Rais Samia - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Sat, 22 Nov 2025 12:20:53 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=6.9.4 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg Rais Samia - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 CAF yampa tuzo Rais Samia https://www.greensports.co.tz/2025/11/22/caf-yampa-tuzo-rais-samia/ https://www.greensports.co.tz/2025/11/22/caf-yampa-tuzo-rais-samia/#respond Sat, 22 Nov 2025 12:20:48 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=14115 Rabat, MoroccoShirikisho la Soka Afrika (CAF) limempa tuzo ya heshima Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tazania, Samia Suluhu Hassan kwa mchango wake mkubwa wakati Tanzania ikiwa mwenyeji wa michuano ya CHAN 2024.Tanzania ilikuwa mwenyeji wa michuano ya CHAN ambayo hushirikisha wachezaji wa ligi za ndani wa timu za mataifa ya Afrika, michuano ambayo wenyeji […]

The post CAF yampa tuzo Rais Samia first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Rabat, Morocco
Shirikisho la Soka Afrika (CAF) limempa tuzo ya heshima Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tazania, Samia Suluhu Hassan kwa mchango wake mkubwa wakati Tanzania ikiwa mwenyeji wa michuano ya CHAN 2024.
Tanzania ilikuwa mwenyeji wa michuano ya CHAN ambayo hushirikisha wachezaji wa ligi za ndani wa timu za mataifa ya Afrika, michuano ambayo wenyeji pia walikuwa Kenya na Uganda.
Katika tuzo hiyo CAF pia imethamini michango ya marais wa Kenya, William Ruto na Yoweri Museveni wa Uganda ambao kama ilivyo kwa Rais Samia nao wamepewa tuzo hiyo.
Katika hafla ya utoaji wa tuzo hiyo, tuzo ya Rais Samia ilipokewa kwa niaba yake na katibu mkuu wa wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Gerson Msigwa.
Katika salamu zake, CAF imesema kuwa imetoa tuzo hiyo kwa viongozi wa Tanzania, Kenya na Uganda kwa lengo la kuthamini maandalizi bora ya michuano hiyo katika nchi hizo tatu za Afrika Mashariki.
Tanzania, Kenya na Uganda pia ndizo nchi zinazotarajia kuwa wenyeji wa michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon) 2027.

The post CAF yampa tuzo Rais Samia first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2025/11/22/caf-yampa-tuzo-rais-samia/feed/ 0
Uwanja kupewa jina la Rais Samia https://www.greensports.co.tz/2024/03/13/uwanja-kupewa-jina-la-rais-samia/ https://www.greensports.co.tz/2024/03/13/uwanja-kupewa-jina-la-rais-samia/#respond Wed, 13 Mar 2024 05:41:28 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=10157 Na mwandishi wetuKatibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Gerson Msigwa amesema uwanja utakaojengwa mkoani Arusha utaitwa Dk Samia Suluhu Hassan kama Rais ataridhia hilo.Ujio wa uwanja huo wa kisasa unaotarajiwa kujengwa hivi karibuni ni kwa ajili ya maandalizi ya fainali za Afrika za mwaka 2027 ambapo Tanzania itakuwa mwenyeji sambamba na Kenya […]

The post Uwanja kupewa jina la Rais Samia first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Gerson Msigwa amesema uwanja utakaojengwa mkoani Arusha utaitwa Dk Samia Suluhu Hassan kama Rais ataridhia hilo.
Ujio wa uwanja huo wa kisasa unaotarajiwa kujengwa hivi karibuni ni kwa ajili ya maandalizi ya fainali za Afrika za mwaka 2027 ambapo Tanzania itakuwa mwenyeji sambamba na Kenya na Uganda.
Akizungumza jijini Dar es Salaam Jumanne hii, Msigwa alisema uwanja huo utabeba zaidi ya watu 30,000 na unatarajiwa kugharimu mabilioni ya fedha.
“Tunaenda kujenga uwanja mkoani Arusha utaogharimu mabilioni ya fedha, utakaoweza kubeba zaidi ya watu 30,000 na tumepanga Rais Samia akiridhia tutauita Dk Samia Suluhu Hassan,” alisema.
Kuhusu ukarabati unaoendelea kwenye Uwanja Benjamin Mkapa, Msigwa alisema Sh bilioni 10 zitatumika kubadilisha viti 60,000 na kuweka vya kisasa vya kukunja ambapo pia kila kiti kitakuwa na namba ili kuwawezesha mashabiki kununua na kupata namba ya kiti atakachokalia.
Katika hatua nyingine, Msigwa alisema kwa sasa kwa kushirikiana na TFF wanataka kuweka nguvu kwa vijana chini ya miaka 20 ili kupata wachezaji watakaocheza fainali za Afrika zitakazofanyika nchini.
“Tunaamini kutakuwa na vijana wenye viwango na uwezo wa kusaidia timu, lakini pia tumefungua milango kwa wachezaji wa nje waje tutawapa hati (pasipoti),” aliongeza.

The post Uwanja kupewa jina la Rais Samia first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/03/13/uwanja-kupewa-jina-la-rais-samia/feed/ 0
Rais Samia aipongeza Stars https://www.greensports.co.tz/2024/01/18/rais-samia-aipongeza-stars/ https://www.greensports.co.tz/2024/01/18/rais-samia-aipongeza-stars/#respond Thu, 18 Jan 2024 20:30:28 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=9355 Na mwandishi wetuRais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ameipongeza timu ya taifa, Taifa Stars kwa mchezo mzuri waliouonesha walipokipiga na Morocco kwenye michuano ya Afcon licha a kufungwa mabao 3-0.“Mchezo mzuri usiku wa leo (jana), vijana wetu Taifa Stars japo bahati haikuwa upande wetu,” aliandika katika salamu zake kupitia ukurasa wake wa mtandao wa X […]

The post Rais Samia aipongeza Stars first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ameipongeza timu ya taifa, Taifa Stars kwa mchezo mzuri waliouonesha walipokipiga na Morocco kwenye michuano ya Afcon licha a kufungwa mabao 3-0.
“Mchezo mzuri usiku wa leo (jana), vijana wetu Taifa Stars japo bahati haikuwa upande wetu,” aliandika katika salamu zake kupitia ukurasa wake wa mtandao wa X zamani Twitter.
Rais Samia pia aliitakia heri timu hiyo na kusema taifa liko nyuma yao katika mechi zinazofuata baada ya jana Jumatano kupoteza kwa Morocco kwenye Uwanja wa Laurent Palou, San Depro nchini Ivory Coast.
Akieleza kuhusu kupoteza mchezo huo, kocha mkuu wa Stars, Adel Amrouche amefafanua kuwa mpango wake ulishindwa kufanya kazi ndio maana walifungwa mabao matatu.
“Mpango wetu wa mchezo ulishindwa. Hatukutarajia hali hii, lakini ninawapongeza Morocco kwa mchezo mzuri pamoja na matokeo mazuri.
“Ubora wa wachezaji wa Morocco ulionesha utofauti na walistahili kushinda ingawa tulitaka matokeo mazuri lakini pia tulifanya makosa binafsi,” alielezea Amrouche na kuongeza:
“Ninajaribu kuwa na matumaini. Tutarekebisha makosa yetu ya mchezo huu na kuongeza umakini katika mechi zijazo, haitakuwa rahisi lakini bado tuna nafasi.”
Kocha wa Morocco, Walid Regragui alisema: “Mechi za kwanza huwa ni ngumu kila mara na tuliiheshimu Tanzania na tumepata ushindi muhimu.
“Tulitaka kufunga mapema na tulipata nafasi, lakini hatimaye bao lilitokana na mpira wa adhabu, baada ya kufunga tulimaliza sehemu ngumu na wakati mwingine katika kipindi cha pili tulikubali kutokuwa na mpira na kusimamia mchezo kama timu kubwa.”
Morocco inaongoza msimamo wa Kundi F kwa pointi tatu ikifuatiwa na DR Congo iliyotoka sare ya bao 1-1 na Zambia inayoshika nafasi ya tatu.
Tanzania inaburuza mkia bila pointi. Januari 21 itapambana na mabingwa wa Afcon 2012, Zambia huku Morocco ikipepetana na DR Congo.

The post Rais Samia aipongeza Stars first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/01/18/rais-samia-aipongeza-stars/feed/ 0
RT wampongeza Rais Samia https://www.greensports.co.tz/2024/01/04/rt-wampongeza-rais-samia/ https://www.greensports.co.tz/2024/01/04/rt-wampongeza-rais-samia/#respond Thu, 04 Jan 2024 16:20:00 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=9154 Na mwandishi wetuShirikishi la Riadha Tanzania (RT), limepongeza hotuba ya Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan kwa kugusa sekta ya ya michezo hususani kutambua mchango mkubwa uliotolewa na wanariadha.Kwa mujibu wa Kaimu Katibu Mkuu RT, Jackson Ndaweka, hotuba ya Rais Samia, mbali ya kugusa sekta mbalimbali, hakuisahau michezo hususani riadha kwa kuchangia mafanikio na kuitangaza […]

The post RT wampongeza Rais Samia first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Shirikishi la Riadha Tanzania (RT), limepongeza hotuba ya Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan kwa kugusa sekta ya ya michezo hususani kutambua mchango mkubwa uliotolewa na wanariadha.
Kwa mujibu wa Kaimu Katibu Mkuu RT, Jackson Ndaweka, hotuba ya Rais Samia, mbali ya kugusa sekta mbalimbali, hakuisahau michezo hususani riadha kwa kuchangia mafanikio na kuitangaza vema Tanzania kimataifa kwa mwaka 2023.
“Sisi kama Riadha Tanzania tumeguswa na hotuba ya mheshimiwa Rais, tumefarijika pale alipotambua mafanikio ya wanariadha wetu Magdalena Shauri na Alphonce Simbu,” alisema Ndaweka na kuongeza:
“Hii itachochea kujituma zaidi na kufanya vizuri kwa vijana wetu na sisi kama shirikisho tunaahidi kujituma na kujipanga zaidi kwa kushirikiana na Serikali hususan wizara yenye dhamana na michezo, wadhamini na wadau mbalimbali ili kuleta mafanikio makubwa zaidi katika medani ya Riadha.”
Katika hotuba yake juzi, Rais Samia akielezea mafanikio katika sekta ya michezo alisema: “Kwenye sekta ya michezo, pamoja na kuimarisha miundombinu ikiwamo ukarabati Uwanja wa Benjamin Mkapa, mwaka huu tumepata mafanikio mengi ya kujivunia ikiwemo timu ya Yanga kupata medali ya pili kwenye Kombe la Shirikisho Afrika.
“Pia binti wa kitanzania Magdalena Shauri kuwa mshindi wa tatu kwenye mbio za Berlin Marathon na mwanariadha Alphonce Simbu kuwa mshindi wa pili kwenye mbio za Shanghai Marathon.”

The post RT wampongeza Rais Samia first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/01/04/rt-wampongeza-rais-samia/feed/ 0
Rais Samia awapa Twiga Stars milioni 200 https://www.greensports.co.tz/2023/12/07/rais-samia-awapa-twiga-stars-milioni-200/ https://www.greensports.co.tz/2023/12/07/rais-samia-awapa-twiga-stars-milioni-200/#respond Thu, 07 Dec 2023 15:54:22 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=8778 Na mwandishi wetuRais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ametoa Sh milioni 200 kwa timu ya Taifa ya Wanawake, Twiga Stars kwa kufuzu fainali ya mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika kwa Wanawake (Wafcoon 2024) zitakazofanyika Morocco.Hayo yamesemwa na Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk Damas Ndumbaro alipokwenda kuwalaki wachezaji na msafara wa timu […]

The post Rais Samia awapa Twiga Stars milioni 200 first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ametoa Sh milioni 200 kwa timu ya Taifa ya Wanawake, Twiga Stars kwa kufuzu fainali ya mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika kwa Wanawake (Wafcoon 2024) zitakazofanyika Morocco.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk Damas Ndumbaro alipokwenda kuwalaki wachezaji na msafara wa timu hiyo Uwanja cha Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), Dar es Salaam leo Alhamisi alfajiri walipowasili kutokea Togo kwenye mchezo wa marudiano kufuzu Wafcon.

“Vijana hawa wanastahili pongezi, tumekuja kuwapokea na kuwapongeza na kuleta salamu za Rais Samia Suluhu Hassan, ametangaza bonasi ya Sh milioni 200 kwa vijana hawa, ni habari nzuri kwao na sisi Watanzania,” alisema Dk Ndumbaro.


Naye mkuu wa msafara, makamu wa kwanza wa rais wa TFF, Athuman Nyamlani alishukuru kwa mapokezi na dua za Wanzania na bonasi ya Rais Samia pamoja na msaada wa tiketi walizopewa na serikali.
Twiga Stars imeungana na mataifa mengine 12 baada ya ushindi wa jumla wa mabao 3-2 dhidi ya Togo juzi na kuandika historia ya kufuzu kwa mara ya pili baada ya kufuzu mara ya kwanza mwaka 2010 katika michuano iliyofanyika Afrika Kusini.
Mataifa mengine yaliyofuzu ni wenyeji Morocco, bingwa mtetezi Afrika Kusini, Botswana, Algeria, Ghana, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Tunisia, Senegal, Zambia, Mali na Nigeria.

The post Rais Samia awapa Twiga Stars milioni 200 first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/12/07/rais-samia-awapa-twiga-stars-milioni-200/feed/ 0
Rais Samia mgeni rasmi Simba Day https://www.greensports.co.tz/2023/08/04/rais-samia-mgeni-rasmi-simba-day/ https://www.greensports.co.tz/2023/08/04/rais-samia-mgeni-rasmi-simba-day/#respond Fri, 04 Aug 2023 07:58:15 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=7226 Na mwandishi wetuTamasha la Simba Day limezidi kupata umaarufu baada ya klabu hiyo kumtangaza Rais Samia Suluhu Hassan kuwa mgeni rasmi.Kwa mujibu wa vyanzo vya habari vya klabu hiyo vilivyopatikana leo, Ijumaa mbali na wageni wengine waalikwa, kiongozi huyo mkuu wa nchi atalipamba tamasha hilo litakalofanyika kwenye Uwanja wa Mkapa jijini, Dar es Salaam. “Tunakushukuru […]

The post Rais Samia mgeni rasmi Simba Day first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Tamasha la Simba Day limezidi kupata umaarufu baada ya klabu hiyo kumtangaza Rais Samia Suluhu Hassan kuwa mgeni rasmi.
Kwa mujibu wa vyanzo vya habari vya klabu hiyo vilivyopatikana leo, Ijumaa mbali na wageni wengine waalikwa, kiongozi huyo mkuu wa nchi atalipamba tamasha hilo litakalofanyika kwenye Uwanja wa Mkapa jijini, Dar es Salaam.

“Tunakushukuru na tanakukaribisha kwa furaha isiyo kifani. Kwa kipekee kabisa, tunakushukuru kwa mchango wako mkubwa kwenye michezo na maendeleo ya Taifa,” ilieleza sehemu ya taarifa ya klabu ya Simba.


Simba inafanya tamasha hilo ikiwa imetanguliwa na mahasimu wake Yanga na kufuatiwa na Singida Big, lengo mojawapo la matamasha hayo pamoja na mambo mengine ni kutangaza wachezaji wote watakaoiwakilisha timu hiyo kwa msimu mpya wa 2023-24.
Katika siku hiyo mashabiki wa Simba wataishuhudia timu yao mpya ikiumana na Power Dynamos ya Zambia, timu ambayo pia huenda ikakutana nayo tena kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika katika hatua ya pili.
Mbali na mechi hiyo, katika tamasha hilo kama ilivyo ada kutakuwa na burudani ya muziki kutoka kwa wasanii mbalimbali.

The post Rais Samia mgeni rasmi Simba Day first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/08/04/rais-samia-mgeni-rasmi-simba-day/feed/ 0
Mo Dewji amshukuru Rais Samia https://www.greensports.co.tz/2023/06/24/mo-dewji-amshukuru-rais-samia/ https://www.greensports.co.tz/2023/06/24/mo-dewji-amshukuru-rais-samia/#respond Sat, 24 Jun 2023 19:39:44 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=6713 Na mwandishi wetuRais wa heshima wa Klabu ya Simba, Mohammed Dewji ‘Mo’ amemshukuru na kumpongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuweka mazingira mazuri ya biashara nchini Tanzania yaliyompelekea kushinda tuzo ya All Africa Business Leaders Awards 2023 upande wa viwanda.Dewji ameshinda tuzo hiyo kwenye kipengele cha Industrialist of the Year usiku wa kuamkia leo Jumamosi […]

The post Mo Dewji amshukuru Rais Samia first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Rais wa heshima wa Klabu ya Simba, Mohammed Dewji ‘Mo’ amemshukuru na kumpongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuweka mazingira mazuri ya biashara nchini Tanzania yaliyompelekea kushinda tuzo ya All Africa Business Leaders Awards 2023 upande wa viwanda.
Dewji ameshinda tuzo hiyo kwenye kipengele cha Industrialist of the Year usiku wa kuamkia leo Jumamosi katika hafla iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Hoteli ya Sun City, Johannesburg, Afrika Kusini.
Kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii, mwekezaji huyo wa Simba SC alieleza furaha yake ya kushinda tuzo hiyo na kumshukuru Rais Samia kwa matunda hayo baada ya kuwarahisishia mazingira ya biashara nchini.
“Nimeheshimiwa na napokea kwa unyenyekevu Tuzo ya All Africa Business Leaders kwa Industrialist of the Year 2023. Naomba nitoe shukrani zangu za dhati kwa Rais wa Tanzania, mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kwa kujenga mazingira mazuri ya biashara nchini ambayo yanawezesha maendeleo makubwa ya viwanda nchi nzima,” aliandika Dewji.
Mbali na tuzo hiyo, Februari, mwaka huu pia jarida la Forbes lilimuorodhesha Dewji kuwa tajiri namba 13 Afrika akifungana na wengine wawili katika nafasi hiyo kwa utajiri wa Dola za Marekani bilioni 1.5 (sawa na Sh 3.5 trilioni).

The post Mo Dewji amshukuru Rais Samia first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/06/24/mo-dewji-amshukuru-rais-samia/feed/ 0
Rais Samia aomba sakata la Fei Toto limalizwe https://www.greensports.co.tz/2023/06/05/rais-samia-aomba-sakata-la-fei-toto-limalizwe/ https://www.greensports.co.tz/2023/06/05/rais-samia-aomba-sakata-la-fei-toto-limalizwe/#respond Mon, 05 Jun 2023 20:28:15 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=6467 Na mwandishi wetuSakata la klabu ya Yanga na kiungo wake, Feisal Salum au Fei Toto huenda likafika mwisho baada ya Rais Samia Suluhu Hassan kuwaomba viongozi wa klabu hiyo kumaliza mzozo wao na mchezaji huyo.Rais Samia ametoa kauli hiyo Ikulu leo Jumatatu wakati wa hafla ya chakula cha jioni aliyowaandalia wachezaji na viongozi wa Yanga […]

The post Rais Samia aomba sakata la Fei Toto limalizwe first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Sakata la klabu ya Yanga na kiungo wake, Feisal Salum au Fei Toto huenda likafika mwisho baada ya Rais Samia Suluhu Hassan kuwaomba viongozi wa klabu hiyo kumaliza mzozo wao na mchezaji huyo.
Rais Samia ametoa kauli hiyo Ikulu leo Jumatatu wakati wa hafla ya chakula cha jioni aliyowaandalia wachezaji na viongozi wa Yanga kuwapongeza kwa kufikia hatua ya fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika.
Yanga imeingia katika mzozo na mchezaji huyo tangu Desemba mwaka jana alipowasilisha maombi ya kutaka kuvunjiwa mkataba lakini uongozi wa Yanga haukukubaliana naye na hadi sasa mzozo huo unaendelea.
Baada ya Yanga kukataa kuvunja mkataba, Fei aliamua kwenda kuishitaki klabu hiyo TFF lakini kamati husika ya TFF haikukubaliana na hoja zake na kwa sasa zipo habari kwamba ana mpango wa kulifikisha suala hilo kwenye Mahakama ya Kimataifa ya Michezo (CAS).
Hivi karibuni Rais wa Yanga, Hersi Said alizungumza na kituo kimoja cha redio na kusema kwamba hawana tatizo na Fei na kumtaka arudi kuitumikia Yanga na kama kuna klabu inayomtaka ijitokeze.
Kwa upande wake Fei ameendelea kusisitiza nia ya kutaka kuihama Yanga akidai kwamba amekuwa akinyanyaswa na hata kutuhumiwa kuuza mechi na aliwahi kufanya mazungumzo na Hersi kwa saa sita lakini hawakufikia muafaka.
Wakati Hersi akimtaka Fei arudi Yanga, mchezaji huyo alinukuliwa akisema kwamba atakuwa tayari kurudi katika klabu hiyo iwapo tu Hersi ataondoka.
Katika hoja yake ya kutaka sakata la Fei Toto na Yanga limalizwe Rais Samia alisema haipendezi kwa klabu hiyo kubwa kama ya Yanga kuwa na ugomvi na Fei Toto.

“Viongozi wa Yanga nina ombi kwenu, sifurahii kusikia mnakuwa na mizozo na wachezaji, na sitaki kusema mengi nataka niwaambie tu ishu ya Fei Toto hebu kaimalizeni, kaimalizeni ili tuangalie mbele,” alisema Rais Samia.


Rais Samia alisema haipendezi klabu kubwa kama ya Yanga iliyofanya kazi nzuri inakuwa na ugomvi na katoto na angependa kupewa mrejesho wa hilo na akawakaribisha viongozi kumpa mrejesho wa suala hilo siku yoyote wakiwa tayari.

The post Rais Samia aomba sakata la Fei Toto limalizwe first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/06/05/rais-samia-aomba-sakata-la-fei-toto-limalizwe/feed/ 0
Rais Samia aongeza pesa Yanga https://www.greensports.co.tz/2023/05/18/rais-samia-aongeza-pesa-yanga/ https://www.greensports.co.tz/2023/05/18/rais-samia-aongeza-pesa-yanga/#respond Thu, 18 May 2023 12:39:08 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=6200 Na mwandishi wetuRais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan kwa mara nyingine ameipongeza Yanga kwa kutinga fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika akisisitiza wameipa heshima nchi na kuahidi kununua kila bao Sh milioni 20.Rais Samia alisema hayo baada ya Yanga kuitoa Marumo Gallants ya Afrika Kusini kwa jumla ya mabao 4-1 na […]

The post Rais Samia aongeza pesa Yanga first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan kwa mara nyingine ameipongeza Yanga kwa kutinga fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika akisisitiza wameipa heshima nchi na kuahidi kununua kila bao Sh milioni 20.
Rais Samia alisema hayo baada ya Yanga kuitoa Marumo Gallants ya Afrika Kusini kwa jumla ya mabao 4-1 na sasa itacheza fainali na USM Alger ya Algeria.
“Pongezi za dhati kwa Klabu ya Yanga kwa kutinga fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika. Mmeandika historia na kuipa nchi yetu heshima kubwa sana. Nawatakia kila la heri katika mchezo wenu wa fainali,” aliandika Rais Samia kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Twitter.
Rais Samia pia leo Alhamisi wakati akizindua minara ya mfumo wa urushaji matangazo ya televisheni ya Azam Media Limited kwa kutumia antena yaani mfumo wa Digital Terrestrial Television (DTT), alisema Serikali itatoa ndege kuipeleka Yanga Algeria na kila bao watakalofunga kwenye fainali atatoa Sh milioni 20.

“Nawapongeza Yanga kwa kufika fainali ila hata Simba japo imeishia njiani, timu hizi zilipoanza mashindano niliwapa motisha lakini kuanzia sasa kila bao litakalofungwa nitatoa Sh milioni 20 na Serikali itatoa ndege kwenda Algeria na itawasubiri hadi mechi imalizike,” alisema Rais Samia.


Rais Samia hata hivyo alifafanua kwamba bao litakalolipiwa fedha hizo ni lile ambalo litasababisha ushindi kwa timu na si vinginevyo.
Awali, Rais Samia alianza kwa kutoa Sh milioni 5 kwa kila bao kwenye hatua ya makundi ya michuano ya klabu Afrika kwa timu za Simba na Yanga kabla ya kupanda hadi Sh milioni 10 kwenye mechi za nusu fainali. Kwenye motisha hiyo hadi sasa Yanga imechota Sh milioni 100.
Pia aliwataka viongozi wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kuhakikisha wanaisaidia na kuipa moyo Yanga kama Serikali inavyofanya ili ifanye vizuri kwenye michezo miwili ya fainali iliyobaki.
Baada ya kauli ya Rais Samia uongozi wa Yanga ulitoa taarifa ya kumshukuru: “Uongozi wa Yanga unapenda kutoa shukrani kwa Rais wetu Samia Suluhu Hassan kwa kutupatia ndege ya kusafiria kwenye mchezo wetu wa pili wa fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika utakaochezwa nchini Algeria dhidi ya USM Alger.”
Wakati huo huo, Rais wa heshima na mwekezaji wa Simba, Mohammed Dewji kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Twitter ameipongeza Yanga kwa kuingia fainali na kuieleza kuwa Tanzania inajivunia kwa mafanikio hayo.
Mechi ya mkondo wa kwanza ya fainali itachezwa Mei 28, Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam na mechi ya marudiano itachezwa Juni 3, mwaka huu nchini Algeria.
Yanga imekuwa timu ya kwanza kwa nchi za Afrika Mashariki na Kati katika miaka ya karibuni kucheza fainali za michuano ya Afrika baada ya Gor Mahia ya Kenya kutwaa lililokuwa taji la Washindi Afrika mwaka 1987 na kucheza fainali mwaka 1979.
Simba waliwahi kucheza fainali ya michuano ya klabu Afrika mwaka 1993 wakati wa mashindano ya Kombe la Caf na kufungwa na Stella Abidjan ya Ivory Coast.

The post Rais Samia aongeza pesa Yanga first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/05/18/rais-samia-aongeza-pesa-yanga/feed/ 0
Rais Samia aipongeza Yanga https://www.greensports.co.tz/2023/05/11/rais-samia-aipongeza-yanga-3/ https://www.greensports.co.tz/2023/05/11/rais-samia-aipongeza-yanga-3/#respond Thu, 11 May 2023 12:54:45 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=6109 Na mwandishi wetuRais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ameipongeza Yanga kwa ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Marumo Gallants ya Afrika Kusini kwenye mchezo wao wa mkondo wa kwanza wa nusu fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika.Yanga ilipata ushindi huo jana Jumatano kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam na sasa inasubiri mechi ya marudiano […]

The post Rais Samia aipongeza Yanga first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ameipongeza Yanga kwa ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Marumo Gallants ya Afrika Kusini kwenye mchezo wao wa mkondo wa kwanza wa nusu fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika.
Yanga ilipata ushindi huo jana Jumatano kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam na sasa inasubiri mechi ya marudiano itakayopigwa Afrika Kusini Mei 17, mwaka huu ikihitaji sare yoyote au kutopoteza kwa zaidi ya bao 1-0 ili kutinga fainali.
Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Twitter, Rais Samia pia aliitaka Yanga kuendelea kuiheshimisha nchi kwa kujipanga kikamilifu kuelekea mechi inayofuata, akisisitiza kuendelea kuwaunga mkono kwa hamasa ya fedha anazotoa.

“Hongereni Yanga kwa ushindi katika mchezo wenu wa raundi ya kwanza ya nusu fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika. Nawatakia maandalizi mema kwa mchezo wenu wa raundi ya pili, muendelee kuiheshimisha nchi yetu. Hamasa yangu inaendelea,” aliandika Rais Samia.


Huo umekuwa mwendelezo wa Rais Samia kuipongeza Yanga kama alivyofanya ilipotinga hatua ya makundi ya michuano hiyo kwa kuitoa Club Africain ya Tunisia na hata ilipotinga robo fainali kwa kuitupa nje Rivers United ya Nigeria.
Mbali na pongezi hizo, Yanga imeendelea kuchota fedha za Rais Samia baada ya kukabidhiwa Sh milioni 20 na Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo, Pindi Chana mara baada ya kumalizika kwa mechi hiyo.
Kupitia hamasa hiyo ya fedha za Rais Samia kwa kila bao litakalofungwa kwenye michuano hiyo, Yanga sasa imechota jumla ya Sh 75 milioni baada ya Sh milioni 55 za mabao yao 11 ya awali.
Awali ahadi hiyo ilikuwa ni Sh 5,000,000 kwa kila bao litakalofungwa na Simba na Yanga kwenye michuano ya klabu Afrika kabla ya Simba kutolewa hatua ya robo fainali na kuvuna Sh milioni 55.
Baadaye, Rais Samia aliongeza fungu hilo na kufikia Sh 10 milioni kwa kila bao litakalofungwa hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo na sasa Yanga inaonekana kuendelea kunufaika vilivyo na hamasa hiyo.
Ikiwa ni mara ya kwanza kwa Rais Samia kuziunga mkono timu za Tanzania kwenye michuano hiyo, pia timu hizo zimeweka historia kwa mara ya kwanza zote mbili kutinga hatua ya robo fainali na sasa Yanga inakaribia kuweka rekodi mpya ya kuingia hatua ya fainali kwa mara ya kwanza.

The post Rais Samia aipongeza Yanga first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/05/11/rais-samia-aipongeza-yanga-3/feed/ 0