Napoli - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Fri, 05 May 2023 08:40:57 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=7.0 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg Napoli - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 Napoli yatwaa taji Serie A https://www.greensports.co.tz/2023/05/05/napoli-yatwaa-taji-serie-a/ https://www.greensports.co.tz/2023/05/05/napoli-yatwaa-taji-serie-a/#respond Fri, 05 May 2023 08:08:42 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=6022 Naples, ItaliaKlabu ya Napoli ya Italia hatimaye imebeba taji la Ligi Kuu Italia au Serie A ikiwa ni mara ya kwanza katika kipindi cha miaka 33 baada ya kutoka sare ya bao 1-1 na Udinese jana Alhamisi usiku.Alikuwa ni Victor Osimhen aliyeifungia Napoli bao la kusawazisha lililoihakikishia timu hiyo pointi moja waliyohitaji ili kutangazwa mabingwa […]

The post Napoli yatwaa taji Serie A first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Naples, Italia
Klabu ya Napoli ya Italia hatimaye imebeba taji la Ligi Kuu Italia au Serie A ikiwa ni mara ya kwanza katika kipindi cha miaka 33 baada ya kutoka sare ya bao 1-1 na Udinese jana Alhamisi usiku.
Alikuwa ni Victor Osimhen aliyeifungia Napoli bao la kusawazisha lililoihakikishia timu hiyo pointi moja waliyohitaji ili kutangazwa mabingwa wa Seria A msimu wa 2022-23 baada ya kuwa nyuma kwa bao la mapema la Udinese lililofungwa na Sandi Lovric.
Napoli sasa watacheza mechi tano zilizobaki za ligi hiyo kwa raha zao wakiwania kuboresha rekodi za ushindi kwani tayari taji la Serie A lipo kwenye himaya yao na tayari jiji la Naples limeshalipuka kwa shangwe na nderemo za mashabiki tangu jana usiku.
Mara ya mwisho Napoli ilibeba taji la Serie A mwaka 1990 ikiwa na gwiji wa soka duniani na nahodha wa zamani wa Argentina, Diego Maradona baada ya kubeba taji lao la kwanza miaka mitatu kabla.
“Kuwaona watu wa Napoli wakiwa na furaha inatosha kukupa fikra za hali waliyo nayo kwa sasa katika fikra zao,” alisema kocha wa Napoli, Luciano Spalletti.

“Hawa watu watalilikumbuka tukio hili pale maisha yanapokuwa magumu, wana kila sababu ya kushangilia jambo hili, unajiona katika hali ya utulivu kwa kuwapa tukio la furaha ya aina hii,” alisema Spalletti.


Napoli mataji yake ya mwisho yalipatikana wakati za zama za Maradona ambaye pia alikuwa nahodha wa timu ya Taifa ya Argentina na ambaye uwanja wa klabu hiyo umepewe jina lake, mataji hayo yalibebwa mwaka 1987 na 1990.
Baada ya mafanikio hayo, Napoli iliangukia katika majanga ya kiuchumi ikafilisika na kushuka hadi ligi ya chini ya Serie C na ingawa waliwahi kubeba taji la Coppa Italia mara tatu, kiu ya mashabiki wa timu hiyo ilikuwa ni kubeba taji la Serie A, kiu ambayo hatimaye imekatwa rasmi jana usiku huku mashabiki zaidi ya 10,000 wakisafiri kutoka Naples ili kuishuhudia timu hiyo ikibeba taji hilo baada ya sare ya ugenini na wengine wakifurahia wakiwa nyumbani..

The post Napoli yatwaa taji Serie A first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/05/05/napoli-yatwaa-taji-serie-a/feed/ 0
Bosi Napoli hataki wachezaji Waafrika https://www.greensports.co.tz/2022/08/04/bosi-napoli-hataki-wachezaji-waafrika/ https://www.greensports.co.tz/2022/08/04/bosi-napoli-hataki-wachezaji-waafrika/#respond Thu, 04 Aug 2022 09:56:35 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=2119 Naples, ItaliaMmiliki na mwenyekiti wa klabu ya Napoli, Aurelio De Laurentiis amesema kwamba klabu yake haitosajili tena wachezaji wa kutoka Afrika hadi hapo wachezaji hao watakapokubali kutoshiriki michuano ya Mataifa ya Afrika (Afcon).Beki Msenegali, Kalidou Koulibaly ambaye kwa sasa anaichezea Chelsea na kiungo Mcameroon, Andre Zambo walikosa mechi kadhaa za Napoli wakati wakiziwakilisha nchi zao […]

The post Bosi Napoli hataki wachezaji Waafrika first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Naples, Italia
Mmiliki na mwenyekiti wa klabu ya Napoli, Aurelio De Laurentiis amesema kwamba klabu yake haitosajili tena wachezaji wa kutoka Afrika hadi hapo wachezaji hao watakapokubali kutoshiriki michuano ya Mataifa ya Afrika (Afcon).
Beki Msenegali, Kalidou Koulibaly ambaye kwa sasa anaichezea Chelsea na kiungo Mcameroon, Andre Zambo walikosa mechi kadhaa za Napoli wakati wakiziwakilisha nchi zao kwenye fainali za Afcon ambazo zilifanyika kati ya Januari na Februari mwaka huu.
“Au vinginevyo wasaini kujitoa kushiriki katika Afcon,” alisema De Laurentiis kauli ambayo Koulibaly aliijibu akionyesha kusikitishwa na msimamo wa bosi wake wa zamani.
“Ni lazima uonyeshe heshima kwa timu ya Taifa kwa sababu huwezi kuzizungumzia timu za Taifa katika namna hii,” alisema Koulibaly.
“Nikiwa ndiye nahodha wa timu ya Senegal nafikiri hiyo si namna nzuri ya kuzizungumzia timu za soka za Afrika lakini namheshimu kama anafikiri timu inaweza kucheza bila ya wachezaji wa Afrika hiyo ni juu yake, si kila mtu ana mtazamo kama wake katika klabu,” aliongeza Kaulibaly.
De Laurentiis ambaye ni mtayarishaji filamu, pia aliipinga michuano iliyotaka kuanzishwa ya European Super League ambayo ilipingwa na wengi akiitaja kuwa ni michuano ya klabu zilizoonekana kuwa na hadhi fulani kwenye soka.
“Huwezi kuanzisha ligi ya super club kwa kuhusisha wanachama wa klabu zenye hadhi ambao wanawaalika wengine, unahitaji kuwa na demokrasia na kuweka milango wazi kwa kila mmoja,” alisema.

The post Bosi Napoli hataki wachezaji Waafrika first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2022/08/04/bosi-napoli-hataki-wachezaji-waafrika/feed/ 0