Novatus Dismas - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Fri, 01 Sep 2023 20:30:08 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=7.0.4 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg Novatus Dismas - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 Novatus huyooo Shakhtar https://www.greensports.co.tz/2023/09/01/novatus-huyooo-shakhtar/ https://www.greensports.co.tz/2023/09/01/novatus-huyooo-shakhtar/#respond Fri, 01 Sep 2023 20:30:07 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=7638 Na mwandishi wetuImeelezwa kuwa Mtanzania, Novatus Dismas (pichani) amekamilisha dili la kujiunga na klabu ya Shakhtar Donetsk ya Ukraine akitokea S.V. Zulte Waregem ya nchini Ubelgiji.Licha ya awali kuwepo kwa taarifa za nyota huyo kuwaniwa na timu za Middlesbrough na Southampton za England lakini jana duru mbalimbali za michezo Ulaya ziliripoti kuwa ni Shakhtar ndio […]

The post Novatus huyooo Shakhtar first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Imeelezwa kuwa Mtanzania, Novatus Dismas (pichani) amekamilisha dili la kujiunga na klabu ya Shakhtar Donetsk ya Ukraine akitokea S.V. Zulte Waregem ya nchini Ubelgiji.
Licha ya awali kuwepo kwa taarifa za nyota huyo kuwaniwa na timu za Middlesbrough na Southampton za England lakini jana duru mbalimbali za michezo Ulaya ziliripoti kuwa ni Shakhtar ndio iliyofanikiwa kunasa saini ya beki huyo.
Novatus anayemudu pia nafasi ya kiungo mkabaji ametajwa kutua kwa mabingwa hao mara mbili mfululizo wa Ligi Kuu ya Ukraine, ikiwa ni siku moja imepita tangu timu hiyo itangazwe kupangwa Kundi H la Ligi ya Mabingwa Ulaya likiwa pia na timu za Barcelona, FC Porto na Royal Antwerp.
Ingawa bado haijawekwa wazi kuhusu mkataba wake na timu hiyo lakini imefafanuliwa kuwa amechukuliwa na timu kwa kandarasi ya muda mrefu.
Nyota huyo ambaye ni miongoni mwa wachezaji tegemeo wa timu ya Taifa ya Tanzania, Stars, alipita katika timu ya vijana ya Azam kisha kupelekwa kwa mkopo Biashara United ya Mara mwaka 2020 kabla ya kurejea tena Azam ambayo ilimuuza Maccabi Tel Aviv ya Israel msimu wa 2020-21.

The post Novatus huyooo Shakhtar first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/09/01/novatus-huyooo-shakhtar/feed/ 0
Novatus ataja siri ya kuwa kiraka https://www.greensports.co.tz/2023/06/20/novatus-ataja-siri-ya-kuwa-kiraka/ https://www.greensports.co.tz/2023/06/20/novatus-ataja-siri-ya-kuwa-kiraka/#respond Tue, 20 Jun 2023 20:40:04 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=6658 Na mwandishi wetuBeki wa Taifa Stars, Novatus Dismas amesema kwamba amekuwa na mafanikio ya kucheza namba tofauti (kiraka) kutokana na kufuata maelekezo maalum ya uchezaji wa nafasi anayopewa kwa wakati husika.Dismas (pichani) amekuwa akitumika kwenye nafasi mbalimbali za ulinzi na amekuwa akizimudu kama kiungo wa ulinzi, beki wa pembeni kabla ya kuonekana akicheza kwa ufasaha […]

The post Novatus ataja siri ya kuwa kiraka first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Beki wa Taifa Stars, Novatus Dismas amesema kwamba amekuwa na mafanikio ya kucheza namba tofauti (kiraka) kutokana na kufuata maelekezo maalum ya uchezaji wa nafasi anayopewa kwa wakati husika.
Dismas (pichani) amekuwa akitumika kwenye nafasi mbalimbali za ulinzi na amekuwa akizimudu kama kiungo wa ulinzi, beki wa pembeni kabla ya kuonekana akicheza kwa ufasaha nafasi ya beki wa kati kwenye kikosi cha Stars.
“Kikubwa ninachoanza kuangalia ni maelekezo ya mwalimu, baada ya maelekezo ndiyo unafanya kitu chako cha ziada, huwezi kufanya cha ziada kabla ya maelekezo maana utakwenda tofauti tu sababu timu ni kikundi cha watu, unapofanya mambo yako kwanza unavuruga vitu vingi.

“Unajua walimu wengi wanaamini nina uwezo wa kuanza na timu kama kiongozi kwenye maeneo tofauti kama kiongozi kwa wenzangu ninaocheza nao, kwa hiyo naweza kucheza kokote kutokana na mawasiliano yangu na wachezaji wengine,” alisema Dismas.


Beki huyo anayekipiga Zulte Waregem ya Ubelgiji ameendelea kuwa lulu baada ya juzi akiwa beki wa kushoto wa Stars, kutoa pasi ya bao pekee kwa Simon Msuva, timu hiyo ilipokuwa ikiumana na Niger kuwania tiketi ya kushiriki Afcon 2023.
Dismas amekuwa akitumika Zulte mara nyingi kama beki wa kati au wa kushoto kulingana na mfumo husika lakini akiwa tayari ametumika kama kiungo mkabaji, beki wa kati na kiungo wa kushoto katika timu nyingine za Azam, Alliance, Maccabi Tel Aviv, Beitar Tel Aviv na Biashara United alizowahi kuzitumikia.

The post Novatus ataja siri ya kuwa kiraka first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/06/20/novatus-ataja-siri-ya-kuwa-kiraka/feed/ 0
Novatus Dismas atakiwa Southampton https://www.greensports.co.tz/2023/05/27/novatus-atakiwa-southampton/ https://www.greensports.co.tz/2023/05/27/novatus-atakiwa-southampton/#respond Sat, 27 May 2023 18:56:44 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=6326 London, EnglandBeki wa pembeni, Mtanzania Novatus Dismas anayekipiga katika klabu ya Zulte Waregem ya Ubelgiji anawaniwa na timu za Southampton na Middlesbrough za England.Novatus (pichani juu) ametajwa kuwaniwa na timu hizo kutokana na uwezo anaoendelea kuuonesha tangu ajiunge na Zulte mwanzoni mwa msimu huu akitokea Maccabi Tel Aviv ya Israel.Kwa mujibu wa gazeti la Daily […]

The post Novatus Dismas atakiwa Southampton first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

London, England
Beki wa pembeni, Mtanzania Novatus Dismas anayekipiga katika klabu ya Zulte Waregem ya Ubelgiji anawaniwa na timu za Southampton na Middlesbrough za England.
Novatus (pichani juu) ametajwa kuwaniwa na timu hizo kutokana na uwezo anaoendelea kuuonesha tangu ajiunge na Zulte mwanzoni mwa msimu huu akitokea Maccabi Tel Aviv ya Israel.
Kwa mujibu wa gazeti la Daily Mail la Uingereza, Southampton inayoshiriki Ligi Kuu England (EPL) inamuwania mchezaji huyo ikichuana na Middlesbrough.
Middlesbrough kwa sasa inapambana katika Ligi ya Championship wakati mambo si mazuri kwa Southampton ambayo tayari imeshuka daraja na inasubiri kucheza Championship msimu ujao.
Novatus mwenye umri wa miaka 20 ambaye ni kiungo mkabaji, akicheza kwa ufasaha pia kama beki wa pembeni, beki wa kati na kiungo wa kushoto, imeelezwa kuwa uwezo wake huo pia umezivutia timu hizo.
Licha ya timu yake kushuka daraja lakini bado Dismas ameendelea kuzivutia klabu kubwa kutokana na kiwango anachokionesha hata anapokuwa kwenye majukumua ya timu ya taifa, Taifa Stars.

The post Novatus Dismas atakiwa Southampton first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/05/27/novatus-atakiwa-southampton/feed/ 0