Simba - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Sun, 09 Aug 2026 19:15:59 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=7.0.4 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg Simba - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 Polisi Kenya watibua sherehe miaka 90 Simba https://www.greensports.co.tz/2026/08/09/polisi-kenya-watibua-sherehe-miaka-90-simba/ https://www.greensports.co.tz/2026/08/09/polisi-kenya-watibua-sherehe-miaka-90-simba/#respond Sun, 09 Aug 2026 19:12:45 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=14825 Na mwandishi wetuSherehe za Simba Day zilizoandamana na kumbukumbu ya miaka 90 tangu kuanzishwa kwa klabu ya Simba zimeingia doa baada ya timu hiyo kuchapwa bao 1-0 na Polisi Kenya, mechi iliyochezwa kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.Simba na Polisi Kenya zimeumana Jumamosi Agosti 8, 2026, mechi iliyotanguliwa na sherehe hizo sambamba na utambulisho […]

The post Polisi Kenya watibua sherehe miaka 90 Simba first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Sherehe za Simba Day zilizoandamana na kumbukumbu ya miaka 90 tangu kuanzishwa kwa klabu ya Simba zimeingia doa baada ya timu hiyo kuchapwa bao 1-0 na Polisi Kenya, mechi iliyochezwa kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.
Simba na Polisi Kenya zimeumana Jumamosi Agosti 8, 2026, mechi iliyotanguliwa na sherehe hizo sambamba na utambulisho wa wachezaji wa timu hiyo kwa ajili ya msimu mpya wa 2026-27.
Sherehe hizo zilipambwa na burudani ya muziki iliyofanywa na wasanii mbalimbali wakiongozwa na Ali Kiba ambapo mashabiki pia walimshuhudia mnyama Simba akiingizwa kunogesha tukio hilo.
Aliyepeleka kilio Simba alikuwa ni mshambuliaji wa zamani wa Singida Black Stars, Elvis Rupia aliyefunga bao hilo pekee katika dakika ya 90 ya mchezo huo.
Simba licha ya kufungwa bao hilo pekee lakini waliweza kukonga nyoyo za mashabiki waliofurika uwanjani hapo kwa kucheza soka safi na la kuvutia.
Timu hiyo ilitengeneza nafasi kadhaa za kufunga ambazo walishindwa kuzitumia huku wapinzani wao kutoka Kenya wakicheza kwa tahadhari kubwa hadi walipopata bao hilo pekee.
Kabla ya kuanza msimu mpya wa Ligi Kuu NBC, Simba itapata nafasi nyingine ya kupima ubora wa kikosi chake kwa kuumana na mahasimu wao Yanga katika mechi ya Ngao ya Jamii itakayopigwa Agosti 12, 2026 kwenye Uwanja wa New Amaan, Zanzibar.
Sherehe za Simba Day hufanyika kila mwaka tangu kuasisiwa mwaka 2009 na aliyekuwa mwenyekiti wa klabu hiyo, Hassan Dalali na katibu wake, Mwina Kaduguda.
Kwa mwaka huu sherehe za Simba Day zimenogeshwa na tukio la kumbukumbu ya miaka 90 tangu kuanzishwa kwa klabu hiyo mwaka 1936.

The post Polisi Kenya watibua sherehe miaka 90 Simba first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2026/08/09/polisi-kenya-watibua-sherehe-miaka-90-simba/feed/ 0
Kelvin Nashon rasmi mali ya Simba https://www.greensports.co.tz/2026/07/19/kelvin-nashon-rasmi-mali-ya-simba/ https://www.greensports.co.tz/2026/07/19/kelvin-nashon-rasmi-mali-ya-simba/#respond Sun, 19 Jul 2026 14:56:44 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=14813 Na mwandishi wetuBaada ya kuwapo uvumi kuhusu Kelvin Nashon kutua Simba, hatimaye klabu hyo imemtangaza rasmi kiungo huyo kuwa mchezaji wao mpya atakayeitumikia timu hiyo kuanzia msimu mpya wa 2026-27.Taarifa hiyo rasmi imepatikana leo Jumapili Julai 19, 2026 kwenye mitandao ya kijamii ya klabu hiyo ikiambatana na picha ya kumkaribisha kiungo huyo fundi kutoka Pamba […]

The post Kelvin Nashon rasmi mali ya Simba first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Baada ya kuwapo uvumi kuhusu Kelvin Nashon kutua Simba, hatimaye klabu hyo imemtangaza rasmi kiungo huyo kuwa mchezaji wao mpya atakayeitumikia timu hiyo kuanzia msimu mpya wa 2026-27.
Taarifa hiyo rasmi imepatikana leo Jumapili Julai 19, 2026 kwenye mitandao ya kijamii ya klabu hiyo ikiambatana na picha ya kumkaribisha kiungo huyo fundi kutoka Pamba Jiji.
Habari za Kelvin kujiunga na Simba zimekuwapo kwa miezi kadhaa lakini hazikuwa zimethibitishwa na klabu hiyo na hivyo sasa ni rasmi kuanzia msimu ujao nyota huyo ambaye pia amewahi kuichezea Singida Black Stars atavaa jezi ya Simba.
Habari za Simba kumtaka kiungo huyo ambaye pia ni mchezaji wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, zilianza kusikika wakati akiwa Singida Black Stars kabla ya kwenda Pamba Jiji, Januari 2025.
Simba ambayo imemaliza Ligi Kuu NBC msimu ulioisha wa 2025-26 ikiwa nafasi ya pili, inaendelea kuimarisha kikosi chake ikiacha baadhi ya wachezaji na kusajili wapya kwa ajili ya msimu mpya wa ligi hiyo na michuano ya kimataifa.
Azam, Yanga nazo zasajili
Wakati Simba ikikamilisha usajili huo Azam FC nao wameendelea kukiimarisha kikosi chao kwa kumsajili winga Henoc Nolia kutoka FC Lupopo ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC).
Mitadao ya Azam kuanzia Jumamosi Julai 18, 2026 imepambwa na picha za mchezaji huyo mpya ambaye ataongeza nguvu katika kikosi cha timu hiyo iliyomaliza nafasi ya tatu katika Ligi Kuu NBC msimu wa 2025-26.
Nao mabingwa watetezi wa Ligi Kuu NBC, Yanga wametangaza kumsajili mshambuliaji Juma Issa Abushiri maarufu Chuga Boy kutoka Fountain Gate FC.
Chuga ndiye mchezaji wa kwanza kutambulishwa na Yanga kwa ajili ya kukiongezea nguvu kikosi cha timu hiyo kwa ajili ya msimu mpya wa 2026-27.

The post Kelvin Nashon rasmi mali ya Simba first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2026/07/19/kelvin-nashon-rasmi-mali-ya-simba/feed/ 0
Chasambi aachwa Simba https://www.greensports.co.tz/2026/07/19/chasambi-aachwa-simba/ https://www.greensports.co.tz/2026/07/19/chasambi-aachwa-simba/#respond Sun, 19 Jul 2026 11:34:52 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=14807 Na mwandishi wetuKlabu ya soka ya Simba imetangaza kuachanana winga wake Ladack Chasambi ambaye sasa ni rasmi hatokuwa na timu hiyo kwa msimu ujao wa 2026-27.Taarifa iliyopatikana Jumamosi Julai 18, 2026 kwenye vyanzo vya habari vya klabu hiyo, imemtaja mchezaji huyo kuwa mmoja wa wachezaji ambao wamepewa nafasi ya kutafuta maisha nje ya Simba.Chasambi alijiunga […]

The post Chasambi aachwa Simba first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Klabu ya soka ya Simba imetangaza kuachanana winga wake Ladack Chasambi ambaye sasa ni rasmi hatokuwa na timu hiyo kwa msimu ujao wa 2026-27.
Taarifa iliyopatikana Jumamosi Julai 18, 2026 kwenye vyanzo vya habari vya klabu hiyo, imemtaja mchezaji huyo kuwa mmoja wa wachezaji ambao wamepewa nafasi ya kutafuta maisha nje ya Simba.
Chasambi alijiunga na Simba Januari 2024 akitokea Mtibwa Sugar ambapo alipandishwa katika kikosi cha kwanza cha timu hiyo baada ya kuonesha uwezo wake kwenye timu ya vijana kabla ya Simba kuvutiwa naye.
Alisajiliwa na Simba wakati huo ikiwa chini ya kocha Abdelhak Benchikha akitajwa kuwa mmoja wa wachezaji waliopewa matumaini makubwa ya kutamba kutokana na uwezo alioanza kuuonesha.
Hali hata hivyo imekuwa tofauti kwa mchezaji huyo ambaye hatimaye Simba imetangaza rasmi kuachana naye.
Chasambi sasa anaungana na mshambuliaji wa timu hiyo, Jonathan Sowah ambaye naye alitangaza kuachwa baada ya kuichezea timu hiyo kwa msimu mmoja tu akitokea Singida Black Stars.
Mchezaji mwingine ambaye Simba imetangaza kuachana naye hivi karibuni ni kiungo mkongwe, Muzamir Yassin ambaye amekuwa na timu hiyo akicheza kwa mafanikio kwa takriban miaka 10.

The post Chasambi aachwa Simba first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2026/07/19/chasambi-aachwa-simba/feed/ 0
Simba yatwaa taji la Shirikisho CRDB https://www.greensports.co.tz/2026/07/05/simba-yabeba-taji-shirikisho-crdb/ https://www.greensports.co.tz/2026/07/05/simba-yabeba-taji-shirikisho-crdb/#respond Sun, 05 Jul 2026 15:42:19 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=14759 Na mwandishi wetuBao pekee la kujifunga la Yahya Zayd limeiwezesha Simba kubeba Kombe la Shirikisho CRDB mbele ya Azam FC katika mechi ya fainali iliyochezwa Jumamosi Julai 4, 2026 kwenye Uwanja wa Gombani, Pemba.Beki huyo tegemeo wa Azam alijifunga bao hilo kwa bahati mbaya na kuineemesha Simba katika dakika ya 62 alipokuwa akijaribu kuokoa krosi […]

The post Simba yatwaa taji la Shirikisho CRDB first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Bao pekee la kujifunga la Yahya Zayd limeiwezesha Simba kubeba Kombe la Shirikisho CRDB mbele ya Azam FC katika mechi ya fainali iliyochezwa Jumamosi Julai 4, 2026 kwenye Uwanja wa Gombani, Pemba.
Beki huyo tegemeo wa Azam alijifunga bao hilo kwa bahati mbaya na kuineemesha Simba katika dakika ya 62 alipokuwa akijaribu kuokoa krosi iliyopigwa na kiungo wa Simba, Elly Mpanzu.
Juhudi za Azam kusaka bao la kusawazisha zilipata pigo dakika chache baadaye walipojikuta wakibaki wachezaji 10 uwanjani baada ya kiungo wao Feisal Salum au Fei Toto kulimwa kadi nyekundu.
Fei, mmoja wa wachezaji muhimu wa Azam alipewa kadi hiyo baada ya kumpiga kiwiko mchezaji wa Simba, Libasse Gueye na mwamuzi kumpa kadi hiyo hapo hapo.
Kutolewa kwa Fei kuliwaweka pagumu wachezaji wa Azam ambapo juhudi zao za kutafuta bao la kusawazisha zilizidi kuwa ngumu na haikushangaza dakika 90 kumalizika Simba wakitowa vifua mbele na bao hilo pekee.
Simba wamelibeba taji hilo lililokuwa likishikiliwa na mahasimu wao Yanga ambao waliweka rekodi kwa kulibeba kwa misimu minne iliyopita.
Katika msimu huu wa 2025-26 Yanga wameishia hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo inayodhaminiwa na Benki ya CRDB ambapo walishindwa kutamba mbele ya Azam baada ya kuchapwa mabao 3-2.

The post Simba yatwaa taji la Shirikisho CRDB first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2026/07/05/simba-yabeba-taji-shirikisho-crdb/feed/ 0
Hapa BMT wametufikirisha kimataifa https://www.greensports.co.tz/2026/06/22/hapa-bmt-wametufikirisha-kimataifa/ https://www.greensports.co.tz/2026/06/22/hapa-bmt-wametufikirisha-kimataifa/#respond Sun, 21 Jun 2026 22:03:57 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=14718 Na Hassan KinguBaada ya Baraza la Michezo la Taifa (BMT) kuipa tuzo klabu ya soka ya Simba, mashabiki wa soka nchini Tanzania waliingia katika mjadala mzito.Mjadala wenyewe ni wa kuipinga BMT kwa kuipa Simba tuzo kwa kigezo gani, kabla ya kujua kigezo, mjadala ulipamba moto kwa mashabiki wa Simba na Yanga kuzodoana vijiweni na mitandaoni.Mashabiki […]

The post Hapa BMT wametufikirisha kimataifa first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na Hassan Kingu
Baada ya Baraza la Michezo la Taifa (BMT) kuipa tuzo klabu ya soka ya Simba, mashabiki wa soka nchini Tanzania waliingia katika mjadala mzito.
Mjadala wenyewe ni wa kuipinga BMT kwa kuipa Simba tuzo kwa kigezo gani, kabla ya kujua kigezo, mjadala ulipamba moto kwa mashabiki wa Simba na Yanga kuzodoana vijiweni na mitandaoni.
Mashabiki hasa wa Yanga waliamini timu yao ndiyo iliyokuwa na hadhi ya kupewa tuzo kutokana na mafanikio yake nchini Tanzania kuanzia mataji ya ligi kuu kwa misimu takriban minne na michuano mingine.
Kimsingi mjadala huu haukupaswa kuwapo lakini ulikuwapo kwa sababu ni hulka ya mashabiki wa timu hizi mbili hasimu kulumbana huku kila mmoja akiamini timu yake ndiyo bora kuliko mwenzake.
Nasema mjadala huu haukupaswa kuwapo kwa sababu tulikuwa tunabishana na kulumbana kwa jambo ambalo wengi wetu tulikuwa hatulijui na hatukusumbuka kulijua badala yake tuliendelea kusumbuka kwa kubishana na kulumbana.
Hatukuwa tunajua kigezo ambacho BMT ilitumia kuipa Simba tuzo hiyo, lakini tulichofanya ni kujiaminisha kuwa Yanga ni bora kuliko Simba na Simba ambao pia walikuwa hawajui kigezo cha BMT kuipa timu yao tuzo nao walijiaminisha kuwa timu yao ni bora kuliko Yanga.
Mjadala huu ulikufa baada ya BMT kuweka wazi kigezo kwamba wao waliangalia mafanikio ya timu kimataifa, Simba walikuwa hawajui kuhusu kigezo lakini waliitetea timu yao na Yanga walikuwa hawajui lolote kuhusu kigezo nao waliamini timu yao ni bora kuliko Simba.
Kumbe kilichotokea ni kwamba BMT waliwaza kimataifa wakati sisi akili zetu ziliwaza kishabiki tena jijini Dar es Salaam katika wilaya ya Ilala mitaa ya Msimbazi, Kariakoo na Twiga na Jangwani.
Tungejaribu kuwaza kimataifa kama BMT na kuwa na fikra na mitazamo ya kimataifa, mjadala huu au malumbano haya yasingekuwapo lakini hatukuwaza huko badala yake mawazo yetu yalikuwa Tanzania, si nje ya Tanzania.
Kwa maana nyingine BMT wao waliwaza mambo ya Cairo, Misri yalipo makao makuu ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF), waliwaza Rabat-Morocco, Lagos-Nigeria, Abidjan-Ivory Coast, Tunis-Tunisia na kwingineko lakini sisi fikra na mitazamo yetu iliishia kuwaza mitaa ya Jangwani na Twiga na Msimbazi na Kariakoo.
Na ndio maana sasa hivi hatusikii tena mjadala na malumbano kuhusu tuzo ya Simba, ni kwa sababu tulijadili na kulumbana tusichokijua, tumeujua ukweli tumeishia kubaki kimya na kuhamishia mijadala na malumbano yetu katika mambo mengine.
Kumalizika kwa malumbano na mjadala huo ni vyema kukawa somo kwa mashabiki wa soka nchini kuwa wadadisi wa mambo kabla ya kuanza kuyajadili tena kujadili kwa kutumia nguvu nyingi katika kushambuliana.
Ndio, kuitetea timu yako si jambo baya lakini lazima ujue unachotetea au kukipinga, je uko sahihi au unatetea na kupinga usichokijua, unatetea au kupinga tuzo ya Simba bila kujua kigezo ambacho kimetumika kutoa tuzo hiyo!

The post Hapa BMT wametufikirisha kimataifa first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2026/06/22/hapa-bmt-wametufikirisha-kimataifa/feed/ 0
Pamba yaibana mbavu Simba https://www.greensports.co.tz/2026/03/20/pamba-yaibana-mbavu-simba/ https://www.greensports.co.tz/2026/03/20/pamba-yaibana-mbavu-simba/#respond Fri, 20 Mar 2026 14:18:04 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=14467 Na mwandishi wetuMatarajio ya Simba kutoka na pointi tatu katika mechi yake ya Ligi Kuu NBC dhidi ya Pamba Jiji yamekwama baada ya timu hizo kutoka sare ya bao 1-1.Matokeo ya mechi hiyo iliyopigwa Alhamisi Machi 19, 2026 kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza yamewakera mashabiki wa Simba waliojipa matumaini ya kubeba pointi tatu hasa […]

The post Pamba yaibana mbavu Simba first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Matarajio ya Simba kutoka na pointi tatu katika mechi yake ya Ligi Kuu NBC dhidi ya Pamba Jiji yamekwama baada ya timu hizo kutoka sare ya bao 1-1.
Matokeo ya mechi hiyo iliyopigwa Alhamisi Machi 19, 2026 kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza yamewakera mashabiki wa Simba waliojipa matumaini ya kubeba pointi tatu hasa baada ya hasimu wao Yanga kutoka sare ya bao 0-0 na TRA United.
Simba ndio waliokuwa wa kwanza kuzichana nyavu za Pamba katika dakika ya 32 kwa bao lililofungwa na Anicet Oura lakini shuti la mbali lililopigwa na James Mwashenga dakika tatu baadaye lilitosha kuipa Pamba bao la kusawazisha.
Kwa matokeo hayo, Simba ambao hadi sasa wamecheza mechi 13 wamefikisha pointi 28 na kutulia nafasi ya tatu wakiachwa kwa tofauti ya pointi tisa na mahasimu wao Yanga wanaoshika usukani wa ligi hiyo wakiwa wamecheza mechi 15.
Katika mechi nyingine ya ligi hiyo, Mashujaa FC waliutumia vyema uwanja wao wa nyumbani wa Lake Tanganyika kulazimisha sare ya bila kufungana na Azam FC.

The post Pamba yaibana mbavu Simba first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2026/03/20/pamba-yaibana-mbavu-simba/feed/ 0
Simba yailaza Singida Black 2-1 https://www.greensports.co.tz/2026/03/12/simba-yailaza-singida-black-2-1/ https://www.greensports.co.tz/2026/03/12/simba-yailaza-singida-black-2-1/#respond Thu, 12 Mar 2026 15:04:54 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=14417 Na mwandishi wetuBaada ya sare mbili za bila kufungana dhidi ya Yanga na Dodoma Jiji, Simba imefufua upya matumaini ya kulisaka taji la Ligi Kuu NBC msimu huu wa 2025-26 baada ya kuichapa Singida Black Stars mabao 2-1.Ushindi huo uliopatikana Jumatano Machi 11, 2026 kwenye Uwanja wa Airtel umeifanya Simba kufikisha pointi 27 ikitulia nafasi […]

The post Simba yailaza Singida Black 2-1 first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Baada ya sare mbili za bila kufungana dhidi ya Yanga na Dodoma Jiji, Simba imefufua upya matumaini ya kulisaka taji la Ligi Kuu NBC msimu huu wa 2025-26 baada ya kuichapa Singida Black Stars mabao 2-1.
Ushindi huo uliopatikana Jumatano Machi 11, 2026 kwenye Uwanja wa Airtel umeifanya Simba kufikisha pointi 27 ikitulia nafasi ya tatu baada ya kucheza mechi 12 wakiwa wamezidiwa na vinara wa ligi hiyo, Yanga kwa tofauti ya pointi tano.
Simba walianza kuzichana nyavu za Singida BS katika dakika ya saba ya mchezo huo kwa bao lililofungwa na Anicet Oura aliyefunga baada ya kuinasa pasi ya Alassane Kante.
Singida BS walifanikiwa kusawazisha bao hilo katika dakika ya 37 mfungaji akiwa ni Mossi Ndumumwe akimalizia pasi aliyounganishiwa na Lamine Jarjou.
Dakika sita kabla ya kutimia dakika 90, Elly Mpanzu aliihakiksihai Simba pointi tatu muhimu kwa kuiandikia Simba bao la pili na la ushindi akiitumia vizuri pasi ya Clatous Chama.
Matokeo hayo yanazidi kuiweka Singida BS pagumu katika ligi hiyo kwani katika mechi 13 ilizocheza hadi sasa imeambulia pointi 19 na inashika nafasi ya 10.
Katika mechi nyingine za ligi hiyo, Azam FC ikiwa ugenini ilitoka kidedea mbele ya Dodoma jiji kwa kuilaza mabao 3-0 wakati Namungo ikiwa ugenini Karatu ilichapwa mabao 2-0 na TRA United.

The post Simba yailaza Singida Black 2-1 first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2026/03/12/simba-yailaza-singida-black-2-1/feed/ 0
Simba yakwama, Yanga yapiga mtu mkono https://www.greensports.co.tz/2026/02/26/simba-yakwama-yanga-yapiga-mtu-mkono/ https://www.greensports.co.tz/2026/02/26/simba-yakwama-yanga-yapiga-mtu-mkono/#respond Thu, 26 Feb 2026 16:33:22 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=14367 Na mwandishi wetuWakati Yanga ikishangilia ushindi mnono wa mabao 5-0 dhidi ya JKT Tanzania katika mechi ya Ligi Kuu NBC, mambo hayakuwa mazuri kwa mtani wake Simba aliyelazimishwa sare ya bila kufungana na Dodoma Jiji FC.Mechi hizo zilizochezwa Jumatano Febuari 25, 2026 ni mechi za mwisho baina ya watani hao wa jadi kabla ya kukutana […]

The post Simba yakwama, Yanga yapiga mtu mkono first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Wakati Yanga ikishangilia ushindi mnono wa mabao 5-0 dhidi ya JKT Tanzania katika mechi ya Ligi Kuu NBC, mambo hayakuwa mazuri kwa mtani wake Simba aliyelazimishwa sare ya bila kufungana na Dodoma Jiji FC.
Mechi hizo zilizochezwa Jumatano Febuari 25, 2026 ni mechi za mwisho baina ya watani hao wa jadi kabla ya kukutana Machi Mosi, 2026 kwenye dimba la New Amaan, Zanzibar katika mwendelezo wa mechi za ligi hiyo.
Karamu ya mabao matano ya Yanga au mkono ilipatikana kwenye Uwanja wa KMC, Kinondoni, Dar es Salaam kwa mabingwa hao watetezi wa ligi kuandika bao la kwanza kunako dakika ya saba mfungaji akiwa ni Mohamed Hussein au Zimbwe Junior baada ya kuinasa pasi ya Prince Dube.
JKT walipambana na kuonesha uhai na hadi timu zinakwenda mapumziko Yanga walikuwa mbele kwa bao hilo pekee licha ya mashambulizi ya mara kwa mara langoni mwa JKT.
Kipindi cha pili mambo yalianza kuwaharibikia JKT katika dakika ya 60 baada ya kufungwa bao la pili, mfungaji akiwa Dilson Depu aliyeitumia vizuri pasi ya Israel Mwenda.
Matumaini ya JKT kutaka bao la kufufua matumaini yalianza kufifia dakika tatu baada baada ya bao la Depu pale, Mudathir Yahya alipoiandikia Yanga bao la tatu.
Mabao mengine mawili ya Yanga yalifungwa na Dube katika dakika ya 83 na Shekhan Khamis aliyekamilisha karamu ya mabao hayo katika dakika ya 89.
Kwa ushindi huo Yanga imejikita kileleni mwa msimamo wa ligi ikiwa na pointi 28 katika mechi 10 sawa na JKT ingawa Yanga ina faida katika mabao ya kufunga na kufungwa.
Kwa upande wa Simba hali ilikuwa tete kwa dakika zote 90 kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma baada ya kulazimishwa sare ya bila kufungana matokeo yanayowafanya mashabiki wa timu hiyo kubaki wakitafakari hatma ya timu yao kabla ya kuivaa Yanga.
Mechi hiyo kwa upande mwingine ilikuwa neema kwa kipa wa Dodoma Jiji, Daniel Mgore ambaye aliibuka mchezaji bora kwa namna ambavyo alifanikiwa kuzima ndoto za washambuliaji wa Simba kupata bao katika dakika zote 90.
Katika mechi nyingine ya ligi hiyo, Azam FC ikiwa nyumbani kwenye dimba la Azam Complex ilitoka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Mtibwa Sugar.

The post Simba yakwama, Yanga yapiga mtu mkono first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2026/02/26/simba-yakwama-yanga-yapiga-mtu-mkono/feed/ 0
Simba yaaga ligi ya mabingwa kwa ushindi https://www.greensports.co.tz/2026/02/15/simba-yaaga-ligi-ya-mabingwa-kwa-ushindi/ https://www.greensports.co.tz/2026/02/15/simba-yaaga-ligi-ya-mabingwa-kwa-ushindi/#respond Sun, 15 Feb 2026 11:08:00 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=14341 Na mwandishi wetuSimba imemaliza kwa kishindo mechi yake ya mwisho ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Stade Malien ya Mali huku ikiaga mashindano hayo katika hatua ya makundi kwa msimu huu wa 2025-26.Ikiwa nyumbani kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam, Jumamosi Februari 14, Simba iliandika bao hilo […]

The post Simba yaaga ligi ya mabingwa kwa ushindi first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Simba imemaliza kwa kishindo mechi yake ya mwisho ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Stade Malien ya Mali huku ikiaga mashindano hayo katika hatua ya makundi kwa msimu huu wa 2025-26.
Ikiwa nyumbani kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam, Jumamosi Februari 14, Simba iliandika bao hilo pekee mapema dakika ya tatu ya mchezo, bao lililofungwa na Anicet Oura.
Ushindi huo wa mechi ya Kundi D hata hivyo haukuwa na maana yoyote kwa Simba badala yake ni ushindi wa mechi ya kukamilisha ratiba ya michuano hiyo mikubwa kwa ngazi ya klabu barani Afrika.
Huo ndio ushindi pekee wa Simba katika kundi hilo, katika mechi zake sita za makundi timu hiyo imepoteza tatu, sare mara mbili na kushinda mechi moja.
Simba imemaliza kundi lake ikiwa mkiani baada ya kukusanya pointi tano wakati Malien wao walishafuzu na ndio vinara wa kundi hilo baada ya kukusanya pointi 11 na wanaungana na Esperance ya Tunisia ambayo pia imefuzu.
Esperance imefuzu hatua ya robo fainali ikiwa na pointi tisa baada ya ushindi wa nyumbani wa mabao 2-0 katika mechi na Petro Atletico ya Angola, mechi ambayo pia imechezwa siku moja na mechi ya Simba na Malien.
Timu nyingine zilizofuzu robo fainali ni Al Hilal ya Sudan na Mamelodi ya Afrika Kusini kutoka Kundi C ambapo Al Hilal imemaliza kundi hilo ikiwa kinara baada ya kukusanya pointi 11.
Katika Kundi B, Al Ahly ya Misri tayari imeshafuzu ikiwa imekusanya pointi tisa huku hatma ya timu ya pili ikisubiri matokeo ya mechi za Jumapili Februari 15, 2026 ambapo Yanga ya Tanzania itacheza na JS Kabylie wakati Al Ahly itaumana na AS FAR Rabat ya Morocco.
Yanga hadi sasa ina pointi tano wakati FAR Rabat ina pointi nane na kwa upande wa Kabylie ina pointi tatu na itacheza mechi yake na Yanga kukamilisha ratiba kwani haina nafasi ya kusonga mbele.

The post Simba yaaga ligi ya mabingwa kwa ushindi first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2026/02/15/simba-yaaga-ligi-ya-mabingwa-kwa-ushindi/feed/ 0
Sare yaitoa rasmi Simba Ligi ya Mabingwa https://www.greensports.co.tz/2026/02/08/sare-yaitoa-rasmi-simba-ligi-ya-mabingwa/ https://www.greensports.co.tz/2026/02/08/sare-yaitoa-rasmi-simba-ligi-ya-mabingwa/#respond Sun, 08 Feb 2026 13:41:38 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=14321 Na mwandishi wetuHesabu za Simba kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika sasa ni rasmi zimefikia tamati kwa msimu huu wa 2025-26 baada ya sare ya bao 1-1 na Petro Atletico ya Angola katika mechi iliyopigwa Jumamosi Februari 7, 2026.Ile hadithi ya haiishi mpaka iishe, hatimaye imekwisha rasmi, Simba sasa itacheza mechi yake ya mwisho ya Kundi […]

The post Sare yaitoa rasmi Simba Ligi ya Mabingwa first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Hesabu za Simba kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika sasa ni rasmi zimefikia tamati kwa msimu huu wa 2025-26 baada ya sare ya bao 1-1 na Petro Atletico ya Angola katika mechi iliyopigwa Jumamosi Februari 7, 2026.
Ile hadithi ya haiishi mpaka iishe, hatimaye imekwisha rasmi, Simba sasa itacheza mechi yake ya mwisho ya Kundi D dhidi ya Stade Malien kwa ajili ya kukamilisha ratiba za ligi hiyo.
Kabla ya mechi na Petro, Simba walikuwa wakijipa matumaini ya ushindi na kuwaombea njaa wapinzani wake wa kundi hilo lakini kwa sare yao na Petro nafasi hiyo haipo, sasa ni kujipanga kwa msimu ujao wa 2026-27.
Wakati Simba ikibaki mkiani na pointi zake mbili, Petro wao wamefikisha pointi sita na kushika nafasi ya tatu huku Stade Malien wakiendelea kushika usukani na pointi zao 11 na Esperance ya pili na pointi sitana timu hizo zitaumana Jumapili katika mechi nyingine ya kundi hilo.
Petro wakiwa nyumbani walianza mchezo kwa kasi na kupata bao la kuongoza katika dakika ya 13 mfungaji akiwa ni Pedro Pinto, bao ambalo lilidumu kwa dakika 45 za kwanza.
Zikiwa zimebakia dakika 10 kabla ya kutimia dakika 90, Simba walifanikiwa kupata bao la kusawazisha lililofungwa na Anicet Ora na kutuliza kelele za mashabiki wa Petro waliokuwa kwenye uwanja wa nyumbani.

The post Sare yaitoa rasmi Simba Ligi ya Mabingwa first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2026/02/08/sare-yaitoa-rasmi-simba-ligi-ya-mabingwa/feed/ 0