Silver Strikers - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Sat, 25 Oct 2025 19:27:40 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=6.9.1 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg Silver Strikers - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 Yanga yafuzu makundi Ligi ya Mabingwa https://www.greensports.co.tz/2025/10/25/yanga-yafuzu-makundi-ligi-ya-mabingwa/ https://www.greensports.co.tz/2025/10/25/yanga-yafuzu-makundi-ligi-ya-mabingwa/#respond Sat, 25 Oct 2025 19:27:39 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=14032 Na mwandishi wetuTimu ya Yanga hatimaye imefuzu hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika ikiichapa Silver Strikers ya Malawi mabao 2-0 na hivyo kufuzu kwa ushindi wa jumla wa mabao 2-1 baada ya kulala kwa bao 1-0 katika mechi ya awali.Yanga iliyokuwa nyumbani kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam leo Jumamosi Oktoba 25, […]

The post Yanga yafuzu makundi Ligi ya Mabingwa first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Timu ya Yanga hatimaye imefuzu hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika ikiichapa Silver Strikers ya Malawi mabao 2-0 na hivyo kufuzu kwa ushindi wa jumla wa mabao 2-1 baada ya kulala kwa bao 1-0 katika mechi ya awali.
Yanga iliyokuwa nyumbani kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam leo Jumamosi Oktoba 25, 2025 mbele ya maelfu ya mashabiki wake walioingia bure uwanjani, ilihofiwa kwamba ingeweza kutolewa kutokana na matokeo ya mechi hiyo ya awali.
Alikuwa ni beki Dickson Job aliyeibua upya matumaini ya timu hiyo kusonga mbele mapema dakika ya sita baada ya kuipatia Yanga bao la kwanza baada ya kuuwahi mpira wa kona uliopigwa na Mohamed Doumbia.
Baada ya bao hilo, Yanga waliongeza kasi ya kusaka bao la pili huku wakitawala vyema eneo la kiungo, juhudi ambazo zilizaa matunda dakika ya 34 kwa bao lililofungwa na Pacome Zouzoua kwa pasi ya Maxi Nzengeli.
Ushindi huo unakuwa umeibua matumaini mapya na kurejesha amani kwa viongozi wa Yanga ambao katika siku za karibuni wamekuwa wakisakamwa na mashabiki wao wakidai kutoridhishwa na kiwango cha uchezaji cha timu hiyo.
Uongozi hatimaye ulifikia hatua ya kumtimua kazi kocha mkuu Romain Folz na majukumu yake kukabidhwia wasaidizi wake ambao wataendelea na jukumu hilo kabla ya kocha mpya kuanza kazi.
Wakati huo huo timu ya Singida Big Stars nayo imefuzu hatua ya makundi Kombe la Shirikisho Afrika baada ya kuibuka na ushndi wa mabao 3-1 dhidi ya Flambeau du Centre FC ya Burundi, mechi iliyopigwa leo kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.
Kwa matokeo hayo timu hiyo inakuwa imesonga mbele kwa ushindi wa jumla ya mabao 4-2 baada ya sare ya bao 1-1 katika mechi ya awali ambayo Singida BS walikuwa ugenini.
Ushindi wa Singida BS unazifanya timu za Tanzania zilizofuzu hatua ya makundi kwenye mashindano ambayo yanaandaliwa na Shirikisho la Soka Afrika (CAF) kufikia tatu baada ya Yanga na Azam FC na kama Simba itafuzu kesho Jumapili, timu hizo zitakuwa nne.

The post Yanga yafuzu makundi Ligi ya Mabingwa first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2025/10/25/yanga-yafuzu-makundi-ligi-ya-mabingwa/feed/ 0
Ugenini pagumu kwa Yanga https://www.greensports.co.tz/2025/10/21/ugenini-pagumu-kwa-yanga/ https://www.greensports.co.tz/2025/10/21/ugenini-pagumu-kwa-yanga/#respond Tue, 21 Oct 2025 15:03:31 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=14012 Na mwandishi wetuMambo si mambo kwa Yanga kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kulala kwa bao 1-0 ugenini dhidi ya Silver Strikers ya Malawi, mechi iliyochezwa Jumamosi hii Oktoba 18, 2025 kwenye Uwanja wa Taifa wa Bingu nchini Malawi.Matokeo hayo yanaiweka Yanga pagumu kwani sasa itakuwa na kazi ya kupindua matokeo ikiwa nyumbani katika […]

The post Ugenini pagumu kwa Yanga first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Mambo si mambo kwa Yanga kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kulala kwa bao 1-0 ugenini dhidi ya Silver Strikers ya Malawi, mechi iliyochezwa Jumamosi hii Oktoba 18, 2025 kwenye Uwanja wa Taifa wa Bingu nchini Malawi.
Matokeo hayo yanaiweka Yanga pagumu kwani sasa itakuwa na kazi ya kupindua matokeo ikiwa nyumbani katika mechi ya marudiano inayotarajia kuchezwa Jumamosi ijayo kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam ili kufufua matumaini ya kuendelea na michuano hiyo.
Bao pekee la Silver Strikers lilipatikana dakika ya 76 mfungaji akiwa ni Adulu baada ya timu hiyo kufanya shambulizi la kushtukiza na Yanga kushindwa kukabiliana nalo.
Yanga ikiwatumia nyota wake Pacome Zouzoua na wengineo walishindwa kuzitumia dakika 14 za mwisho kupata bao la kusawazisha na kuongeza la pili kwani hadi mwisho wa mchezo matokeo yalibaki kuwa mazuri kwa wenyeji Silver.
Matokeo yoyote ya sare au kufungwa kwenye mechi ya marudiano yataifanya Yanga kupata aibu kwa kuaga mapema michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika bila kugusa hatua ya makundi.
Kwa kipindi kirefu mashabiki wa Yanga wamekuwa wakimlalamikia kocha wao Romain Folz kwa madai kuwa ameshindwa kuifanya timu yao icheze vizuri na bila shaka matokeo ya mechi na Silver yanazidi kumuweka pagumu kocha huyo.

The post Ugenini pagumu kwa Yanga first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2025/10/21/ugenini-pagumu-kwa-yanga/feed/ 0