Raja Casablanca - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Thu, 30 Mar 2023 19:19:04 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=7.0.2 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg Raja Casablanca - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 Simba yatua Morocco https://www.greensports.co.tz/2023/03/30/simba-yatua-morocco/ https://www.greensports.co.tz/2023/03/30/simba-yatua-morocco/#respond Thu, 30 Mar 2023 19:18:50 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=5637 Na mwandishi wetuKikosi cha timu ya Simba kimewasili salama leo nchini Morocco tayari kwa mechi yao ya kukamilisha hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Raja Casablanca.Simba iliyoondoka na wachezaji 13 jana ikitokea Kilimanjaro walikolazimika kulala kwa usiku mmoja baada ya ndege yao kupata hitilafu, ilifika Morocco saa tatu asubuhi sawa na […]

The post Simba yatua Morocco first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Kikosi cha timu ya Simba kimewasili salama leo nchini Morocco tayari kwa mechi yao ya kukamilisha hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Raja Casablanca.
Simba iliyoondoka na wachezaji 13 jana ikitokea Kilimanjaro walikolazimika kulala kwa usiku mmoja baada ya ndege yao kupata hitilafu, ilifika Morocco saa tatu asubuhi sawa na saa sita mchana kwa saa za Afrika Mashariki.
Kabla ya kutua Morocco, Wekundu hao walipokuwa Qatar waliungana na wachezaji wengine wanne waliokuwa Taifa Stars; Aishi Manula, Beno Kakolanya, Mzamiru Yassin na Shomari Kapombe ambao nao walianza safari hiyo wakiwa Dar es Salaam juzi.
Ofisa Habari wa Simba, Ahmed Ally amezungumza na GreenSports kutoka Casablanca na kueleza kuwa mchezaji mwingine aliyeongezeka baada ya kuwasili Morocco ni Pape Sakho aliyekuwa na timu ya taifa ya Senegal.
Alieleza kuwa timu hiyo ilitarajia kufanya mazoezi jana saa nne usiku huu kwenye Uwanja wa Mohamed V, utakapopigwa mchezo huo saa 7 usiku wa kuamkia Jumamosi.

“Kila kitu kipo sawa, tumefika salama hapa Casablanca na leo tutafanya mazoezi kwenye Uwanja wa Mohamed V kwa ajili ya mechi hiyo. Sakho tayari naye ameshafika na sasa tunawasubiri Chama (Clatous), Inonga (Henock) na Saido (Ntibazonkiza) ambao wataingia muda wowote,” alisema Ally.


Alisema kuwasili kwa wachezaji hao kutakuwa kumekamilisha kikosi kamili kuelekea mechi hiyo ambayo Simba inahitaji ushindi kulinda heshima lakini tayari imeshafuzu hatua ya robo fainali.
Katika Kundi C, Raja ipo kileleni kwa pointi 13 ikifuatiwa na Simba yenye pointi tisa, kisha Horoya AC ya Guinea yenye pointi nne na Vipers ya Uganda yenye pointi mbili ambao tayari wameshapewa mkono wa kwaheri katika mashindano hayo.

The post Simba yatua Morocco first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/03/30/simba-yatua-morocco/feed/ 0
Safari ya Simba Morocco yaiva https://www.greensports.co.tz/2023/03/29/safari-ya-simba-morocco-yaiva/ https://www.greensports.co.tz/2023/03/29/safari-ya-simba-morocco-yaiva/#respond Wed, 29 Mar 2023 20:04:36 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=5627 Na mwandishi wetuKikosi cha Simba kimeendelea leo na safari yake ya kuelekea Morocco kwa mechi yao na Raja Casablanca baada ya jana kukwama kusafiri kutokana na hitilafu ya ndege waliyopanda.Simba ilianza juzi safari yake hiyo kwenye Kiwanja cha Ndege cha Julius Nyerere (JNIA), Dar es Salaam kupitia Kilimanjaro ambapo walipofika hapo ndege hiyo ilipata hitilafu […]

The post Safari ya Simba Morocco yaiva first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Kikosi cha Simba kimeendelea leo na safari yake ya kuelekea Morocco kwa mechi yao na Raja Casablanca baada ya jana kukwama kusafiri kutokana na hitilafu ya ndege waliyopanda.
Simba ilianza juzi safari yake hiyo kwenye Kiwanja cha Ndege cha Julius Nyerere (JNIA), Dar es Salaam kupitia Kilimanjaro ambapo walipofika hapo ndege hiyo ilipata hitilafu na kulazimika kulala mpaka jana.
Meneja wa Habari na Mawasiliano Simba, Ahmed Ally alieleza kuwa safari hiyo ya kupitia Qatar kuelekea Morocco imeanza jana saa tano asubuhi.

“Kulikuwa na hitilafu ya ndege tulipofika Kilimanjaro, hivyo tumelala hapa na saa tano tunatarajia kuanza safari ya kuelekea Morocco kupitia Qatar tayari kwa ajili ya mechi na Raja, na kila kitu kinaendelea kama kilivyokuwa,” alisema Ally.


Simba wameondoka na kikosi cha wachezaji 13 huku wachezaji wengine ambao wanaotumikia timu zao za taifa wakitarajia kujiunga moja kwa moja Morocco.
Mchezo huo na Raja wa kukamilisha hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika unatarajia kupigwa Jumamosi hii kwenye Uwanja wa Mohamed V, Casablanca.
Simba tayari imeshafuzu hatua ya robo fainali baada ya kufikisha pointi tisa zilizowaweka kwenye nafasi ya pili ya msimamo wa Kundi C ambalo linaongozwa na Raja yenye pointi 12.

The post Safari ya Simba Morocco yaiva first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/03/29/safari-ya-simba-morocco-yaiva/feed/ 0
Raja yaivuruga Simba kwa Mkapa https://www.greensports.co.tz/2023/02/19/raja-yaivuruga-simba-kwa-mkapa/ https://www.greensports.co.tz/2023/02/19/raja-yaivuruga-simba-kwa-mkapa/#respond Sun, 19 Feb 2023 07:49:45 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=5212 Na mwandishi wetuJumamosi imekuwa siku ya hovyo kwa timu ya Simba baada ya kukubali kichapo cha mabao 3-0 mbele ya Raja Casablanca kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam.Matokeo hayo yanatibua rekodi nzuri ya Simba katika mechi za makundi za CAF kwenye uwanja huo, rekodi ambayo imekuwa ikiambatana na usemi maarufu wa kwa Kwa Mkapa […]

The post Raja yaivuruga Simba kwa Mkapa first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Jumamosi imekuwa siku ya hovyo kwa timu ya Simba baada ya kukubali kichapo cha mabao 3-0 mbele ya Raja Casablanca kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam.
Matokeo hayo yanatibua rekodi nzuri ya Simba katika mechi za makundi za CAF kwenye uwanja huo, rekodi ambayo imekuwa ikiambatana na usemi maarufu wa kwa Kwa Mkapa hatoki mtu.
Hata hivyo Jumamosi ya Februari 18, 2023, ametoka mtu Kwa Mkapa, tena ametoka kwa ushindi wa kishindo, ‘mtu huyo’ ni Raja Casablanca, timu kutoka nchini Morocco.
Mambo yalianza kuwaharibikia Simba katika dakika ya 30 baada ya Hamza Khaba kuandika bao la kwanza kwa shuti la nje kidogo ya 18 akiitumia pasi ya Zakaria Habti.
Simba wakiitambua ahadi ya Sh 5 milioni ya Rais Samia Suluhu Hassan kwa kila bao, walipambana na kulisakama lango la Raja, mfano dakika ya 35, Pape Sakho alishindwa kuitumia vizuri pasi aliyopewa na Saido Ntibazonkiza kuipatia Simba bao. Sakho baadaye alitolewa na kuingia Moses Phiri.
Ntibazonkiza ambaye amerejea kwa mara nyingine kwenye kikosi cha Simba baada ya kukosekana mechi iliyopita, alionyesha uhai na kuongoza vyema mashambulizi pamoja na Clatous Chama lakini hadi mapumziko, wageni Raja walikuwa mbele kwa bao hilo.
Kipindi cha pili kasi ya Simba iliongezeka na mara kadhaa walilifikia lango la Raja ambao kwa muda wa takriban dakika 20 kazi yao kubwa ilikuwa kuokoa na kuvuruga mipango ya Simba.
Mabadiliko yaliyofanywa na kocha Roberto Olivieira a’ Robertinho ya kuwatoa John Bocco na nafasi yake kuingia Jean Baleke na Ismail Sawadogo na nafasi yake kuingia John Mkude yalizidi kuipa nguvu Simba lakini nafasi kadhaa ilizotengeneza timu hiyo hazikuzaa matunda.
Bocco kabla ya kutoka alipata nafasi nzuri lakini akajichanganya wakati wa kupiga mpira na Baleke naye muda mfupi baada ya kuingia aliunganishiwa pande na Chama lakini akashindwa kuipa Simba bao.
Simba ilikatishwa tamaa dakika ya 83 iliporuhusu bao la pili lililofungwa na Soufian Benjdida kabla ya kuruhusu la tatu dakika tatu baadaye lililofungwa kwa penalti na Mokaden. Penalti hiyo ilitokana na rafu ya Joash Onyango katika eneo la penalti.
Baada ya matokeo hayo, kocha Robertinho alisema kwamba kazi bado inaendelea kwa mechi zilizobaki ambazo wanaweza kuzitumia kuipatia Simba mafanikio.
Kwa Raja huo ni ushindi wa pili mkubwa baada ya ushindi wa mabao 5-0 katika mechi ya kwanza dhidi ya Vipers ya Uganda wakati Simba inakuwa imepoteza mchezo wa pili baada ya kulala kwa bao 1-0 katika mechi ya kwanza dhidi ya Horoya ya Guinea.
Kikosi cha Simba kilichoanza: Manula, Kapombe, Zimbwe Jr, Onyango, Inonga, Sawadogo, Ntibazonkiza, Mzamiru, Bocco, Chama na Phiri.

The post Raja yaivuruga Simba kwa Mkapa first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/02/19/raja-yaivuruga-simba-kwa-mkapa/feed/ 0
Raja watua Dar kuikabili Simba https://www.greensports.co.tz/2023/02/16/raja-watua-dar-kuikabili-simba/ https://www.greensports.co.tz/2023/02/16/raja-watua-dar-kuikabili-simba/#respond Thu, 16 Feb 2023 16:57:36 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=5167 Na mwandishi wetuWapinzani wa Simba SC, Raja Casablanca wametua nchini mchana wa leo tayari kwa mchezo wao wa pili wa hatua ya makundi wa Ligi ya Mabingwa Afrika.Timu hiyo ya Morocco imetua kwenye Uwanja cha Ndege cha Julius Nyerere (JNIA) huku wachezaji wake wakionekana na furaha na zaidi wakisisitiza wanaifahamu Simba wakijua ni timu kubwa […]

The post Raja watua Dar kuikabili Simba first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Wapinzani wa Simba SC, Raja Casablanca wametua nchini mchana wa leo tayari kwa mchezo wao wa pili wa hatua ya makundi wa Ligi ya Mabingwa Afrika.
Timu hiyo ya Morocco imetua kwenye Uwanja cha Ndege cha Julius Nyerere (JNIA) huku wachezaji wake wakionekana na furaha na zaidi wakisisitiza wanaifahamu Simba wakijua ni timu kubwa lakini wamekuja kupambana kutafuta pointi.
Raja wametua wakiwa wanaongoza Kundi C kwa pointi tatu baada ya kuibuka na ushindi wa nyumbani wa mabao 5-0 dhidi ya Vipers ya Uganda, ikitegemea upinzani mkali kutoka kwa Simba.
Simba katika mechi hiyo itaingia uwanjani kwa nia ya kupambana ili kuvuna pointi tatu za kwanza baada ya kukubali kipigo cha bao 1-0 dhidi ya Horoya ya Guinea kwenye mechi ya kwanza.
Kocha wa Simba, Roberto Oliveira ‘Robertinho’ amesisiiza kuwa jeshi lake liko tayari kuwakabili Raja na kuchukua pointi tatu katika mchezo huo utakaopigwa kwenye dimba la Mkapa, Dar es Salaam Jumamosi hii.
Robertinho amesema kinachompa matumaini ya ushindi katika mchezo huo ni utimamu na utayari waliokuwa nao wachezaji wake ambao wameonesha nia ya wazi kutaka kushinda mchezo huo.

“Dhamira yetu ni moja tu kwenye mchezo huo, pointi tatu bila kujali ukubwa na ubora wa mpinzani sababu hata Simba ni timu bora ndio maana imefika hatua hii na watu wajue kwenye hatua tuliyopo hakuna timu ndogo,” alisema Robertinho raia wa Brazil.


Kocha huyo amesema kurejea kwa baadhi ya wachezaji waliokuwa majeruhi kama Saido Ntibazonkiza, Jonas Mkude na Peter Banda kumemuongezea nafasi pana ya kuchagua kikosi kitakachoanza na kumpa matokeo mazuri kwenye mchezo huo unaosubiriwa kwa hamu na mashabiki wengi nchini.
Simba itaingia uwanjani ikiwa nafasi ya tatu katika kundi lake ikiwa haina pointi sawa na Vipers inayoburuza mkia huku Horoya ikiwa nafasi ya pili na pointi tatu kama Raja lakini ikizidiwa kwa mabao ya kufunga.

The post Raja watua Dar kuikabili Simba first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/02/16/raja-watua-dar-kuikabili-simba/feed/ 0