Salah - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Sat, 10 Jan 2026 18:08:53 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=6.9.4 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg Salah - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 Salah hataki Misri ilewe sifa https://www.greensports.co.tz/2026/01/08/salah-hataki-misri-ilewe-sifa/ https://www.greensports.co.tz/2026/01/08/salah-hataki-misri-ilewe-sifa/#respond Thu, 08 Jan 2026 19:01:55 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=14257 Rabat, MoroccoNahodha na mshambuliaji wa timu ya taifa ya Misri, Mohamed Salah amepuuza habari inayoiweka timu yao katika orodha ya timu zinazopewa nafasi kubwa kubeba taji ya michuano ya Afcon 2025 inayoendelea nchini Morocco.Salah ambaye pia ni mshambuliaji wa timu ya Liverpool ya England, badala yake amesema kwamba wanachofanya katika fainali za Afcon ni kuweka […]

The post Salah hataki Misri ilewe sifa first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Rabat, Morocco
Nahodha na mshambuliaji wa timu ya taifa ya Misri, Mohamed Salah amepuuza habari inayoiweka timu yao katika orodha ya timu zinazopewa nafasi kubwa kubeba taji ya michuano ya Afcon 2025 inayoendelea nchini Morocco.
Salah ambaye pia ni mshambuliaji wa timu ya Liverpool ya England, badala yake amesema kwamba wanachofanya katika fainali za Afcon ni kuweka mkazo kwa kila mechi wanayocheza.
Misri kwa sasa inapambana kusaka taji la nane la Afcon, tayari imefuzu hatua ya robo fainali baada ya kuichapa Benin mabao 3-1 huku Salah akiwa moto kwenye mechi hiyo akifunga bao la tatu na hadi sasa ana mabao matatu katika fainali hizo.
Timu hiyo imeonesha kiwango cha kuvutia katika Afcon 2025 lakini Salah yuko makini katika matarajio makubwa ambayo yanahusishwa na timu hiyo kwa kupewa nafasi kubwa ya kubeba taji.

“Tuna wachezaji wachanga na wengi wao wanacheza soka nyumbani Misri, tunachofanya ni kuipigania nchi yetu na baada ya hapo tutaona tutakapofika, kila mmoja hapa anataka kujitoa katika ubora wake,” alisema Salah.


Katika fainali za Afcon zinazoendelea, Salah hadi sasa amekosa mechi moja ya hatua ya makundi dhidi ya Angola, mechi ambayo Misri walicheza wakiwa tayari wamefuzu hatua ya mtoano (16 bora) na kukutana na Benin.
Uamuzi wa kocha Hossam Hassan kumuweka benchi mchezaji huyo ulionekana kuwa na faida kubwa kwa namna ambavyo alikuwa tishio katika mechi dhidi ya timu sumbufu ya Benin na hatimaye kutoka na ushindi.
Salah pia aliipongeza Benin akisema kwamba Misri ilicheza dhidi ya timu nzuri yenye kocha bora na mfumo mzuri na wana furaha kwa kupata ushindi ingawa anakiri haikuwa kazi rahisi.
.

The post Salah hataki Misri ilewe sifa first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2026/01/08/salah-hataki-misri-ilewe-sifa/feed/ 0
Rooney ataka Salah asugue benchi https://www.greensports.co.tz/2025/11/24/rooney-ataka-salah-asugue-benchi/ https://www.greensports.co.tz/2025/11/24/rooney-ataka-salah-asugue-benchi/#respond Mon, 24 Nov 2025 15:05:51 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=14131 Liverpool, EnglandMshambuliaji wa zamani wa Man United na timu ya taifa ya England, Wayne Rooney amemtaka kocha wa Liverpool, Arne Slot kumtupa benchi mshambuliaji wake Mohamed Salah kama njia ya kusaka ubora katika timu.Rooney ametoa kauli hiyo baada ya matokeo ya Jumamosi ambapo Liverpool ilichapwa mabao 3-0 na Nottingham Forest na hivyo kuishusha timu hiyo […]

The post Rooney ataka Salah asugue benchi first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Liverpool, England
Mshambuliaji wa zamani wa Man United na timu ya taifa ya England, Wayne Rooney amemtaka kocha wa Liverpool, Arne Slot kumtupa benchi mshambuliaji wake Mohamed Salah kama njia ya kusaka ubora katika timu.
Rooney ametoa kauli hiyo baada ya matokeo ya Jumamosi ambapo Liverpool ilichapwa mabao 3-0 na Nottingham Forest na hivyo kuishusha timu hiyo hadi nafasi ya 11 kwenye msimamo wa Ligi Kuu England.
Katika mechi hiyo, Salah alishindwa kutoa asisti au kufunga bao katika kipigo hicho ambacho ni cha sita katika mechi saba za ligi hiyo zilizopita.
Rooney ambaye pia amewahi kuwa kocha lakini hakupata mafanikio, katika hoja yake dhidi ya Salah alisema kwamba mchezaji huyo hana msaada kwa timu hata kwenye ulinzi.
Rooney alisema suala hilo linaweza kuwa linawagusa hata wachezaji wengine waliosajiliwa ambao wapo kwenye benchi na wanamuona si mwenye kukimbia kama inavyotakiwa.

“Kama mimi ningekuwa Arne Slot ningejaribu kufanya maamuzi makubwa ili yawe na matokeo chanya kwa timu yote, unapokuwa hushindi mechi unatakiwa kuwa mpambanaji na mgumu kushindwa,” alisema Rooney.


Rooney alisema Slot anatakiwa kufanya maamuzi ya kuwafanya wachezaji wawe wapambanaji na wasioshindwa na kila mchezaji awe anakimbia na watakapoanza kushinda mechi anaweza kumrudisha kwenye timu na kuwa mwenye bidii zaidi.
Sambamba na Salah ambaye amewahi kuwa mfungaji bora wa ligi hiyo, Rooney pia aliwagusia wachezaji wengine wakongwe kwenye timu akiwamo nahodha Van Dijk akisema kuwa hawapo katika ubora kama ilivyokuwa msimu uliopita na hawaisaidii timu.
Rooney pia alisema kwamba huenda kifo cha mchezaji mwenzao Diogo Jota kilichotokana na ajali ya gari kimechangia kuharibu mambo katika timu hiyo ambayo alisema inapitia wakati mgumu.

The post Rooney ataka Salah asugue benchi first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2025/11/24/rooney-ataka-salah-asugue-benchi/feed/ 0
Ukame wa mabao wa Salah haumsumbui Slot https://www.greensports.co.tz/2025/10/25/ukame-wa-mabao-wa-salah-haumsumbui-slot/ https://www.greensports.co.tz/2025/10/25/ukame-wa-mabao-wa-salah-haumsumbui-slot/#respond Sat, 25 Oct 2025 17:25:19 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=14029 Liverpool, EnglandKocha wa Liverpool, Arne Slot amesisitiza kuwa ukame wa mabao unaomkabili mshambuliaji wake Mohamed Salah ni jambo la mwisho kabisa kati ya mambo yanayoweza kumfanya awe mwenye wasiwasi.Salah au Mo, mmoja wa washambuliaji tegemeo wa Liverpool, msimu huu amekuwa na wakati mgumu kuzifumania nyavu akiwa hadi sasa na mechi sita zilizopita bila ya bao […]

The post Ukame wa mabao wa Salah haumsumbui Slot first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Liverpool, England
Kocha wa Liverpool, Arne Slot amesisitiza kuwa ukame wa mabao unaomkabili mshambuliaji wake Mohamed Salah ni jambo la mwisho kabisa kati ya mambo yanayoweza kumfanya awe mwenye wasiwasi.
Salah au Mo, mmoja wa washambuliaji tegemeo wa Liverpool, msimu huu amekuwa na wakati mgumu kuzifumania nyavu akiwa hadi sasa na mechi sita zilizopita bila ya bao na anaonekana kama amepoteza ubora uliozoeleka.
Msimu huu Salah ana mabao matatu hadi sasa na moja kati ya hayo amefunga kwa penalti na Jumatano iliyopita kwenye mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Eintracht Frankfurt ambayo Liverpool ilishinda, Salah alijikuta akicheza kwa dakika 16 za mwisho.
Ushindi huo dhidi ya Eintracht Frankfurt umekuwa faraja kubwa kwa timu hiyo baada ya kupitia kipindi kigumu cha matokeo mabaya hali ambayo pia imechangia kuwapo mjadala kuhusu Salah na ukame wake wa mabao na jinsi mshambuliaji huyo anavyopoteza nafasi za kufunga ingawa Slot hana wasiwasi katika hilo.

“Sijui kama ni kasi imepungua au la, ni jambo gumu, naweza kuja na sababu kadhaa ambazo pia sina uhakika kama ni sahihi, kwa ujumla wachezaji huwa wanapoteza nafasi na Mo pia ni binadamu, hatujamzowea kupoteza nafasi licha ya nafasi hizo kuwa nyingi kwa sasa tena mfululizo lakini haya mambo hutokea,” alisema Slot.


Jumamosi hii Liverpool itajitupa uwanjani kukabiliana na Brentford na bila shaka Slot na Salah wanaimani kwamba mechi hiyo inaweza kuwa mwanzo mpya kwa mshambuliaji huyo.

The post Ukame wa mabao wa Salah haumsumbui Slot first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2025/10/25/ukame-wa-mabao-wa-salah-haumsumbui-slot/feed/ 0
Salah nyota wa msimu EPL https://www.greensports.co.tz/2025/05/24/salah-nyota-wa-msimu-epl/ https://www.greensports.co.tz/2025/05/24/salah-nyota-wa-msimu-epl/#respond Sat, 24 May 2025 19:28:44 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=13497 Liverpool, EnglandMshambuliaji wa Liverpool, Mohamed Salah ametangazwa kuwa nyota wa msimu wa 2024-25 wa Ligi Kuu England (EPL).Mara ya kwanza Salah kubeba tuzo hiyo ambayo mshindi wake hupatikana kupitia kura zinazopigwa zikihusisha mashabiki na wataalam wa soka, ilikuwa msimu wa 2017-18.Salah, 32 ambaye ameiongoza Liverpool kubeba taji la EPL msimu huu aliwashinda wachezaji wenzake wa […]

The post Salah nyota wa msimu EPL first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Liverpool, England
Mshambuliaji wa Liverpool, Mohamed Salah ametangazwa kuwa nyota wa msimu wa 2024-25 wa Ligi Kuu England (EPL).
Mara ya kwanza Salah kubeba tuzo hiyo ambayo mshindi wake hupatikana kupitia kura zinazopigwa zikihusisha mashabiki na wataalam wa soka, ilikuwa msimu wa 2017-18.
Salah, 32 ambaye ameiongoza Liverpool kubeba taji la EPL msimu huu aliwashinda wachezaji wenzake wa Liverpool Virgil van Dijk na Ryan Gravenberch ambaye ametwaa tuzo ya mchezaji bora kijana wa msimu.
Wengine waliokuwa wakiwania tuzo hiyo na Salah ni Declan Rice wa Arsenal, Alexander Isak wa Newcastle, Bryan Mbeumo wa Brentford pamoja na Morgan Gibbs-White na Chris Wood wa Nottingham Forest..
Hii pia inakuwa mara ya kwanza tangu msimu wa 2018-19 kwa mchezaji wa Man City kutobea tuzo ya msimu husika.
Kesho Jumapili. Salah ataingia uwanjani kucheza mechi ya mwisho ya msimu dhidi ya Crsytal Palace huku tayari akiwa amezifumania nyavu mara 28 ambayo ni mabao matano kumzidi Alexander Isak wa Newcastle.
Msimu huu pia Salah ameumaliza kwa kuweka rekodi ya kuwa mchezaji wa kigeni mwenye mabao mengi zaidi katika historia ya EPL akiwa amemzidi Sergio Aguero aliyekuwa akishikilia rekodi hiyo.
Salah ambaye mwezi huu pia alitangazwa kuwa mchezaji bora na Chama cha Waandishi wa Habari za Soka pia ameongeza miaka miwili katika mkataba wake ambao sasa utamfanya aendelee kuwa na Liverpool hadi mwaka 2027.

The post Salah nyota wa msimu EPL first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2025/05/24/salah-nyota-wa-msimu-epl/feed/ 0
Salah haiwazii hatma yake Liverpool https://www.greensports.co.tz/2025/01/01/salah-haiwazii-hatma-yake-liverpool/ https://www.greensports.co.tz/2025/01/01/salah-haiwazii-hatma-yake-liverpool/#respond Wed, 01 Jan 2025 17:54:48 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=12549 Liverpool, EnglandMshambuliaji wa Liverpool, Mohamed Salah amesema bado hajaamua lolote kuhusu mambo yake ya baadaye na klabu hiyo wakati huu akiendelea kudhihirisha ubora wake.Salah hivi karibuni ameifungia Liverpool bao moja katika ushindi wa mabao 5-0 dhidi ya West Ham na kutoa pasi zilizozaa mabao mengine mawili katika ushindi huo.Wachezaji wengine wa Liverpool, Virgil van Dijk […]

The post Salah haiwazii hatma yake Liverpool first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Liverpool, England
Mshambuliaji wa Liverpool, Mohamed Salah amesema bado hajaamua lolote kuhusu mambo yake ya baadaye na klabu hiyo wakati huu akiendelea kudhihirisha ubora wake.
Salah hivi karibuni ameifungia Liverpool bao moja katika ushindi wa mabao 5-0 dhidi ya West Ham na kutoa pasi zilizozaa mabao mengine mawili katika ushindi huo.
Wachezaji wengine wa Liverpool, Virgil van Dijk na Trent Alexander-Arnold kama ilivyo kwa Salah nao wapo katika miezi yao sita ya mwisho kabla ya mikataba yao kufikia ukomo ingawa Salah ndiye amekuwa mjadala zaidi.
Na ingawa kumekuwa na hofu kwamba anaweza akaondoka Liverpool, Salah amesema fikra zake kwa sasa zipo katika kuhakikisha anashinda taji akiwa na timu hiyo na yuko mbali na mpango wowote wa kusaini mkataba mpya.

“Hapana hilo jambo kwa sasa lipo mbali, na sitaki kuwe na chochote kwenye vyombo vya habari, kitu pekee kilicho katika fikra zangu ni kutaka Liverpool ibebe taji la ligi, nataka kuwa mmoja wa wahusika wa jambo hilo” alisema Salah.


Alifafanua kwamba atafanya kila kilicho bora kwa ajili ya timu kushinda taji na kwa sasa ni timu chache zinazowakaribia hivyo wanahitaji kuwa makini na kuendelea na kasi yao.
Kwa upande wake kocha wa Liverpool, Arne Slot amesema hana wasiwasi na wachezaji hao waandamizi kwamba wanaweza kuanza mazungumzo na klabu nyingine Januari Mosi kwa kuwa anaamini amekuwa mwenye usimamizi wa hatma yao.

The post Salah haiwazii hatma yake Liverpool first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2025/01/01/salah-haiwazii-hatma-yake-liverpool/feed/ 0
Salah aanza kuaga Liverpool https://www.greensports.co.tz/2024/12/02/salah-aanza-kuaga-liverpool/ https://www.greensports.co.tz/2024/12/02/salah-aanza-kuaga-liverpool/#respond Mon, 02 Dec 2024 12:40:54 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=12301 Liverpool, EnglandMshambuliaji wa Liverpool, Mohamed Salah amesema ushindi wa timu hiyo wa mabao 2-0 wa jana Jumamosi dhidi ya Man City ni mechi ya mwisho kwake kuivaa timu hiyo kwenye dimba la Anfield.Kauli ya mchezaji hiyo inaashiria kwamba ataihama timu hiyo huku habari zaidi zikidai kwamba vigogo wa klabu ya PSG ya Ufaransa wako katika […]

The post Salah aanza kuaga Liverpool first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
Liverpool, England
Mshambuliaji wa Liverpool, Mohamed Salah amesema ushindi wa timu hiyo wa mabao 2-0 wa jana Jumamosi dhidi ya Man City ni mechi ya mwisho kwake kuivaa timu hiyo kwenye dimba la Anfield.
Kauli ya mchezaji hiyo inaashiria kwamba ataihama timu hiyo huku habari zaidi zikidai kwamba vigogo wa klabu ya PSG ya Ufaransa wako katika mkakati mzito wa kumsajili mchezaji huyo.
Katika mechi ya jana Salah ndiye aliyetoa pasi iliyozaa bao la kwanza la Liverpool lililofungwa na Cody Gakpo na baada ya hapo akafunga bao la pili kwa penalti iliyotolewa baada ya Luis Diaz kuchezewa rafu na Stefan Ortega.
Ushindi huo umeifanya Liverpool kushika usukani katika Ligi Kuu England (EPL) ikiwa mbele kwa tofauti ya tisa na kuwaacha Man City ambao ni mabingwa watetezi kwa tofauti ya pointi 11.
Mara baada ya mechi hiyo Salah aliulizwa kuhusu mambo ya baadaye ndani ya Liverpool na kukiri kwamba huenda hiyo ikawa mechi yake ya mwisho dhidi Man City huku mkataba wake na Liverpool ukifikia ukomo mwishoni mwa msimu huu.

“Ukweli ni kwamba haya ni mambo yangu, hadi sasa hii ndiyo mechi yangu ya mwisho kuichezea Liverpool dhidi ya Man City kwa hiyo nilienda kuifurahia, mazingira yalikuwa ya kuvutia, hivyo naifurahia kila hatua, ni matumaini kwamba tutashinda taji la ligi na baada ya hapo mengine yatafuata,” alisema Salah.


Akifafanua zaidi kuhusu hatma yake ndani ya kikosi cha Liverpool Salah alisema kwamba huu ni mwezi Desemba na hajapata ofa yoyote ya kubaki katika klabu hiyo kwa hiyo huenda yeye ni wa kuondoka zaidi kuliko wa kubaki.
“Mnajua nimekuwa katika klabu hii kwa miaka mingi, hakuna klabu kama hii lakini mwisho wa siku si suala langu peke yangu, na kama nilivyosema hii ni Desemba na hakuna lolote lililofanyika kuhusu mambo yangu ya baadaye katika klabu hii,” alisema Salah.
Salah pia amekuwa akihusishwa kwenda kucheza soka Saudi Arabia ingawa PSG ndio wanaotajwa zaidi kuisaka saini ya mshambuliaji huyo kwa imani kwamba watamsajili baada ya msimu huu akiwa mchezaji huru.

The post Salah aanza kuaga Liverpool first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/12/02/salah-aanza-kuaga-liverpool/feed/ 0
Rodrygo kumrithi Salah Liverpool https://www.greensports.co.tz/2024/09/26/rodrygo-atajwa-kumrithi-salah-liverpool/ https://www.greensports.co.tz/2024/09/26/rodrygo-atajwa-kumrithi-salah-liverpool/#respond Thu, 26 Sep 2024 05:56:15 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=11944 Madrid, HispaniaLiverpool imeanza kupiga hesabu za kumsajili mshambuliaji wa Real Madrid, Rodrygo ili achukue nafasi ya Mohamed Salah baada ya kuwapo habari kwamba Salah anajipanga kuihama timu hiyo.Hivi karibuni, Salah, 32, mshambuliaji tegemeo wa Liverpool na timu ya taifa ya Misri, japo hakuwa wazi lakini alisema huu unaweza kuwa msimu wake wa mwisho kuvaa jezi […]

The post Rodrygo kumrithi Salah Liverpool first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Madrid, Hispania
Liverpool imeanza kupiga hesabu za kumsajili mshambuliaji wa Real Madrid, Rodrygo ili achukue nafasi ya Mohamed Salah baada ya kuwapo habari kwamba Salah anajipanga kuihama timu hiyo.
Hivi karibuni, Salah, 32, mshambuliaji tegemeo wa Liverpool na timu ya taifa ya Misri, japo hakuwa wazi lakini alisema huu unaweza kuwa msimu wake wa mwisho kuvaa jezi ya Liverpool.
Kauli hiyo inaonesha kwamba huenda Liverpool ikamkosa mshambuliaji huyo ambaye kwa muda mrefu amekuwa akiwindwa na klabu kadhaa za Saudi Arabia na ndio maana Liverpool imeanza mapema hesabu za mtu wa kuziba nafasi hiyo.
Katika harakati hizo, chanzo kimoja cha habari kimeripoti kuwa jina la Rodrygo, ambaye pia ni mshambuliaji wa timu ya Brazil ndilo linalotajwa zaidi na kuonekana anaweza kuwa mtu sahihi wa kuchukua nafasi hiyo.
Kwa upande wa Rodrygo kinachoonekana ni kwamba huenda akawa tayari kwa changamoto mpya hasa kutokana na ushindani wa namba ambao unatajwa katika kikosi cha kwanza cha Real Madrid.


Tangu Real Madrid imsajili Kylian Mbappe kumekuwa na hofu kuhusu nafasi ya Rodrygo ingawa kocha Carlo Ancelotti amekuwa akiwapa nafasi washambuliaji watatu kwenye kikosi cha kwanza.
Msimu uliopita, Real Madrid ilibeba mataji ya La Liga na Ligi ya Mabingwa Ulaya ambapo kwa La Liga Rodrygo alifunga mabao 10 katika mechi 34 na kwa Ligi ya Mabingwa alifunga mabao matano.
Rodrygo, 23, pamoja na kufunga mabao hayo, jina lake halimo katika wachezaji wanaowania tuzo ya Ballon d’Or jambo ambalo alisema limemsikitisha kwa kuwa anaamini alipaswa kuwamo.
Wachezaji wa Real Madrid waliomo katika orodha ya wanaowania tuzo hiyo ni Vinícius Júnior, Jude Bellingham, Federico Valverde, Toni Kroos, Antonio Rüdiger, Dani Carvajal na Mbappe.

The post Rodrygo kumrithi Salah Liverpool first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/09/26/rodrygo-atajwa-kumrithi-salah-liverpool/feed/ 0
Salah atangaza kuondoka Liverpool https://www.greensports.co.tz/2024/09/02/salah-atangaza-kuondoka-liverpool/ https://www.greensports.co.tz/2024/09/02/salah-atangaza-kuondoka-liverpool/#respond Mon, 02 Sep 2024 20:42:48 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=11850 Liverpool, EnglandMshambuliaji wa timu ya Liverpool, Mohamed Salah amesema kwamba huenda huu ukawa msimu wake wa mwisho kuichezea timu hiyo.Salah ambaye jana Jumapili aliiwakilisha Liverpool katika ushindi wa 3-0 dhidi ya Man United kwenye Ligi Kuu England (EPL), mkataba wake na timu hiyo unafikia ukomo mwishoni mwa msimu huu wa 2024-25.Katika mechi hiyo, Salah, 32, […]

The post Salah atangaza kuondoka Liverpool first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Liverpool, England
Mshambuliaji wa timu ya Liverpool, Mohamed Salah amesema kwamba huenda huu ukawa msimu wake wa mwisho kuichezea timu hiyo.
Salah ambaye jana Jumapili aliiwakilisha Liverpool katika ushindi wa 3-0 dhidi ya Man United kwenye Ligi Kuu England (EPL), mkataba wake na timu hiyo unafikia ukomo mwishoni mwa msimu huu wa 2024-25.
Katika mechi hiyo, Salah, 32, ambaye pia ni mshambuliaji wa timu ya taifa ya Misri, alifunga bao moja na kutoa asisti mbili.
“Nimekuwa na kipindi kizuri cha mapumziko ya kiangazi, nimekuwa na muda mrefu wa kukaa peke yangu na kufikiria mazuri, kama unavyofahamu huu ni mwaka wangu wa mwisho katika klabu hii,” alisema Salah.
Salah alisema anachotaka ni kuufurahia msimu huu na hadhani kama atakuwa mtu mwenye fikra nyingi badala yake anachoona ni kwamba yuko huru kucheza soka na mambo yajayo yatajulikana.
“Hakuna mtu yeyote aliyezungumza nami kuhusu mkataba wangu, kwa hiyo kilicho sahihi ni kuwa nitacheza katika msimu wangu wa mwisho na baada ya msimu tutaona itakavyokuwa, si juu yangu,” alisema Salah.
Septemba mwaka jana Liverpool ilikataa ofa ya Pauni 150 milioni kutoka klabu ya Al Ittihad ya Saudi Arabia na ingawa zipo habari za klabu hiyo kuanza upya mpango wa kumtaka Salah lakini jambo hilo bado halijawa rasmi.
Kwa upande wake kocha wa Liverpool, Arne Slot alisema kwamba hatojadili suala la mchezaji huyo kuhusu mkataba wake badala yake anachofahamu ni kwamba Salah ni mchezaji wao na jambo hilo linampa furaha.
Wachezaji wengine wa Liverpool ambao mikataba yao inafikia ukomo mwishoni mwa msimu huu ni pamoja n nahodha Virgil van Dijk na Trent Alexander-Arnold.

The post Salah atangaza kuondoka Liverpool first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/09/02/salah-atangaza-kuondoka-liverpool/feed/ 0
Salah aahidi kuipigania Liverpool https://www.greensports.co.tz/2024/05/22/salah-aahidi-kuipigania-liverpool/ https://www.greensports.co.tz/2024/05/22/salah-aahidi-kuipigania-liverpool/#respond Wed, 22 May 2024 07:50:24 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=11069 Liverpool, EnglandMshambuliaji wa Liverpool, Mohamed Salah ameonesha dalili zote za kubaki Liverpool baada ya kuahidi kuendelea kuipigania mataji timu hiyo kwa nguvu zote licha ya kuondoka kwa kocha Jurgen Klopp.Salah anaingia katika mwaka wake wa mwisho wa mkataba wake wa sasa na hadi sasa hakuna makubaliano yoyote yaliyofikiwa baina ya klabu na mchezaji huyo ili […]

The post Salah aahidi kuipigania Liverpool first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Liverpool, England
Mshambuliaji wa Liverpool, Mohamed Salah ameonesha dalili zote za kubaki Liverpool baada ya kuahidi kuendelea kuipigania mataji timu hiyo kwa nguvu zote licha ya kuondoka kwa kocha Jurgen Klopp.
Salah anaingia katika mwaka wake wa mwisho wa mkataba wake wa sasa na hadi sasa hakuna makubaliano yoyote yaliyofikiwa baina ya klabu na mchezaji huyo ili kumuongezea mkataba zaidi ya muda uliobaki.
Majira ya kiangazi msimu uliopita, Liverpool ilikataa ofa ya Pauni milioni 150 ili kumuuza Salah katika klabu ya Al Ittihad ya Saudi Arabia ingawa kwa sasa zipo habari kwamba klabu hiyo huenda ikaamsha upya mpango huo.
Mara baada ya Klopp kuaga rasmi Liverpool na kocha mpya, Arne Slot kutangazwa rasmi, majaliwa ya Salah katika klabu hiyo yalianza kujadiliwa na kukawa na hofu kwamba huenda naye akaondoka.
Kupitia mitandao ya kijamii, Salah hata hivyo ameupinga mpango wowote wa kuondoka baada ya kusema kwamba atakuwa na Liverpool msimu ujao na azma yake ni kuipa mafanikio timu hiyo.

“Tunajua kwamba mataji ndio kitu muhimu na tutafanya kila kinachowezekana kuliwezesha hilo msimu ujao, mashabiki wetu wana haki katika hilo na tutapambana hakuna mfano,” alisema Salah.


Salah, 31, pia alimpongeza kocha anayeondoka Klopp ambaye hivi karibuni walitibuana katika mechi dhidi ya West Ham kwa kinachodhaniwa kuwa alichukia kuwekwa benchi na kocha huyo.
“Ni jambo kubwa kubeba mataji na kupata uzoefu nawe katika miaka saba iliyopita, nakutakia heri kwa mambo yako yajayo, natumaini tutakutana tena,” alisema Salah katika posti yake kwenye mitandao ya kijamii iliyoambatana na picha yake akiwa na Klopp.

The post Salah aahidi kuipigania Liverpool first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/05/22/salah-aahidi-kuipigania-liverpool/feed/ 0
Klopp, Salah wamaliza utata https://www.greensports.co.tz/2024/05/04/klopp-salah-wamaliza-utata/ https://www.greensports.co.tz/2024/05/04/klopp-salah-wamaliza-utata/#respond Sat, 04 May 2024 18:57:35 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=10839 Liverpool, EnglandKocha wa Liverpool, Jürgen Klopp amesema kwamba mzozo ulioibuka kati yake na mshambuliaji wake, Mohamed Salah mwishoni mwa wiki iliyopita katika mechi yao na West Ham haupo tena.Klopp na Salah walionekana katika picha za televisheni wakitoleana kauli zilizoashiria kuwapo mzozo baina yao wakati wa mechi hiyo iliyoisha kwa sare ya mabao 2-2.Baada ya mechi […]

The post Klopp, Salah wamaliza utata first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Liverpool, England
Kocha wa Liverpool, Jürgen Klopp amesema kwamba mzozo ulioibuka kati yake na mshambuliaji wake, Mohamed Salah mwishoni mwa wiki iliyopita katika mechi yao na West Ham haupo tena.
Klopp na Salah walionekana katika picha za televisheni wakitoleana kauli zilizoashiria kuwapo mzozo baina yao wakati wa mechi hiyo iliyoisha kwa sare ya mabao 2-2.
Baada ya mechi hiyo, Salah ambaye alizozana na kocha wake wakati akiingia uwanjani kutokea benchi, alisema kwamba ‘moto ungeweza kuwaka’ iwapo angeamua kuzungumza kilichojiri.
Katika mkutano na waandishi wa habari jana Ijumaa, Klopp hakutaka kuelezea kwa nini waliingia katika mzozo yeye na mchezaji wake badala yake alisisitiza kwamba jambo hilo limepita na kwa sasa wanaangalia mbele.

“Yote yamemalizwa, hakuna tatizo, kama tungekuwa hatujuani kwa muda mrefu sina hakika kama tungeweza kulifanyia kazi suala hilo, lakini tunajuana kwa muda mrefu na vile vile tunaheshimiana,” alisema Klopp.


Klopp alisisitiza kwamba hakuna tatizo na mambo ya aina hiyo wanaweza kuyamaliza wao wenyewe bila ya kuwapo matarajio ya kuingiliwa na watu wengine wa nje.
Sare dhidi ya West Ham imezidi kufifisha matumaini ya Liverpool kubeba taji la Ligi Kuu England (EPL) kwani kwa sasa inashika nafasi ya tatu ikiwa imeachwa na vinara Arsenal kwa tofauti ya pointi tano zikiwa zimebaki mechi tatu kabla ya kumalizika kwa ligi hiyo.

The post Klopp, Salah wamaliza utata first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/05/04/klopp-salah-wamaliza-utata/feed/ 0