Simba-Mtibwa - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Thu, 25 Jun 2026 05:27:57 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=7.0 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg Simba-Mtibwa - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 Yanga, Simba zakoleza vita ya taji ligi kuu https://www.greensports.co.tz/2026/06/25/yanga-simba-zakoleza-vita-ya-taji-ligi-kuu/ https://www.greensports.co.tz/2026/06/25/yanga-simba-zakoleza-vita-ya-taji-ligi-kuu/#respond Thu, 25 Jun 2026 05:27:55 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=14732 Na mwandishi wetuMahasimu wa soka Tanzania, Yanga na Simba wameendelea kukoleza vita ya kulisaka taji la Ligi Kuu NBC baada ya kila mmoja kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 katika mechi zilizochezwa Jumatano Juni 24, 2026.Yanga walikua kwenye Uwanja wa New Amaan, Zanzibar walitoka na ushindi huo dhidi ya Azam FC wakati Simba ushindi wao […]

The post Yanga, Simba zakoleza vita ya taji ligi kuu first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Mahasimu wa soka Tanzania, Yanga na Simba wameendelea kukoleza vita ya kulisaka taji la Ligi Kuu NBC baada ya kila mmoja kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 katika mechi zilizochezwa Jumatano Juni 24, 2026.
Yanga walikua kwenye Uwanja wa New Amaan, Zanzibar walitoka na ushindi huo dhidi ya Azam FC wakati Simba ushindi wao dhidi ya Mtibwa Sugar ulipatikana kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.
Matokeo hayo yameiwezesha kila timu kuvuna pointi tatu, Yanga wakiendelea kujiimarisha kileleni mwa msimamo wa ligi hiyo kwa kufikisha pointi 69 katika michezo 28 waliyocheza hadi sasa.
Kwa upande wa Simba wameendelea kujiimarisha katika nafasi ya pili wakifikisha pointi 67 baada ya kucheza mechi 28 kama ilivyo Yanga na hivyo kuzidiwa kwa pointi mbili tu.
Yanga ambao Jumapili iliyopita walitolewa na Azam kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho kwa kufungwa mabao 3-2, walikuja tofauti katika mechi ya ligi na kucheza kwa kiwango cha juu.
Ushindi wa Yanga ulianza kupatikana dakika ya 41 kwa bao lililofungwa na Ibrahim Bacca aliyemalizia kazi ya Prince Dube ambaye pia ndiye aliyeibuka mchezaji bora wa mechi hiyo.
Baada ya bao hilo, mpira ulizidi kuwa wa ushindani kwa pande zote, Yanga wakisaka bao la kuongeza huku Azam wakipambana kusawazisha lakini hadi dakika 45 zinamalizika hakuna bao jingine lililopatikana.
Kipindi cha pili timu zote zilikianza kwa nguvu mpya na kuonesha nia ya kutaka bao lakini walikuwa Yanga waliopata bao dakika ya 71 lililofungwa kwa penalti na Depu baada ya mchezaji huyo kuchezewa rafu ndani ya eneo la 18.
Dakika nane baada ya kuingia bao hilo, Pacome Zouzoua aliwainua vitini mashabiki wa Yanga alipofunga bao la tatu akiutumia mpira uliopigwa na Dube na kuokolewa.
Kwa upande wa Simba bao lao la kwanza lilipatikana mapema dakika ya tisa mfungaji akiwa ni beki wa kati wa timu hiyo, Rushine De Reuck aliyefunga kwa mkwaju wa penalti, bao lililodumu kwa dakika 45 za kwanza.


Kipindi cha pili, Simba waliendelea kuutawala mchezo na kufanikiwa kupata bao la pili katika dakika ya 77, bao lililofungwa na Seleman Mwalimu akiitumia pasi ya Anicett Oura.
Karamu ya mabao ya Simba katika mechi hiyo ilihitimishwa dakika ya 90 ya mchezo huo kwa bao lililofungwa na Oura.
Matokeo hayo yanazidi kukoleza vita ya mahasimu hao wa soka nchini Tanzania katika kuliwania taji la ligi kwa msimu huu wa 2025-26 unaoelekea ukingoni huku kila timu ikiwa na mechi mbili mkononi.
Matokeo ya mechi nyingine za ligi hiyo ni kama ifuatavyo
KMC 2-3 Namungo FC
Dodoma Jiji 0–0 JKT
Fountain Gate 0-1 Mashujaa
TRA Unite 1-1 Coastal Union
Pamba Jiji 02 Mbeya City
Singida BS 3-1 Prisons

The post Yanga, Simba zakoleza vita ya taji ligi kuu first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2026/06/25/yanga-simba-zakoleza-vita-ya-taji-ligi-kuu/feed/ 0