Namungo - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Wed, 13 Dec 2023 10:42:11 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=7.0 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg Namungo - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 Namungo yaachana na Kitambi https://www.greensports.co.tz/2023/12/13/namungo-yaachana-na-kitambi/ https://www.greensports.co.tz/2023/12/13/namungo-yaachana-na-kitambi/#respond Wed, 13 Dec 2023 10:42:10 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=8857 Na mwandishi wetuUongozi wa Namungo umetangaza kuachana na kocha wao, Denis Kitambi na kumshukuru kwa ushirikiano wake katika muda wote aliodumu na timu hiyo.Namungo imeeleza hayo leo Jumatano kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii ambapo imeandika: “Uongozi wa Namungo FC unapenda kumshukuru Kocha Denis Kitambi kwa muda wote aliotumikia timu kwa ushirikiano mkubwa ndani […]

The post Namungo yaachana na Kitambi first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Uongozi wa Namungo umetangaza kuachana na kocha wao, Denis Kitambi na kumshukuru kwa ushirikiano wake katika muda wote aliodumu na timu hiyo.
Namungo imeeleza hayo leo Jumatano kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii ambapo imeandika: “Uongozi wa Namungo FC unapenda kumshukuru Kocha Denis Kitambi kwa muda wote aliotumikia timu kwa ushirikiano mkubwa ndani ya timu yetu.”
Kitambi anakuwa kocha wa pili kuondoka Namungo msimu huu baada ya Cedric Kaze aliyejiuzulu Oktoba 22, mwaka huu baada ya kuiongoza Namungo katika mechi sita za awali bila ya ushindi.
Kitambi anaondoka Namungo baada ya kuiongoza timu hiyo katika mechi saba ambapo ilishinda mechi nne, sare mbili na kufungwa moja.
Hata hivyo, tetesi zinaeleza kuwa kocha huyo yuko mbioni kutua Geita Gold kuchukua nafasi ya Hemed Morocco ambaye anaonekana kuwa na matokeo ya kusuasua kwa timu hiyo inayoshika nafasi ya 14 ikiwa imeshinda mechi tatu, sare nne na kufungwa mara tano.

The post Namungo yaachana na Kitambi first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/12/13/namungo-yaachana-na-kitambi/feed/ 0
Namungo yavuruga hesabu za Simba https://www.greensports.co.tz/2023/05/04/namungo-yavuruga-hesabu-za-simba/ https://www.greensports.co.tz/2023/05/04/namungo-yavuruga-hesabu-za-simba/#respond Thu, 04 May 2023 05:12:31 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=6003 Na mwandishi wetuNamungo imevuruga hesabu za Simba kuishusha Yanga kileleni na hatimaye kubeba taji la Ligi Kuu NBC baada ya kuilazimisha sare ya bao 1-1 matokeo ambayo yanakuwa faraja kwa Yanga.Katika mechi baina ya timu hizo iliyopigwa Jumatano hii kwenye Uwanja wa Majaliwa mjini Ruangwa Lindi, Simba ndio waliokuwa wa kwanza kupata bao lililofungwa na […]

The post Namungo yavuruga hesabu za Simba first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Namungo imevuruga hesabu za Simba kuishusha Yanga kileleni na hatimaye kubeba taji la Ligi Kuu NBC baada ya kuilazimisha sare ya bao 1-1 matokeo ambayo yanakuwa faraja kwa Yanga.
Katika mechi baina ya timu hizo iliyopigwa Jumatano hii kwenye Uwanja wa Majaliwa mjini Ruangwa Lindi, Simba ndio waliokuwa wa kwanza kupata bao lililofungwa na Jean Baleke katika dakika ya 27 kufuatia mpira wa faulo uliopigwa na Saido Ntibazonkiza.
Dakika sita kabla ya timu hizo kwenda mapumziko, Namungo walizima matarajio ya Simba kutoka na pointi zote tatu baada ya kusawazisha bao kupitia kwa Hassan Kabunda.
Kabunda alifunga bao hilo akiuwahi mpira ambao kipa wa Simba, Ally Salim alishindwa kuuokoa, mpira huo ulitokana na kona iliyochongwa na mchezaji wa zamani wa Simba, Shiza Kichuya.
Simba hata hivyo katika mechi hiyo haikuwatumia wachezaji wake wengi tegemeo ambao wamezoeleka kuwamo katika kikosi cha kwanza isipokuwa Ntibazonkiza, Baleke na Joash Onyango ambao hawakuweza kuisaidia timu hiyo kupata ushindi.
Matokeo hayo sasa yanaiweka Simba pagumu katika mbio za kuivua Yanga taji la ligi kwani yanafifisha matumaini yaliyoibuka baada ya timu hiyo kuwachapa mahasimu wao Yanga mabao 2-0 hivi karibuni.
Ilitarajiwa kwamba baada ya ushindi wa mechi na Yanga, Simba ingeendelea kutoa vichapo huku ikiisubiri Yanga iteleze japo kwenye mechi moja pamoja na sare moja ili Simba ineemeke na faida ya mabao ya kufunga.
Simba sasa inakuwa imefikisha pointi 64 ikitanguliwa na Yanga inayoshika usukani wa ligi kwa tofauti ya pointi nne lakini Yanga imecheza mechi 26 hadi sasa wakati Simba imecheza mechi 27.
Kwa hali ilivyo sasa Yanga inahitaji ushindi wa mechi mbili tu ili ifikishe pointi 74 ambazo haziwezi kufikiwa na timu yoyote kwenye ligi hiyo ambayo imebakisha kati ya mechi tatu hadi nne kabla ya kufikia tamati.
Yanga inasubiri kuumana na Singida Alhamisi hii katika mechi nyingine ngumu ambayo Simba itaombea Yanga ipate matokeo mabaya ili walau matumaini ya timu hiyo yaanze kurejea katika mechi zilizobakia.

The post Namungo yavuruga hesabu za Simba first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/05/04/namungo-yavuruga-hesabu-za-simba/feed/ 0
Yanga yajiimarisha kileleni https://www.greensports.co.tz/2023/02/05/yanga-yajiimarisha-kileleni-2/ https://www.greensports.co.tz/2023/02/05/yanga-yajiimarisha-kileleni-2/#respond Sun, 05 Feb 2023 06:06:52 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=5007 Na mwandishi wetuYanga imeendelea kujiimarisha kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu NBC ikiendeleza dhamira yake ya kulitetea taji la ligi hiyo baada ya kuichapa Namungo FC mabao 2-0.Katika mechi hiyo iliyopigwa kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam Jumamosi hii jioni, Yanga ilinufaika kwa mabao ya Dickson Job kipindi cha kwanza na Stephan Aziz Ki […]

The post Yanga yajiimarisha kileleni first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Yanga imeendelea kujiimarisha kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu NBC ikiendeleza dhamira yake ya kulitetea taji la ligi hiyo baada ya kuichapa Namungo FC mabao 2-0.
Katika mechi hiyo iliyopigwa kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam Jumamosi hii jioni, Yanga ilinufaika kwa mabao ya Dickson Job kipindi cha kwanza na Stephan Aziz Ki mapema kipindi cha pili.
Job alifunga bao hilo akiunganisha kwa kichwa kona iliyochongwa na Djuma Shaaban wakati Aziz Ki aliyatumia makosa ya kipa wa Namungo, Deo Munishi Dida aliyejichanganya wakati wa kuokoa na kujikuta akimpasia mpira Aziz Ki ambaye aliumiliki vizuri kabla ya kufumua shuti lilikokwenda wavuni.
Kwa ushindi huo Yanga sasa inakuwa imefikisha pointi 59 ikiendelea kuwakimbia mahasimu wao Simba wanaoshika nafasi ya pili wakiwa na pointi 53 ikiwa ni tofauti ya pointi zile zile sita.
Katika mechi nyingine ya ligi hiyo iliyochezwa Jumamosi hii, Azam ilishindwa kutamba ugenini mbele ya Dodoma Jiji baada ya kulala kwa mabao 2-1.
Azam hata hivyo inaendelea kubaki katika nafasi yake ya tatu ikiwa na pointi 43 wakati Dodoma Jiji inachupa kutoka nafasi ya 12 hadi ya 10 ikiwa imefikisha pointi 24 sawa na Mbeya City lakini zikitofautiana mabao ya kufunga na kufungwa.
Yanga ingeweza kupata bao la tatu kama mshambualiaji wao nyota, Fiston Mayele angetulia na kuwa makini lakini akiwa katika nafasi nzuri ya kufunga alishindwa kufanya hivyo.
Ligi hiyo itaendelea tena Jumapili hii kwa mechi kati ya Ihefu watakaokuwa wenyeji wa Mbeya City wakati Ruvu Shooting wataikaribisha KMC.

The post Yanga yajiimarisha kileleni first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/02/05/yanga-yajiimarisha-kileleni-2/feed/ 0