Serengeti Boys - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Sun, 31 May 2026 12:19:01 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=7.0 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg Serengeti Boys - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 Wawili Serengeti Boys waitwa Taifa Stars https://www.greensports.co.tz/2026/05/31/wawili-serengeti-boys-waitwa-taifa-stars/ https://www.greensports.co.tz/2026/05/31/wawili-serengeti-boys-waitwa-taifa-stars/#respond Sun, 31 May 2026 12:18:59 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=14668 Na mwandishi wetuKocha mkuu wa timu ya taifa ya Tanzania, ‘Taifa Stars’, Miguel Gamondi amewaita katika kikosi chake wachezaji wawili wa timu ya vijana chini ya miaka 17 ya Tanzania maarufu Serengeti Boys.Taarifa ya TFF iliyopatikana Ijumaa Mei 29, 2026 iliwataja wachezaji hao kuwa ni Kassim Juma na Luqman Mbalasalu ambao watajiunga katika kikosi hicho […]

The post Wawili Serengeti Boys waitwa Taifa Stars first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Kocha mkuu wa timu ya taifa ya Tanzania, ‘Taifa Stars’, Miguel Gamondi amewaita katika kikosi chake wachezaji wawili wa timu ya vijana chini ya miaka 17 ya Tanzania maarufu Serengeti Boys.
Taarifa ya TFF iliyopatikana Ijumaa Mei 29, 2026 iliwataja wachezaji hao kuwa ni Kassim Juma na Luqman Mbalasalu ambao watajiunga katika kikosi hicho baada ya Juni 2, 2026.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo iliyosainiwa na ofisa habari na mawasiliano wa TFF, Cliford Ndimbo, Taifa Stars itacheza mechi ya kirafiki iliyopo kwenye kalenda ya Fifa dhidi ya Uganda Cranes, Ijumaa, Juni 5, 2026.
Baada ya mechi hiyo, Stars itaingia tena uwanjani Jumanne, Juni 9, 2026 kwa mechi yake ya pili dhidi ya timu ya Rwanda, mechi zote hizo zitachezwa mjini Marakech, Morocco.
Wachezaji wengine wa timu hiyo waliotajwa katika kikosi cha Gamondi, wameanza kuingia kambini tangu Ijumaa iliyopita.
Kwa upande wa Serengeti Boys, timu hiyo itacheza mechi ya fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon) chini ya miaka 17 dhidi ya Senegal, mechi itakayochezwa mjini Rabat, Morocco, usiku wa Jumanne, Juni 2, 2026 kwenye Uwanja wa Moulay El Hassan.

The post Wawili Serengeti Boys waitwa Taifa Stars first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2026/05/31/wawili-serengeti-boys-waitwa-taifa-stars/feed/ 0
Rais Samia aipongeza Serengeti Boys, awajaza noti https://www.greensports.co.tz/2026/05/31/rais-samia-aipongeza-serengeti-boys-awajaza-noti/ https://www.greensports.co.tz/2026/05/31/rais-samia-aipongeza-serengeti-boys-awajaza-noti/#respond Sun, 31 May 2026 08:48:44 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=14660 Na mwandishi wetuRais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ameipongeza timu ya taifa ya vijana chini ya miaka 17, Serengeti Boys na kuipa zawadi ya Sh milioni 500.Pongezi hizo zimekuja baada ya timu hiyo kufuzu hatua ya fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon) kwa vijana chini ya miaka 17 ikiitoa […]

The post Rais Samia aipongeza Serengeti Boys, awajaza noti first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ameipongeza timu ya taifa ya vijana chini ya miaka 17, Serengeti Boys na kuipa zawadi ya Sh milioni 500.
Pongezi hizo zimekuja baada ya timu hiyo kufuzu hatua ya fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon) kwa vijana chini ya miaka 17 ikiitoa Misri kwa penalti 4-3 katika mechi ya nusu fainali iliyopigwa mjini Rabat, Morocco
Sambamba na pongezi na fedha hizo, Rais Samia pia ameahidi kuwapa viwanja wachezaji hao mkoani Morogoro kama wakifanikiwa kuibwaga Senegal na kubeba taji la michuano hiyo.
Ahadi hiyo ya Rais Samia iliwekwa wazi na Waziri Mkuu, Dk Mwigulu Nchemba ambaye akiwa ofisini kwake mjini Dodoma ambapo alisema kiongozi huyo mkuu wa nchi amewapongeza wachezaji hao kwa jinsi walivyoiwakilisha vyema nchi kimataifa.
“Rais ameelekeza kwamba katika kuthamini mafanikio yao kwa kufikia hatua ya fainali anawapa zawadi y Sh milioni 500,” alisema Dk Nchemba.
Dk Nchemba alifafanua kuwa timu hiyo ikibeba taji kila mchezaji atapewa kiwanja mjini Morogoro na kuongeza kuwa Serikali imeandaa ndege maalum kwa ajili ya wachezaji hao watakaporejea nchini baada ya mechi hiyo.
Wakati huo huo, kocha wa zamani wa Arsenal, Arsene Wenger ambaye kwa sasa ni mkurugenzi wa maendeleo ya soka wa Fifa, ameipongeza timu hiyo kwa mafanikio iliyoyapata dhidi ya timu imara iliyokutana.
Wenger alisema kwamba anaamini kuwa timu hiyo itaonekana kwenye fainali za Kombe la Dunia hivi karibuni.
Serengeti sasa inasubiri kuumana na timu ya taifa ya Senegal katika mechi ya fainali ambayo itachezwa usiku wa Jumanne, Juni 2, 2026.

The post Rais Samia aipongeza Serengeti Boys, awajaza noti first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2026/05/31/rais-samia-aipongeza-serengeti-boys-awajaza-noti/feed/ 0
Serengeti Boys vitani dhidi ya Senegal https://www.greensports.co.tz/2026/05/31/serengeti-boys-vitani-dhidi-ya-senegal/ https://www.greensports.co.tz/2026/05/31/serengeti-boys-vitani-dhidi-ya-senegal/#respond Sun, 31 May 2026 08:44:14 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=14655 Rabat, MoroccoTimu ya soka ya Tanzania ya vijana chini ya miaka 17, Serengeti Boys, inasubiri kuikabili Senegal katika fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon) kwa vijana chini ya miaka 17.Serengeti imefikia hatua hiyo baada ya kuitoa Misri kwa mikwaju ya penalti 4-3 katika mechi ya nusu fainali baada ya sare ya bila kufungana.Ushindi […]

The post Serengeti Boys vitani dhidi ya Senegal first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Rabat, Morocco
Timu ya soka ya Tanzania ya vijana chini ya miaka 17, Serengeti Boys, inasubiri kuikabili Senegal katika fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon) kwa vijana chini ya miaka 17.
Serengeti imefikia hatua hiyo baada ya kuitoa Misri kwa mikwaju ya penalti 4-3 katika mechi ya nusu fainali baada ya sare ya bila kufungana.
Ushindi wa Serengeti Boys ni rekodi ya kujivunia kwa timu hiyo ambayo imefikia hatua hiyo kwa mara ya kwanza katika historia ya Tanzania na sasa inasubiri kucheza mechi ya fainali usiku wa Jumanne, Juni 2, 2026 katika Uwanja wa Moulay El Hassan mjini Rabat.
Serengeti Boys ambayo iliingia katika michuano hiyo ikionesha kila dalili za kufika mbali, sasa ina kibarua kigumu dhidi ya Senegal moja ya timu zenye hadhi katika soka barani Afrika.
Mashabiki wa Serengeti Boys sasa wanasubiri kuiona timu yao ikiweka historia nyingine mpya na ya kipekee kwa kubeba taji la michuano hiyo.
Senegal wao wameweka heshima hadi kufikia hatua ya fainali wakiwa wamewatoa wenyeji Morocco mbele ya mashabiki wao jambo linalodhihirisha kwamba mechi yao na Serengeti itakuwa ngumu.
Ushindi wa Senegal dhidi ya Morocco ulianzia kwa bao la Mouhamed Wagne lakini wenyeji Morocco walipambana na kusawazisha kupitia kwa Ismail El Aoud na ndipo timu hizo zilipoingia kwenye mikwaju ya penalti na Senegal kushinda kwa penalti 7-6.
Morocco sasa itaumana na Misri katika mechi ya kusaka mshindi wa tatu ambayo itachezwa usiku wa Jumatatu, Juni 1, 2026.

The post Serengeti Boys vitani dhidi ya Senegal first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2026/05/31/serengeti-boys-vitani-dhidi-ya-senegal/feed/ 0