Saido Ntibazonkiza - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Tue, 18 Jun 2024 13:43:53 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=7.0 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg Saido Ntibazonkiza - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 Saido aachwa Simba https://www.greensports.co.tz/2024/06/18/saido-aachwa-simba/ https://www.greensports.co.tz/2024/06/18/saido-aachwa-simba/#respond Tue, 18 Jun 2024 13:43:52 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=11368 Na mwandishi wetuKlabu ya Simba imeweka wazi leo Jumanne kuachana na kiungo mshambuliaji wake, Saido Ntobazonkiza baada ya kudumu Msimbazi kwa msimu mmoja na nusu.Taarifa hiyo imetolewa na Simba kupitia kurasa zao za mitandao ya kijamii ambapo imetoa shukrani kwa mchezaji huyo raia wa Burundi kwa utumishi wake katika muda wote aliokuwepo hapo.Saido aliyewahi kukipiga […]

The post Saido aachwa Simba first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
Saido Ntibazonkiza

Na mwandishi wetu
Klabu ya Simba imeweka wazi leo Jumanne kuachana na kiungo mshambuliaji wake, Saido Ntobazonkiza baada ya kudumu Msimbazi kwa msimu mmoja na nusu.
Taarifa hiyo imetolewa na Simba kupitia kurasa zao za mitandao ya kijamii ambapo imetoa shukrani kwa mchezaji huyo raia wa Burundi kwa utumishi wake katika muda wote aliokuwepo hapo.
Saido aliyewahi kukipiga Yanga msimu wa 2020-21 ndiye kinara wa mabao wa timu hiyo katika msimu wa 2023-24 uliomalizika hivi karibuni ambapo alitupia mabao 11.
Katika msimu wake wa kwanza kutua Simba katika dirisha dogo la 2022-23 alifunga mabao 17 na kufungana ufungaji bora wa Ligi Kuu NBC na aliyekuwa mshambuliaji wa Yanga, Fiston Mayele anayekipiga Pyramid ya Misri kwa sasa.
Saido mmoja wa wachezaji mahiri na mwenye uhakika kwenye mikwaju ya penalti pia aliwahi kung’ara na timu ya Geita Gold mara baada ya kuondoka Yanga.
Hatua ya Simba kuachana na mchezaji huyo inawafanya wachezaji walioachwa kuwa wawili baada ya aliyekuwa nahodha, John Bocco ambaye kwa sasa ni kocha wa timu ya vijana ya Simba chini ya miaka 17 naye kupewa mkono wa kwaheri.

The post Saido aachwa Simba first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/06/18/saido-aachwa-simba/feed/ 0
Ntibazonkiza arejea kundini https://www.greensports.co.tz/2023/02/15/ntibazonkiza-arejea-kundini/ https://www.greensports.co.tz/2023/02/15/ntibazonkiza-arejea-kundini/#respond Wed, 15 Feb 2023 04:59:33 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=5134 Na mwandishi wetuWakati Simba ikijipanga kwa mechi yao ya wikiendi hii dhidi ya Raja Casablanca imeeleza kurejea kwa kiungo mshambuliaji wao, Saido Ntibazonkiza ambaye alikosekana kwenye mechi iliyopita.Saido hakuwepo kwenye mchezo wa kwanza wa hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Horoya AC akielezwa ni majeruhi. Katika mechi hiyo, Simba ilifungwa bao […]

The post Ntibazonkiza arejea kundini first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Wakati Simba ikijipanga kwa mechi yao ya wikiendi hii dhidi ya Raja Casablanca imeeleza kurejea kwa kiungo mshambuliaji wao, Saido Ntibazonkiza ambaye alikosekana kwenye mechi iliyopita.
Saido hakuwepo kwenye mchezo wa kwanza wa hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Horoya AC akielezwa ni majeruhi. Katika mechi hiyo, Simba ilifungwa bao 1-0.
Akizungumza Jumanne hii jijini Dar es Salaam, Ofisa Habari wa Simba, Ahmed Ally alisema mchezaji ameshatengemaa, amepumzika kama ilivyotakiwa na sasa atajiunga na kambi ya timu hiyo kuelekea mechi ijayo akiwa fiti.

“Saido ambaye hatukusafiri naye Guinea alikuwa na majeraha kama tulivyoeleza, akapewa muda wa kupumzika, kupata matibabu pia lakini sasa ametengemaa na timu itakaporejea kambini naye atarejea, hii ni kusema kwamba atakuwa sehemu ya mchezo,” alisema Ally.


Ofisa huyo pia aligusia kurejea kwa majeruhi mwingine, Peter Banda ambaye atajiunga na kambi kisha atafanyiwa vipimo ili madaktari wajiridhishe kama atakuwa sehemu ya mchezo au la.
Pia alitolea ufafanuzi kukosekana kwa kiungo wa kati, Sadio Kanoute ambaye ataukosa mchezo huo utakaopigwa Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam kutokana na kutumikia adhabu ya kadi tatu za njano.
“Sadio alioneshwa kadi ya njano kwenye mchezo wetu na Horoya, sasa tunathibitisha kwamba Kanoute ataukosa mchezo kutokana na kadi tatu za njano. Kikanuni kadi alizopata hatua ya awali anaondoka nazo hadi hatua ya makundi, ndiyo maana kadi aliyopata majuzi inamfanya aukose mchezo ujao,” alisema.
Katika hatua nyingine, Ally alitangaza kushuka kwa bei za viingilio vya mchezo huo ambapo viti vya mzunguko vilivyokuwa Sh 5,000 sasa ni Sh 3,000, VIP C imeshuka kutoka Sh 20,000 hadi Sh 10,000 huku VIP B ikisalia Sh 20,000 na VIP A ni Sh 30,000.
Pia, Ally alitangaza kauli mbiu yao kuelekea mchezo huo dhidi ya Wamorocco hao ni Moto ni Ule Ule, kwa Mkapa hatoki mtu, akidai moto ulioziunguza timu nyingine za Kaskazini mwa Afrika kwenye Uwanja wa Mkapa zilipokuja kucheza na Simba, ndiyo utakaowaangamiza wapinzani wao hao.

The post Ntibazonkiza arejea kundini first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/02/15/ntibazonkiza-arejea-kundini/feed/ 0