Rooney - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Thu, 03 Apr 2025 18:53:38 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=6.8 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg Rooney - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 Rooney bado kidogo asajiliwe Barca https://www.greensports.co.tz/2025/04/01/rooney-bado-kidogo-asajiliwe-barca/ https://www.greensports.co.tz/2025/04/01/rooney-bado-kidogo-asajiliwe-barca/#respond Tue, 01 Apr 2025 19:25:43 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=13182 London, EnglandMshambuliaji wa zamani wa Man United na timu ya taifa ya England, Wayne Rooney amesema kuwa ilikuwa bado kidogo ajiunge na Barcelona mwaka 2010.Katika kipindi hicho Barelona au Barca ilisifika duniani kote kwa soka la uhakika huku ikibeba mataji ikiwa na mshambuliaji nyota Lionel Messi na viungo Xavi na Iniesta.Akizungumza katika kipindi cha michezo […]

The post Rooney bado kidogo asajiliwe Barca first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

London, England
Mshambuliaji wa zamani wa Man United na timu ya taifa ya England, Wayne Rooney amesema kuwa ilikuwa bado kidogo ajiunge na Barcelona mwaka 2010.
Katika kipindi hicho Barelona au Barca ilisifika duniani kote kwa soka la uhakika huku ikibeba mataji ikiwa na mshambuliaji nyota Lionel Messi na viungo Xavi na Iniesta.
Akizungumza katika kipindi cha michezo cha BBC, Rooney pia alisema kwamba Real Madrid na Chelsea nazo zilimtaka lakini ilikuwa Barca chini ya Pep Guardiola ndiyo iliyomvutia zaidi.
“Nilipowaambia Man United mwaka 2010 kwamba sitaki kusaini mkataba mpya na kuwasilisha ombi la uhamisho, klabu tatu zilikuja zikitaka kunisajili,” alisema Roney.

“Manchester City imekuwa ikizungumzwa mara kwa mara kuwa ni mojawapo lakini sikuwahi kudhani kwamba ilikuwa chaguo langu, timu zilizowasilisha maombi ya kunitaka ni Real Madrid, Chelsea na Barcelona,” alisema Rooney.

Rooney alisema kwamba katika fikra zake alikuwa tayari kuondoka Man United na kwenda kucheza soka Hispania na mazungumzo ya awali yalishaanza kufanyika.
Pia Rooney alisema mpango wa kujiunga na Real Madrid nao kwa siku kadhaa ilionekana wenye kufanikiwa lakini alikuwa akiifikiria zaidi Barcelona na namna ambavyo angefiti katika kikosi kilichokuwa na Messi, Iniesta, Xavi na Sergio Busquets.
Rooney ambaye kabla ya kusajiliwa Man United alikuwa akiichezea Everton tangu utotoni, alisema kwamba mwishowe aliamua kubaki Man United lakini alivutiwa zaidi na Barca iliyokuwa na kikosi bora wakati huo na kila mchezaji angependa kucheza katika timu hiyo.

The post Rooney bado kidogo asajiliwe Barca first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2025/04/01/rooney-bado-kidogo-asajiliwe-barca/feed/ 0
Rooney ataka Man United isukwe upya https://www.greensports.co.tz/2024/05/17/rooney-ataka-man-united-isukwe-upya/ https://www.greensports.co.tz/2024/05/17/rooney-ataka-man-united-isukwe-upya/#respond Fri, 17 May 2024 07:37:34 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=10997 Manchester, EnglandMshambuliaji mkongwe Man United, Wayne Rooney amesema timu hiyo inahitaji mabadiliko makubwa katika usajili ambapo ameshauri timu mpya iundwe kupitia nahodha Bruno Fernandes.Man United ipo nafasi ya nane kwenye Ligi Kuu England (EPL) na Mei 25 itaikabili Man City katika fainali ya Kombe la FA, mechi ambayo inatakiwa ishinde ili kujihakikishia nafasi ya kucheza […]

The post Rooney ataka Man United isukwe upya first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Manchester, England
Mshambuliaji mkongwe Man United, Wayne Rooney amesema timu hiyo inahitaji mabadiliko makubwa katika usajili ambapo ameshauri timu mpya iundwe kupitia nahodha Bruno Fernandes.
Man United ipo nafasi ya nane kwenye Ligi Kuu England (EPL) na Mei 25 itaikabili Man City katika fainali ya Kombe la FA, mechi ambayo inatakiwa ishinde ili kujihakikishia nafasi ya kucheza michuano ya klabu Ulaya.
Fernandes amekuwa mchezaji pekee ambaye ameonesha kiwango kilichovutia wengi na hadi sasa ndiye anayeongoza kwa mabao timu hiyo akiwa amezifumania nyavu mara 10 na kutoa asisti saba na kuwazidi wenzake wote.
“Unalazimika kuijenga timu kupitia Bruno, ni mchezaji pekee wa kiwango, ana tabia ya upambanaji, nafikiri inatakiwa kuwaacha wachezaji wachanga pamoja na Bruno, nafikiri kunatakiwa kufanywa mabadiliko makubwa, iwe hivyo,” alisema Rooney.
Rooney mmoja wafungaji bora waliowahi kuichezea Man United hata hivyo alitahadharisha kwamba jambo hilo si la kufanywa kwa mwaka mmoja badala yake linahitaji miaka kadhaa.

“Kushindana katika ligi hii unahitaji wachezaji walio bora na msininukuu vibaya, wachezaji hawa ni wazuri na ni wachezaji wa ligi kuu lakini ili kushindana na Manchester City, Liverpool, Arsenal unahitaji wachezaji walio bora,” alisema Rooney.


Akimzungumzia Marcus Rashford, Rooney alisema, “Sote tunamfahamu Marcus ana sifa za kucheza katika ligi ya juu, najaribu kufikiria kwamba huenda huu ni wakati wake wa kwenda kucheza soka sehemu nyingine, japo sina uhakika na hilo.”
Rooney alisema kwamba Rashford anatakiwa kulitafakari jambo hilo, kujiuliza maswali na hatimaye arudi katika uchezaji ambao wote tunajua anaweza kuwa.

The post Rooney ataka Man United isukwe upya first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/05/17/rooney-ataka-man-united-isukwe-upya/feed/ 0
Rooney akataa ofa Saudi Arabia https://www.greensports.co.tz/2023/10/14/rooney-akataa-ofa-saudi-arabia/ https://www.greensports.co.tz/2023/10/14/rooney-akataa-ofa-saudi-arabia/#respond Sat, 14 Oct 2023 13:24:29 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=8090 London, EnglandKocha Birmingham Wayne Rooney alikataa ofa ya kwenda kufanya kazi Saudi Arabia kwenye ligi kuu ya nchini humo ‘Saudi Pro Ligi’ na kuchagua kurudi England kuinoa timu hiyo inayoshiriki ligi ya Championship.Rooney, mshambuliaji wa zamani wa klabu za Man United, Everton na timu ya taifa ya England, hivi karibuni aliachana na timu ya D.C […]

The post Rooney akataa ofa Saudi Arabia first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

London, England
Kocha Birmingham Wayne Rooney alikataa ofa ya kwenda kufanya kazi Saudi Arabia kwenye ligi kuu ya nchini humo ‘Saudi Pro Ligi’ na kuchagua kurudi England kuinoa timu hiyo inayoshiriki ligi ya Championship.
Rooney, mshambuliaji wa zamani wa klabu za Man United, Everton na timu ya taifa ya England, hivi karibuni aliachana na timu ya D.C United ya Marekani na Jumatano iliyopita alitangazwa rasmi kuwa kocha mpya wa Birmingham.
Ofisa Mtendaji Mkuu (CEO) wa Birmingham, Garry Cook alisema kwamba alijaribu kumshawishi Rooney aende Saudi Arabia wakati yeye akiwa CEO wa Saudi Pro Ligi lakini jambo hilo halikufanikiwa.
Kama Rooney angekubali kwenda kufundisha timu Saudi Arabia, angekuwa anaungana na mchezaji mwenzake wa zamani wa timu ya England, Steven Gerrard ambaye kwa sasa anainoa timu ya Al-Ettifaq ya Saudi Arabia.
Rooney alisema kwamba uamuzi wake wa kukataa kwenda Saudi Arabia haumaanishi kuwakosea heshima makocha waliochagua kwenda huko badala yake alisema uamuzi huo ni wake binafsi ambao umezingatia mendeleo yake na njia tofauti aliyoichagua.

“Nilijifikiria mimi na kuamua kurudi katika soka la England ni jambo zuri, ni jambo ambalo nimekuwa nikitaka kulifanya, katika wiki nne au sita zilizopita nilikuwa na ofa katika klabu nyingine lakini tangu nizungumze na Birmingham, uamuzi ulikuwa rahisi,” alisema Rooney.


Birmingham kwa sasa inashika nafasi ya sita kwenda Championship na mechi ya kwanza ya Rooney akiwa na timu hiyo itakuwa Oktoba 21 dhidi ya Middlesbrough.

The post Rooney akataa ofa Saudi Arabia first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/10/14/rooney-akataa-ofa-saudi-arabia/feed/ 0
Rooney ataka Birmingham irudi EPL https://www.greensports.co.tz/2023/10/13/rooney-ataka-birmingham-irudi-epl/ https://www.greensports.co.tz/2023/10/13/rooney-ataka-birmingham-irudi-epl/#respond Fri, 13 Oct 2023 06:08:19 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=8077 London, EnglandKocha mpya wa timu ya Birmingham, Wayne Rooney amesema kwamba anaamini timu hiyo inatakiwa kuwa kwenye Ligi Kuu England (EPL) na lengo lake ni kufanikisha jambo hilo.Rooney, 37, aliyekuwa kocha wa timu ya D.C United ya Marekani, ametangazwa rasmi juzi Jumatano kuinoa timu hiyo inayoshiriki ligi ya Championship kwa mkataba wa miaka mitatu na […]

The post Rooney ataka Birmingham irudi EPL first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

London, England
Kocha mpya wa timu ya Birmingham, Wayne Rooney amesema kwamba anaamini timu hiyo inatakiwa kuwa kwenye Ligi Kuu England (EPL) na lengo lake ni kufanikisha jambo hilo.
Rooney, 37, aliyekuwa kocha wa timu ya D.C United ya Marekani, ametangazwa rasmi juzi Jumatano kuinoa timu hiyo inayoshiriki ligi ya Championship kwa mkataba wa miaka mitatu na nusu.

“Nataka kuijenga Birmingham, haipo mahali ambapo ilikuwa kwa miaka 10 iliyopita na sasa hii ni changamoto na fursa ya kuirudisha huko,” alisema Rooney nahodha na mshambuliaji wa zamani wa timu ya taifa England.


Uamuzi wa kumpa Rooney majukumu ya kuinoa Birmingham umechukuliwa na wamiliki wapya wa klabu hiyo, Shelby Companies Limited (SCL) wa nchini Marekani ambao waliamua kuachana na kocha John Eustace aliyeinoa timu hiyo kwa takriban miezi 15.
Birmingham kwa sasa inashika nafasi ya sita kwenye ligi ya Championship ambapo mtihani wa kwanza wa Rooney na timu hiyo utakuwa Oktoba 21 katika mechi dhidi ya Middlesbrough, timu inayonolewa na mchezaji mwenzake wa zamani wa Man United, Michael Carrick.
Rooney ambaye pia amewahi kuichezea Everton, tayari amefanya kikao na wachezaji wa timu hiyo na kuelezea ubora wa wachezaji vijana waliopo, wachezaji ambao amesema anaweza kuwaendeleza kwani hilo jambo ambalo amekuwa akijaribu kulifanya wakati wote tangu awe kocha.

The post Rooney ataka Birmingham irudi EPL first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/10/13/rooney-ataka-birmingham-irudi-epl/feed/ 0
Rooney kuinoa Birmingham https://www.greensports.co.tz/2023/10/10/rooney-kuinoa-birmingham/ https://www.greensports.co.tz/2023/10/10/rooney-kuinoa-birmingham/#respond Tue, 10 Oct 2023 19:30:48 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=8045 London, EnglandMshambuliaji wa zamani wa England, Wayne Rooney anadaiwa kukubali kibarua cha kuinoa timu ya Birmingham City ikiwa ni siku chache baada ya kuachana na D.C United ya Marekani.Rooney ambaye kabla ya kuugeukia ukocha, aliwahi pia kuzichezea timu za Everton na Man United, alifikia makubaliano ya kuachana na DC United baada ya mambo kutokuwa mazuri […]

The post Rooney kuinoa Birmingham first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

London, England
Mshambuliaji wa zamani wa England, Wayne Rooney anadaiwa kukubali kibarua cha kuinoa timu ya Birmingham City ikiwa ni siku chache baada ya kuachana na D.C United ya Marekani.
Rooney ambaye kabla ya kuugeukia ukocha, aliwahi pia kuzichezea timu za Everton na Man United, alifikia makubaliano ya kuachana na DC United baada ya mambo kutokuwa mazuri katika klabu hiyo.
Taarifa za chanzo kimoja cha habari zilidai kuwa Rooney akiwa Birmingham atakuwa akilipwa mara tatu kumzidi kocha aliyetimuliwa, John Eustace.
Birmingham, timu iliyowahi kutamba kwenye Ligi Kuu England (EPL) kwa sasa inashiriki ligi ya Championship ikiwa na mkakati wa kuhakikisha inarudi EPL.
Rooney mara baada ya kuachana na DC United alinukuliwa akisema kwamba anadhani umefika wakati sahihi kwake kurudi England ingawa alidai kwamba hakuwa mwenye kuyajui mambo yake baadaye.

The post Rooney kuinoa Birmingham first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/10/10/rooney-kuinoa-birmingham/feed/ 0
Muacheni Ronaldo aondoke- Rooney https://www.greensports.co.tz/2022/08/08/muacheni-ronaldo-aondoke-rooney/ https://www.greensports.co.tz/2022/08/08/muacheni-ronaldo-aondoke-rooney/#respond Mon, 08 Aug 2022 13:41:04 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=2276 New York, MarekaniMshambuliaji wa zamani wa Man Utd, Wayne Rooney amejitosa katika sakata la usajili wa Cristiano Ronaldo akiitaka timu hiyo kuachana na mchezaji huyo kama inataka kujenga timu yenye mafanikio.Ronaldo mwenye umri wa miaka 37 alisajiliwa Man Utd msimu uliopita akitokea Juventus lakini sasa anataka kuondoka kwa kinachodaiwa kuwa ni kukosa nafasi kwenye Ligi […]

The post Muacheni Ronaldo aondoke- Rooney first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

New York, Marekani
Mshambuliaji wa zamani wa Man Utd, Wayne Rooney amejitosa katika sakata la usajili wa Cristiano Ronaldo akiitaka timu hiyo kuachana na mchezaji huyo kama inataka kujenga timu yenye mafanikio.
Ronaldo mwenye umri wa miaka 37 alisajiliwa Man Utd msimu uliopita akitokea Juventus lakini sasa anataka kuondoka kwa kinachodaiwa kuwa ni kukosa nafasi kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya ingawa kocha mpya wa timu hiyo, Erik ten Hag bado anamtaka mchezaji huyo ambaye ana mwaka mmoja katika mkataba wake.
“Nafikiri United inatakiwa kumuacha Cristiano Ronaldo aondoke, si kwamba Ronaldo hawezi kucheza katika timu ya Ten Hag, hapana, anaweza kucheza kwenye timu yoyote,” alisema Rooney ambaye kwa sasa ni kocha wa timu ya DC United inayoshiriki Major League Soccer nchini Marekani.
“Ronny wakati wote anaweza kufunga magoli, lakini kwa mtazamo wangu ni kwamba United haiko tayari kwa changamoto ya kupigania taji kwa sasa, hivyo lengo ni lazima liwe kuijenga timu ya kupigania taji la ligi kwa miaka mitatu au minne ijayo na kwa jambo hilo ni lazima kuwe na mipango.”
Man Utd ilianza mtihani wake wa kwanza wa Ligi Kuu England msimu wa 2022/23 jana Jumapili kwa kuumana na Brighton, mechi ambayo Ronaldo alisugua benchi akiishuhudia timu hiyo ikilala kwa mabao 2-1 kwenye dimba la Old Trafford.
Rooney hata hivyo alisema kwamba ana matumaini, Ten Hag ataweza kutengeneza mfumo wa uchezaji ulio wazi katika timu hiyo, “Sijaweza kujua nini wanakifanya kuhusu mpango wao kiuchezaji au kuijua aina yao ya uchezaji ila nafikiri moja ya mambo makubwa mtayaona kutoka kwa Ten Hag, anajitahidi kuweka alama yake katika mfumo wa uchezaji.”

The post Muacheni Ronaldo aondoke- Rooney first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2022/08/08/muacheni-ronaldo-aondoke-rooney/feed/ 0