Simba - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Tue, 22 Apr 2025 10:08:52 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=6.8 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg Simba - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 Simba yailaza Stellenbosch 1-0 https://www.greensports.co.tz/2025/04/20/simba-yailaza-stellenbosch-1-0/ https://www.greensports.co.tz/2025/04/20/simba-yailaza-stellenbosch-1-0/#respond Sun, 20 Apr 2025 16:23:52 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=13285 Na mwandishi wetuSimba imeanza vizuri mechi ya kwanza ya nusu fainali Kombe la Shirikisho Afrika kwa kuilaza Stellenbosch ya Afrika Kusini bao 1-0 kwenye Uwanja wa Amaan, Zanzibar, leo Jumapili, Aprili 20, 2025.Bao pekee la Simba lilipatikana dakika ya 45 mfungaji akiwa ni Jean Ahoua kwa mpira wa adhabu uliokwenda moja kwa moja hadi wavuni […]

The post Simba yailaza Stellenbosch 1-0 first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
Na mwandishi wetu
Simba imeanza vizuri mechi ya kwanza ya nusu fainali Kombe la Shirikisho Afrika kwa kuilaza Stellenbosch ya Afrika Kusini bao 1-0 kwenye Uwanja wa Amaan, Zanzibar, leo Jumapili, Aprili 20, 2025.
Bao pekee la Simba lilipatikana dakika ya 45 mfungaji akiwa ni Jean Ahoua kwa mpira wa adhabu uliokwenda moja kwa moja hadi wavuni na kumshinda kipa Oscarine Masuluke.
Bao hilo liliibua utata baada ya wachezaji wa Stellenbosch kugomea wakidai wachezaji wa Simba waliotea hivyo kulazimika kutumia VAR kabla ya kutangazwa kuwa ni bao halali.
Simba waliutawala vyema mchezo huo kwa wachezaji wake kuonesha ubora wao wa kutengeneza nafasi nyingi za kufunga lakini tatizo la umaliziaji liliendelea kuiathiri timu hiyo.
Moja ya nafasi ya mapema Simba kuipata ni pale Kibu Dennis alipoambaa na mpira akiwa upande wa kushoto wa Stellenbosch na kupiga krosi ambayo Shomari Kapombe alibinuka vyema na kuupiga mpira staili ya tikitaka lakini mpira huo ulipaa nje ya lango.
Kasi ya Simba iliendelea na katika dakika ya 30, Ahoua aliunasa mpira na kumuunganishia Elly Mpanzu ambaye aliukokota kidogo kabla ya kufumua shuti kali la mguu wa kushoto ambalo liliokolewa vyema na kipa wa Stelenbosch.
Baada ya kuona kasi ya Simba inawazidi wachezaji wa Stellenbosch walianza kucheza rafu na mwamuzi kulazimika kuwapa kadi za njano Enyimnaya na Jabaar kwa kuwachezea rafu Mpanzu na Kibu.
Dakika tano baadaye Stellenbosch nao walijibu shambulizi baada ya kipa kuokoa mpira wa kona na kuwasaidia kutengeneza shambulizi lililoelekezwa upande wa kulia wa Simba.
Shambulizi hilo hata hivyo lilikwama baada ya Zimbwe Jr aliyehamia upande huo kumdhibiti mchezaji wa Stellenbosch wakati huo Kapombe anayecheza zaidi upande wa kulia akiwa amehamia upande wa kushoto ambao anacheza Zimbwe.
Kipindi cha pili, Stellenbosch walikianza kwa kufanya mabadiliko kadhaa yaliyoonekana kuwapa uhai na kumuweka katika wakati mgumu kipa Musa Camara wa Simba.


Simba nao walibadilika na kuanza kulisakama lango la wapinzani wao kwa kutengeneza nafasi nyingi ambazo hata hivyo walikwama katika kuzitumia nafasi hizo.
Nafasi mojawapo ya mwisho ni ile waliyoipata ikiwa imebaki dakika moja katika dakika sita za nyongeza baada ya Ahoua kuunganishiwa pasi ya chinichini na Mpanzu naye kumlamba chenga kipa Masuluke lakini shuti alilopiga la mguu wa kushoto lilitoka nje.
Katika mechi hiyo timu zote zilifanya mabadiliko kadhaa, Stellenbosch wakiwatoa De Jong na kumuingiza Bans na Jabaar ambaye nafasi yake aliingia Palace.
Simba iliwatoa Zimbwe na kuingia Valentine Nouma, Kibu akaingia Joshua Mutale, Deborah Fernandes akaingia kuchukua nafasi ya Chamaou Karabou wakati Ateba akaingia kuchukua nafasi ya Steven Mukwala.
Timu hizo zinatarajia kurudiana Aprili 27 nchini Afrika Kusini, mechi ambayo mshindi atajikatia moja kwa moja tiketi ya kucheza mechi ya fainali ya michuano hiyo dhidi ya mshindi wa mechi ya nusu fainali nyingine kati ya CS Constantine na RS Berkane.

The post Simba yailaza Stellenbosch 1-0 first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2025/04/20/simba-yailaza-stellenbosch-1-0/feed/ 0
Simba yaingia mkataba wa bilioni 38 https://www.greensports.co.tz/2025/04/17/simba-yaingia-mkataba-wa-bilioni-38/ https://www.greensports.co.tz/2025/04/17/simba-yaingia-mkataba-wa-bilioni-38/#respond Thu, 17 Apr 2025 09:50:02 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=13266 Na mwandishi wetuKlabu ya Simba imetangaza kuingia mkataba wa miaka mitano wenye thamani ya Sh bilioni 38 za Kitanzania na Kampuni ya Jayrutty Investment ambayo itahusika na mauzo ya jezi na mambo mengine.Hafla ya kusaini mkataba huo ilifanyika Jumatano hii Aprili 16, 2025 na kuhudhuriwa na viongozi wa Simba na wadau mbalimbali wa michezo akiwamo […]

The post Simba yaingia mkataba wa bilioni 38 first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
Na mwandishi wetu
Klabu ya Simba imetangaza kuingia mkataba wa miaka mitano wenye thamani ya Sh bilioni 38 za Kitanzania na Kampuni ya Jayrutty Investment ambayo itahusika na mauzo ya jezi na mambo mengine.
Hafla ya kusaini mkataba huo ilifanyika Jumatano hii Aprili 16, 2025 na kuhudhuriwa na viongozi wa Simba na wadau mbalimbali wa michezo akiwamo naibu waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Hamis Mwinjuma ‘MwanaFA’.
Menyekiti wa kamati ya tenda ya Simba, Seif Muba alisema kwamba walipokea barua nyingi za maombi ya tenda hiyo lakini ofa ya Jayrutty imewashawishi kuwapa tenda hiyo.
Muba alisema kwa mantiki hiyo wamekubali kuwapa Jayrutty haki ya matumizi ya nembo ya klabu ya Simba kwa vile mbali na fedha kuna manufaa mengine mengi kwa klabu yao.
Alisema awali kampuni nane zilijitokeza lakini ni sita ndizo zilizowasilisha madokezo yao na kila kitu kilikuwa wazi kabla ya Jayrutty kushinda tenda hiyo na tayari wameweka kiasi cha Sh bilioni 38.
Akizungumzia mkataba huo, Mkurugenzi wa Jayrutty Investment, Joseph Rwagasira alizitaja baadhi ya faida ambazo klabu ya Simba itazipata kupitia mkataba huo kwa kipindi chote cha miaka mitano.
Rwegasira alisema jambo la kwanza watakalofanya ni kuijengea klabu hiyo uwanja wenye uwezo wa kuchukua mashabiki kati ya 10,000 hadi 12,000 na watafanya hivyo katika uwanja wa klabu hiyo uliopo Bunju, nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.
Alisema kwamba mbali na ujenzi huo lakini pia kila mwaka watatoa Sh milioni 100 kwa ajili ya soka la vijana, sh milioni 100 nyingine kwa maandalizi ya msimu na kiasi kingine kama hicho kwa ajili ya tamasha la Simba Day.
Sambamba na hilo, Jayrutty pia watatoa Sh milioni 450 kwa kila mwaka fedha ambazo zitakwenda kwa wachezaji wakati jezi za klabu hiyo sasa zitatengenezwa na kampuni kubwa duniani ingawa hakuitaja jina.
Kwa upande wake naibu waziri Mwana FA alisema serikali inapongeza kuingia kwa mkataba huo huku akielezea kuvutiwa zaidi na mpango wa ujenzi wa uwanja.
Mwana FA alisema uwanja huo unaweza kutumiwa kwa mechi za ndani wakati zile za kimataifa zikiendelea kuchezwa kwenye Uwanja wa Mkapa ambao pia utakuwa umepunguziwa matumizi.

The post Simba yaingia mkataba wa bilioni 38 first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2025/04/17/simba-yaingia-mkataba-wa-bilioni-38/feed/ 0
Camara shujaa, Simba ikiitoa Al Masry kwa penalti 4-1 https://www.greensports.co.tz/2025/04/10/camara-shujaa-simba-ikiitoa-al-masry-kwa-penalti-4-1/ https://www.greensports.co.tz/2025/04/10/camara-shujaa-simba-ikiitoa-al-masry-kwa-penalti-4-1/#respond Wed, 09 Apr 2025 22:01:59 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=13229 Na mwandishi wetuKipa Musa Camara ameibuka shujaa kwa kuokoa mikwaju miwili ya penalti na kuiwezesha Simba kufuzu nusu fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika kwa kuitoa Al Masry ya Misri kwa penalti 4-1.Ikiwa nyumbani kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam Jumatano hii Aprili 9, 2025, Simba ilitoka na ushindi wa mabao 2-0 katika dakika […]

The post Camara shujaa, Simba ikiitoa Al Masry kwa penalti 4-1 first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Kipa Musa Camara ameibuka shujaa kwa kuokoa mikwaju miwili ya penalti na kuiwezesha Simba kufuzu nusu fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika kwa kuitoa Al Masry ya Misri kwa penalti 4-1.
Ikiwa nyumbani kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam Jumatano hii Aprili 9, 2025, Simba ilitoka na ushindi wa mabao 2-0 katika dakika 90 za kawaida hivyo kuingia kwenye mikwaju ya penalti baada ya timu hizo kuwa na matokeo ya jumla ya sare ya mabao 2-2.
Sare hiyo ya jumla imekuja baada ya Simba kulala kwa 2-0 katika mechi ya kwanza baina ya timu hizo iliyopigwa, Ismailia, Misri, Jumatano iliyopita.
Mikwaju ya penalti
Simba ndio waliokuwa wa kwanza kupiga penalti iliyopigwa na Jean Ahoua ambaye alikwenda taratibu na kuujaza mpira wavuni kwa shuti la mguu wa kulia lililomshinda kipa, Mahmoud Gad.
Baada ya hapo Camara akaonesha ushujaa wake kwa kuokoa kwa miguu shuti la chinichini lililopigwa na Mido Gaber wakati Simba wakafunga penalti ya pili iliyopigwa kiufundi na Steven Mukwala.
Mukwala alirudi nyuma na kumchambua vyema kipa ambaye alijikuta akiruka upande wake wa kulia na mpira kujaa wavuni upande wa kushoto.
Al Masry walifanikiwa kupata bao katika penalti yao ya pili mfungaji akiwa Ben Youssef wakati Simba nao wakapata bao kwenye penalti ya tatu mfungaji akiwa Kibu Denis.


Camara kwa mara nyingine akaonesha umahiri wake kwa kuokoa penalti ya tatu ya Masry iliyopigwa na Mahmoud Hamada na kipa huyo kuruka upande wa kulia na kuuwahi mpira.
Baada ya hapo Shomari Kapombe akakamilisha hesabu kwa kuifungia Simba penalti ya nne ambayo ilifanya uwanja ulipuke kwa shangwe kutoka kwa mashabiki wa Simba na kuipa Simba ushindi wa 4-1 moja kwa moja hadi nusu fainali.
Kapombe baada ya kufunga penalti hiyo alikimbiliwa na wachezaji wenzake na benchi zima la ufundi na kushangilia na mchezaji huyo ambaye alivua jezi na kubaki na fulana ya ndani iliyoandikwa Jesus 100% yaani Yesu asilimia 100.
Dakika 90 zilivyokuwa
Katika dakika 90 za kawaida, Simba waliandika bao lao la kwanza dakika ya 22 mfungaji akiwa Elly Mpanzu wakati bao la pili lilifungwa na Steven Mukwala dakika ya 32.
Simba kama ilivyokuwa katika mechi ya kwanza baina ya timu hizo, kwa mara nyingine ilifanikiwa kuutawala mchezo na kutengeneza nafasi nyingi za kufunga lakini tatizo lilikuwa katika umaliziaji.
Kwa jinsi hali ya mchezo ilivyokuwa Simba walikuwa na kila sababu ya kumaliza dakika 90 wakiwa washindi kwa zaidi ya mabao matatu na kusingekuwa na sababu ya kuingia kwenye penalti.

Al Masry kama kawaida yao walionekana kuzidiwa na kutumia mara kwa mara mbinu ya kuchelewesha muda kwa kujiangusha na wakati mwingine kuingia katika mzozo na watu wa huduma ya kwanza.
Kutokana na matukio hayo kujitokeza mara kwa mara, haikushangaza mechi kuchezwa kwa dakika 10 za nyongeza baada ya 90 za kawaida kukamilika.
Rais Samia awapongeza
Wakati huo huo, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan kupitia mtandao wa X (Twitter) aliipongeza Simba kwa ushindi huo ambao aliutaja kuwa ni burudani kwa Watanzania wote.
“Pongezi za dhati kwa Klabu ya Simba kwa ushindi katika mchezo wa mashindano ya Kombe la Shirikisho Afrika, ushindi wenu ni furaha kwa mashabiki wenu na burudani kwa Watanzania wote. Ninawatakia kila la kheri katika nusu fainali,” ilijieleza taarifa hiyo ya rais.
Baada ya ushindi huo, Simba sasa inasubiri kucheza mechi ya nusu fainali na mshindi wa mechi kati ya Zamalek ya Misri na Stellenbosch ya Afrika Kusini.

The post Camara shujaa, Simba ikiitoa Al Masry kwa penalti 4-1 first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2025/04/10/camara-shujaa-simba-ikiitoa-al-masry-kwa-penalti-4-1/feed/ 0
Mwamposa aitwa mechi ya Simba, AL Masry https://www.greensports.co.tz/2025/04/05/mwamposa-aitwa-mechi-ya-simba-al-masry/ https://www.greensports.co.tz/2025/04/05/mwamposa-aitwa-mechi-ya-simba-al-masry/#respond Sat, 05 Apr 2025 13:07:21 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=13210 Na mwandishi wetuKlabu ya soka ya Simba imezungumza na mhubiri maarufu Tanzania, Boniface Mwamposa ili awe mgeni maalum wa mechi yao ya robo fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Al Masry ya Misri.Kauli hiyo imetolewa leo Jumamosi Aprili 5, 2025 na msemaji wa klabu hiyo, Ahmed Ally akiwa jijini Dar es Salaam kwa […]

The post Mwamposa aitwa mechi ya Simba, AL Masry first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Klabu ya soka ya Simba imezungumza na mhubiri maarufu Tanzania, Boniface Mwamposa ili awe mgeni maalum wa mechi yao ya robo fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Al Masry ya Misri.
Kauli hiyo imetolewa leo Jumamosi Aprili 5, 2025 na msemaji wa klabu hiyo, Ahmed Ally akiwa jijini Dar es Salaam kwa ziara inayoaminika kuwa na lengo la kuitangaza mechi hiyo.
Mwamposa au Bulldozer ambaye pia waumini wake wanamwita kwa jina la mtume ni miongoni mwa wahubiri wenye ushawishi mkubwa miongoni mwa waumini wa dini ya kikristo nchini.
Akizungumzia uamuzi wa kumualika Bulldozer na kauli yake kuonekana kwenye vyanzo vya habari vya klabu ya Simba, Ally alisema safari hii wamedhamiria kualika kila mtu mwenye mchango kwenye jamii.

“Safari hii tumedhamiria Ubaya Ubwela na tunaalika kila mtu mwenye mchango kwenye jamii hii, wachawi wengi ndugu zangu, kuna watu wamekunja nafsi, kwa hiyo namtangaza mgeni mwingine maalum, Mtume Boniface Mwamposa. Tunafanya naye mazungumzo.” alisema Ally.


Katika kuwataka mashabiki wa Simba kuhudhuria kwa wingi katika mechi hiyo, Ally pia alinukuliwa akisema kwamba ni lazima wanasimba wajitofautishe na mashabiki wa timu nyingine kwa kutobaki nyumbani siku ya mechi.
“Siku hiyo unabaki nyumbani unafanya nini, tujitofautishe an mashabiki wa timu nyingine, tofauti ya wao na sisi siku hiyo wao wanabaki nyumbani na sisi tunakwenda Uwanja wa Mkapa,” alisema Ally.
Mgeni mwingine maalum katika mechi hiyo ni rais wa TFF, Wallace Karia ambaye pia ni rais wa Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (Cecafa) na mjumbe wa kamati ya utendaji ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF).
Simba itaumana na Al Masry katika mechi ya pili ya robo fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika, mechi itakayopigwa Aprili 9, 2025 kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam.
Katika mechi ya kwanza baina ya timu hizo iliyopigwa Aprili 2, 2025, Ismailia, Misri, Simba ikiwa ugenini ililala kwa mabao 2-0.

The post Mwamposa aitwa mechi ya Simba, AL Masry first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2025/04/05/mwamposa-aitwa-mechi-ya-simba-al-masry/feed/ 0
Al Masry yailaza Simba 2-0 https://www.greensports.co.tz/2025/04/02/al-masry-yailaza-simba-2-0/ https://www.greensports.co.tz/2025/04/02/al-masry-yailaza-simba-2-0/#respond Wed, 02 Apr 2025 19:50:02 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=13196 Ismailia, MisriMambo si mazuri kwa Simba nchini Misri baada ya kulala kwa mabao 2-0 mbele ya Al Masry katika mechi ya robo fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika iliyopigwa leo Jumatano, Aprili 2, 2025.Simba iliyokuwa ugenini licha ya kulisakama lango la Al Masry kwa mashambulizi ya mara kwa mara lakini walishindwa kutumia nafasi nyngi walizotengeneza […]

The post Al Masry yailaza Simba 2-0 first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Ismailia, Misri
Mambo si mazuri kwa Simba nchini Misri baada ya kulala kwa mabao 2-0 mbele ya Al Masry katika mechi ya robo fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika iliyopigwa leo Jumatano, Aprili 2, 2025.
Simba iliyokuwa ugenini licha ya kulisakama lango la Al Masry kwa mashambulizi ya mara kwa mara lakini walishindwa kutumia nafasi nyngi walizotengeneza na hatimaye kupoteza mechi hiyo.
Kwa matokeo hayo Simba sasa itakuwa na kazi ngumu ya kufanya Aprili 9 timu hizo zitakaporudiana kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.
Mambo yalianza kuwaribikia Simba dakika ya 16 ya mchezo huo baada ya wenyeji Al Masry kuandika bao la kwanza lililofungwa na Abdelrahim Degmoum kwa shuti kali la mguu wa kushoto.
Shuti hilo la chinichini awali ilionekana kama kipa wa Simba Musa Camara angeudaka mpira huo lakini ulidunda na kumpoteza kabla ya kujaa wavuni.
Baada ya bao hilo Simba walionesha dhamira ya kutaka kusawazisha na dakika kama tano za mwisho kabla ya mapumziko, Al Masry walikuwa na kazi ya kuokoa na kujaribu kuchelewesha muda kwa namna ambavyo Simba waliwaweka katika wakati mgumu.
Tatizo la umaliziaji hata hivyo liliigharimu Simba kuanzia dakika ya 46 baada ya Kibu Denis kupora mpira na kuonesha uwezo binafsi lakini akiwa katika nafasi ambayo ilitarajiwa angetoa pasi alifumua shuti lililotoka nje.
Dakika tano baadaye, Elly Mpanzu alichezewa rafu na Tahir Taim na mwamuzi kuamuru upigwe mpira wa adhabu lakini shuti alilopiga Jean Ahoua liliokolewa na kipa wa Al Masry.
Simba walifanya shambulizi lingine dakika ya 70 baada ya Shomary Kapombe kutoa pasi ya kichwa kwa Ateba ambaye wakati akielekea kwenye lango la AL Masry kipa alimzuia kwa mkono na hatimaye mpira kutoka nje.
Tukio hilo liliwaamsha wachezaji wa Simba ambao waliamini mwamuzi angetoa penalti lakini hakufanya hivyo licha ya Ateba kulala chini akilalamikia kuumia na alichofanya mwamuzi ni kusimamisha mchezo.
Dakika ya 82 Kapombe alimuunganishia pasi Mpanzu ambaye licha ya kumtoka kipa lakini shuti alilopiga lilipaa juu ya lango na kuwaachia mshangao mashabiki wake.
Katika dakika ya 85 Steven Mukwala aliyeingia kuchukua nafasi ya Ateba alipiga krosi iliyompita Kibu na kutua miguuni mwa Kapombe lakini mchezaji huyo alishindwa kuumiliki vyema mpira miguuni na hatimaye mpira huo kutua mikononi mwa kipa wa Al Masry.
Wakati wote huo Al Masry walikuwa wakijihami na kusogea na mpira mara chache mno kwenye lango la Simba kabla ya kuwashtukiza kwa bao la dakika ya 89 lililotokana na juhudi za wachezaji walioingia kipindi cha pili ambao ni John Okoye aliyefunga akiitumia krosi ya Mohammed Hussein (si wa Simba).

The post Al Masry yailaza Simba 2-0 first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2025/04/02/al-masry-yailaza-simba-2-0/feed/ 0
Davids akiri mechi na Al Masry ngumu https://www.greensports.co.tz/2025/04/01/davids-akiri-mechi-na-al-masry-ngumu/ https://www.greensports.co.tz/2025/04/01/davids-akiri-mechi-na-al-masry-ngumu/#respond Tue, 01 Apr 2025 19:28:55 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=13184 Cairo, MisriSimba kesho Jumatano Aprili 2, 2025 inaanza kuisaka tiketi ya nusu fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika ikiwa ugenini kuumana na Al Masry ya Misri huku kocha wa timu hiyo Fadlu Davids akikiri mechi itakuwa ngumu.Wawakilishi hao pekee wa Tanzania katika michuano hiyo inayoandaliwa na Shirikisho la Soka Afrika (CAF) tayari wapo nchini Misri […]

The post Davids akiri mechi na Al Masry ngumu first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Cairo, Misri
Simba kesho Jumatano Aprili 2, 2025 inaanza kuisaka tiketi ya nusu fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika ikiwa ugenini kuumana na Al Masry ya Misri huku kocha wa timu hiyo Fadlu Davids akikiri mechi itakuwa ngumu.
Wawakilishi hao pekee wa Tanzania katika michuano hiyo inayoandaliwa na Shirikisho la Soka Afrika (CAF) tayari wapo nchini Misri kwa takriban wiki moja sasa.
Simba baada ya mechi hiyo ya kwanza ya hatua ya robo fainali watarudiana na Al Masry Aprili 9 kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.
Davids anaamini uzoefu walioupata kwa kuwa kwao nchini Misri kujiandaa na mechi hiyo utakuwa na manufaa kwao ingawa mechi itakuwa ngumu.
Kocha huyo ambaye alijiunga na Simba Julai mwaka jana amefanikiwa kutengeneza timu iliyotoa ushindani ambayo imemaliza mechi zake za hatua ya makundi ikiwa kinara wa kundi lake.
Akizungumzia matarajio yake katika hatua ya robo fainali, Davids kupitia mahojiano yaliyochapishwa kwenye mtandao wa CAF alisema kila mechi itakuwa ngumu lakini yuko tayari kwa changamoto ya michuano hiyo pamoja na ligi ya ndani.
Baada ya kupangwa kuanza na Al Masry katika robo fainali, Davids alisema walimkubali mpinzani huyo wakitambua kuwa kwa hatua waliyofikia kila timu unayopangiwa ni ngumu.

“Tumemkubali mpinzani wetu, kila timu utakayocheza nayo itakuwa ngumu na wao wanafanya vizuri kwenye ligi ya nchini Misri, mechi itakuwa ngumu hasa unapocheza mbali na nyumbani,” alisema Davids.


Davids licha ya kukiri ugumu huo pia aliendelea kusisitiza kwamba wamefanya maandalizi ya mchezo huo nchini Misri na kujizoesha vyema na mazingira pamoja na kucheza na baadhi ya timu za nchini Misri.
“Mechi haitokuwa rahisi ni kama zilivyo mechi nyingine za robo fainali lakini tuko tayari,” alisema Davids.
Akizungumzia umuhimu wa kuwa kinara katika kundi lake, Davids alisema hilo ni jambo zuri kwani inakupa nafasi ya kucheza mechi ya pili kwenye uwanja wa nyumbani mbele ya mashabiki wako na hivyo kuwa faida.

“Hilo ni jambo zuri unacheza ugenini kwanza na kwa aina ya matokeo unajua nini cha kufanya na kukitarajia na aina ya matokeo unayohitaji ili kufuzu,” alisema.


Davids alifafanua kwa kusema kwamba wanapokuwa mbele ya mashabiki wao Dar es Salaam itawapa faida ya kucheza mechi ya pili nyumbani kwani wanafahamu kuwa katika mashindano haya inapofikia hatua ya robo fainali mechi zinakuwa ngumu hasa unapocheza ugenini.
“Ni lazima uwe katika ubora kwa kila sekunde ya mchezo ili uweze kufuzu hatua inayofuata,” alisema Davids.

The post Davids akiri mechi na Al Masry ngumu first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2025/04/01/davids-akiri-mechi-na-al-masry-ngumu/feed/ 0
Kibu afuta ukame wa mabao Simba ikiilaza Dom Jiji 6-0 https://www.greensports.co.tz/2025/03/14/kibu-afuta-ukame-wa-mabao-simba-ikiilaza-dom-jiji-6-0/ https://www.greensports.co.tz/2025/03/14/kibu-afuta-ukame-wa-mabao-simba-ikiilaza-dom-jiji-6-0/#respond Fri, 14 Mar 2025 20:27:21 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=13128 Na mwandishi wetuSimba imeilaza Dodoma Jiji 6-0 katika mechi ya Ligi Kuu NBC ilyopigwa leo Ijumaa Machi 14, 2025 kwenye Uwanja wa KMC, Dar es Salaam huku Kibu Denis akifunga mabao mawili kati ya hayo na kuwa kama amefuta ukame wa mabao. Kibu ambaye pia ameibuka mchezaji bora wa mechi hiyo, amekuwa na mchango mkubwa […]

The post Kibu afuta ukame wa mabao Simba ikiilaza Dom Jiji 6-0 first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Simba imeilaza Dodoma Jiji 6-0 katika mechi ya Ligi Kuu NBC ilyopigwa leo Ijumaa Machi 14, 2025 kwenye Uwanja wa KMC, Dar es Salaam huku Kibu Denis akifunga mabao mawili kati ya hayo na kuwa kama amefuta ukame wa mabao.

Kibu Denis akiwa ameshika tuzo yake ya mchezaji bora wa mchezo


Kibu ambaye pia ameibuka mchezaji bora wa mechi hiyo, amekuwa na mchango mkubwa katika mabao ya timu hiyo kwenye ligi msimu huu lakini ni mara ya kwanza kuifungia Simba tangu afanye hivyo takriban mwaka mmoja na miezi minne iliyopita.
Mashabiki wa Simba wanakumbuka mara ya mwisho Kibu kuifungia bao timu yao ilikuwa kwenye mechi dhidi ya mahasimu wao Yanga, mechi ambayo Simba ililala kwa mabao 5-1 huku bao pekee la Simba likifungwa na Kibu.
Baada ya kufunga bao la kwanza hii leo, Kibu alishangilia huku akionesha kama ishara ya kujifuta na kuanza upya akiwa kama anawaambia mashabiki hao kwamba sasa wataona makali yake kwani amefuta ukame uliokuwa ukimuandama.
Kwa ushindi huo Simba sasa imefikisha pointi 57 katika mechi 22 ikiwa nafasi ya pili nyuma ya vinara Yanga wanaoshika usukani wakiwa na pointi 58 katika mechi 22 kama za Simba.
Ushindi wa mechi ya leo ambayo ni ya kiporo ulianzia dakika ya 16 kwa bao la Elly Mpanzu ambaye aliizidi ujanja safu ya ulinzi ya Dom Jiji baada ya kuinasa pasi ya Kibu na kufumua shuti lililojaa wavuni.
Simba waliongeza bao la pili dakika ya 21 lililofungwa na Jean Ahoua ambaye aliitumia pasi ya chinichini ya Mohamed Hussein kabla ya kuupiga mpira uliogonga mwamba na kumshinda kipa Allain Ngereka.
Dom Jiji walipachikwa bao la tatu dakika ya 45 lililofungwa tena na Ahoua na kwa mara nyingine pasi ya Kibu ndiyo iliyozaa bao hilo.
Mambo yaliendelea kuwa magumu kwa Dom Jiji kwani dakika moja tu baada ya kuanza kipindi cha pili, walipachikwa bao la nne mfungaji akiwa Steven Mukwala kwa kisigino akimalizia kazi nzuri ya Mpanzu.
Kibu aliwainua kwa mara nyingine vitini mashabiki wa Simba katika dakika ya 54 akifunga bao la kichwa kwa mpira wa kona ambapo alishangilia bao hilo kwa kuonesha ishara ya kujisafisha na ukame wa mabao uliokuwa ukimuandama.
Mashabiki wa Simba waliinuliwa tena vitini na Kibu ambaye aliifungia timu hiyo bao la sita na la mwisho katika dakika ya 65.
Simba pamoja na mabao hayo bado waliendelea kulisakama lango la Dom Jiji na dakika ya 88 bado kidogo wapate bao la saba kupitia kwa Ahoua lakini uimara wa kipa Ngereka ulikuwa kikwazo baada ya kuokoa shuti la Ahoua alilopiga chinichini.

The post Kibu afuta ukame wa mabao Simba ikiilaza Dom Jiji 6-0 first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2025/03/14/kibu-afuta-ukame-wa-mabao-simba-ikiilaza-dom-jiji-6-0/feed/ 0
Mechi Yanga, Simba yaahirishwa https://www.greensports.co.tz/2025/03/08/mechi-yanga-simba-yaahirishwa/ https://www.greensports.co.tz/2025/03/08/mechi-yanga-simba-yaahirishwa/#respond Sat, 08 Mar 2025 12:41:33 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=13102 Na Hassan KinguMechi ya Ligi Kuu NBC baina ya mahasimu wa soka nchini Tanzania, Yanga na Simba iliyokuwa ichezwe leo Jumamosi Machi 8, 2025, imeahirishwa.Uamuzi huo umetangazwa leo Jumamosi Machi 8 na Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) na taarifa zake kutufikia saa takriban nne kabla ya muda wa kuchezwa mechi hiyo.Mechi ilipangwa kuchezwa majira […]

The post Mechi Yanga, Simba yaahirishwa first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
Na Hassan Kingu
Mechi ya Ligi Kuu NBC baina ya mahasimu wa soka nchini Tanzania, Yanga na Simba iliyokuwa ichezwe leo Jumamosi Machi 8, 2025, imeahirishwa.
Uamuzi huo umetangazwa leo Jumamosi Machi 8 na Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) na taarifa zake kutufikia saa takriban nne kabla ya muda wa kuchezwa mechi hiyo.
Mechi ilipangwa kuchezwa majira ya saa moja na robo usiku kwenye Uwanja wa Mkapa Dar es Salaam na uamuzi huo umefikiwa baadhi ya mashabiki wakiwa tayari wamefika uwanjani hapo.
Uamuzi wa bodi hiyo umekuja baada ya kuibuka sintofahamu kutokana na kitendo cha Simba ambao ni timu mgeni kuzuiwa na timu mwenyeji ambao ni Yanga kuutumia uwanja husika kwa ajili ya mazoezi kama taratibu zinavyotaka.
Simba baada ya kuzuiwa kufanya mazoezi iliwasilisha malalamiko yake TPLB huku ikielezea nia yake ya kutoshiriki mechi hiyo baada ya kunyimwa haki yao ya kikanuni ya kuutumia uwanja huo kwa ajili ya mazoezi.
Bodi kupitia Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi ya TPLB iliitisha kikao cha dharura na baada ya taarifa mbalimbali kuwafikia kutoka kwa maofisa wake na vyanzo husika ilibaini mambo kadhaa.
Kamati hiyo ilibaini kuwa Simba wakati wakielekea uwanjani kuitumia haki yao ya kuutumia uwanja huo kwa mazoezi haikuwasiliana na ofisa yeyote wa mchezo.


Simba pia haikuwasiliana na timu mwenyeji wala mamlaka ya uwanja kuhusu nia yao ya kuutumia uwanja huo kwa mazoezi ili maandalizi yafanyike kikanuni.
Kamati pia ilibaini kuwa walinzi ambao baadhi yao walifahamika kwa sura kuwa ni wa Yanga walishiriki tukio la kuzuia basi la Simba kuingia uwanjani kinyume na taratibu za mchezo wa ligi kuu.
Bodi pia ilipokea taarifa ya ofisa usalama wa mchezo ambayo imeainisha matukio kadhaa yaliyoambatana na tukio la Simba kuzuiwa kufanya mazoezi.
Kutokana na matukio yote hayo bodi imeona yanahitaji uchunguzi ambao hauwezi kukamilika kwa wakati na hivyo imeamua kuiahirisha mechi hiyo.
“Kutokana na matukio hayo bodi, kupitia kamati ya uendeshaji imeamua kuahirisha mchezo husika ili kutoa nafasi ya kupata taarifa zaidi zitakazosaidia kufanya maamuzi ya haki,” ilieleza kwa ufafanuzi sehemu ya taarifa ya bodi.
Bodi pia imeahidi kutoa taarifa kamili kuhusu tukio hilo na kutangaza tarehe ya mchezo huo mapema iwezekanavyo.
Pigo kwa Yanga, mashabiki
Uamuzi wa kuahirisha mechi hiyo utakuwa pigo kubwa kwa mashabiki ambao baadhi yao wamesafiri kutoka mikoani na hata nje ya nchi kwa ajili ya kushuhudia mechi hiyo.
Mashabiki hao bila shaka wengi wao waliamini kuwa mechi inapochezwa Jumamosi, wnaaweza kuwa na muda wa kutosha kurejea mikoani kuendelea na shughuli zao kama kawaida kuanzia Jumatatu.
Kwa upande wa Yanga pia haijulikani hali itakuwaje kutokana na uamuzi huo kwani walishaahidi mapema katika taarifa yao kwamba hawatokuwa tayari kucheza mechi siku nyingine zaidi ya leo.
Je wataafikiana na uamuzi wa bodi kuahirisha mechi au watasimamia msimamo wao wa kutokuwa tayari kucheza mechi hiyo siku nyingine zaidi ya leo?

The post Mechi Yanga, Simba yaahirishwa first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2025/03/08/mechi-yanga-simba-yaahirishwa/feed/ 0
Mechi Yanga, Simba njia panda https://www.greensports.co.tz/2025/03/08/mechi-ya-yanga-simba-njia-panda/ https://www.greensports.co.tz/2025/03/08/mechi-ya-yanga-simba-njia-panda/#respond Sat, 08 Mar 2025 11:26:11 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=13095 Na Hassan KinguUtata umeibuka kuhusu mechi ya Simba na Yanga ambayo imepangwa kuchezwa leo Jumamosi Machi 8, 2025 na huenda mechi hiyo isichezwe baada ya Simba kuzuiwa kufanya mazoezi.Yanga ambao ni wenyeji wa mechi hiyo wanadaiwa kuwazuia Simba kufanya mazoezi siku moja kabla ya mechi kwa sababu ambazo hazijawekwa wazi ingawa nao wametoa taarifa leo […]

The post Mechi Yanga, Simba njia panda first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
Na Hassan Kingu
Utata umeibuka kuhusu mechi ya Simba na Yanga ambayo imepangwa kuchezwa leo Jumamosi Machi 8, 2025 na huenda mechi hiyo isichezwe baada ya Simba kuzuiwa kufanya mazoezi.
Yanga ambao ni wenyeji wa mechi hiyo wanadaiwa kuwazuia Simba kufanya mazoezi siku moja kabla ya mechi kwa sababu ambazo hazijawekwa wazi ingawa nao wametoa taarifa leo Jumamosi wakisisitiza mechi ipo kama kawaida.
Simba katika raarifa yao walielezea kitendo cha kuzuiwa kufanya mazoezi na kuitaja kanuni ya ligi kuu inayotaka timu mgeni kufanya mazoezi kwenye uwanja itakayochezwa mechi angalau siku moja kabla ya mechi.
Katika hoja yao Simba wanadai kunyimwa fursa ya kufanya mazoezi katika Uwanja wa Benjamin Mkapa na wenyeji wa mechi Yanga kwa makusudi licha ya kufika uwanjani katika muda husika.
Baada ya kufika uwanjani Ijumaa kwa ajili ya mazoezi, waliarifiwa na meneja uwanja kuwa hana maelekezo ya kuruhusu mazoezi kufanyika bila ya taarifa ya kamishna wa mchezo husika.


Katika hali ambayo haikutarajiwa, Simba katika taarifa yao wanadai kuwa hata baada ya kamishna wa mchezo kufika, mabaunsa wanaoaminika kuwa wa Yanga walizuia msafara wa Simba kuingia uwanjani hapo kufanya mazoezi.
Iliwachukua Simba saa takriban mbili kutafuta ufumbuzi wa suala hilo lakini jitihada zao hazikuzaa matunda na hatimaye wakaamua kuondoka eneo hilo kwa sababu walizozitaja kuwa ni za kiusalama.
Kutokana na sakata hilo, Simba wameahidi kutoshiriki katika mchezo wao na Yanga na kutaka hatua stahiki zichukuliwe dhidi ya wahusika wote.
Taarifa ya Yanga
Baada ya uamuzi huo wa Simba, Yanga nao wametoa taarifa wakisisitiza kwamba mchezo wao dhidi ya Simba uliopangwa kufanyika leo Jumamosi ya Machi 8, 2025 upo pale pale kama ilivyopangwa na hakuna mabadiliko yoyote.
Yanga kama wenyeji wa mchezo wamedai kufuata taratibu zote husika kama inavyoelekezwa kwenye kanuni za ligi hiyo na maandalizi yote yapo tayari.


Zaidi ya hilo uongozi wa Yanga umeahidi kupeleka timu uwanjani na hautakuwa tayari kucheza mchezo huo siku nyingine tofauti na leo yaani Jumamosi ya Machi 8, 2025.
Wakati Yanga wakitoa kauli hiyo, kiongozi mmoja mwandamizi wa Simba amenukuliwa katika vyanzo mbalimbali vya habari akisema kwamba Simba hawatopeleka timu hadi wahusika wa kadhia hiyo watakapoadhibiwa na mamlaka husika za soka.
Mazingira yote hayo yanaifanya mechi hiyo maarufu kwa jina la Kariakoo au Dar Derby kuwa njia panda hadi wakati huu.

The post Mechi Yanga, Simba njia panda first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2025/03/08/mechi-ya-yanga-simba-njia-panda/feed/ 0
Namba ngumu Simba, Yanga https://www.greensports.co.tz/2025/03/08/namba-ngumu-simba-yanga/ https://www.greensports.co.tz/2025/03/08/namba-ngumu-simba-yanga/#respond Sat, 08 Mar 2025 09:12:17 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=13091 Na Hassan KinguMashabiki Simba na Yanga wanacharurana kuelekea mechi yao ya Jumamosi Machi 8, 2025, kila upande ukitamba kuwa bora kumshinda mwenzake lakini namba ambazo haziongopi zina jibu tofauti.Kwa mujibu wa namba ubora wa timu hizo katika Ligi Kuu NBC msimu huu hautofautiani kwa sana, ukweli wa namba unatupa picha tofauti kuhusu majigambo na kuzodoana […]

The post Namba ngumu Simba, Yanga first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
Na Hassan Kingu
Mashabiki Simba na Yanga wanacharurana kuelekea mechi yao ya Jumamosi Machi 8, 2025, kila upande ukitamba kuwa bora kumshinda mwenzake lakini namba ambazo haziongopi zina jibu tofauti.
Kwa mujibu wa namba ubora wa timu hizo katika Ligi Kuu NBC msimu huu hautofautiani kwa sana, ukweli wa namba unatupa picha tofauti kuhusu majigambo na kuzodoana kunakoendeea mitaani baina ya mashabiki wa timu hizo.
Mashabiki wangezifanyia tafakuri namba, wangekuwa na hofu kuelekea mechi ya Machi 8 badala ya kujigamba na kuzodoana kwa kuwa ukiziangalia timu zote 16 za kwenye ligi, Yanga na Simba ndizo zenye muendelezo mzuri wa ushindi.
Yanga inashika usukani wa ligi hiyo ikiwa na pointi 58 ikifuatiwa na Simba yenye pointi 54, hivyo tofauti baina ya timu hizo ni pointi nne.
Pointi nne ni nyingi lakini Simba ipo nyuma kwa mchezo mmoja, imecheza mechi 21, Yanga imecheza mechi 22, kutokana na ubora wa timu hizo kwa namna zinazovyoshinda mechi zao tofauti yao kimsingi ni pointi moja.
Tunaamini Simba watashinda kama wanavyoshinda Yanga dhidi ya timu nyingine, hivyo tofauti itabaki pointi moja ambayo kimsingi ni ndogo na rahisi kuipoteza wakati wowote.
Maana yake ni kwamba mashabiki Yanga hawana sababu ya kujiamini kwamba wameshalibeba taji la ligi kwa mtaji wa pointi moja ambayo wanaweza kuipoteza wakati wowote, ni hivyo hivyo kwa Simba wapo nyuma kwa pointi moja na wana kazi ya kuisaka.
Kwa kuziangalia namba maana yake ni kwamba mechi ya Machi 8 inabaki kuwa muhimu kwa timu zote kuhakikisha zinashinda, ikishinda Yanga itakuwa faida zaidi kwani tofauti itakuwa ya pointi nne zenye uhakika si sawa na hizi za sasa wakati Simba ina kiporo cha mechi moja.


Ni hivyo hivyo ikishinda Simba itakuwa imeisogelea Yanga na kujitofautisha kwa pointi moja ya uhakika na kama wote wataendelea kushinda mechi zao hadi ligi itakapofikia tamati maana yake ni kwamba Simba italibeba taji ikiitangulia Yanga kwa pointi mbili.
Kwa shabiki ambaye ataziangalia timu hizo kwa kuzichambua namba atauona ukweli wa pointi hizo ulivyo na ambavyo utazitesa timu hizo, tofauti kwa sasa ni pointi moja au mbili.
Matokeo ya sare baina ya timu hizo kidogo yatakuwa msaada kwa Yanga kwa kuwa itajinasua katika tofauti ya pointi moja na kutanguliwa mechi moja badala yake itakuwa pointi moja ya uhakika ambayo hata hivyo ugumu wake upo pale pale. Ukipoteza mechi moja tu umwekwisha, ukitoka sare moja tu umejiweka pabaya.
Vyovyote itakavyokuwa Yanga inatakiwa kushinda mechi ya leo ili kujiweka pazuri katika kulibeba taji kama ambavyo Simba inatakiwa kushinda ili kuwaweka Yanga pagumu katika mbio za kulibeba taji.
Nje ya namba za pointi kuna namba za magoli, hapa ndipo Yanga wanapoweza kujivunia kwani wamewaacha Simba kwa tofauti ya mabao 12, Yanga wana mabao 48, Simba 36, hii inaweza kuwa faida kubwa kama timu zitafungana pointi.
Yanga hata hivyo hawawezi kuangalia idadi ya mabao hayo ni kujiaminisha kuwa ni mtaji wa kulibeba taji badala yake wanatakiwa kuendelea na wimbi la ushindi katika mechi zao zilizobaki, hapo tu wataweza kulitetea vyema taji hilo.

Namba nyingine
Namba nyingine ni za mabao ya kufungwa, Simba ina ahueni kwani imefungwa mabao manane dhidi ya Yanga iliyofungwa mabao tisa, lakini pia hii haiwezi kuwa na maana yoyote badala yake kila timu inatakiwa kushinda mechi zilizo mbele yake.
Pia kuna namba za uwiano wa mabao, Yanga ikiwa 49 Simba 38, hizi namba mwisho wa siku pia haziwezi kuwa na maana yoyote badala yake la muhimu ni timu kupata ushindi.
Ukiachana na namba za pointi ambazo ni muhimu kuliko namba zozote kwenye ligi, namba nyingine yaani za mabao ya kufunga, kufungwa na uwiano zitakuwa na maana tu pale timu zitakapofungana pointi katika mechi zao za mwisho.
Ili kujitoa katika namba hizo ngumu na zinazoleta hofu za kulibeba taji, tunajikuta tukirudi katika hoja ile ile ya kwamba kila timu inatakiwa ishinde kila mechi, na mtaji wa kwanza muhimu kuushinda ni hii mechi yao ya Machi 8.

The post Namba ngumu Simba, Yanga first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2025/03/08/namba-ngumu-simba-yanga/feed/ 0