua hiyo zitapigwa Mei 8 kabla ya mechi za marudiano
Mei 15, mwaka huu.

The post Matumaini ya Simba yalivyotoweka Afrika Kusini first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2022/04/26/matumaini-ya-simba-yalivyotoweka-afrika-kusini/feed/ 0
Bwalya: Tunataka rekodi kwa Orlando https://www.greensports.co.tz/2022/04/24/bwalya-tunataka-rekodi-kwa-orlando/ https://www.greensports.co.tz/2022/04/24/bwalya-tunataka-rekodi-kwa-orlando/#respond Sun, 24 Apr 2022 12:43:19 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=587 Na mwandishi wetuKiungo mchezeshaji wa Simba, Larry Bwalya amejinasibu kuwa wanatakakuweka rekodi na kufuta kushindwa kwa timu za Tanzania kufikia hatuaya nusu fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika.Saa chache baadaye Simba itaingia dimbani kuumana na Orlando Piratesya Afrika Kusini kuwania tiketi ya nusu fainali ya michuanKombe laShirikisho Afrika.Mara ya mwisho Simba ilifika fainali ya michuano […]

The post Bwalya: Tunataka rekodi kwa Orlando first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Kiungo mchezeshaji wa Simba, Larry Bwalya amejinasibu kuwa wanataka
kuweka rekodi na kufuta kushindwa kwa timu za Tanzania kufikia hatua
ya nusu fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika.
Saa chache baadaye Simba itaingia dimbani kuumana na Orlando Pirates
ya Afrika Kusini kuwania tiketi ya nusu fainali ya michuanKombe la
Shirikisho Afrika.
Mara ya mwisho Simba ilifika fainali ya michuano hiyo wakati huo
ikiitwa Kombe la CAF mwaka 1993 na sasa Simba inataka kurudia rekodi
yake hiyo msimu huu kwa kutinga nusu fainali na kwenda fainali baada
ya kukwama kwenye robo fainali ya Klabu Bingwa Afrika msimu uliopita.
Bwalya amedai kuwa wanafahamu nini wamekwenda kufanya dhidi ya Orlando
na ingawa wana faida ya ushindi wa bao 1-0 walioupata kwenye mechi ya
awali Jumapili iliyopita lakini bado wana kitu cha kufanya kuhakikisha
wanapita hatua hiyo kwa kishindo.
“Tunajua kwa nini tumekuja kwenye mechi hii ta marudiano, lengo ni
kushindana na kama kocha alivyosema ni muda mrefu tangu timu ya
Tanzania ifike nusu fainali kwa mashindano ya Afrika kwa hiyo kama
timu kama wachezaji mmoja mmoja tunajua hii mechi ina umuhimu kiasi
gani.
“Haitakuwa mechi nyepesi, Orlando wako nyumbani na sisi tuna faida ya
ushindi, hatutakiwi kuitegemea, inabidi tupambane kuhakikisha
tunaingia nusu fainali, hilo ndiyo litakuwa la muhimu zaidi kwa sasa,”
alisema Bwalya anayetumia mguu wa kushoto.
Mechi hiyo itapigwa saa 1.00 usiku kwa saa za Afrika Mashariki kwenye
dimba la Orlando, Soweto mjini Johannesburg, mshindi wa matokeo ya
jumla ya mechi hiyo atacheza na mshindi wa mechi ya Al Ittihadi dhidi
ya Al Ahly Tripoli, zote za Libya.
Na Simba itaingia uwanjani hapo ikiwa na mtihani mwingine kuhakikisha
haifanyi makosa dhidi ya timu za Afrika Kusini kama ilivyotokea msimu
uliopita walipong’olewa na Kaizer Chiefs kwa ushindi wa jumla wa mabao
4-3. Simba ilichapwa mabao 4-0 ugenini kabla ya kushinda mabao 3-0
nyumbani.
Mechi nyingine za hatua hiyo zinazopigwa leo ni TP Mazembe
ikiikaribisha Pyramids huku Tripoli ikiwa mwenyeji wa Ittihad. Mechi
zote mbili za awali baina ya timu hizo ziliisha kwa suluhu. Kesho RS
Berkane iliyopoteza ugenini kwa mabao 2-1 dhidi ya Al Masry
itahitimisha ratiba ya hatua hiyo ikiwa nyumbani.

The post Bwalya: Tunataka rekodi kwa Orlando first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2022/04/24/bwalya-tunataka-rekodi-kwa-orlando/feed/ 0