Mzize - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz Michezo na Burudani ni zaidi ya ajira Wed, 08 Jan 2025 18:23:06 +0000 en-GB hourly 1 https://wordpress.org/?v=6.8 https://www.greensports.co.tz/wp-content/uploads/2021/09/cropped-WhatsApp-Image-2021-09-02-at-13.12.19-1-32x32.jpeg Mzize - Greensports: Michezo na Burudani https://www.greensports.co.tz 32 32 Nyota ya Mzize yang’ara CAF https://www.greensports.co.tz/2025/01/08/nyota-ya-mzize-yangara-caf/ https://www.greensports.co.tz/2025/01/08/nyota-ya-mzize-yangara-caf/#respond Wed, 08 Jan 2025 18:23:05 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=12604 Cairo, MisriMshambuliaji wa Yanga, Clement Mzize ametajwa kuwa mchezaji wa wiki wa michuano ya klabu inayoandaliwa na Shirikisho la Soka Afrika (CAF).Mzize ambaye ametajwa kwenye tovuti ya CAF, Jumamosi iliyopita aliiwakilisha vyema Yanga katika mechi ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya TP Mazembe ya DR Congo na Yanga kutoka na ushindi wa […]

The post Nyota ya Mzize yang’ara CAF first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Cairo, Misri
Mshambuliaji wa Yanga, Clement Mzize ametajwa kuwa mchezaji wa wiki wa michuano ya klabu inayoandaliwa na Shirikisho la Soka Afrika (CAF).
Mzize ambaye ametajwa kwenye tovuti ya CAF, Jumamosi iliyopita aliiwakilisha vyema Yanga katika mechi ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya TP Mazembe ya DR Congo na Yanga kutoka na ushindi wa mabao 3-1.
Mshambuliaji huyo ambaye anadaiwa kuwindwa na klabu kadhaa za barani Afrika alifunga mabao mawili katika ushindi huo wakati bao jingine la timu yake lilifungwa na Stephane Aziz Ki.
Katika mabao aliyofunga dhidi ya Mazembe, bao la Mzize lililovutia wengi ni lile la kwanza alilofunga kwa shuti la umbali wa mita 30 na kuzama wavuni kwa juu akimuacha mlinda mlango Aliufati Badara akiruka bila mafanikio.
Mzize sasa anakuwa amefikisha mabao matatu katika Ligi ya Mabingwa Afrika msimu huu wakati timu yake ya Yanga ikipambana kuwania kufuzu hatua ya robo fainali ya michuano hiyo ikitokea Kundi A.
Timu nyingine zilizo kundi moja na Yanga ni Al Hilal ya Sudan ambayo tayari imefuzu robo fainali ikisubiri timu nyingine moja ya kuungana nao kutoka kundi hilo.
MC Alger ya Algeria inashika nafasi ya pili ikiwa imekusanya pointi tano, Yanga ya tatu na pointi zake nne wakati Mazembe inaburuza mkia ikiwa na pointi mbili.
Yanga inayonolewa na kocha Saed Ramovic, itamalizia mechi zake mbili zilizobaki Januari 12 ikiwa ugenini dhidi ya Al Hilal na Januari 18 itakuwa mwenyeji wa MC Alger.

The post Nyota ya Mzize yang’ara CAF first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2025/01/08/nyota-ya-mzize-yangara-caf/feed/ 0
Zahera amtaka Mzize aondoke Yanga https://www.greensports.co.tz/2024/04/18/zahera-amtaka-mzize-aondoke-yanga/ https://www.greensports.co.tz/2024/04/18/zahera-amtaka-mzize-aondoke-yanga/#respond Thu, 18 Apr 2024 19:44:50 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=10667 Na mwandishi wetuKocha wa zamani wa Yanga, Mwinyi Zahera amesema huu ni wakati sahihi wa mshambuliaji wa Clement Mzize kuihama Yanga na kutafuta changamoto kwingine ili kuimarisha kipaji na uwezo alionao.Zahera ameeleza hayo leo Alhamisi wakati kukiwa na fununu za mchezaji huyo ambaye makabrasha yake yanaonesha ana miaka 20, kuwaniwa na baadhi ya timu vigogo […]

The post Zahera amtaka Mzize aondoke Yanga first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Kocha wa zamani wa Yanga, Mwinyi Zahera amesema huu ni wakati sahihi wa mshambuliaji wa Clement Mzize kuihama Yanga na kutafuta changamoto kwingine ili kuimarisha kipaji na uwezo alionao.
Zahera ameeleza hayo leo Alhamisi wakati kukiwa na fununu za mchezaji huyo ambaye makabrasha yake yanaonesha ana miaka 20, kuwaniwa na baadhi ya timu vigogo ikiwemo Azam FC na Watford inayoshiriki Ligi ya Championship nchini England.
Zahera ambaye kwa sasa anainoa Namungo FC ameeleza: “Lazima (Mzize) aende nje ya nchi, maana hapa hawezi kuwa na muendelezo mazuri na kufanya zaidi ya sasa, sababu anazijua timu zote.
Zahera alifafanua kuwa anafahamu jinsi wanavyojifunza lakini kwa maendeleo yake lazima aende nje apate utofauti namna ya kucheza, ufundishwaji wake pia hata mbinu ni tofauti sana.

“Kwa nafasi yake anapaswa kusaidia timu kwenda mbali kama ilivyokuwa kwa Mayele (Fiston) ambaye alikuwa namba moja kwa ushambuliaji na asilimia 90 timu ilitegemea mabao yake na yeye sasa anapaswa kuwa hivyo kwa timu nyingine maana ameshakaa Yanga na bado hana uhakika wa nafasi lakini anafanya vizuri kulingana na umri wake,” alisema Zahera.


Mzize ambaye kwenye ushindi wa mwisho wa Yanga wa mabao 3-0 dhidi ya Singida FG alitoa asisti mbili, Zahera anaamini huu ni wakati wake wa kuwa mshambuliaji kiongozi wa timu kubwa.
Alisema kwamba jambo hilo litawezekana endapo Mzize atakubali kutafuta changamoto nyingine katika mataifa mengine yaliyoendelea zaidi kimiundombinu ya soka.
Mzize anayepata upinzani wa namba kutoka kwa Joseph Guede na Kennedy Musonda, licha ya kutofunga mabao mengi msimu huu lakini mpaka sasa ametoa pasi tano za mabao akizidiwa pasi tatu na kinara Kipre Junior wa Azam mwenye asisti nane.
Katika kikosi ch Yanga, Mzize anazidiwa na Stephane Aziz Ki na Kouassi Yao ambao kila mmoja ana asisti saba.

The post Zahera amtaka Mzize aondoke Yanga first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/04/18/zahera-amtaka-mzize-aondoke-yanga/feed/ 0
Mzize abeba tuzo ya NIC https://www.greensports.co.tz/2024/02/08/mzize-abeba-tuzo-ya-nic/ https://www.greensports.co.tz/2024/02/08/mzize-abeba-tuzo-ya-nic/#respond Thu, 08 Feb 2024 07:03:20 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=9631 Na mwandishi wetuMshambuliaji wa Yanga, Clement Mzize ameibuka mshindi wa tuzo ya mchezaji bora wa mwezi Januari wa klabu hiyo inayodhaminiwa na Shirika la Bima la Taifa (NIC).Mzize ametwaa tuzo hiyo akiwashinda wachezaji wenzake, Gift Fredy na Willson Chigombo kutoka kikosi cha vijana ambaye alifanya vizuri kwenye michuano ya Kombe la Mapinduzi iliyomalizika Zanzibar hivi […]

The post Mzize abeba tuzo ya NIC first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Mshambuliaji wa Yanga, Clement Mzize ameibuka mshindi wa tuzo ya mchezaji bora wa mwezi Januari wa klabu hiyo inayodhaminiwa na Shirika la Bima la Taifa (NIC).
Mzize ametwaa tuzo hiyo akiwashinda wachezaji wenzake, Gift Fredy na Willson Chigombo kutoka kikosi cha vijana ambaye alifanya vizuri kwenye michuano ya Kombe la Mapinduzi iliyomalizika Zanzibar hivi karibuni.
Akizungumza baada ya kushinda tuzo hiyo inayotokana na kupigiwa kura na mashabiki wa timu hiyo, Mzize aliwashukuru wote waliompigia kura na kueleza kuwa tuzo hiyo imemuongezea ari ya kujituma zaidi ili kuingia tena kwenye kinyang’anyiro siku zijazo.

“Nawapongeza mashabiki wa Yanga, kwa kunipigia kura maana tuzo hii imeniongezea ari ya kuzidi kujituma kuisaidia timu yangu lakini na mafanikio yangu binafsi,” alisema Mzize.


Baada ya kuibuka mshindi mshambuliaji huyo anatarajiwa kupewa kitita cha Sh 4,000,000, pamoja na kombe dogo.
Mbali na Mzize wachezaji wengine wa Yanga ambao wamewahi kushinda tuzo hiyo ni Stephane Aziz Ki (Oktoba), Pacome Zouzoua (Novemba) na Djigui Diarra aliyeibuka mshindi wa Desemba.
Wakati huo huo, taarifa za ndani kutoka Yanga zinaeleza kuwa kipa namba moja wa timu hiyo, Diarra alitarajiwa kujiunga na wenzake jioni ya Jumatano akitokea kwao Mali alikokwenda kuitumikia timu yake ya taifa iliyokuwa ikishiriki michuano ya Afcon inayoendea nchini Ivory Coast.

The post Mzize abeba tuzo ya NIC first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2024/02/08/mzize-abeba-tuzo-ya-nic/feed/ 0
Aucho, Pacome, Mzize wawania tuzo ya mwezi https://www.greensports.co.tz/2023/11/30/aucho-pacome-mzize-wawania-tuzo-ya-mwezi/ https://www.greensports.co.tz/2023/11/30/aucho-pacome-mzize-wawania-tuzo-ya-mwezi/#respond Thu, 30 Nov 2023 19:43:21 +0000 https://www.greensports.co.tz/?p=8700 Na mwandishi wetuWachezaji Pacome Zouzoua, Khalid Aucho na Clement Mzize wameingia katika kinyang’anyiro cha kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa Yanga kwa Mwezi Novemba.Nyota hao wameingia kwenye kinyang’anyiro hicho baada ya kutoa mchango mkubwa kwa timu hiyo katika mechi walizocheza za mwezi huo.Huo ni utaratibu ambao klabu hiyo imejiwekea tangu kuanza kwa msimu huu ukiwa […]

The post Aucho, Pacome, Mzize wawania tuzo ya mwezi first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>

Na mwandishi wetu
Wachezaji Pacome Zouzoua, Khalid Aucho na Clement Mzize wameingia katika kinyang’anyiro cha kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa Yanga kwa Mwezi Novemba.
Nyota hao wameingia kwenye kinyang’anyiro hicho baada ya kutoa mchango mkubwa kwa timu hiyo katika mechi walizocheza za mwezi huo.
Huo ni utaratibu ambao klabu hiyo imejiwekea tangu kuanza kwa msimu huu ukiwa na lengo la kuongeza hamasa kwa wachezaji wake kujituma na kuipa mafanikio timu katika mashindano yote wanayoshiriki.
Mbali na tuzo hiyo pia mchezaji hujinyakulia kitita cha Sh milioni 4 taslimu na zawadi nyingine kutoka kwa wadhamini wa tuzo hiyo, Shirika la Bima la Taifa (NIC).
Kiungo wa Burkinafaso, Stephen Aziz Ki, ndiye mchezaji wa kwanza kuibuka mshindi wa tuzo hiyo kwa mwezi uliopita baada ya kuwashinda wachezaji wenzake, Maxi Nzengeli na beki Dickson Job.

The post Aucho, Pacome, Mzize wawania tuzo ya mwezi first appeared on Greensports: Michezo na Burudani.

]]>
https://www.greensports.co.tz/2023/11/30/aucho-pacome-mzize-wawania-tuzo-ya-mwezi/feed/ 0