Raheem - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Sat, 30 Jul 2022 12:20:42 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=6.9.1 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg Raheem - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 Raheem Sterling aanza kutakata Chelsea https://www.greensports.co.tz/2022/07/30/sterling-aanza-kutakata-chelsea/ https://www.greensports.co.tz/2022/07/30/sterling-aanza-kutakata-chelsea/#respond Sat, 30 Jul 2022 12:03:25 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=2044 Milan, ItaliaMshambuliaji wa zamani wa Man City, Raheem Sterling ameanza kutakata katika klabu yake mpya ya Chelsea baada ya kufunga goli jana jioni wakati timu hiyo ilipoibuka na ushindi wa mabao 3-1 mbele ya Udinese ya Italia katika mechi ya kirafiki iliyopigwa kwenye Uwanja wa Dacia.Sterling alijiunga na Chelsea hivi karibuni, uhamisho ambao kwa kiasi […]

The post Raheem Sterling aanza kutakata Chelsea first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Milan, Italia
Mshambuliaji wa zamani wa Man City, Raheem Sterling ameanza kutakata katika klabu yake mpya ya Chelsea baada ya kufunga goli jana jioni wakati timu hiyo ilipoibuka na ushindi wa mabao 3-1 mbele ya Udinese ya Italia katika mechi ya kirafiki iliyopigwa kwenye Uwanja wa Dacia.
Sterling alijiunga na Chelsea hivi karibuni, uhamisho ambao kwa kiasi kikubwa ulichangiwa na shauku ya mchezaji huyo kukosa nafasi ya kucheza mara kwa mara katika kikosi cha kwanza cha Man City ambao pia walikuwa wakisita kumruhusu aondoke lakini hatimaye alitua Chelsea katika kipindi hiki cha usajili wa majira ya kiangazi. Katika kipindi hicho uvumi ulienea kuwa Man City ilisita kumruhusu Sterling aondoke kwa kilichodaiwa kuwa ni hofu kwamba huenda atakuwa mwiba kwao katika Ligi Kuu England, Kombe la FA, Kombe la Ligi na hata Ligi ya Mabingwa Ulaya. Na swali ni je baada ya kuanza kutakata katika mechi ya kirafiki, je ataendelea kutakata hata katika michuano hiyo ikiwamo kuiadhibu timu yake ya zamani ya Man City?
Sterling katika mechi ya jana alifunga bao lake hilo ambalo ni la kwanza tangu ajiunge na timu hiyo katika dakika ya 37 alipoinasa pasi ya Joginho, hilo likiwa bao la pili kwa Chelsea katika mechi hiyo, la kwanza likifungwa na N’Golo Kante dakika ya 20.
Wenyeji Udinese hata hivyo walipambana na dakika chache kabla ya timu kwenda mapumziko, Gerard Deulofeu aliipatia Udinese bao pekee na ubao kusomeka 2-1 lakini juhudi za timu hiyo kutaka kusawazisha hazikuzaa matunda badala yake wakajikuta wakipachikwa bao la tatu lililofugwa na Maon Mount, sekunde kadhaa kabla ya mpira kumalizika.
Matokeo hayo mazuri kwa Chelsea yamekuja ikiwa ni siku chache tangu timu hiyo ikumbane na kipigo cha mabao 4-0 kingine katika mechi ya kirafiki ya kujinoa kwa ajili ya msimu wa 2022/23 dhidi ya mahasimu wao wa London, Arsenal matokeo ambayo kocha wa timu hiyo, Thomas Tuchel alielezea jinsi yalivyomkera.

The post Raheem Sterling aanza kutakata Chelsea first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2022/07/30/sterling-aanza-kutakata-chelsea/feed/ 0