Polisi Kenya - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Sun, 09 Aug 2026 19:12:46 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=7.0.2 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg Polisi Kenya - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 Polisi Kenya watibua sherehe miaka 90 Simba https://www.greensports.co.tz/2026/08/09/polisi-kenya-watibua-sherehe-miaka-90-simba/ https://www.greensports.co.tz/2026/08/09/polisi-kenya-watibua-sherehe-miaka-90-simba/#respond Sun, 09 Aug 2026 19:12:45 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=14825 Na mwandishi wetuSherehe za Simba Day zilizoandamana na kumbukumbu ya miaka 90 tangu kuanzishwa kwa klabu ya Simba zimeingia doa baada ya timu hiyo kuchapwa bao 1-0 na Polisi Kenya, mechi iliyochezwa kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.Simba na Polisi Kenya zimeumana Jumamosi Agosti 8, 2026, mechi iliyotanguliwa na sherehe hizo sambamba na utambulisho […]

The post Polisi Kenya watibua sherehe miaka 90 Simba first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Sherehe za Simba Day zilizoandamana na kumbukumbu ya miaka 90 tangu kuanzishwa kwa klabu ya Simba zimeingia doa baada ya timu hiyo kuchapwa bao 1-0 na Polisi Kenya, mechi iliyochezwa kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.
Simba na Polisi Kenya zimeumana Jumamosi Agosti 8, 2026, mechi iliyotanguliwa na sherehe hizo sambamba na utambulisho wa wachezaji wa timu hiyo kwa ajili ya msimu mpya wa 2026-27.
Sherehe hizo zilipambwa na burudani ya muziki iliyofanywa na wasanii mbalimbali wakiongozwa na Ali Kiba ambapo mashabiki pia walimshuhudia mnyama Simba akiingizwa kunogesha tukio hilo.
Aliyepeleka kilio Simba alikuwa ni mshambuliaji wa zamani wa Singida Black Stars, Elvis Rupia aliyefunga bao hilo pekee katika dakika ya 90 ya mchezo huo.
Simba licha ya kufungwa bao hilo pekee lakini waliweza kukonga nyoyo za mashabiki waliofurika uwanjani hapo kwa kucheza soka safi na la kuvutia.
Timu hiyo ilitengeneza nafasi kadhaa za kufunga ambazo walishindwa kuzitumia huku wapinzani wao kutoka Kenya wakicheza kwa tahadhari kubwa hadi walipopata bao hilo pekee.
Kabla ya kuanza msimu mpya wa Ligi Kuu NBC, Simba itapata nafasi nyingine ya kupima ubora wa kikosi chake kwa kuumana na mahasimu wao Yanga katika mechi ya Ngao ya Jamii itakayopigwa Agosti 12, 2026 kwenye Uwanja wa New Amaan, Zanzibar.
Sherehe za Simba Day hufanyika kila mwaka tangu kuasisiwa mwaka 2009 na aliyekuwa mwenyekiti wa klabu hiyo, Hassan Dalali na katibu wake, Mwina Kaduguda.
Kwa mwaka huu sherehe za Simba Day zimenogeshwa na tukio la kumbukumbu ya miaka 90 tangu kuanzishwa kwa klabu hiyo mwaka 1936.

The post Polisi Kenya watibua sherehe miaka 90 Simba first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2026/08/09/polisi-kenya-watibua-sherehe-miaka-90-simba/feed/ 0