Rodri - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Fri, 03 Jan 2025 20:25:49 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=6.8 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg Rodri - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 Rodri ashangaa Ronaldo kuhoji Ballon d’Or https://www.greensports.co.tz/2025/01/03/rodri-ashangaa-ronaldo-kuhoji-ballon-dor/ https://www.greensports.co.tz/2025/01/03/rodri-ashangaa-ronaldo-kuhoji-ballon-dor/#respond Fri, 03 Jan 2025 20:25:48 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=12573 Manchester, EnglandKiungo wa Man City, Rodri amesema kwamba anashindwa kuelewa ni kwa nini Cristiano Ronaldo anahoji yeye kuteuliwa na hatimaye kushinda tuzo ya Ballon d’Or mwaka 2024.Ronaldo ambaye ni mshindi wa tuzo hiyo kwa mara tano amesema mshambuliaji wa Real Madrid, Vinícius Júnior ndiye aliyetakiwa kushinda tuzo hiyo badala ya Rodri.Akifafanua kuhusu Vinicius, Ronaldo alisema […]

The post Rodri ashangaa Ronaldo kuhoji Ballon d’Or first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Manchester, England
Kiungo wa Man City, Rodri amesema kwamba anashindwa kuelewa ni kwa nini Cristiano Ronaldo anahoji yeye kuteuliwa na hatimaye kushinda tuzo ya Ballon d’Or mwaka 2024.
Ronaldo ambaye ni mshindi wa tuzo hiyo kwa mara tano amesema mshambuliaji wa Real Madrid, Vinícius Júnior ndiye aliyetakiwa kushinda tuzo hiyo badala ya Rodri.
Akifafanua kuhusu Vinicius, Ronaldo alisema kwamba mshambuliaji huyo ameshinda taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya na alifunga goli kwenye mechi ya fainali.
Alipoulizwa kuhusu hoja hiyo ya Ronaldo, Rodri alisema anashangaa kwa sababu Ronaldo anafahamu kuliko mtu mwingine yeyote namna tuzo hiyo inavyotolewa na zaidi ya yote jinsi mshindi anavyopatikana.

“Mwaka huu (2024) waandishi wa habari ambao walipiga kura wameona mimi nafaa kuwa mshindi na huenda ni waandishi hawa hawa ambao kuna wakati walimpigia kura yeye kushinda na fikiria wakati huo angekubali,” alisema Rodri.


Baada ya Rodri kutangazwa mshindi wa tuzo hiyo, Real Madrid waligomea hafla za utoaji tuzo hiyo zilizofanyika Oktoba mwaka jana jijini Paris, Ufaransa.
Rodri alipewa tuzo hiyo kwa namna ambavyo alicheza soka la kuvutia katika msimu ambao aliisaidia Man City kubeba taji la Ligi Kuu England na Hispania kubeba Kombe la Ulaya 2024 au Euro 2024 nchini Ujerumani.
Kwa upande wa Vinicius alikuwa akitajwa kuwa na sifa za kubeba tuzo hiyo baada ya kuisaidia Real Madrid kubeba taji la Ligi Kuu Hispania au La Liga na lile la Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Vinicius ambaye pia ni mchezaji wa timu ya taifa ya Brazil hata hivyo naye alibeba tuzo ya mwanasoka bora wa mwaka wa Fifa.

The post Rodri ashangaa Ronaldo kuhoji Ballon d’Or first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2025/01/03/rodri-ashangaa-ronaldo-kuhoji-ballon-dor/feed/ 0
Rodri ambwaga Vinicius Ballon d’Or https://www.greensports.co.tz/2024/10/30/rodri-ambwaga-vinicius-ballon-dor/ https://www.greensports.co.tz/2024/10/30/rodri-ambwaga-vinicius-ballon-dor/#respond Wed, 30 Oct 2024 20:24:32 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=12164 Paris, UfaransaKiungo wa Man City na timu ya taifa ya Hispania, Rodri ameibuka kinara wa tuzo ya Ballon d’Or 2024 akimbwaga mshambuliaji wa Real Madrid na timu ya taifa ya Brazil, Vinicius Junior.Rodri na Vinicius ni miongoni mwa majina yaliyochomoza na kutajwa zaidi na wachambuzi wa soka kwamba mmoja wao angeibuka kinara wa tuzo hiyo […]

The post Rodri ambwaga Vinicius Ballon d’Or first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
Paris, Ufaransa
Kiungo wa Man City na timu ya taifa ya Hispania, Rodri ameibuka kinara wa tuzo ya Ballon d’Or 2024 akimbwaga mshambuliaji wa Real Madrid na timu ya taifa ya Brazil, Vinicius Junior.
Rodri na Vinicius ni miongoni mwa majina yaliyochomoza na kutajwa zaidi na wachambuzi wa soka kwamba mmoja wao angeibuka kinara wa tuzo hiyo iliyotolewa usiku wa kuamkia leo Jumanne.
Sambamba na wawili hao jina jingine ambalo lilionekana kutajwa mara kadhaa ni la mshambuliaji mwingine wa Real Madrid na timu ya taifa ya England, Jude Bellingham.
Baada ya Rodri kutangazwa mshindi waliofuata baada yake ni Vinicius na Bellingham huku Rodri akibebwa na mafanikio yake Man City waliobeba taji la Ligi Kuu England na Hispania alikobeba taji la Ulaya maarufu Euro 2024.
Inadaiwa Real Madrid haikuwakilishwa katika tuzo hizo baada ya kubaini kwamba Vinicius aliyepewa nafasi kubwa hakuwa kinara wa tuzo hiyo.
Awali akizungumzia kitendo cha Real Madrid kutowakilishwa kwenye tuzo hiyo, kocha wa Man City, Pep Guardiola ambaye kama ilivyo Rodri naye anatokea Hispania alisema yote ni sawa.
“Kama Real Madrid watataka kwenda sawa, kama hawatataka pia sawa, kama watataka kutoa pongezi sawa kama hawatataka kutoa pongezi pia hilo ni sawa,” alisema Pep.
Pep alifafanua kwamba unapokuwa wa pili au wa tatu katika tuzo hizo maana yake ni kwamba umefanya kitu cha kipekee, maana yake ni kwamba umekuwa na mwaka mzuri na unatakiwa uridhike.
Rodri ni mchezaji wa kwanza wa Man City kushinda tuzo ya Ballon d’Or na ni mchezaji wa kwanza wa Ligi Kuu England kushinda tuzo hiyo tangu Cristiano Ronaldo ashinde tuzo hiyo mwaka 2008.

The post Rodri ambwaga Vinicius Ballon d’Or first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/10/30/rodri-ambwaga-vinicius-ballon-dor/feed/ 0
Rodri ndio basi msimu huu https://www.greensports.co.tz/2024/09/27/rodri-ndio-basi-msimu-huu/ https://www.greensports.co.tz/2024/09/27/rodri-ndio-basi-msimu-huu/#respond Fri, 27 Sep 2024 20:53:41 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=11950 Manchester, EnglandKiungo wa Man City, Rodri atazikosa mechi zote za msimu huu kutokana na majeraha ya misuli ya mguu aliyoyapata Jumapili iliyopita.Rodri, 28, aliumia Jumapili katika mechi ya Ligi Kuu England (EPL) dhidi ya Arsenal iliyoisha kwa sare ya mabao 2-2 baada ya kugongana na Thomas Partey.Akithibitisha kuhusu mchezaji huyo, kocha wa Man City, Pep […]

The post Rodri ndio basi msimu huu first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Manchester, England
Kiungo wa Man City, Rodri atazikosa mechi zote za msimu huu kutokana na majeraha ya misuli ya mguu aliyoyapata Jumapili iliyopita.
Rodri, 28, aliumia Jumapili katika mechi ya Ligi Kuu England (EPL) dhidi ya Arsenal iliyoisha kwa sare ya mabao 2-2 baada ya kugongana na Thomas Partey.
Akithibitisha kuhusu mchezaji huyo, kocha wa Man City, Pep Guardiola alisema kwamba Rodri amefanyiwa upasuaji asubuhi ya leo Ijumaa na atakosa mechi zote za msimu huu.
“Amefanyiwa upasuaji asubuhi hii kwa hiyo atakuwa hapa msimu ujao, kwa msimu huu ndio amefika mwisho,” alisema Pep.
Pep aliwahi kusema kwamba mchezaji huyo hakuwa na mbadala katika kampeni zao za kulisaka taji la EPL msimu uliopita ambapo walifanikiwa kuwazidi waliokuwa wapinzani wao wakuu Arsenal na kubeba taji hilo mara ya nne mfululizo.
Katika msimu huo, Rodri alikosa mechi tano za timu hiyo na kati ya hizo Man City ilipoteza nne na kwa mantiki hiyo huenda pengo hilo likawaathiri kwa mara nyingine msimu huu.

“Ni bahati mbaya tumepata habari zisizofurahisha lakini haya mambo huwa yanajitokeza, tutakuwa naye kumuunga mkono hatua kwa hatua wakati akipata matibabu ili apone, alichotupa hatuna mchezaji anayefanana naye,” alisema Pep.


Pep alisema kwa sasa klabu inalifanyia tathmini tatizo la mchezaji huyo kabla ya kuamua kama watasajili mchezaji mwingine katika dirisha dogo la Januari na kutafuta namna ya kucheza mechi nyingi zilizobaki bila ya kuwa na mchezaji wao muhimu.

The post Rodri ndio basi msimu huu first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/09/27/rodri-ndio-basi-msimu-huu/feed/ 0
Rodri: Wachezaji mbioni kugoma https://www.greensports.co.tz/2024/09/18/rodri-wachezaji-mbioni-kugoma/ https://www.greensports.co.tz/2024/09/18/rodri-wachezaji-mbioni-kugoma/#respond Wed, 18 Sep 2024 05:44:35 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=11923 Manchester, EnglandKiungo wa Man City na timu ya taifa ya Hispania, Rodri (pichani) ameema kwamba wachezaji wapo mbioni kufanya mgomo kutokana na mzigo wa ratiba ngumu yenye mechi nyingi za soka.Kwa msimu uliopita pekee, Rodri amecheza jumla ya mechi 63 za Man City pamoja na timu yake ya taifa katika msimu ambao ulifikia ukomo Julai […]

The post Rodri: Wachezaji mbioni kugoma first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Manchester, England
Kiungo wa Man City na timu ya taifa ya Hispania, Rodri (pichani) ameema kwamba wachezaji wapo mbioni kufanya mgomo kutokana na mzigo wa ratiba ngumu yenye mechi nyingi za soka.
Kwa msimu uliopita pekee, Rodri amecheza jumla ya mechi 63 za Man City pamoja na timu yake ya taifa katika msimu ambao ulifikia ukomo Julai 14 baada ya fainali za Kombe la Ulaya au Euro 2024.
Mchezaji huyo msimu huu anakabiliwa na mzigo wa mechi nyingi zaidi kuanzia Man City ambayo itashiriki Ligi ya Mabingwa Ulaya, michuano ambayo msimu huu itakuwa katika utaratibu mpya.
Zaidi ya hilo pia atashiriki michuano mipya ya klabu ya dunia ambayo itaanza mwezi Juni na hivyo huenda akajikuta akiwa na mzigo wa mechi nyingi zaidi kuliko ilivyokuwa msimu uliopita.
Alipoulizwa kama ratibu ngumu yenye mechi nyingi inaweza kuwafanya wachezaji wafanye mgomo, Rodri bla kupepesa alisema anadhani wanakaribia kufanya jambo hilo.

“Nadhani tunakaribia katika hilo, ni rahisi kuelewa, nafikiri ni jambo lililo wazi, nadhani kama utamuuliza mchezaji yeyote atasema hivyo hivyo, si mawazo ya Rodri au mtu mwingine mmoja, bali ni wazo la jumla kwa wachezaji wote,” alisema.


Rodri, 28, hata hivyo alisema hajui nini kitakachotokea lakini anachofahamu ni kwa wakati huu ni kwamba jambo hilo linawapa shida kwa sababu wao ndio wanaotaabika.
Mchezaji wa kimataifa anayeshiriki Ligi ya Mabingwa na Kombe la Dunia la Klabu anaweza akafikisha mechi 85 au zaidi kwa msimu huu na Rodri tangu ajiunge na Man City mwaka 2019 amekuwa akicheza mechi zaidi ya 50 za klabu kwa msimu idadi ambayo anasema tayari ni kubwa.

The post Rodri: Wachezaji mbioni kugoma first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/09/18/rodri-wachezaji-mbioni-kugoma/feed/ 0