Serengeti Girls - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Sun, 16 Mar 2025 10:29:53 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=6.9.4 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg Serengeti Girls - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 Serengeti Girls yakwama Zambia https://www.greensports.co.tz/2025/03/15/serengeti-girls-yakwama-zambia/ https://www.greensports.co.tz/2025/03/15/serengeti-girls-yakwama-zambia/#respond Sat, 15 Mar 2025 18:47:52 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=13136 Na mwandishi wetuTimu ya wasichana chini ya miaka 17 ya Tanzania maarufu Serengeti Girls imekwama katika kuwania kufuzu kucheza fainali za Kombe la Dunia 2025 baada ya kulala kwa bao 1-0 mbele ya Zambia.Katika mechi hiyo iliyopigwa leo Jumamosi Machi 15, 20225 ambayo Serentgeti ilikuwa ugenini Zambia kwenye Uwanja wa levy Mwanawasa mjini Ndola bao […]

The post Serengeti Girls yakwama Zambia first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
Na mwandishi wetu
Timu ya wasichana chini ya miaka 17 ya Tanzania maarufu Serengeti Girls imekwama katika kuwania kufuzu kucheza fainali za Kombe la Dunia 2025 baada ya kulala kwa bao 1-0 mbele ya Zambia.
Katika mechi hiyo iliyopigwa leo Jumamosi Machi 15, 20225 ambayo Serentgeti ilikuwa ugenini Zambia kwenye Uwanja wa levy Mwanawasa mjini Ndola bao pekee la washindi lilipatikana dakika ya 52 na Natsha Nkaka,
Kwa kipigo hicho ndoto za Serengeti Girls kucheza fainali za Kombe la Dunia zinakuwa zimeyeyuka rasmi timu hiyo ikiwa imefungwa jumla ya mabao 4-0 baada ya kulala kwa mabao 3-0 katika mechi ya kwanza iliyopigwa Jumapili iliyopita mjini Dar es Salaam.
Baada ya kupata ushindi huo timu ya Zambia maarufu Copper Princesses inakuwa imesonga mbele ikisubiri kuumana na mshindi wa mechi kati ya Benin na DR Congo.
Fainali za Kombe la Dunia kwa timu za wasichana chini ya miaka 17 zitafanyika nchini Morocco kuanzia Oktoba 17 mwaka huu.

The post Serengeti Girls yakwama Zambia first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2025/03/15/serengeti-girls-yakwama-zambia/feed/ 0
Serengeti Girls yalala 3-0 https://www.greensports.co.tz/2025/03/10/serengeti-girls-yalala-3-0/ https://www.greensports.co.tz/2025/03/10/serengeti-girls-yalala-3-0/#respond Mon, 10 Mar 2025 18:48:39 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=13119 Na mwandishi wetuTimu ya wasichana chini ya miaka 17 ya Tanzania ‘Serengeti Girls’ imeshindwa kutamba katika kuwania kufuzu Kombe la Dunia baada ya kulala kwa mabao 3-0 mbele ya Zambia.Katika mechi hiyo iliyopigwa Jumapili hii Machi 9, 2025 kwenye Uwanja wa Azam Complex, wenyeji Serengeti walionesha matumaini kipindi cha kwanza na timu hizo kutoka uwanjani […]

The post Serengeti Girls yalala 3-0 first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Timu ya wasichana chini ya miaka 17 ya Tanzania ‘Serengeti Girls’ imeshindwa kutamba katika kuwania kufuzu Kombe la Dunia baada ya kulala kwa mabao 3-0 mbele ya Zambia.
Katika mechi hiyo iliyopigwa Jumapili hii Machi 9, 2025 kwenye Uwanja wa Azam Complex, wenyeji Serengeti walionesha matumaini kipindi cha kwanza na timu hizo kutoka uwanjani zikiwa hazijafungana.
Zambia au Copper Princesses walianza kuinyanyasa Serengeti Girls dakika ya 64 kwa bao la Grace Phiri kabla ya kuongeza la pili dakika ya 80 lililofungwa na Mercy Chipasula.


Matumaini ya Serengeti kupata japo bao la kufutia machozi hayakuwezekana badala yake timu hiyo ilibugizwa bao la tatu lililofungwa na Mercy tena safari hii kwa penalti katika dakika ya 89.
Timu hizo zinatarajia kurudiana Jumamosi ijayo mjini Ndola, Zambia kwenye dimba la Levy Mwanawasa na baada ya hapo mshindi baina ya timu hizo ataumana na mshindi wa mechi kati ya DR Congo na Benin.
Katika mechi nyingine ya kuwania kufuzu fainali hizo, Cameroon ikiwa nyumbani iliilaza Ethiopia mabao 5-2.
Fainali za Kombe la Dunia kwa timu za wasichana chini ya miaka 17 zinatarajia kuchezwa Oktoba mwaka huu nchini Morocco.

The post Serengeti Girls yalala 3-0 first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2025/03/10/serengeti-girls-yalala-3-0/feed/ 0