Rasmus Hojlund - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Sat, 09 Aug 2025 14:13:11 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=7.0 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg Rasmus Hojlund - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 Man Utd kumpiga bei Hojlund https://www.greensports.co.tz/2025/08/03/man-utd-kumpiga-bei-hojlund/ https://www.greensports.co.tz/2025/08/03/man-utd-kumpiga-bei-hojlund/#respond Sun, 03 Aug 2025 20:15:06 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=13770 Manchester, EnglandMan United inadaiwa kuwa katika mpango wa kumuuza mshambuliaji wake, Rasmus Hojlund kwa ada inayotajwa kufikia Pauni 30 milioni.Habari hizo zimekuja ikiwa ni siku chache tangu mshambuliaji huyo kutoka Denmark afunge mabao mawili katika mechi dhidi ya Bournemouth iliyopigwa Jumatano iliyopita mjini Chicago.Mara baada ya mechi hiyo, waandishi walitaka kujua msimamo wa Hojlund baada […]

The post Man Utd kumpiga bei Hojlund first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Manchester, England
Man United inadaiwa kuwa katika mpango wa kumuuza mshambuliaji wake, Rasmus Hojlund kwa ada inayotajwa kufikia Pauni 30 milioni.
Habari hizo zimekuja ikiwa ni siku chache tangu mshambuliaji huyo kutoka Denmark afunge mabao mawili katika mechi dhidi ya Bournemouth iliyopigwa Jumatano iliyopita mjini Chicago.
Mara baada ya mechi hiyo, waandishi walitaka kujua msimamo wa Hojlund baada ya habari kwamba Man United ina mpango wa kumsajili mshambuliaji Benjamin Sesko anayekipiga katika klabu ya RB Leipzig.
Mpango wa kumsajili Sesko mwenye umri wa miaka 22 ambaye pia anawindwa na Newcastle unatajwa kuwa sababu kubwa ambayo inaweza kutoa ushawishi kwa Man United kumpiga bei Hojlund.
Suala la kumuuza mshambuliaji huyo pia huenda likachangiwa na hoja ya kwamba Man United inataka kujiweka sawa katika kanuni za Ligi Kuu England zinazohusu faida.
Ikitokea Man United kumuuza mshambuliaji huyo kwa Pauni 30 milioni, itakuwa hasara kwa timu hiyo kwa kuwa thamani yake inatajwa kufikia Pauni 43 milioni, alisajiliwa Man United kwa mkataba wa miaka mitano akiwa ameitumikia miwili hadi sasa.
Tangu kufunguliwa kwa dirisha la usajili wa Majira ya Kiangazi, Man United imetumia Pauni 130 kusajili wachezaji wawili ambao ni Bryan Mbeumo na matheus Cunha.
Hojlund alisajiliwa na Man United wakati wa kocha Erik ten Hag na ingawa kulikuwa na matumaini makubwa lakini hadi sasa bado hajaonesha kile kilichotarajiwa na wengi.

The post Man Utd kumpiga bei Hojlund first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2025/08/03/man-utd-kumpiga-bei-hojlund/feed/ 0
Straika Hojlund asaini Man United https://www.greensports.co.tz/2023/08/05/straika-hojlund-asaini-man-united/ https://www.greensports.co.tz/2023/08/05/straika-hojlund-asaini-man-united/#respond Sat, 05 Aug 2023 14:37:59 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=7246 Manchester, EnglandManchester United imekamilisha usajili wa straika, Rasmus Hojland (pchani kushoto) kutoka Atalanta ya Italia kwa ada ya Pauni 72 milioni na mchezaji huyo kusaini mkataba wa miaka mitano.Hojlund raia wa Denmark mwenye miaka 20 alijiunga na Atalanta inayocheza Ligi ya Serie A nchini Italia, mwaka 2022 na hadi sasa ameifungia timu hiyo mabao 10 […]

The post Straika Hojlund asaini Man United first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Manchester, England
Manchester United imekamilisha usajili wa straika, Rasmus Hojland (pchani kushoto) kutoka Atalanta ya Italia kwa ada ya Pauni 72 milioni na mchezaji huyo kusaini mkataba wa miaka mitano.
Hojlund raia wa Denmark mwenye miaka 20 alijiunga na Atalanta inayocheza Ligi ya Serie A nchini Italia, mwaka 2022 na hadi sasa ameifungia timu hiyo mabao 10 katika mechi 34 za msimu uliopita.
“Si siri kwamba nimekuwa shabiki wa klabu hii kubwa tangu nikiwa mtoto mdogo, nilikuwa na ndoto za kuja hapa nikiwa mchezaji wa Manchester United,” alisema Hojlund.
Hojlund anakuwa ni usajili wa tatu wa kocha Erik ten Hag tangu dirisha la usajili majira ya kiangazi kuanza, ameshawasajili Mason Mount kutoka Chelsea na kipa Mcameroon, Andre Onana kutoka Inter Milan ya Italia.
Hojlund pia alikuwa akiwindwa na klabu kadhaa barani Ulaya ikiwamo PSG ya Ufaransa lakini sasa ni rasmi kwamba klabu hiyo imeshamkosa straika huyo ambaye pia anaichezea timu ya Taifa ya Denmark.
Straika huyo hata hivyo atazikosa mechi za ufunguzi za msimu mpya wa 2023-24 utakaoanza siku chache zijazo kutokana na majeraha madogo madogo aliyoyapata wakati akiiwakilisha Atalanta katika mechi za kirafiki hivi karibuni.

“Hakika nina furaha isiyo kifani kwa kupata fursa hii ya kuifanya ndoto yangu itimie, na nina dhamira ya kulipa imani niliyooneshwa katika klabu hii, bado mapema mno katika maisha yangu ya soka lakini nipo tayari kucheza na kundi hili kubwa la wachezaji wa hadhi ya juu duniani,” alisema Hojlund.


Hojlund alianza kuonesha umahiri wa kuzifumania nyavu akiwa kwao Denmark kabla ya kusajiliwa na Sturm Graz ya Austria mwaka 2020.

Tayari nyota yake imeshaanza kung’ara timu ya Taifa ya Denmar ambayo hadi sasa ameichezea mechi sita na kufunga mabao sita katika mbio za timu hiyo kuwania kufuzu fainali za Kombe la Ulaya 2024 au Euro 2024.

The post Straika Hojlund asaini Man United first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/08/05/straika-hojlund-asaini-man-united/feed/ 0
Man United, Hojlund kimeeleweka https://www.greensports.co.tz/2023/07/31/man-united-hojlund-kimeeleweka/ https://www.greensports.co.tz/2023/07/31/man-united-hojlund-kimeeleweka/#respond Mon, 31 Jul 2023 06:16:10 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=7198 Manchester, EnglandKlabu ya Manchester United ipo tayari kulipa Pauni 64 milioni pamoja na nyongeza ya Pauni 8 milioni kwa ajili ya kumsajili mshambuliaji Rasmus Hojlund (pichani) kutoka klabu ya Atlanta ya Italia.Hojlund, 20, raia wa Denmark usajili wake ukikamilika atakuwa mchezaji wa tatu mpya kwenye kikosi cha kocha Erik ten Hag baada ya Mason Mount […]

The post Man United, Hojlund kimeeleweka first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Manchester, England
Klabu ya Manchester United ipo tayari kulipa Pauni 64 milioni pamoja na nyongeza ya Pauni 8 milioni kwa ajili ya kumsajili mshambuliaji Rasmus Hojlund (pichani) kutoka klabu ya Atlanta ya Italia.
Hojlund, 20, raia wa Denmark usajili wake ukikamilika atakuwa mchezaji wa tatu mpya kwenye kikosi cha kocha Erik ten Hag baada ya Mason Mount na Andre Onana.
Hojlund ametokea kuwa chaguo la kwanza kwa Ten Hag baada ya mpango wa kumsajili Harry Kane na Victor Osimhen kukwama na anaamini mchezaji huyo yuko katika umri sahihi hasa kwa kuwa Ten Hag anataka kuwekeza kwa wachezaji wa umri mdogo.
Awali klabu ya Atlanta ilitangaza kuwa ipo tayari kumuuza Hojlund kwa Pauni 77 milioni wakati Man United ilishikilia msimamo wa kutokuwa tayari kutoa zaidi ya Pauni 60 milioni kwa mchezaji huyo.
Man United hata hivyo inadaiwa kulegeza msimamo na imekubali kutoa pesa zaidi ikiwa na matarajio ya kumpata mchezaji huyo kabla ya siku ya mwisho ya kipindi cha usajili cha majira ya kiangazi.
Katika kinachoonekana kuwa Atlanta nayo ipo tayari kumuuza mchezaji huyo, juzi Jumamosi klabu hiyo ilimsajili mshambuliaji mpya, El Bilal Toure ambaye anatajwa kuwa mbadala wa Hojlund.
Hojlund ametokea kuwa mmoja wa washambuliaji mahiri, msimu uliopita wa 2022-23, aliifungia Atlanta mabao tisa katika mechi 32 na kabla ya hapo akiwa Sturm Graz ya Copenhagen, aliifungia timu hiyo mabao 27 na pia ana mabao sita katika mechi sita za timu ya Taifa ya Denmark.

The post Man United, Hojlund kimeeleweka first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/07/31/man-united-hojlund-kimeeleweka/feed/ 0