Simba Day - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Tue, 16 Sep 2025 09:51:18 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=7.0 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg Simba Day - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 Mbosso anogesha Simba Day, Gor yapigwa 2-0 https://www.greensports.co.tz/2025/09/12/mbosso-anogesha-simba-day-gor-yapigwa-2-0/ https://www.greensports.co.tz/2025/09/12/mbosso-anogesha-simba-day-gor-yapigwa-2-0/#respond Fri, 12 Sep 2025 19:22:21 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=13891 Na mwandishi wetuSimba imeilaza Gor Mahia ya Kenya mabao 2-0 katika mechi maalum ya Tamasha ya Simba Day lililofanyika Jumatano hii, Septemba 10, 2025 kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam huku msanii wa bongo fleva, Mbosso akinogesha tamasha hilo.Kabla ya mechi hiyo kulikuwa na budurani mbalimbali zilizoteka maelfu ya mashabiki wa klabu hiyo waliofurika […]

The post Mbosso anogesha Simba Day, Gor yapigwa 2-0 first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Simba imeilaza Gor Mahia ya Kenya mabao 2-0 katika mechi maalum ya Tamasha ya Simba Day lililofanyika Jumatano hii, Septemba 10, 2025 kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam huku msanii wa bongo fleva, Mbosso akinogesha tamasha hilo.
Kabla ya mechi hiyo kulikuwa na budurani mbalimbali zilizoteka maelfu ya mashabiki wa klabu hiyo waliofurika uwanjani hapo kuanzia saa sita mchana wakifurahia utambulisho wa wachezaji na matukio mengine ya kuvutia.
Mashabiki hao kwa kiasi kikubwa waliupendezesha uwanja huo kwa jezi zao nyekundu, wengi wao wakiwa na jezi mpya za kampuni ya Jayrutty ambayo imeingia mkataba wa udhamini na Simba wenye thamani ya Sh bilioni 38.5.
Kwa kawaida tamasha la Simba Day ambalo lina miaka zaidi ya 10 sasa, hufanyika katika siku za mapumziko ya wiki yaani Jumamosi au Jumapili lakini mwaka huu limefanyika katikati ya wiki kutokana na muingiliano ya matukio ya kimichezo nchini Tanzania.
Ilitarajiwa mashabiki wangekuwa wachache lakini hali imekuwa tofauti, mashabiki wa Simba wameujaza Uwanja wa Mkapa wenye uwezo wa kuchukua mashabiki zaidi ya 60,000 huku wakiupendezesha kwa jezi za rangi nyekundu.
Mbali na burudani ya muziki kutoka kwa Mboso ambaye aliimba nyimbo zake nyingi zinazopendwa pia ilikuwapo bendi maarufu ya muziki wa dansi ya Twanga Pepeta pamoja na DJ maarufu DJ Sinyorita, mwanadada ambaye naye alipokewa vyema na mashabiki wa klabu hiyo.
Burudani nyingine iliyokuwa kivutio kwa mashabiki wa Simba ni mechi ya wachezaji wa zamani wa timu hiyo yaani Veterans waliocheza na KT Veterans, mechi ambayo iliisha kwa timu hizo kutoka sare ya mabao 2-2.
Katika mechi hii, mashabiki wa Simba walipata fursa ya kuwaona kwa mara nyingine nyota wao wa zamani wakionesha ubora wao wakiwamo Mussa Hassan Mgosi, Juma Jabu, Emmanuel Gabriel, Haruna Moshi ‘Boban’, Said Sued, Duwa Said na wengineo.
Matukio hayo na mengineyo kwa pamoja yamelifanya tamasha la Simba Day kuwa moja ya matukio makubwa ya kimichezo na burudani nchini kwa namna ambavyo limewakutanisha wana Simba wenye hadhi tofauti.
Katika tamasha hilo, ukiacha mashabiki waliofika uwanjani, wapo mashabiki wengine wengi kote Tanzania ambao walikuwa wakifuatilia tukio hilo moja kwa moja kwenye televisheni wakiwa majumbani mwao au kwenye kumbi za starehe.
Katika mechi na Gor Mahia, mabao ya Simba yalifungwa na Abdulrazak Hamza katika dakika ya sita wakati bao la pili lilifungwa na Steven Mukwala dakika ya 65.

The post Mbosso anogesha Simba Day, Gor yapigwa 2-0 first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2025/09/12/mbosso-anogesha-simba-day-gor-yapigwa-2-0/feed/ 0
Simba Day tamu, Mnyama ampiga APR 2-0 https://www.greensports.co.tz/2024/08/04/simba-day-tamu-mnyama-ampiga-apr-2-0/ https://www.greensports.co.tz/2024/08/04/simba-day-tamu-mnyama-ampiga-apr-2-0/#respond Sat, 03 Aug 2024 21:30:05 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=11706 Na mwandishi wetuSimba Day, leo Jumamosi Agosti 3, 2024 imekuwa tamu kwa mashabiki wa timu hiyo baada ya kuichapa APR ya Rwanda mabao 2-0 huku mashabiki wakijivunia kuujaza Uwanja wa Mkapa unaochukua mashabiki zaidi ya 60,000.Mechi hiyo ilikuwa maalum kwa timu hiyo kujiandaa na msimu mpya wa 2024-25, ilitanguliwa na matukio mbalimbali yakiwamo ya kijamii […]

The post Simba Day tamu, Mnyama ampiga APR 2-0 first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Simba Day, leo Jumamosi Agosti 3, 2024 imekuwa tamu kwa mashabiki wa timu hiyo baada ya kuichapa APR ya Rwanda mabao 2-0 huku mashabiki wakijivunia kuujaza Uwanja wa Mkapa unaochukua mashabiki zaidi ya 60,000.
Mechi hiyo ilikuwa maalum kwa timu hiyo kujiandaa na msimu mpya wa 2024-25, ilitanguliwa na matukio mbalimbali yakiwamo ya kijamii kabla ya kufanyika utambulisho wa wachezaji wapya wa timu hiyo na wale wa zamani.
Simba au Mnyama ilikianza kipindi cha kwanza bila kuonesha kasi yoyote, iliandika bao lake la kwanza dakika moja baada ya kuanza kipindi cha pili, mfungaji akiwa ni nyota wake mpya Deborah Fernandes.
APR hawakuonesha kushtushwa na bao hilo waliendelea kucheza soka lao la kawaida kabla ya kujikuta wakifungwa bao la pili dakika 20 baadaye mfungaji akiwa ni Edwin Balua.
Ukiacha mabao hayo, kipindi cha kwanza kilionekana kuwa kigumu kwa timu zote ambapo Simba haikuonesha uhai kama walivyo APR ingawa kulikuwa na kosakosa za hapa na pale.
Katika kosakosa hizo, dakika ya 37, Farbrice Ngoma alimuunganishia pasi ndefu beki Mohammed Hussein ‘Zimbwe Junior’ ambaye akiwa aliumiliki mpira huo vizuri na kufanikiwa kuzalisha kona ambayo haikuwa na madhara kwa APR.
APR nao walifanya shambulizi dakika moja kabla ya mapumziko ambapo Nyibizi Ramadhan akiwa anaelekea kwenye lango la Simba alichezewa rafu na Ngoma na mwamuzi kuamuru upigwe mpira wa adhabu ambao mpigaji, Saydou Dauda alipiga shuti lililopaa juu ya lango.
Simba hata hivyo itabidi wajilaumu kwa kushindwa kupata bao la penalti iliyotolewa dakika ya 42 baada ya Joshua Mutale kuangushwa ndani ya eneo la 18 wakati akielekea kuonana na kipa wa APR, Piere Inshimwe.
Mpigaji wa penalti hiyo, Stephen Mukwale licha ya kumchambua vyema kipa wa APR ambaye aliruka upande wake wa kulia, shuti la Mukwale hata hivyo lilikwenda upande wa kushoto wa kipa huyo na kugonga mwamba.
Kocha wa Simba, Fadllu Daud aliitumia vyema mechi hiyo kuwapima wachezaji wake kwa namna ambavyo alifanya mabadiliko ya wachezaji ikiwamo kuwapa nafasi makipa watatu.
Alianza na Ally Salim ambaye baadaye aliumia na kumpisha Mussa Camara ambaye naye baadaye alitolewa na kumpisha Hussein Abel.
Simba Jumamosi ijayo itaumana na mahasimu wao Yanga katika mechi ya Ngao ya Jamii ambapo kocha wa Simba akiizungumzia mechi hiyo pamoja na mambo mengine alisema jambo kubwa ni suala la kujiandaa kiakili.

The post Simba Day tamu, Mnyama ampiga APR 2-0 first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/08/04/simba-day-tamu-mnyama-ampiga-apr-2-0/feed/ 0
Simba Day imenoga asubuhi hadi jioni https://www.greensports.co.tz/2023/08/06/simba-day-imenoga-asubuhi-hadi-jioni/ https://www.greensports.co.tz/2023/08/06/simba-day-imenoga-asubuhi-hadi-jioni/#respond Sun, 06 Aug 2023 20:30:56 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=7256 Na mwandishi wetuAgosti 6, Jumamosi, 2023 itabaki katika kumbukumbu za mashabiki wa Simba, walivyoanza kuifurahia Simba Day asubuhi kwa kulitikisa jiji la Dar hadi kuhitimisha kwa ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Power Daynamos ya Zambia.Gumzo tangu asubuhiKuanzia mida ya asubuhi, mashabiki wa Simba walionesha kila dalili za kuimaliza siku vizuri, mitaa mbalimbali jijini Dar […]

The post Simba Day imenoga asubuhi hadi jioni first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Agosti 6, Jumamosi, 2023 itabaki katika kumbukumbu za mashabiki wa Simba, walivyoanza kuifurahia Simba Day asubuhi kwa kulitikisa jiji la Dar hadi kuhitimisha kwa ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Power Daynamos ya Zambia.
Gumzo tangu asubuhi
Kuanzia mida ya asubuhi, mashabiki wa Simba walionesha kila dalili za kuimaliza siku vizuri, mitaa mbalimbali jijini Dar es Salaam hasa kwenye matawi ya klabu hiyo furaha, hamasa na matumaini makubwa vyote vilijidhihirisha.
Wanachama na mashabiki wa timu hiyo wakiwa katika mavazi ya rangi nyekundu na nyeupe wengi wao walionekana wakiwa wamejiandaa kuelekea kwenye Uwanja wa Mkapa kwa ajili ya Simba Day.
Hali hiyo ilijidhihirisha nyakati za asubuhi zaidi lakini kadri muda ulivyokwenda tukio kubwa lililofuata ni la wanachama hao kuonekana kwa makundi wakielekea vituoni kupanda mabasi hadi Kwa Mkapa.
Makundi mengine ya wanachama yalikodi magari hasa aina ya Coaster, magari hayo yalipambwa na bendera za klabu hiyo zenye maandishi mbalimbali yanayopongeza mafanikio ya klabu ya Simba na maandalizi ya msimu mpya wa 2023-24 au kukejeli matukio ya mahasimu wao Yanga.


Bodaboda, bajaji
Hapo hapo bodaboda na bajaji nazo hazikuwa nyuma, ilikuwa kawaida kuona bajaji au bodaboda zilizotoa kila ishara kwamba walikuwa ni mashabiki wa Simba wanaelekea kwa Mkapa kwenye kilele cha Simba Day.
Baadhi ya bodaboda zilitawaliwa na miziki ya singeli ambayo kwa kiasi kikubwa nyimbo zake zilikuwa za kusifia mafanikio ya klabu ya simba, ilikuwa kero kwa baadhi ya watu kwa namna nyimbo hizo zilivyoimbwa kwa sauti za juu.
Taratibu mida ya saa tisa hadi 10 utulivu ulianza kurejea mitaani, mashabiki wa Simba na wengine baadhi wa Yanga safari hii walionekana kwa makundi wakiwa kwenye televisheni.
Hii haikuwa kwenye vibanda umiza pekee au baa na klabu za starehe kama ilivyozoeleka, bali hali hiyo pia ilionekana kwenye baadhi ya maduka yaliyokuwa wazi, mashabiki wa Simba na hata wasio wa Simba walikuwa wakiangalia ‘live’ kilichokuwa kikiendelea Kwa Mkapa.
Wakati huo tayari Kwa Mkapa kumefurika mashabiki wenye jezi nyekundu na nyeupe, aliyeshuhudia hali ilivyokuwa mitaani na baadaye kwa Mkapa, atakubali kwamba ilikuwa kielelezo tosha cha namna ambavyo Simba Day ililiteka jiji la Dar kuanzia asubuhi.
Zaidi ya hilo kile kilichokuwa kikizungumzwa kwamba tiketi za Simba Day zimeisha kilianza kujidhihirisha katika mida hii kwa namna ambavyo uwanja ulifurika na kupambwa kwa rangi nyekundu na nyeupe.
Kwa Mkapa
Ukiachana na burudani ya muziki, Kwa Mkapa kulikuwa na matukio makubwa matatu, kwanza ni utambulisho wa wachezaji, pili ni ujio wa mgeni rasmi na tatu ni mechi ya Simba na Power Daynamos.
Katika utambulisho wa wachezaji, mashabiki wa Simba walipata nafasi ya kuwaona wachezaji wapya na wa zamani ambao wataiwakilisha timu hiyo katika msimu mpya wa 2023-24.

Kilichokuwa kikisubiriwa kwa hamu katika tukio hilo ni kile kilichoitwa sapraizi wa kipa mpya, tofauti na matarajio ya wengi kwamba kipa huyo angekuwa kutoka nje ya nchi au jina lolote kubwa, Simba imemtangaza Abel Hussein aliyekuwa KMC ambaye amejiunga na timu hiyo.
Tukio la pili ni lile ambalo baadhi ya mashabiki walilitilia shaka, nani angekuwa mgeni rasmi, je ni kweli Rais Samia Suluhu Hassan angefika katika tamasha hilo au zilikuwa mbwembwe tu zilizotengenezwa?
Jibu likapatikana baada ya kiongozi huyo mkuu wa nchi kuwasili uwanjani na kupokewa kwa shangwe kabla ya kusalimiana na wachezaji wa timu zote na viongozi, na kupiga nao picha kabla ya kukabidhiwa jezi na baadye kutoa hotuba na hivyo kuingia katika historia ya kulipamba tamasha la 15 la Simba Day.
Mechi ilivyokuwa
Simba iliandika bao la kwanza katika dakika ya tano ya mchezo huo, ni bao tamu lililofungwa na nyota mpya wa timu hiyo, Willy Onana ambaye amewathibitishia mashabiki wa timu hiyo kwamba uongozi wao haukufanya kosa kumsajili.
Onana baada ya kuinasa pasi ya Muzamir Yassin, aliambaa na mpira kabla ya kupiga shuti la kiufundi lililojaa wavuni na kuwaamsha vitini mashabiki wa Simba.
Baada ya hapo ufundi mwingi ulitawala, wachezaji wa Simba hasa Clatous Chota Chama kama kawaida yake, mara kadhaa alifanikiwa kuwafanya mashabiki wafurahie burudani ya soka lililojaa ufundi ambao pia ulishuhudiwa kufanywa na beki Inonga.
Simba mbali na wachezaji mmoja mmoja kuonesha uwezo wake, kwa ujumla walifanikiwa kuonesha ubora wa kumiliki mpira kwa muda mrefu na kufika mara kwa mara kwenye lango la Dynamos ingawa hadi mapumziko walikuwa na bao hilo hilo moja.

Kipindi cha pili, Dynamos walianza kulisakama lango la Simba na kushindwa kuzitumia vizuri nafasi mbili za wazi, ya kwanza ikipotezwa na Thomas Chideli katika dakika ya 47, Chideli akiwa karibu na kipa Ally Salim alipiga shuti lililopaa juu ya lango.
Dakika mbili baadaye, Ally Salim aliokoa mpira uliopigwa na Joshua Mutale na mpira huo kumkuta Mutale tena ambaye kwa mshangao wa wengi alipiga shuti la mguu wa kushoto ambalo si tu lilipaa juu bali alikuwa kama vile beki wa Simba anaondoa hatari kwenye lango lake.
Simba walianza kuwageuzia kibao Dynamos na katika dakika ya 75 juhudi zao zilizaa matunda kwa bao la kichwa lililofungwa na nyota mwingine mpya wa timu hiyo, Fabrice Mwamba ambaye aliunganisha krosi iliyochongwa na Saido Ntibazonkiza na hivyo kutihimisha tamasha la Simba Day jioni kwa ushindi wa mabao 2-0.
Katika kipindi hicho pia mashabiki wa Simba walipewa ladha ya soka ‘waliloli-miss’ muda mrefu kutoka kwa Luis Maquissone ambaye mara kadha alionesha maufundi lakini kubwa ni pale alipopiga krosi katika dakika ya 88 na mshambuliaji mkongwe John Bocco kujitwisha kichwani lakini alishindwa kuzifumania nyavu.

The post Simba Day imenoga asubuhi hadi jioni first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/08/06/simba-day-imenoga-asubuhi-hadi-jioni/feed/ 0