Ronaldo - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Mon, 09 Mar 2026 20:09:30 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=6.9.4 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg Ronaldo - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 Ronaldo amfuata daktari Madrid https://www.greensports.co.tz/2026/03/08/ronaldo-amfuata-daktari-madrid/ https://www.greensports.co.tz/2026/03/08/ronaldo-amfuata-daktari-madrid/#respond Sun, 08 Mar 2026 09:02:00 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=14405 Riyadh, Saudi ArabuaNahodha wa timu ya taifa ya Ureno, Cristiano Ronaldo amelazimika kwenda Madrid, Hispania kwa ajili ya matibabu ya misuli baada ya hali kuwa mbaya tofauti na ilivyodhaniwa awali.Ronaldo, 41, ambaye kwa sasa anaichezea klabu ya Al Nassr ya Saudi Arabia akiwa ameifungia mabao 21 katika mechi 22 za msimu huu, alilazimika kufanyiwa mabadiliko […]

The post Ronaldo amfuata daktari Madrid first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Riyadh, Saudi Arabua
Nahodha wa timu ya taifa ya Ureno, Cristiano Ronaldo amelazimika kwenda Madrid, Hispania kwa ajili ya matibabu ya misuli baada ya hali kuwa mbaya tofauti na ilivyodhaniwa awali.
Ronaldo, 41, ambaye kwa sasa anaichezea klabu ya Al Nassr ya Saudi Arabia akiwa ameifungia mabao 21 katika mechi 22 za msimu huu, alilazimika kufanyiwa mabadiliko katika mechi ya Jumamosi Machi, 6, 2026 dhidi ya Al Fahya, mechi ambayo Al Nassr ilipata ushindi wa mabao 3-1.
Akizungumzia tukio hilo, kocha wa Al Nassr, Jorge Jesus alisema kwamba Ronaldo anakwenda Madrid ambapo atapatiwa matibabu na mtaalam wake binafsi wa viungo na baada ya hapo atapata muda wa kupumzika.
Haijaweza kufahamika haraka kama mchezaji huyo mwenye rekodi ya kushinda tuzo za Ballon d’Or mara tano atapona haraka na kuiwakilisha Ureno katika mechi za kirafiki dhidi ya Mexico hapo Machi 29 mwaka huu na nyingine dhidi ya Marekani itakayochezwa Aprili Mosi.

“Katika mechi yake ya mwisho Cristiano alitoka uwanjani akiwa na matatizo ya misuli, baada ya kufanyiwa vipimo ilionekana wazi kuwa tatizo lilikuwa kubwa kuliko tulivyodhani, anahitaji muda apone na arudi haraka kuisaidia timu,” alisema Jorge.


Ronaldo ambaye hadi sasa ana rekodi ya kufunga mabao 965 katika maisha yake ya soka la ushindani, amewahi kusema kwamba hatarajii kustaafu soka hadi atakapofunga mabao 1,000.
Katika siku za karibuni mchezaji huyo alikuwa katika mgomo baridi na kukosa mechi kadhaa sababu ikidaiwa kuwa ni kutokubaliana na masuala kadhaa ya uwekezaji katika klabu ya Al Nassr ingawa baadaye alisitisha mgomo huo.
Ronaldo alijiunga na Al Nassr Desemba 2022 baada ya mkataba wake na Manchester United kufutwa, kwa sasa ndiye mchezaji anayelipwa fedha nyingi zaidi duniani, mshahara wake unafikia Pauni 177 milioni na Juni mwaka jana alisaini mkataba mwingine wa miaka miwili.

The post Ronaldo amfuata daktari Madrid first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2026/03/08/ronaldo-amfuata-daktari-madrid/feed/ 0
Ronaldo kumiliki klabu ya soka https://www.greensports.co.tz/2023/06/08/ronaldo-kumiliki-klabu-ya-soka/ https://www.greensports.co.tz/2023/06/08/ronaldo-kumiliki-klabu-ya-soka/#respond Thu, 08 Jun 2023 16:47:45 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=6524 Madrid, HispaniaWinga Cristiano Ronaldo amesema kwamba baada ya kustaafu soka ataufanyia kazi mpango wa kumiliki klabu ya soka.Ronaldo kwa sasa ana mkataba na klabu ya Al-Nassr ya Saudi Arabia ambao unafikia ukomo Juni 2025 lakini kwa sasa ameanza kupanga mambo yake ya baadaye nje ya soka la ushindani.“Siwezi kujitoa katika wazo la kuwa mmiliki wa […]

The post Ronaldo kumiliki klabu ya soka first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Madrid, Hispania
Winga Cristiano Ronaldo amesema kwamba baada ya kustaafu soka ataufanyia kazi mpango wa kumiliki klabu ya soka.
Ronaldo kwa sasa ana mkataba na klabu ya Al-Nassr ya Saudi Arabia ambao unafikia ukomo Juni 2025 lakini kwa sasa ameanza kupanga mambo yake ya baadaye nje ya soka la ushindani.
“Siwezi kujitoa katika wazo la kuwa mmiliki wa klabu,” alisema Ronaldo mbele ya waandishi wa habari jijini Madrid katika mkutano wa uzinduzi wa biashara yake mpya ya maji ya chupa.
“Ni jambo ambalo nililifikiria miaka michache iliyopita, ningependa niwe mmiliki wa klabu, naelekea mwisho wa maisha yangu ya soka katika miaka miwili au mitatu ijayo,” alisema.
Ronaldo, 38, ambaye alijiunga na Al Nassr Januari mwaka huu baada ya kuachana na Man United, pia alielezea kufurahishwa kwake na uamuzi wa nyota mwenzake wa zamani wa Real Madrid, Karim Benzema kuhamia Saudi Arabia.
Benzema, 35, alikataa kuongeza mkataba wa mwaka mmoja Real Madrid na badala yake akaamua kujiunga na klabu ya Al Ittihad ya Saudi Arabia.

“Nilijua baada ya mimi kwenda Saudi Arabia nitakuwa nimefungua njia, Karim (Benzema) amekwenda na nina hakika wengine wengi watafuata, miaka miwili au mitatu Ligi ya Saudi itakuwa moja ya ligi muhimu duniani, ningependa wachezaji mastaa waje Saudi Arabia hakuna tatizo kwenye ligi, tunachotaka ni ushindani,” alisema Ronaldo.


Mchezaji mwingine aliyetarajiwa kwenda Saudi Arabia kujiunga na klabu ya Al-Hilal ni Lionel Messi aliyekuwa PSG ya Ufaransa lakini jana Jumatano ilithibitishwa kwamba ameamua kwenda nchini Marekani kujiunga na Inter Miami FC inayoshiriki Ligi Kuu ya Soka Mareakni.
Wachezaji wengine mastaa wanaotajwa kuwa na mipango ya kwenda kucheza soka Saudi Arabia ni Sergio Busquets, N’Golo Kante, Jordi Alba, Roberto Firmino, Sergio Ramos, Angel Di Maria na Iago Aspas.

The post Ronaldo kumiliki klabu ya soka first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/06/08/ronaldo-kumiliki-klabu-ya-soka/feed/ 0
Ronaldo ampiku Messi kwa kipato https://www.greensports.co.tz/2023/05/03/ronaldo-ampiku-messi-kwa-kipato/ https://www.greensports.co.tz/2023/05/03/ronaldo-ampiku-messi-kwa-kipato/#respond Wed, 03 May 2023 18:39:48 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=6001 New York, MarekaniCristiano Ronaldo ndiye mwanamichezo anayelipwa fedha nyingi zaidi duniani kwa sasa akiwabwaga wanasoka wenzake, Lionel Messi na Kylian Mbappe wa PSG.Kwa mujibu wa taarifa za mwaka 2023 za jarida maarufu duniani la mambo ya uchumi la Forbes, Ronaldo ameshika namba moja tangu ajiunge na klabu ya Al Nassr ya Saudi Arabia na mshahara […]

The post Ronaldo ampiku Messi kwa kipato first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

New York, Marekani
Cristiano Ronaldo ndiye mwanamichezo anayelipwa fedha nyingi zaidi duniani kwa sasa akiwabwaga wanasoka wenzake, Lionel Messi na Kylian Mbappe wa PSG.
Kwa mujibu wa taarifa za mwaka 2023 za jarida maarufu duniani la mambo ya uchumi la Forbes, Ronaldo ameshika namba moja tangu ajiunge na klabu ya Al Nassr ya Saudi Arabia na mshahara wake kuongezea karibu mara mbili ya aliokuwa akiupata awali.
Ronaldo alichukua uamuzi wa kuihama Man United mwaka jana na kujiunga na klabu hiyo ya Saudi Arabia huku akiwashutumu wamiliki wa klabu yake ya zamani, baadhi ya wachezaji na kocha wake.
Kwa sasa mchezaji huyo ana mkataba na klabu ya Al Nassr ambao unafikia ukomo mwaka 2025 na kwa mujibu wa Forbes pato lake lilifikia dola 136 milioni huku mshahara wake wa mwaka ukidaiwa kuongezeka na unakadiriwa kufikia dola 75 milioni.
Baadhi ya vyombo vya habari vilidai kwamba mkataba wake na klabu hiyo ya Saudi Arabia una thamani ya Dola 219.98 milioni.
Kwa mujibu wa Forbes, Messi anashika nafasi ya pili akiwa na pato linalofikia Dola 130 milioni wakati nafasi ya tatu inashikiliwa na Mbappe ambaye pato lake linafikia Dola 120 milioni.
Nafasi ya nne inashikiliwa na nyota wa mpira wa kikapu, LeBron James ambaye pato lake linafikia Dola 119.5 milioni huku bondia wa Mexico, Canelo Alvarez akifunga idadi ya tano bora kwa pato linalofikia Dola 110 milioni.
Orodha kamili ya wanamichezo 10 wanaolipwa fedha nyingi zaidi duniani ni kiasi cha fedha wanachopata ni kama ifuatavyo…

  1. Cristiano Ronaldo (Dola 136 milioni)
  2. Lionel Messi (Dola 130 milioni)
  3. Kylian Mbappe (Dola 120 milioni)
  4. Lebron James (Dola 119.5 milioni)
  5. Canelo Alvarez (Dola 110 milioni)
  6. Dustin Johnson (Dola 107 milioni)
  7. Phil Mickelson (Dola 106 milioni)
  8. Stephan Curry (Dola 100.4 milioni)
  9. Roger Federer (Dola 95.1 milioni)
  10. Kevin Durant (Dola 89.1 milioni)

The post Ronaldo ampiku Messi kwa kipato first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/05/03/ronaldo-ampiku-messi-kwa-kipato/feed/ 0
Ronaldo aweka rekodi ya mabao 500 https://www.greensports.co.tz/2023/02/10/ronaldo-aweka-rekodi-ya-mabao-500/ https://www.greensports.co.tz/2023/02/10/ronaldo-aweka-rekodi-ya-mabao-500/#respond Fri, 10 Feb 2023 07:46:01 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=5080 Saudi ArabiaCristiano Ronaldo jana Alhamisi aliifungia Al Nassr mabao manne katika mechi ya ligi dhidi ya Al Wehda, hapo hapo akaweka rekodi ya kufunga mabao 500 katika klabu mbalimbali alizochezea hadi sasa.Winga huyo wa zamani wa Man United na Real Madrid, alifunga mabao hayo pekee kwenye mchezo huo uliopigwa kwenye Uwanja wa King Abdulaziz na […]

The post Ronaldo aweka rekodi ya mabao 500 first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Saudi Arabia
Cristiano Ronaldo jana Alhamisi aliifungia Al Nassr mabao manne katika mechi ya ligi dhidi ya Al Wehda, hapo hapo akaweka rekodi ya kufunga mabao 500 katika klabu mbalimbali alizochezea hadi sasa.
Winga huyo wa zamani wa Man United na Real Madrid, alifunga mabao hayo pekee kwenye mchezo huo uliopigwa kwenye Uwanja wa King Abdulaziz na Al Nassr kutoka na ushindi wa mabao 4-0.
Ronaldo ambaye ana miaka 38 sasa, alifunga bao la kwanza dakika ya 21 na kuwa bao lake la 500 katika klabu mbalimbali kabla ya kuongeza mengine matatu likiwamo moja la penalti na hivyo kufikisha jumla ya mabao 503.
Desemba mwaka jana Ronaldo alivunja mkataba na Man United na kusaini mkataba na Al Nassr ya Saudi Arabia, mkataba utakaofikia ukomo mwaka 2025 huku ikidaiwa kuwa kwa mwaka analipwa Dola 75 milioni.
Baada ya kucheza mechi mbili za Al Nassr bila bao, hatimaye alifunga bao moja na sasa ameongeza mabao mengine manne na hivyo kufikisha idadi ya mabao matano tangu ajiunge na timu hiyo.
Kwa ushindi huo, Al Nassr sasa inashika usukani wa ligi hiyo kubwa nchini Saudi Arabia ikiwa imecheza mechi 16 na ina pointi 37 sawa na Al Shabab zikitofautiana kwa mabao ya kufunga na kufungwa huku Al Shabab ikicheza mechi 17 wakati Al Nassr imecheza mechi 16.

The post Ronaldo aweka rekodi ya mabao 500 first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/02/10/ronaldo-aweka-rekodi-ya-mabao-500/feed/ 0
Polisi wamuonya Ronaldo https://www.greensports.co.tz/2022/08/18/polisi-wamuonya-ronaldo/ https://www.greensports.co.tz/2022/08/18/polisi-wamuonya-ronaldo/#respond Thu, 18 Aug 2022 20:48:55 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=2461 Manchester, EnglandPolisi wa Manchester wamemuonya mshambuliaji wa Manchester United, Cristiano Ronaldo baada ya kudaiwa kuvunja simu ya shabiki wa soka siku ambayo timu yake ilishindwa kutamba mbele ya Everton katika mechi iliyopigwa Aprili mwaka huu.Baada ya Man Utd kulala kwa bao 1-0 kwenye dimba la Goodison Park katika mechi ya msimu uliopita, picha za vyanzo […]

The post Polisi wamuonya Ronaldo first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Manchester, England
Polisi wa Manchester wamemuonya mshambuliaji wa Manchester United, Cristiano Ronaldo baada ya kudaiwa kuvunja simu ya shabiki wa soka siku ambayo timu yake ilishindwa kutamba mbele ya Everton katika mechi iliyopigwa Aprili mwaka huu.
Baada ya Man Utd kulala kwa bao 1-0 kwenye dimba la Goodison Park katika mechi ya msimu uliopita, picha za vyanzo mbalimbali vya habari zilimuonyesha Ronaldo akiiangusha chini simu ya shabiki wakati akitoka uwanjani kuelekea kwenye vyumba vya kubadilishia nguo.
Ronaldo hata hivyo baadaye aliomba radhi kwa tukio hilo na polisi wametoa taarifa yao Jumatano hii kuhusu kilichojiri katika tukio hilo.
“Tunaweza kuthibitisha kwamba mtu mwenye umri wa miaka 37 kwa hiari yake alifika na kuhojiwa akihusishwa na tukio kushambulia na uharibifu,” ilieleza taarifa hiyo.
“Tuhuma hizo zinahusisha tukio lililojitokeza katika mechi kati ya Everton na Manchester United kwenye Uwanja wa Goodison Park, siku ya Jumamosi, Aprili 9, suala hilo limeshughulikiwa katika mazingira ya tahadhari na kufikia hitimisho.”

The post Polisi wamuonya Ronaldo first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2022/08/18/polisi-wamuonya-ronaldo/feed/ 0
Muacheni Ronaldo aondoke- Rooney https://www.greensports.co.tz/2022/08/08/muacheni-ronaldo-aondoke-rooney/ https://www.greensports.co.tz/2022/08/08/muacheni-ronaldo-aondoke-rooney/#respond Mon, 08 Aug 2022 13:41:04 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=2276 New York, MarekaniMshambuliaji wa zamani wa Man Utd, Wayne Rooney amejitosa katika sakata la usajili wa Cristiano Ronaldo akiitaka timu hiyo kuachana na mchezaji huyo kama inataka kujenga timu yenye mafanikio.Ronaldo mwenye umri wa miaka 37 alisajiliwa Man Utd msimu uliopita akitokea Juventus lakini sasa anataka kuondoka kwa kinachodaiwa kuwa ni kukosa nafasi kwenye Ligi […]

The post Muacheni Ronaldo aondoke- Rooney first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

New York, Marekani
Mshambuliaji wa zamani wa Man Utd, Wayne Rooney amejitosa katika sakata la usajili wa Cristiano Ronaldo akiitaka timu hiyo kuachana na mchezaji huyo kama inataka kujenga timu yenye mafanikio.
Ronaldo mwenye umri wa miaka 37 alisajiliwa Man Utd msimu uliopita akitokea Juventus lakini sasa anataka kuondoka kwa kinachodaiwa kuwa ni kukosa nafasi kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya ingawa kocha mpya wa timu hiyo, Erik ten Hag bado anamtaka mchezaji huyo ambaye ana mwaka mmoja katika mkataba wake.
“Nafikiri United inatakiwa kumuacha Cristiano Ronaldo aondoke, si kwamba Ronaldo hawezi kucheza katika timu ya Ten Hag, hapana, anaweza kucheza kwenye timu yoyote,” alisema Rooney ambaye kwa sasa ni kocha wa timu ya DC United inayoshiriki Major League Soccer nchini Marekani.
“Ronny wakati wote anaweza kufunga magoli, lakini kwa mtazamo wangu ni kwamba United haiko tayari kwa changamoto ya kupigania taji kwa sasa, hivyo lengo ni lazima liwe kuijenga timu ya kupigania taji la ligi kwa miaka mitatu au minne ijayo na kwa jambo hilo ni lazima kuwe na mipango.”
Man Utd ilianza mtihani wake wa kwanza wa Ligi Kuu England msimu wa 2022/23 jana Jumapili kwa kuumana na Brighton, mechi ambayo Ronaldo alisugua benchi akiishuhudia timu hiyo ikilala kwa mabao 2-1 kwenye dimba la Old Trafford.
Rooney hata hivyo alisema kwamba ana matumaini, Ten Hag ataweza kutengeneza mfumo wa uchezaji ulio wazi katika timu hiyo, “Sijaweza kujua nini wanakifanya kuhusu mpango wao kiuchezaji au kuijua aina yao ya uchezaji ila nafikiri moja ya mambo makubwa mtayaona kutoka kwa Ten Hag, anajitahidi kuweka alama yake katika mfumo wa uchezaji.”

The post Muacheni Ronaldo aondoke- Rooney first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2022/08/08/muacheni-ronaldo-aondoke-rooney/feed/ 0
Ten Hag: Msimsakame Ronaldo https://www.greensports.co.tz/2022/08/06/ten-hag-acheni-kumsakama-ronaldo/ https://www.greensports.co.tz/2022/08/06/ten-hag-acheni-kumsakama-ronaldo/#respond Sat, 06 Aug 2022 07:26:12 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=2249 Manchester, EnglandKatika hali ambayo haikutarajiwa, kocha Erik ten Hag amesema si sahihi kumsakama Cristiano Ronaldo peke yake kwa kutoka nje kabla ya mechi ya Man United na Rayo Vallecano wakati kuna wachezaji wengine waliofanya hivyo.Ronaldo katika mechi hiyo alicheza kwa dakika 45 za kwanza na kutolewa lakini akatoka uwanjani dakika 10 kabla ya mechi kumalizika […]

The post Ten Hag: Msimsakame Ronaldo first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Manchester, England
Katika hali ambayo haikutarajiwa, kocha Erik ten Hag amesema si sahihi kumsakama Cristiano Ronaldo peke yake kwa kutoka nje kabla ya mechi ya Man United na Rayo Vallecano wakati kuna wachezaji wengine waliofanya hivyo.
Ronaldo katika mechi hiyo alicheza kwa dakika 45 za kwanza na kutolewa lakini akatoka uwanjani dakika 10 kabla ya mechi kumalizika na ingawa wako wachezaji wengine waliotoka, Ronaldo amejikuta akisakamwa zaidi yeye kwenye vyombo vya habari na kukawa na taarifa kwamba Ten Hag hatompanga katika mechi ya kwanza ya Man Utd ya Ligi Kuu England hapo kesho dhidi ya Brighton.
Akifafanua kuhusu kusakamwa kwa mchezaji huyo, Ten Hag alisema si sahihi kumuangalia Ronaldo peke yake na kuwaacha wachezaji wengine waliotoka uwanjani mapema katika mechi hiyo ya kirafiki iliyopigwa kwenye dimba la Old Trafford na kumalizika kwa sare ya bao 1-1.
“Na sasa ninachotaka kusema ni kwamba waliotoka uwanjani kabla ya mechi walikuwa wachezaji wengi lakini anayeangaliwa ni Cristiano, hiyo si sahihi, kwa hiyo mkafanye utafiti na mtaona ni wachezaji wengi waliotoka,” alisema Ten Hag jana jioni.
“Watajeni, wasahihisheni na baada ya hapo endeleeni na mengine, nafikiri nimesema ya kutosha kuhusu hilo, si sahihi,” alisisitiza Ten Hag.
Ronaldo ambaye hakuwamo katika ziara ya maandalizi ya msimu wa 2022/23 katika nchi za Thailand na Australia na kukosa mechi kadhaa za kirafiki, amecheza mechi moja tu kwa dakika 45 huku ikidaiwa kwamba hayuko fiti lakini huenda akapangwa katika mechi ya kesho baada ya Anthony Martial kuumia.
Akizungumzia maandalizi ya timu yake kwa ujumla kwa ajili ya mechi ya kesho, Ten Hag alisema, “Nimeridhishwa na timu yote, tunafanya vizuri, hali ni nzuri na Cristiano anafanya bidii sana, nina furaha kuwa naye, nilishasema kabla tuna mshambuliaji wa kiwango cha juu, hakika nina furaha yuko hapa katika kikosi, na tunasimamia mipango yetu.”
Habari za ndani zinadai kuwa Man Utd bado inahaha kusajili kiungo na mshambuliaji kabla ya siku ya mwisho ya usajili ambayo ni Septemba mosi, hawajakata tamaa kwa Frankie de Jong, kiungo wa Barcelona ambaye pia anatakiwa na Chelsea ingawa Ten Hag hakutaka kumzungumzia mchezaji huyo kwa madai kwamba hayuko tayari kuzungumzia mchezaji mwenye mkataba na timu nyingine.

The post Ten Hag: Msimsakame Ronaldo first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2022/08/06/ten-hag-acheni-kumsakama-ronaldo/feed/ 0
Ten Hag kumpanga Ronaldo Jpili? https://www.greensports.co.tz/2022/08/05/ten-hag-kumpanga-ronaldo-jpili/ https://www.greensports.co.tz/2022/08/05/ten-hag-kumpanga-ronaldo-jpili/#respond Fri, 05 Aug 2022 20:46:41 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=2242 London, EnglandHabari ya Cristiano Ronaldo kutocheza mechi ya kwanza ya Ligi Kuu England huenda ikabadilika baada ya kuumia kwa Anthony Martial na hivyo kumfanya kocha Erik ten Hag kubadili msimamo na kumpa nafasi mchezaji huyo.Man United itaanza mechi yake ya kwanza ya Ligi Kuu England Jumapili hii dhidi ya Brighton, mechi ambayo tayari ilishaelezwa kwamba […]

The post Ten Hag kumpanga Ronaldo Jpili? first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

London, England
Habari ya Cristiano Ronaldo kutocheza mechi ya kwanza ya Ligi Kuu England huenda ikabadilika baada ya kuumia kwa Anthony Martial na hivyo kumfanya kocha Erik ten Hag kubadili msimamo na kumpa nafasi mchezaji huyo.
Man United itaanza mechi yake ya kwanza ya Ligi Kuu England Jumapili hii dhidi ya Brighton, mechi ambayo tayari ilishaelezwa kwamba Ten Hag alishaamua kutompa nafasi Ronaldo ambaye tangu kumalizika msimu wa 2021/22 hakuonekana katika timu hiyo kwa kilichodaiwa kuwa ni matatizo ya kifamilia ingawa inadhaniwa kuwa ni mgomo baridi wa kushinikiza kuondoka.
Man United imefanya ziara ya takriban wiki mbili katika nchi za Thailand na Australia na kucheza mechi kadhaa za kirafiki ambazo Ronaldo hakushiriki kabla ya kujitokeza Jumapili iliyopita katika mechi nyingine ya kirafiki na Rayo Vallecano iliyoisha kwa sare ya bao 1-1, mechi ambayo alicheza dakika 45 za mwanzo kabla ya kutolewa lakini akaondoka uwanjani zikiwa zimebakia dakika 10 mpira kumalizika.
Matukio yote hayo hayajamfurahisha Ten Hag ambaye inadaiwa ameamua kutompa nafasi katika mechi na Brighton japo amedai kwamba mchezaji huyo hayuko fiti lakini kuumia kwa Martial kunamfanya Ten Hag afikirie upya ama kumpa nafasi Ronaldo au kuja na mpango mwingine.
Msimu uliopita haukuwa mzuri kwa Martial na ilionekana kama maisha yake ya soka Man Utd yalikuwa yakielekea ukingoni lakini ameonyesha kuja na ari mpya katika mechi za kirafiki za hivi karibuni ingawa wako wanaodhani kuwa kukosekana kwa Ronaldo ni sababu mojawapo ya nyota ya Martial kung’ara katika mechi hizo.
Juhudi za Martial zimemfanya Ten Hag kumkubali mchezaji huyo na kuanza kumpigia hesabu kwa ajili ya kuisaidia timu hiyo katika msimu wa 2022/23 hasa akiamini anaweza kucheza vizuri nafasi ya winga na hivyo kumuweka benchi Ronaldo lisingekuwa jambo kubwa.
Martial hata hivyo kwa sasa anasumbuliwa na misuli baada ya kuumia katika mechi dhidi ya Atletico Madrid mjini Oslo, Norway na sasa anatarajia kuwa nje akijiuguza kwa kipindi cha siku tano hadi 10 na hapo ndipo nafasi ya Ronaldo inapoanza kujadiliwa na wachambuzi wakijiuliza kuhusu atakachofanya Ten Hag ili kuwa na mtu mzoefu kikosini hasa katika safu ya ushambuliaji.
Na ingawa Ten Hag ameshasema kwamba Ronaldo hayuko fiti lakini sasa huenda akalazimika kumuingiza katika hesabu zake au kumpa nafasi hiyo Marcus Rashford au kuja na mpango mwingine hapo Jumapili.

The post Ten Hag kumpanga Ronaldo Jpili? first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2022/08/05/ten-hag-kumpanga-ronaldo-jpili/feed/ 0
Ten Hag: Alichofanya Ronaldo hakikubaliki https://www.greensports.co.tz/2022/08/03/ten-hag-alichofanya-ronaldo-hakikubaliki/ https://www.greensports.co.tz/2022/08/03/ten-hag-alichofanya-ronaldo-hakikubaliki/#respond Wed, 03 Aug 2022 11:52:45 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=2106 Manchester, EnglandKocha wa Man Utd, Erik ten Hag amewalaumu baadhi ya wachezaji wake wakiongozwa na Cristiano Ronaldo ambao walitoka uwanjani Jumapili iliyopita kabla ya mechi yao ya kirafiki dhidi ya Rayo Vallecano kumalizika.Man Utd katika mechi hiyo iliyopigwa kwenye dimba la Old Trafford ilitoka sare ya bao 1-1 ambapo Ronaldo alicheza kwa dakika 45 za […]

The post Ten Hag: Alichofanya Ronaldo hakikubaliki first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Manchester, England
Kocha wa Man Utd, Erik ten Hag amewalaumu baadhi ya wachezaji wake wakiongozwa na Cristiano Ronaldo ambao walitoka uwanjani Jumapili iliyopita kabla ya mechi yao ya kirafiki dhidi ya Rayo Vallecano kumalizika.
Man Utd katika mechi hiyo iliyopigwa kwenye dimba la Old Trafford ilitoka sare ya bao 1-1 ambapo Ronaldo alicheza kwa dakika 45 za kwanza na kutolewa lakini zikiwa zimesalia dakika 10 mpira kumalizika alionekana na baadhi ya wachezaji wakitoka nje ya uwanja jambo ambalo Ten Hag amesema kwamba halikubaliki.
Ronaldo amekosa ziara ya maandalizi ya msimu wa 2022/23 katika nchi za Australia na Thailand na kwa mara ya kwanza alionekana katika mechi hiyo ya Jumapili lakini hakuweza kuisaidia timu yake kupata ushindi kabla ya kuondoka akiwaacha wachezaji wenzake wakiumana.
“Sisi ni timu, ni wamoja hiyo maana yake ni kwamba unatakiwa ubaki uwanjani hadi mwisho, kwa yeyote aliyehusika kuondoka mapema hili halikubaliki,” alisema Ten Hag.
Ronaldo ambaye kwa sasa ana umri wa miaka 37 mara kwa mara amekuwa akisisitiza azma yake kutaka kuachana na timu hiyo ambayo aliwahi kuichezea miaka ya nyuma kabla ya kutimkia Real Madrid na Juventus, bado ana mwaka mmoja katika mkataba wake lakini shauku ya kutaka kucheza Ligi ya Mabingwa ndiyo inayomfanya atake kuihama timu hiyo ambayo itacheza Europa Ligi.
Man Utd itauanza msimu mpya wa 2022/23 wa Ligi Kuu England Jumapili hii dhidi ya Brighton huo ukiwa mtihani wa kwanza kwa Ten Hag huku baadhi ya wachambuzi wakisubiri kwa hamu kuona kama Ronaldo atapewa nafasi katika mechi hiyo baada ya kukosekana kwenye maandalizi ya timu hiyo kwa kinachoaminika kuwa ni mgomo wa kushinikiza kuondoka.

The post Ten Hag: Alichofanya Ronaldo hakikubaliki first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2022/08/03/ten-hag-alichofanya-ronaldo-hakikubaliki/feed/ 0
Saha: Ronaldo mbinafsi https://www.greensports.co.tz/2022/08/02/saha-ronaldo-mbinafsi/ https://www.greensports.co.tz/2022/08/02/saha-ronaldo-mbinafsi/#respond Tue, 02 Aug 2022 09:05:39 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=2089 London, EnglandNyota wa zamani wa Man United, Louis Saha ameamua kumtolea uvivu Cristiano Ronaldo kwa kumwita mbinafsi anayejiangalia yeye zaidi.Saha ambaye amewahi kucheza katika klabu ya Man United na Ronaldo na kuna wakati alidaiwa kuvutiwa na mafanikio ya mchezaji huyo hadi kuiga utaratibu wake wa mazoezi, amedai kwamba Ronaldo anazungumzia mambo yasiyo na uhalisia kwa […]

The post Saha: Ronaldo mbinafsi first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

London, England
Nyota wa zamani wa Man United, Louis Saha ameamua kumtolea uvivu Cristiano Ronaldo kwa kumwita mbinafsi anayejiangalia yeye zaidi.
Saha ambaye amewahi kucheza katika klabu ya Man United na Ronaldo na kuna wakati alidaiwa kuvutiwa na mafanikio ya mchezaji huyo hadi kuiga utaratibu wake wa mazoezi, amedai kwamba Ronaldo anazungumzia mambo yasiyo na uhalisia kwa kutaka kwake kuvunja mkataba na klabu hiyo.
Ronaldo mwenye umri wa miaka 37 sasa, ameshaweka wazi nia yake ya kutaka kuondoka katika klabu hiyo lakini kinachoonekana ni kwamba wakala wake Jorge Mendes licha ya kufanya juhudi kumtafutia timu ya hadhi yake, inaonekana kumekuwa na ugumu kuipata timu hiyo hali inayomfanya abaki kuwa mchezaji wa Man United jambo ambalo Ronaldo anaona ugumu kulikubali.
Mazingira hayo ndiyo yaliyomuibua Saha ambaye anamuona mchezaji huyo mwenzake wa zamani kuwa ni mbinafsi ingawa alitahadharisha kwamba hakuna mtu anayeweza kuwa na hitimisho la moja kwa moja kwa mambo anayofanya Ronaldo.
Saha alisema: “Mimi si Cristiano lakini ni mtu ambaye naweza kuwa katika nafasi ya mashabiki wa Manchester United, naona ni kama vile haonyeshi kwamba sasa inatosha kwa kile anachokifanya, anajifikiria yeye mwenyewe.”
“Siwezi kumfanyia tathmini na kuwa na hitimisho la moja kwa moja kwa sababu ni mchezaji muhimu na mimi sipo katika nafasi yake lakini ningependa kuona anabaki Man United kwa sababu ni mchezaji mkubwa, kwa sababu ni mchezaji mzuri na hakuna wa kumfanyia tathmini kwa sababu tu ya kile anachotaka kwenye maisha yake binafsi ya soka,” alisema.
Shauku ya Ronaldo kutaka kuihama Man United kwa kiasi kikubwa inadaiwa kuchangiwa na timu hiyo kukosa nafasi ya kushiriki Ligi ya Mabingwa Ulaya na hivyo anataka Man United ivunje mkataba wake na kumruhusu aondoke akiwa mchezaji huru kwani hataki kucheza Europa Ligi, michuano ambayo hakuwahi kuicheza na pengine anaona si hadhi yake.
Katika hilo Saha anasema Ronaldo anataka mambo yasiyo na uhalisia kwa kudhani kuwa Man United wanaweza kuvunja mkataba wake na kumpa ruhusa ya kuondoka kwa sababu tu msimu uliopita mambo hayakuwa mazuri.
Ronaldo hakushiriki katika ziara ya maandalizi ya msimu wa 2022/23 ya timu hiyo katika nchi za Thailand na Australia kwa kile kilichodaiwa kuwa ni matatizo ya kifamilia lakini habari zisizo rasmi zilidai kuwa alichofanya ni mgomo baridi kushinikiza kuruhusiwa aondoke katika klabu hiyo.
Jumapili iliyopita kwenye dimba la Old Trafford, Ronaldo alifanya kitendo kilichoshangaza wengi katika mechi ya kirafiki dhidi ya Rayo Vallecano ambayo ilikuwa mechi yake ya kwanza kwenye timu hiyo tangu kumalizika kwa msimu wa 2021/22.
Baada ya kucheza kwa dakika 45 za kwanza na kutolewa, Ronaldo baadaye alionekana akitoka nje ya uwanja wakati mechi ikiendelea, maofisa wa Man United walikataa kusema lolote kama aliruhusiwa na kocha Erik ten Hag au aliamua tu kujiondokea huku timu hiyo ikitoka sare ya bao 1-1 huku bao la Man United likifungwa na Amad Diallo aliyeingia kipindi cha pili akichukua nafasi ya Ronaldo.
Klabu za Bayern Munich, Barcelona na Atletico Madrid zimewahi kuhusishwa na mchezaji huyo lakini zote baadaye kwa nyakati tofauti zilijiweka kando na mpango huo, pia amewahi kutakiwa na klabu kdhaa za Marekani na moja ya Saudi Arabia kwa mikataba inayotajwa kuwa minono lakini Ronaldo mwenyewe hajashawishika kujiunga na timu hizo.

The post Saha: Ronaldo mbinafsi first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2022/08/02/saha-ronaldo-mbinafsi/feed/ 0