Pamba Jiji - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Thu, 06 Mar 2025 18:47:34 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=6.9.1 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg Pamba Jiji - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 Yanga yaitandika Pamba 3-0 https://www.greensports.co.tz/2025/03/01/yanga-yaitandika-pamba-3-0/ https://www.greensports.co.tz/2025/03/01/yanga-yaitandika-pamba-3-0/#respond Sat, 01 Mar 2025 20:56:35 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=13064 Na mwandishi wetuMabingwa watetezi wa Ligi Kuu NBC, Yanga wameendelea na kasi yao ya kulisaka taji la ligi hiyo baada ya kuinyuka Pamba Jiji mabao 3-0 katika mechi iliyopigwa Ijumaa hii kwenye dimba la CCM Kirumba mjini Mwanza.Ushindi huo umeifanya Yanga kuzidi kujichimbia kileleni mwa msimamo wa ligi hiyo wakiwa wamefikisha pointi 58 na kuendelea […]

The post Yanga yaitandika Pamba 3-0 first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu NBC, Yanga wameendelea na kasi yao ya kulisaka taji la ligi hiyo baada ya kuinyuka Pamba Jiji mabao 3-0 katika mechi iliyopigwa Ijumaa hii kwenye dimba la CCM Kirumba mjini Mwanza.
Ushindi huo umeifanya Yanga kuzidi kujichimbia kileleni mwa msimamo wa ligi hiyo wakiwa wamefikisha pointi 58 na kuendelea kuimarisha matumaini yao ya kulitetea taji.
Yanga inafuatiwa na Simba inayoshika nafasi ya pili ikiwa na pointi 51 ingawa Yanga imecheza michezo 22 ikiwa imewazidi Simba kwa michezo miwili.
Beki wa kushoto Shedrack Boka ndiye aliyekuwa wa kwanza kuziona nyavu za Pamba baada ya kuandika bao la kwanza katika dakika ya 27 kwa mpira wa adhabu.
Baada ya hapo mabao mengine ya Yanga yalifungwa na Stephane Aziz Ki ambaye aliingia akitokea benchi kuchukua nafasi ya Khalid Aucho.
Aziz Ki aliifungia Yanga bao la pili kwa kichwa dakika ya 74 kabla ya kuongeza bao la tatu dakika tatu baadaye kwa shuti kali la nje ya 18.

The post Yanga yaitandika Pamba 3-0 first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2025/03/01/yanga-yaitandika-pamba-3-0/feed/ 0
Yanga yaitandika Pamba 4-0 https://www.greensports.co.tz/2024/10/04/yanga-yaitandika-pamba-4-0/ https://www.greensports.co.tz/2024/10/04/yanga-yaitandika-pamba-4-0/#respond Fri, 04 Oct 2024 07:20:15 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=11977 Na mwandishi wetuYanga imeendeleza ubabe katika Ligi Kuu NBC baada ya kuichapa Pamba Jiji mabao 4-0 katika mechi iliyopigwa Alhamisi hii jioni kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.Kwa mara nyingine nyota ya beki wa timu hiyo, Ibrahim Hamas ‘Bacca’ imeendelea kung’ara baada ya kuandika bao la kwanza katika dakika ya tano ya […]

The post Yanga yaitandika Pamba 4-0 first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Yanga imeendeleza ubabe katika Ligi Kuu NBC baada ya kuichapa Pamba Jiji mabao 4-0 katika mechi iliyopigwa Alhamisi hii jioni kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.
Kwa mara nyingine nyota ya beki wa timu hiyo, Ibrahim Hamas ‘Bacca’ imeendelea kung’ara baada ya kuandika bao la kwanza katika dakika ya tano ya mchezo huo.
Bacca pia ndiye aliyefunga bao pekee la ushindi la timu hiyo katika mechi nyingine ya ligi hiyo dhidi ya Ken Gold, mechi ambayo Yanga ilitoka na ushindi wa bao 1-0.
Stephane Aziz Ki aliihakikishia Yanga kwenda mapumziko ikiwa mbele kwa mabao mawili baada ya kuandika bao la la pili katika dakika ya 45.
Mambo yaliendelea kuwaharibikia Pamba ambao walijikuta wakibugizwa bao la tatu zikiwa zimepita takriban dakika 10 baada ya timu kutoka mapumziko mfungaji akiwa ni Maxi Nzengeli.
Zikiwa zimebakia dakika tano mpira kumalizika, Kennedy Musonda alikamilisha karamu ya mabao ya Yanga baada ya kufunga bao la nne na kuihakikishia Yanga pointi tatu muhimu.
Mambo yaliwaharibikia zaidi Pamba ambao walilazimika kucheza pungufu kwa kipindi chote cha pili baada ya mchezaji wake Saleh Abdullah kupewa kadi nyekundu kwa kumchezea rafu Shedrack Boka wa Yanga.
Kwa ushindi huo Yanga ambao ni mabingwa watetezi wa ligi hiyo sasa wamefikisha pointi 12 katika mechi nne wakiwa hawajapoteza hata mechi moja.
Katika mechi nyingine ya ligi hiyo, Azam FC ikiwa ugenini ilitoka na ushindi wa bao 1-0 mbele ya Namungo wakati KMC nayo ikiwa nyumbani iliichapa Kagera Sugar bao 1-0.

The post Yanga yaitandika Pamba 4-0 first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/10/04/yanga-yaitandika-pamba-4-0/feed/ 0
Makalla aijaza pesa Pamba Jiji https://www.greensports.co.tz/2024/01/26/makalla-aijaza-pesa-pamba-jiji/ https://www.greensports.co.tz/2024/01/26/makalla-aijaza-pesa-pamba-jiji/#respond Fri, 26 Jan 2024 20:18:08 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=9457 Na mwandishi wetu Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Amos Makalla ameipa Klabu ya Pamba Jiji Sh milioni 5 ikiwa ni sehemu ya hamasa kwa ajili ya kuikabili Biashara United kwenye Ligi ya Championship. Akizungumza wakati wa hafla fupi ya utoaji fedha hizo leo Ijumaa katika ofisi yake, Makalla alisema fedha hizo ni kwa ajili ya […]

The post Makalla aijaza pesa Pamba Jiji first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Amos Makalla ameipa Klabu ya Pamba Jiji Sh milioni 5 ikiwa ni sehemu ya hamasa kwa ajili ya kuikabili Biashara United kwenye Ligi ya Championship.

Akizungumza wakati wa hafla fupi ya utoaji fedha hizo leo Ijumaa katika ofisi yake, Makalla alisema fedha hizo ni kwa ajili ya hamasa ya ushindi wa Pamba kuelekea mchezo huo muhimu.

“Nawaomba muendelee kushirikiana na kupambana ili Pamba ifanye vizuri na hatimaye irejee ligi kuu,” alisema Makalla.

Naye Mkurugenzi mtendaji wa timu ya Pamba Jiji, Alhaji Majogoro amemshukuru Makalla kwa kuendelea kuisaidia klabu yao kila wakati.

Kwa upande wake nahodha wa timu hiyo, Jerson Tegete alimshukuru Makalla kwa mchango wake kwenye klabu hiyo na kuahidi kupambana kuirejesha timu hiyo kwenye Ligi Kuu NBC.

The post Makalla aijaza pesa Pamba Jiji first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/01/26/makalla-aijaza-pesa-pamba-jiji/feed/ 0