Nairobi United - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Mon, 26 Jan 2026 19:43:00 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=6.9.1 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg Nairobi United - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 Azam, Singida mambo mazuri https://www.greensports.co.tz/2026/01/26/azam-singida-mambo-mazuri/ https://www.greensports.co.tz/2026/01/26/azam-singida-mambo-mazuri/#respond Mon, 26 Jan 2026 19:40:23 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=14294 Na mwandishi wetuJumapili ya Januari 26, 2026 imekuwa siku nzuri kwa Azam FC na Singida Black Stars, kila moja imetoka na ushindi katika michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika, Azam ikiilaza Nairobi United na Singida ikiichapa Otôho.Azam wakiwa ugenini waliichapa Nairobi United mabao 2-1 wakati Singida wakiwa nyumbani waliichapa Otoho ya Congo Brazzavile bao 1-0.Azam […]

The post Azam, Singida mambo mazuri first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Jumapili ya Januari 26, 2026 imekuwa siku nzuri kwa Azam FC na Singida Black Stars, kila moja imetoka na ushindi katika michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika, Azam ikiilaza Nairobi United na Singida ikiichapa Otôho.
Azam wakiwa ugenini waliichapa Nairobi United mabao 2-1 wakati Singida wakiwa nyumbani waliichapa Otoho ya Congo Brazzavile bao 1-0.
Azam waliokuwa ugenini Nairobi, Kenya waliianza vibaya mechi hiyo kwa kuchapwa bao la dakika ya 13 lililofungwa na Dancan Omala akiitumia vizuri pasi ya Michael Karamor.
Iliwachukua dakika nne wawakilishi hao wa Tanzania kusawazisha bao hilo kupitia kwa Jephte Kitambala ambaye alifumua shuti baada ya kuinasa pasi ya Yoro Diaby.
Timu hizo ziliendelea kupambana kila moja ikisaka bao la kuongoza lakini walikuwa ni Azam waliopata bao la ushindi dakika ya 78, bao lililotokana na shuti la Himid Mao na mpira kugonga mwamba kabla ya kumgonga kipa wa Nairobi United, Ernest Mohamed kabla ya kujaa wavuni.
Nao Singida walineemeka kwa bao pekee la Elvis Rupia na kutoka kifua mbele kwa ushindi huo mwembamba ambao ulitosha kuwatoa Otoho vichwa chini.

The post Azam, Singida mambo mazuri first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2026/01/26/azam-singida-mambo-mazuri/feed/ 0