Pa Omar Jobe - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Thu, 01 Feb 2024 19:07:24 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=7.0.2 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg Pa Omar Jobe - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 Jobe kuwanyamazisha wasiomuamini https://www.greensports.co.tz/2024/02/01/jobe-kuwanyamazisha-wasiomuamini/ https://www.greensports.co.tz/2024/02/01/jobe-kuwanyamazisha-wasiomuamini/#respond Thu, 01 Feb 2024 19:07:24 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=9546 Na mwandishi wetuMshambuliaji mpya wa Simba, Pa Omar Jobe (pichani) amesema kuwa atawanyamazisha kwa kufunga mabao kila atakapopata nafasi ili kuwathibitishia wale ambao hawana imani na kiwango chake.Jobe ambaye jana Jumatano alicheza mechi ya kwanza akiwa Simba alifunga bao moja kwenye ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Tembo FC kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho […]

The post Jobe kuwanyamazisha wasiomuamini first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Mshambuliaji mpya wa Simba, Pa Omar Jobe (pichani) amesema kuwa atawanyamazisha kwa kufunga mabao kila atakapopata nafasi ili kuwathibitishia wale ambao hawana imani na kiwango chake.
Jobe ambaye jana Jumatano alicheza mechi ya kwanza akiwa Simba alifunga bao moja kwenye ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Tembo FC kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) FA.
Mchezaji huyo alisema ana kitu cha kuwaonesha mashabiki wa Simba na kwamba hakuwa kwenye kiwango bora kwa sababu ametoka kwenye mapumziko.
“Nikiwa hapa kazi yangu ni kufunga mimi ni mshambuliaji natakiwa kupachika mabao kwa ajili ya klabu ndio maana niko hapa. Watu wana mashaka na mimi kutokana na muonekano wangu lakini hilo si muhimu, nimecheza Ulaya na kufunga mabao 13 msimu uliopita,” alisema Jobe.
“Jana kiwango hakikuwa kizuri, nilipoteza nafasi ya kwanza mpira ulienda nje lakini yote ni mpira wa miguu kama mshambuliaji unapata nafasi unapoteza sio jambo zuri.

“Unajua Simba ni klabu kubwa barani Afrika kabla ya kuja hapa nililijua hili, hata nchini Togo watu wanaizungumzia hata nilipokuja hapa watu wamenipongeza,” alisema Jobe.


Jobe raia wa Gambia ametua Simba hivi karibuni kurithi mikoba ya Jean Baleke aliyerejea TP Mazembe kabla ya kupelekwa Al Ittihad ya Libya kwa mkopo pia.

The post Jobe kuwanyamazisha wasiomuamini first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/02/01/jobe-kuwanyamazisha-wasiomuamini/feed/ 0
Moloko out Yanga, Simba yashusha straika https://www.greensports.co.tz/2024/01/15/moloko-out-yanga-simba-yashusha-straika/ https://www.greensports.co.tz/2024/01/15/moloko-out-yanga-simba-yashusha-straika/#respond Mon, 15 Jan 2024 19:07:06 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=9323 Na mwandishi wetuKlabu ya Yanga imeeleza kuachana na winga Jesus Moloko (pichani) raia wa DR Congo huku watani zao, Simba SC wakiweka wazi usajili wa straika wao mpya, Pa Omar Jobe kutoka Gambia.Moloko anapishana na Jobe katika viunga vya Kariakoo, Dar es Salaam zilizopo maskani ya timu hizo baada ya kudumu Jangwani kwa misimu miwili […]

The post Moloko out Yanga, Simba yashusha straika first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Klabu ya Yanga imeeleza kuachana na winga Jesus Moloko (pichani) raia wa DR Congo huku watani zao, Simba SC wakiweka wazi usajili wa straika wao mpya, Pa Omar Jobe kutoka Gambia.
Moloko anapishana na Jobe katika viunga vya Kariakoo, Dar es Salaam zilizopo maskani ya timu hizo baada ya kudumu Jangwani kwa misimu miwili na nusu.
Yanga imeweka wazi hilo leo Jumatatu kwenye mitandao yake ikieleza kuachana na mchezaji huyo wa zamani wa AS Vita ya DR Congo baada ya makubaliano ya pande zote mbili.
Simba nao wameeleza kuinasa saini ya Pa Jobe raia wa Gambia, kuongeza nguvu katika kikosi chao kama ambavyo hivi karibuni kocha wao, Abdelhak Benchikha alivyonukuliwa akieleza kuhitaji mshambuliaji mpya katika kikosi hicho.
Jobe amejiunga na Simba baada ya kumalizana na FC Zhenis ya Kazakhstan na tayari ametuma ujumbe akieleza: “Habari mashabiki wa Simba, mimi ni Pa One, natumai tutaonana hivi karibuni na kufunga mabao mengi, twenzetu.”

The post Moloko out Yanga, Simba yashusha straika first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/01/15/moloko-out-yanga-simba-yashusha-straika/feed/ 0