Ruvu Shooting - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Sat, 13 May 2023 09:43:38 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=6.9.4 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg Ruvu Shooting - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 Simba haijakata tamaa Ligi Kuu NBC https://www.greensports.co.tz/2023/05/13/simba-haijakata-tamaa-ligi-kuu-nbc-2/ https://www.greensports.co.tz/2023/05/13/simba-haijakata-tamaa-ligi-kuu-nbc-2/#respond Sat, 13 May 2023 09:38:08 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=6142 Na mwandishi wetuSimba haijakata tamaa na taji la Ligi Kuu NBC, ushindi wa mabao 3-0 mbele ya Ruvu Shooting umeifanya ifikishe pointi 67, ushindi ambao utakuwa na maana kubwa kama Jumamosi itakuwa siku mbaya kwa Yanga mbele ya Dodoma Jiji.Kwa ushindi huo, Simba inayoshika nafasi ya pili katika ligi hiyo, imeisogelea Yanga kwa tofauti ya […]

The post Simba haijakata tamaa Ligi Kuu NBC first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Simba haijakata tamaa na taji la Ligi Kuu NBC, ushindi wa mabao 3-0 mbele ya Ruvu Shooting umeifanya ifikishe pointi 67, ushindi ambao utakuwa na maana kubwa kama Jumamosi itakuwa siku mbaya kwa Yanga mbele ya Dodoma Jiji.
Kwa ushindi huo, Simba inayoshika nafasi ya pili katika ligi hiyo, imeisogelea Yanga kwa tofauti ya pointi nne huku ikiombea matokeo mabaya katika mechi zilizobaki za timu hiyo kuanzia mechi na Dodoma Jiji Jumamosi hii.
Ushindi wa Simba uliopatikana Ijumaa hii usiku kwenye Uwanja wa Azam Complex utabaki kuwa furaha ya Simba pekee na hautoisumbua Yanga kama timu hiyo itafanikiwa kuchota pointi zote tatu mbele ya Dodoma Jiji.
Mechi na Dodoma itakuwa ya 28 kwa Yanga kama ilivyo Simba na iwapo itashinda itatawazwa rasmi kinara wa Ligi Kuu NBC msimu wa 2022/23 kwa kufikisha pointi 74 ambazo haziwezi kufikiwa na timu yoyote.
Ikitokea Yanga itashindwa au kutoka sare mbele ya Dodoma Jiji, hapo itakuwa imejichelewesha katika kutawazwa kinara wa ligi na kuzidi kufufua matumaini ya Simba ambayo kocha msaidizi wa timu hiyo, Juma Mgunda hivi karibuni alinukuliwa akisema kwamba bado hawajakata tamaa katika mbio za kulisaka taji hilo hadi mwisho utakapofika.
Simba katika mechi na Dodoma ilianza kuhesabu mabao yake katika dakika ya 29 mfungaji akiwa Clatous Chama kabla ya Pape Sakho kuhitimisha mabao mawili katika dakika za 71 na la pili katika dakika za nyongeza.
Kwa upande mwingine ushindi wa Simba umekuwa balaa kubwa kwa Ruvu Shooting inayochechemea mkiani katika msimamo wa ligi hiyo ikiwa imefikisha pointi 20 katika mechi 28 na sasa ni kama vile inasubiri siku tu za kutangazwa rasmi kushuka daraja na kuachana na Ligi Kuu NBC.

The post Simba haijakata tamaa Ligi Kuu NBC first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/05/13/simba-haijakata-tamaa-ligi-kuu-nbc-2/feed/ 0
Simba kuikabili Ruvu Azam Complex https://www.greensports.co.tz/2023/05/11/simba-kuikabili-ruvu-azam-complex/ https://www.greensports.co.tz/2023/05/11/simba-kuikabili-ruvu-azam-complex/#respond Thu, 11 May 2023 13:01:19 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=6112 Na mwandishi wetuSimba kesho Ijumaa inatarajia kushuka dimbani katika Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam kuvaana na Ruvu Shooting ikiwa ni mchezo wa raundi ya 28 wa Ligi Kuu NBC iliyoko ukingoni.Simba inaingia kwenye mchezo huo ikiwa na kumbukumbu ya kulazimishwa sare ya bao 1-1 na Namungo na kuharibu hesabu zao za kuupigania ubingwa […]

The post Simba kuikabili Ruvu Azam Complex first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
Kocha Juma Mgunda wa Simba (kulia) akitoa maelekezo kwa wachezaji wake.

Na mwandishi wetu
Simba kesho Ijumaa inatarajia kushuka dimbani katika Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam kuvaana na Ruvu Shooting ikiwa ni mchezo wa raundi ya 28 wa Ligi Kuu NBC iliyoko ukingoni.
Simba inaingia kwenye mchezo huo ikiwa na kumbukumbu ya kulazimishwa sare ya bao 1-1 na Namungo na kuharibu hesabu zao za kuupigania ubingwa wa ligi hiyo msimu huu, mchezo uliopigwa kwenye Uwanja wa Majaliwa, Lindi.
Timu hizo zinakutana zikiwa katika nafasi tofauti kwenye msimamo, Simba ipo nafasi ya pili ikiwa na pointi 64 wakati Ruvu Shooting inaburuza mkia kwa pointi 20 na baada ya mchezo huo timu zote zitabakiwa na mechi mbili kila moja kabla ya msimu kuisha.
Kuelekea mchezo huo, kocha msaidizi wa Simba, Juma Mgunda amesema maandalizi yao yanakwenda vizuri na wachezaji wake wapo katika hali nzuri kuwakabili Ruvu.
Mgunda alisema mchezaji atakayeukosa mchezo huo ni kipa Aishi Manula anayeuguza maumivu ya nyonga lakini waliobaki wapo katika hali nzuri na lengo lao ni kushinda mchezo huo ili kupoza machungu ya mashabiki wao.

“Tupo tayari kwa mchezo, wachezaji wangu wote wapo sawa kimbinu na hata kiakili, naamini utakuwa mchezo wa ushindani kutokana na Ruvu Shooting kuhitaji ushindi ili kujinasua na janga la kushuka daraja,” alisema Mgunda.


Kocha Mkuu wa Ruvu, Mbwana Makata alisema wamejiandaa kuikabili Simba, ingawa mchezo utakuwa mgumu kutokana na ubora wa timu wanayokwenda kukutana nayo.
“Nikiri tu huu ni mchezo mgumu sana kwetu sababu tunakutana na timu bora kuliko tulivyo sisi na mbaya zaidi wametoka kujeruhiwa pamoja na yote tutapambana kuona wapi tutaishia lakini mambo ni magumu kwetu,” alisema Makata.
Kocha huyo alisema hakuna mchezaji atakayekosa kwenye mchezo huo kutokana na kadi au majeruhi hivyo pamoja na ugumu wa mchezo lakini wamedhamiria kupambana ili kupata ushindi.

The post Simba kuikabili Ruvu Azam Complex first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/05/11/simba-kuikabili-ruvu-azam-complex/feed/ 0
Azam, Ruvu Shooting vitani https://www.greensports.co.tz/2023/04/21/azam-ruvu-shooting-vitani/ https://www.greensports.co.tz/2023/04/21/azam-ruvu-shooting-vitani/#respond Fri, 21 Apr 2023 19:53:48 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=5892 Na mwandishi wetuTimu ya Azam imekiri kuwa na kibarua kigumu kuelekea mchezo wao wa kesho wa Ligi Kuu NBC dhidi ya Ruvu Shooting, ikikiri ni mchezo mgumu kwao kulingana na mazingira ya timu zote mbili.Kocha Msaidizi wa Azam, Aggrey Morris amesema wanauchukulia mchezo huo utakaopigwa Uwanja wa Jamhuri, Morogoro kwa umakini mkubwa kutokana na nafasi […]

The post Azam, Ruvu Shooting vitani first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Timu ya Azam imekiri kuwa na kibarua kigumu kuelekea mchezo wao wa kesho wa Ligi Kuu NBC dhidi ya Ruvu Shooting, ikikiri ni mchezo mgumu kwao kulingana na mazingira ya timu zote mbili.
Kocha Msaidizi wa Azam, Aggrey Morris amesema wanauchukulia mchezo huo utakaopigwa Uwanja wa Jamhuri, Morogoro kwa umakini mkubwa kutokana na nafasi iliyopo Ruvu wakitambua namna gani wapinzani wao wanauhitaji ushindi.
“Mchezo tunaocheza na Ruvu ni mchezo tunaouchukulia kwa umakini mkubwa, ukiangalia msimamo ulivyo, siku zote ukicheza na timu ya hali kama hii ndiyo inaogopesha kabisa, hilo tunalijua, tunaiheshimu ni timu ya ushindani, upinzani utakuwa mkubwa lakini tumejipanga kufanya vizuri,” alisema Aggrey.
Azam yenye pointi 50 katika nafasi ya nne, inautafuta ushindi kuipiku Singida BS iliyo nafasi ya tatu kwa pointi 51 wakati Ruvu iliyo nafasi ya 15 kwa pointi 20 inapambana kujinasua isishuke daraja.
Ofisa Habari wa Ruvu, Masau Bwire ameeleza kuwa wanatambua ugumu wa mechi hiyo kutokana na mahitaji ya timu zote mbili lakini mipango yao ni kutumia mechi nne zilizobaki kujinasua na janga la kushuka daraja hivyo anafahamu ugumu utakaokuwepo.
“Azam wanatafuta nafasi ya tatu ili pengine iwe rahisi kushiriki mashindano ya Caf (Shirikisho la Soka Afrika), na sisi tunapambana kuhakikisha tunashinda mechi zilizosalia ili tuendelee kuwepo kwenye ligi msimu ujao na hatuhitaji kupoteza mechi hizi, kuna marekebisho mengi tumefanya kuhakikisha tunasalia,” alisema Bwire.
Katika mechi tano za mwisho za ligi, Azam imeshinda mbili, sare moja na kufungwa mbili wakati Ruvu imeshinda michezo miwili na kufungwa mitatu. Mechi ya kwanza iliyozikutanisha timu hizo msimu huu iliisha kwa sare ya mabao 2-2.
Mechi nyingine ya ligi itakayopigwa kesho itazikutanisha Dodoma Jiji dhidi ya KMC Uwanja wa Jamhuri Dodoma. Mechi ya kwanza, KMC ilishinda kwa bao 1-0.

The post Azam, Ruvu Shooting vitani first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/04/21/azam-ruvu-shooting-vitani/feed/ 0
Ruvu: Mapambano yanaendelea https://www.greensports.co.tz/2023/02/18/ruvu-mapambano-yanaendelea/ https://www.greensports.co.tz/2023/02/18/ruvu-mapambano-yanaendelea/#respond Sat, 18 Feb 2023 16:34:05 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=5205 Na mwandishi wetuLicha ya kufungwa mabao 3-2 na Geita Gold, timu ya Ruvu Shooting imeeleza kuwa bado ina nafasi ya kuendelea kupambana kuhakikisha inatoka kwenye mstari wa kushuka daraja.Kocha wa Ruvu, Mbwana Makata ameeleza kuwa ingawa walipambana na kuchomoa mabao mawili waliyotanguliwa lakini makosa ya dakika za mwisho yaliwaponza na kuwapa bao wapinzani wao licha […]

The post Ruvu: Mapambano yanaendelea first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Licha ya kufungwa mabao 3-2 na Geita Gold, timu ya Ruvu Shooting imeeleza kuwa bado ina nafasi ya kuendelea kupambana kuhakikisha inatoka kwenye mstari wa kushuka daraja.
Kocha wa Ruvu, Mbwana Makata ameeleza kuwa ingawa walipambana na kuchomoa mabao mawili waliyotanguliwa lakini makosa ya dakika za mwisho yaliwaponza na kuwapa bao wapinzani wao licha ya kuwa vijana wake walijituma mno.
Alisema kwa matokeo hayo bado wana nafasi, wanakwenda kujipanga zaidi kwa mchezo unaofuata dhidi ya Kagera Sugar wakitaka kurekebisha makosa, wapate matokeo na kujitoa mkiani mwa msimamo wa ligi.

“Mechi hiyo imeshapita na sasa akili zetu zimehamia kwenye mechi na Kagera na zinazofuata, tunarekebisha makosa ili kufufua matumaini ya kuepuka kushuka daraja, nina imani tukishinda mechi mbili tatu tutasogea juu na tutapambana mpaka mwisho tuone kilichopo, kwa sasa bado mapema sana,” alisema Makata.


Naye kocha msaidizi wa Geita Gold, Mathias Wandiba alisema wanawashukuru wachezaji kwa kujituma kwao na kupata matokeo kwa kuwa mchezo ulikuwa mgumu kutokana na mazingira halisi ya Ruvu kuhitaji pointi ili kujinasua mkiani, pia aliwashukuru mashabiki wao kujitokeza kwa wingi kuwaunga mkono uwanjani.
Ruvu ipo nafasi ya 15 ikiwa na pointi 17 wakati Geita ipo nafasi ya tano na ina pointi 34 baada ya wote kushuka dimbani mara 23.

The post Ruvu: Mapambano yanaendelea first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/02/18/ruvu-mapambano-yanaendelea/feed/ 0