Paul Pogba - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Sat, 29 Nov 2025 11:49:44 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=7.0 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg Paul Pogba - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 Pogba kurejea dimbani https://www.greensports.co.tz/2025/11/22/pogba-kurejea-dimbani/ https://www.greensports.co.tz/2025/11/22/pogba-kurejea-dimbani/#respond Sat, 22 Nov 2025 12:54:22 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=14121 Monacxo, UfaransaKiungo wa timu ya Monaco, Paul Pogba anajiandaa kucheza mechi ya kwanza akiwa na timu hiyo baada ya kuwa nje ya soka kwa kipindi kirefu kutokana na adhabu aliyopewa kwa kosa la kutumia dawa za kuongeza nguvu.Pogba, 32, alijiunga na Monaco, timu ya Ligi 1 ya Ufaransa kipindi cha majira ya kiangazi mwaka jana […]

The post Pogba kurejea dimbani first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Monacxo, Ufaransa
Kiungo wa timu ya Monaco, Paul Pogba anajiandaa kucheza mechi ya kwanza akiwa na timu hiyo baada ya kuwa nje ya soka kwa kipindi kirefu kutokana na adhabu aliyopewa kwa kosa la kutumia dawa za kuongeza nguvu.
Pogba, 32, alijiunga na Monaco, timu ya Ligi 1 ya Ufaransa kipindi cha majira ya kiangazi mwaka jana baada ya adhabu aliyokuwa akikabiliwa nayo ya kufungiwa miaka minne kupunguzwa na Mahakama ya Kimataifa ya Michezo (CAS) hadi miezi 19.
Nyota huyo wa zamani wa timu ya taifa ya Ufaransa iliyobeba Kombe la Dunia mwaka 2018 aliingia katika kashfa ya utumiaji dawa za kuongeza nguvu hali iliyomfanya apotee kwenye soka na kudhaniwa kwamba huo ungekuwa mwisho wake.
Pogba ambaye pia amewahi kuichezea Man United, mara ya mwisho alionekana kwenye soka la ushindani, Septemba 2023 wakati huo akiichezea Juventus kwenye mechi ya Serie A dhidi ya Empoli.
Klabu ya Monaco ilimpa muda wa kufanya mazoezi kujiweka fiti na alitarajiwa kuanza kuichezea timu hiyo mapema mwezi huu kabla ya kupatwa na matatizo ya enka yaliyomuweka kando lakini kwa sasa jina lake limo katika orodha ya wachezaji wa Monaco ambao leo Jumamosi Novemba 22, 2025 watakabiliana na Rennes.
Baada ya kufanyiwa vipimo Agosti 2023, Pogba alikutwa na hatia na Februari 2024 alipewa adhabu ya kufungiwa miaka minne ingawa mwenyewe alidai kuna kosa lilifanyika alipopewa kilichoitwa dawa za kuongeza nguvu wakati nia haikuwa hiyo.
Moja ya kumbukumbu za Pogba kwa mashabiki wa Ufaransa ni siku alipofunga bao wakati Ufaransa ikiilaza Croatia 4-2 katika mechi ya fainal ya Kombe la Dunia 2018 nchini Ufaransa.

The post Pogba kurejea dimbani first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2025/11/22/pogba-kurejea-dimbani/feed/ 0
Pogba alalama kufungiwa miaka 4 https://www.greensports.co.tz/2024/03/01/pogba-alalama-kufungiwa-miaka-4/ https://www.greensports.co.tz/2024/03/01/pogba-alalama-kufungiwa-miaka-4/#respond Fri, 01 Mar 2024 08:41:38 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=9964 Juventus, ItaliaKiungo wa Juventus, Paul Pogba ameeleza kushtushwa na kusikitishwa baada ya kufungiwa kujihusisha na soka kwa miaka minne kwa kosa la kutumia madawa ya kusisimua misuli.Pogba, 30, ambaye pia ni mchezaji wa timu ya taifa ya Ufaransa alisimamishwa kujihusisha na soka Septemba mwaka jana baada ya vipimo vya awali kubaini kuwa mwili wake ulikuwa […]

The post Pogba alalama kufungiwa miaka 4 first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Juventus, Italia
Kiungo wa Juventus, Paul Pogba ameeleza kushtushwa na kusikitishwa baada ya kufungiwa kujihusisha na soka kwa miaka minne kwa kosa la kutumia madawa ya kusisimua misuli.
Pogba, 30, ambaye pia ni mchezaji wa timu ya taifa ya Ufaransa alisimamishwa kujihusisha na soka Septemba mwaka jana baada ya vipimo vya awali kubaini kuwa mwili wake ulikuwa na madawa hayo.
“Kila kitu nilichokifanikisha katika maisha yangu ya soka nimeporwa,” alisema Pogba katika taarifa yake na kusisitiza kwamba anakusudia kukata rufaa.
Pogba alifanyiwa vipimo vya ghafla Agosti 20 mwaka jana mara baada ya mechi ya kwanza ya Juventus ya msimu wa 2023-24.
Vipimo hivyo baadaye vilithibitishwa na Tume ya Kudhibiti Madawa (Nado) nchini Italia katika vipimo vya mara ya pili vilivyofanywa Oktoba na waendesha mashtaka wa Nado kuomba afungiwe miaka minne.
Pogba alisema kwamba anaamini matokeo ya vipimo hivyo hayakuwa sahihi na hakuwahi kufahamu kama amewahi kutumia dawa za kuongea nguvu kwa makusudi au kwa kutojua.

“Baada ya kumaliza vikwazo nilivyowekewa kisheria habari kamili itakuwa wazi,’ alisema Pogba na kusisitiza kuhusu nia yake ya kukata rufaa kwenye Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhisho ya Michezo (Cas).


Wakala wa Pogba, Rafael Pimenta alisema kwamba jambo pekee ambalo ana uhakika nalo ni kwamba mchezaji huyo hakuwahi kutaka kuvunja sheria.
Pogba ambaye pia aliwahi kukipiga Man United, akiwa Juventus mshahara wake kwa mwaka ulikuwa Pauni 6.8 milioni lakini tangu asimamishwe Septemba mwaka jana, pato hilo lilishuka na kuishia Pauni 2,054 kwa mwezi.

The post Pogba alalama kufungiwa miaka 4 first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/03/01/pogba-alalama-kufungiwa-miaka-4/feed/ 0
Wataka Pogba afungiwe miaka minne https://www.greensports.co.tz/2023/12/07/wataka-pogba-afungiwe-miaka-minne/ https://www.greensports.co.tz/2023/12/07/wataka-pogba-afungiwe-miaka-minne/#respond Thu, 07 Dec 2023 15:30:28 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=8772 Milan, ItaliaWaendesha mashtaka wa tume ya kudhibiti madawa ya yaliyopigwa marufuku michezoni wa nchini Italia wameomba kiungo wa Juventus na timu ya taifa ya Ufaransa, Paul Pogba afungiwe miaka minne.Pogba (pichani) ambaye alikuwa kwenye timu ya taifa ya Ufaransa iliyobeba Kombe la Dunia mwaka 2018, baada ya kufanyiwa vipimo alibainika kutumia madawa ya kusisimua misuli […]

The post Wataka Pogba afungiwe miaka minne first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Milan, Italia
Waendesha mashtaka wa tume ya kudhibiti madawa ya yaliyopigwa marufuku michezoni wa nchini Italia wameomba kiungo wa Juventus na timu ya taifa ya Ufaransa, Paul Pogba afungiwe miaka minne.
Pogba (pichani) ambaye alikuwa kwenye timu ya taifa ya Ufaransa iliyobeba Kombe la Dunia mwaka 2018, baada ya kufanyiwa vipimo alibainika kutumia madawa ya kusisimua misuli ambayo hayaruhusiwi kwa wanamichezo.
Baada ya kukutwa na tuhuma hizo, Pogba hakutaka suala hilo limalizwe kwa kufanya mazungumzo ya awali na waendesha mashtaka hao, na hiyo maana yake ni kwamba atapandishwa katika mahakama ya kupambana na madawa ya kuongeza nguvu ili kujibu tuhuma zinazomkabili.
Adhabu ya kufungiwa miaka minne pia inatambuliwa duniani katika kanuni zinazohusu makosa hayo lakini adhabu hiyo inaweza kupunguzwa iwapo mchezaji huyo ataweza kuthibitisha kwamba hakuwa amekusudia kufanya kosa analohusishwa nalo.
Vipimo vilivyobaini kwamba Pogba anatumia madawa hayo vilifanyika Agosti mwaka huu katika mechi kati ya Juventus na Udinese na kutangazwa mwezi mmoja baadaye ingawa katika mechi hiyo Pogba alikuwa benchi.
Pogba alirudi kwa mara nyingine katika klabu ya Juventus mwaka 2022 baada ya kuondoka Man United lakini alipitia kipindi kigumu akiandamwa na balaa la majeruhi.

The post Wataka Pogba afungiwe miaka minne first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/12/07/wataka-pogba-afungiwe-miaka-minne/feed/ 0
Pogba kufungiwa miaka minne https://www.greensports.co.tz/2023/09/12/pogba-kufungiwa-miaka-minne/ https://www.greensports.co.tz/2023/09/12/pogba-kufungiwa-miaka-minne/#respond Tue, 12 Sep 2023 16:18:54 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=7727 Milan, ItaliaKiungo wa Juventus, Paul Pogba amebainika kutumia dawa za kusisimua misuli na huenda akajikuta akifungiwa kucheza soka kwa miaka minne.Agosti 20 katika mechi ya Serie A kati ya Juventus na Udinese, Pogba ambaye alikuwa katika benchi la Juventus, alichukulwa vipimo na Kamisheni ya Kuzuia Dawa za Kusisimua Misuli ya Italia (Nado).Taarifa ya Nado iliyopatikana […]

The post Pogba kufungiwa miaka minne first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Milan, Italia
Kiungo wa Juventus, Paul Pogba amebainika kutumia dawa za kusisimua misuli na huenda akajikuta akifungiwa kucheza soka kwa miaka minne.
Agosti 20 katika mechi ya Serie A kati ya Juventus na Udinese, Pogba ambaye alikuwa katika benchi la Juventus, alichukulwa vipimo na Kamisheni ya Kuzuia Dawa za Kusisimua Misuli ya Italia (Nado).
Taarifa ya Nado iliyopatikana jana Jumatatu ilieleza kuwa baada ya kipimo hicho Pogba anasubiri vipimo vingine vya ziada kabla ya kushitakiwa na huenda akafungiwa kucheza soka miaka minne.
Kwa sasa Nado wameamua kumsimamisha Pogba wakati akisubiri taratibu nyingine zikiendelea kabla ya kuchukuliwa kwa uamuzi wa mwisho ambao pia utatoa ufafanuzi wa tukio zima.
Klabu ya Juventus ilitoa taarifa kuhusu kilichotokea kwa ufupi pamoja na kusimamishwa kwa mchezaji huyo na kuahidi kuweka wazi hatua inayofuata katika sakata hilo hapo baadaye.
“Tunasubiri matokeo ya vipimo vingine na kwa sasa hatuwezi kusema lolote, jambo linalotia shaka ni kwamba Paul Pogba katu hakuwahi kuwa na dhamira ya kuvunja sheria,” alisema Rafaela Pimenta ambaye ni wakala wa Pogba.
Kilichomkuta Pogba ni pigo jingine kwa mchezaji huyo ambaye tangu atue Juventus akitokea Man United zaidi ya mwaka mmoja uliopita amekuwa akiandamwa na majeraha hadi kushindwa kuiwakilisha Ufaransa kwenye fainali za Kombe la Dunia zilizofanyika Qatar, Novemba na Desemba mwaka jana.
Kabla ya kadhia ya madawa ya kusisimua misuli kuibuka, inadaiwa Pogba alinukuliwa akisema kwamba anafikiria kustaafu soka.
Baada ya kuwa na wakati mgumu msimu uliopita, ilitarajiwa Pogba angeiwakilisha vizuri Juventus msimu huu, timu ambayo msimu uliopita iliandamwa na kashfa ya upangaji matokeo lakini hadi sasa mchezaji huyo amecheza mechi mbili tu tena akitokea benchi.

The post Pogba kufungiwa miaka minne first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/09/12/pogba-kufungiwa-miaka-minne/feed/ 0
Jina la Pogba laibukia Saudi Arabia https://www.greensports.co.tz/2023/07/13/jina-la-pogba-laibukia-saudi-arabia/ https://www.greensports.co.tz/2023/07/13/jina-la-pogba-laibukia-saudi-arabia/#respond Thu, 13 Jul 2023 07:21:17 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=6931 Milan, ItaliaKiungo wa timu ya Taifa ya Ufaransa na klabu ya Juventus, Paul Pogba (pichani) ametajwa kuwa miongoni mwa wachezaji wanaotakiwa Saudi Arabia akiwa ameandaliwa mkataba wenye thamani ya Pauni 128 milioni.Gazeti moja linaloandika zaidi habari za michezo nchini Italia lilitoa taarifa hiyo bila kuweka wazi jina la timu inayomtaka mchezaji huyo ingawa inadhaniwa timu […]

The post Jina la Pogba laibukia Saudi Arabia first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Milan, Italia
Kiungo wa timu ya Taifa ya Ufaransa na klabu ya Juventus, Paul Pogba (pichani) ametajwa kuwa miongoni mwa wachezaji wanaotakiwa Saudi Arabia akiwa ameandaliwa mkataba wenye thamani ya Pauni 128 milioni.
Gazeti moja linaloandika zaidi habari za michezo nchini Italia lilitoa taarifa hiyo bila kuweka wazi jina la timu inayomtaka mchezaji huyo ingawa inadhaniwa timu zenye nia ya kumsajili kiungo huyo ni kati ya Al Nassr au Al-Ittihad.
Timu hizo mahasimu za jijini Riyadh zinapambana kujiimarisha kwa kusajili wachezaji wenye majina makubwa barani Ulaya na hadi sasa kila moja imefanikiwa kuwasajili mastaa mbalimbali wa Ulaya wakiwamo wachezaji wawili wa zamani wa Real Madrid.
Wachezaji hao mastaa ni Cristiano Ronaldo aliyejiunga na Al-Nassr Januari mwaka huu ingawa alitokea Man United na Karim Benzema ambaye amejiunga na Al-Ittihad mapema mwezi uliopita.
Pogba amekuwa na wakati mgumu Juventus kutokana na kuandamwa na janga la kuwa majeruhi na hivyo kushindwa kuisaidia timu hiyo tangu ajiunge nayo kabla ya msimu uliopita akitokea Man United.
Mchezaji huyo amekuwa na msimu mbaya hadi kushindwa kuiwakilisha Ufaransa kwenye fainali za Kombe la Dunia zilizofanyika Qatar na kufikia tamati Desemba mwaka jana ingawa Ufaransa ilifikia hatua ya fainali kabla ya kubwaga na Argentina waliobeba kombe.
Kwa hali hiyo kabla ya kusajiliwa na klabu yoyote ya Saudi Arabia tatizo la kuwa majeruhi ambalo limemuandama mchezaji huyo ni kati ya mambo yatakayoangaliwa ndipo uamuzi wa kumsajili au kuachana naye ufanyike.

The post Jina la Pogba laibukia Saudi Arabia first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/07/13/jina-la-pogba-laibukia-saudi-arabia/feed/ 0
Pogba benchi bado linamhusu https://www.greensports.co.tz/2023/02/02/pogba-benchi-bado-linamhusu/ https://www.greensports.co.tz/2023/02/02/pogba-benchi-bado-linamhusu/#respond Thu, 02 Feb 2023 06:01:14 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=4958 Milan, ItaliaKiungo wa Juventus, Paul Pogba hatokuwa fiti kucheza mechi ya robo fainali ya Coppa Italia dhidi ya Lazio jioni ya leo Alhamisi ingawa mshambuliaji, Dusan Vlahovic anatarajia kuwamo kwenye kikosi cha kwanza.Wachezaji hao ambao wamekuwa wakisubiriwa kwa muda mrefu hatimaye wameanza kurudi ambapo Jumapili watakuwa kwenye benchi katika mechi ya Serie A baada ya […]

The post Pogba benchi bado linamhusu first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Milan, Italia
Kiungo wa Juventus, Paul Pogba hatokuwa fiti kucheza mechi ya robo fainali ya Coppa Italia dhidi ya Lazio jioni ya leo Alhamisi ingawa mshambuliaji, Dusan Vlahovic anatarajia kuwamo kwenye kikosi cha kwanza.
Wachezaji hao ambao wamekuwa wakisubiriwa kwa muda mrefu hatimaye wameanza kurudi ambapo Jumapili watakuwa kwenye benchi katika mechi ya Serie A baada ya kucheza mechi ya kirafiki iliyohusisha kikosi cha akiba.
Vlahovic hakuiwakilisha Juventus katika mechi yoyote tangu Oktoba mwaka jana lakini katika mechi ya kirafiki majuzi dhidi ya Monza aliingia uwanjani dakika ya 65 kuchukua nafasi ya Mattia De Seiglio.
Katika mechi hiyo ambayo Juventus ililala kwa mabao 2-0, Pogba naye alikuwa kwenye benchi lakini kocha Massimiliano Allegri hakumpa nafasi ya kucheza.
“Ukiacha Bonucci (Lonardo) ambaye bado hajawa fiti kabisa, mchezaji mwingine pekee ambaye hatokuwapo kutokana na kutokuwa sawa ni Pogba,” alisema Allegri katika mkutano na waandishi wa habari jana Jumatano.
“Ni bahati mbaya kwamba unapokuwa nje ya uwanja kwa muda mrefu na kuanza kwa kasi kucheza kuna hali ya kujiona kama una maumivu, labda katika wiki chache atakuwa vizuri na katika kiwanngo cha juu,” aliema Allegri.
Pogba hakuwahi kucheza katika mechi yoyote ya ligi ya Juventu tangu asajiliwe kwa mara nyingine na klabu hiyo mwaka jana majira ya kiangazi.
Juventus inakabiliwa na hali ngumu kwenye Serie A ikiwa imenyang’anywa pointi 15 baada ya kubainika kutoa taarifa za uwongo za matumizi ya fedha na sasa imeangukia nafasi ya 10 hivyo ina kazi ya kufanya ili kurudi nafasi za juu.
“Klabu inajua pa kujitetea katika hilo lakini hilo kwetu haliwezi kuwa sababu, ni lazima twende tukafanye kinachohitajika kufanywa,” alisema Allegri.

“Labda ni mara ya kwanza kwa klabu kunyang’anywa pointi 15, tulikuwa nafasi ya tatu na ghafla tumeshushwa chini, sasa tunatakiwa kuanza tena, ni lazima tukabiliane na hali halisi kwa kadri inavyowezekana,” alisema Allegri.


The post Pogba benchi bado linamhusu first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/02/02/pogba-benchi-bado-linamhusu/feed/ 0