Shakira - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Fri, 05 Jun 2026 19:09:53 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=7.0 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg Shakira - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 Shakira, Burna Boy kutoa burudani Kombe la Dunia https://www.greensports.co.tz/2026/06/05/shakira-burna-boy-kutoa-burudani-kombe-la-dunia/ https://www.greensports.co.tz/2026/06/05/shakira-burna-boy-kutoa-burudani-kombe-la-dunia/#respond Fri, 05 Jun 2026 19:09:51 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=14686 Mexico City, MexicoMwanamuziki wa Colombia, Shakira (pichani) atatoa burudani kwa kuimba wimbo maalum katika hafla ya fainali za Kombe la Dunia 2026 mjini Mexico City kabla ya mechi ya ufunguzi ya fainali hizo.Shakira atapanda jukwaani Juni 11, 2026 kuzipamba fainali hizo katika dimba la Azteca kabla ya mechi ya ufunguzi kati ya wenyeji Mexico watakaoumana […]

The post Shakira, Burna Boy kutoa burudani Kombe la Dunia first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Mexico City, Mexico
Mwanamuziki wa Colombia, Shakira (pichani) atatoa burudani kwa kuimba wimbo maalum katika hafla ya fainali za Kombe la Dunia 2026 mjini Mexico City kabla ya mechi ya ufunguzi ya fainali hizo.
Shakira atapanda jukwaani Juni 11, 2026 kuzipamba fainali hizo katika dimba la Azteca kabla ya mechi ya ufunguzi kati ya wenyeji Mexico watakaoumana na Afrika Kusini.
Wimbo maarufu wa Dai Dai wa lugha ya kitaliano ambao maana yake isiyo rasmi ni ‘twende pamoja au ‘njoo’ ulizinduliwa na kutangazwa kuwa ndio wimbo rasmi wa fainali hizo ambazo pia zitafanyika katika nchi za Canada na Marekani.
Katika kutoa burudani hiyo, Shakira atakuwa pamoja na mwanamuziki wa Nigeria, Burn Boy wakati wasanii wengine watakaotoa burudani ni J Balvin pia wa Colombia na Tyla wa Afrika Kusini.
Kwa Shakira hii si mara ya kwanza kupata fursa ya kutumbuiza kwenye fainali za Kombe la Dunia, anakumbukwa mwaka 2010 nchini Afrika Kusini alipotamba na kibao cha ‘Waka Waka This time for Afrika’.
Shakira ambaye amewahi kuwa mpenzi wa beki wa zamani wa Barcelona na timu ya taifa ya Hispania, Gerard Pique, pia alipata nafasi ya kutoa burudani kwenye fainali za Kombe la Dunia 2006 nchini Ujerumani na 2014 nchini Brazil.
Kwa mujibu wa Fifa, hafla za ufunguzi wa fainali za Kombe la Dunia zitafanyika kabla ya kila mechi ya kwanza katika nchi zote tatu mwenyeji za fainali hizo.
Kwa Canada burudani ya muziki itatolewa na wasanii Michael Bublé na Alanis Morissette mjini Toronto Juni 12 kwenye Uwanja wa BMO kabla ya mechi kati ya wenyeji Canada dhidi ya Bosnia & Herzegovina.
Nchini Marekani, burudani hiyo itatolewa na Katy Perry na Future mjini Los Angeles katika Uwanja wa SoFi kabla ya mechi kati ya wenyeji Marekani dhidi ya Paraguay ambayo pia itachezwa Juni 12.

The post Shakira, Burna Boy kutoa burudani Kombe la Dunia first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2026/06/05/shakira-burna-boy-kutoa-burudani-kombe-la-dunia/feed/ 0